Jinsi Ya Kufanya Tathmini Kwenye Kiwanja/Nyumba Kwa Lengo La Kujenga/Kutunza Utajiri

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Tathmini hii inafanyika kwenye nyumba ambazo ni kwa ajili ya KUJENGA/KUTUNZA utajiri. Nyumba za kuishi jenga au nunua kwa kuzingatia mapenzi yako binafsi (au mapenzi ya familia yako) pengine hata bila kufuata misingi hii ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
flyerdesign_07122022_171805.png


Viashiria vinne (4) vya kupata tathmini ya kipato endelevu (return on investment, ROI) cha nyumba yako ni;-

Moja.

Kipato chanya na endelevu (Positive Cash-flow Return)

Mbili.

Kupanda thamani kwa nyumba.

Tatu.

Kukuza mtaji fedha (Equity-build up). Hii ni pale ambapo unatumia mkopo kumiliki nyumba za kupangisha. Na kodi ya nyumba ya kila mwezi hukusanywa na kupelekwa benki kama marejesho ya mikopo.

Nne.

Kodi ya majengo serikalini. Hii kwa hapa Tanzania haina manufaa ya kifedha. Hivyo kwetu sisi Watanzania ni viashiria vitatu (3) tu unatakiwa kutumia ili kupata makadirio ya jumla ya kipato endelevu.

Tathmini hii umegawanyika katika sehemu kuu mbili (2);-

(a) Mazingira yanayozunguka nyumba yako.

Hapa unaangalia sera za serikali za mitaa na serikali kuu. Hapa unatakiwa kufahamu mambo ya msingi nitakayokushirikisha hapa chini.

(b) Tathmini ya mapato na matumizi ya nyumba husika.

Unatakiwa kufahamu yafuatayo;-

✓ Jumla ya makadirio ya kodi kwa kila mwaka.

✓ Jumla ya makadirio ya matumizi.

✓ Jumla ya idadi ya miezi ambayo hutakuwa na wapangaji.

✓ Njia bora ya kuuza nyumba unayomiliki na miaka utakayomiliki nyumba hiyo.

Taarifa Za Mazingira Ya Kiwanja/Nyumba Unayotaka Kumiliki.

Malengo na mipango ya mji kwenye ardhi husika. Unatakiwa kufahamu lengo la ofisi za mipango miji. Hii itakusaidia kupata thamani halisi ya kiwanja au nyumba unayotaka kujenga.

Unatakiwa kufahamu jinsi biashara inavyofanyika kwenye mtaa unaotaka kumiliki nyumba. Biashara na uwekezaji wa eneo husika ni moja ya sababu kubwa ya kupata mafanikio makubwa au kushindwa kwenye uwekezaji wako.

Watumie viongozi wa eneo lako (wilaya au mkoa) kufahamu mipango miji ya eneo unalotaka kuwekeza.

Wawekezaji wengi hafanyi mambo ninayoandika hapa. Hii ni moja ya sababu ya kushindwa kutengeneza pesa kwenye ardhi na majengo.

Unapofahamu picha halisi ya mji unaowekeza baada ya miaka kumi inakuwa ni sababu ya kukufanya uendelee kutengeneza pesa kwa miaka mingi.

Andika Vigezo Vyako Vya Kiuwekezaji Kabla Ya Kwenda Eneo La Tathmini.

Vigezo vya uwekezaji ni yale mambo ambayo yanakuongoza kuchagua, kumiliki na kusimamia nyumba zenye kiasi kikubwa cha kipato endelevu cha kila mwezi. Vigezo vyako vinaweza kugawanyika katika sehemu zifuatazo;-

Moja.

Aina ya ardhi na majengo unayotaka kuwekeza. Ardhi ghafi, majengo ya biashara, majengo ya makazi, majengo ya ofisi, majengo ya viwanda na kadhalika.

Pili.

Mkoa/wilaya unayotaka kuwekeza, kiasi cha kipato endelevu, miaka utakayomiliki nyumba yako, kiwango unachotarajia cha kupanda thamani, na kiasi cha kipato endelevu. Pia, nchi au bara inaweza kuingia kwenye orodha endapo unawekeza kimataifa.

Huu Mfano Halisi Wa Vigezo Vya Kiuwekezaji.

ENEO; Wilaya ya Bahi, Jijini Dodoma.

Aina ya jengo; Nyumba ya familia nyingi.

Kipato endelevu; 12% (au zaidi) kila mwaka kama kipato halisi (net rental income).

Miaka ya kumiliki; miaka 20 ijayo.

Faida wakati wa kununua; Zaidi ya 15% ya bei iliyopo sokoni ya kununulia ardhi au nyumba.

Kiwango cha kupanda thamani; angalau 7% kila mwaka kwa nyumba au zaidi ya 10% kwa viwanja na majengo kila mwaka.

Mtaji fedha wangu; kuanzia tshs. 2,000,000 hadi tshs.5,000,000.

Kiasi cha juu cha mtaji; Tshs.9,000,000.

Haya ni sehemu ya maarifa yanayoweza kukusaidia kujenga/kutunza utajiri kupitia viwanja na nyumba.

Jiunge na mafunzo ya siku 10 (05 -15 januari 2023) ili uweze kufahamu mengi kuhusu uwekezaji huu. Pia, utaendelea kushirikiana na mimi kwenye safari yako ya kutunza au kujenga utajiri kupitia viwanja na nyumba.

Ombi langu; Naomba Uwe Rafiki Kwa Kujiunga Na Kundi Hili.

Mafunzo yatafanyika kwenye kundi la whatsapp liitwalo TANZANIA REAL ESTATE TEAM (TRT). Mafunzo ni bure kabisa. Ofa hii ni kwa ajili ya marafiki zangu ambao watakubali kuungana na familia ya TRT.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi wa majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom