Kwa Takribani miaka 40 Sasa Nimegundua Ukiwa na MTAJI au UZOEFU, Utaishi Uchumi wakati au wa juu

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
Habari zenu woote
Naamini niko jukwa sahihi kushare uzoefu wangu kwenye biashara.
Sasa leo napenda kushare nanyi uzoefu wangu kwa kuangalia circle yangu, nimegundua ngazi 3 kiuchumi:

1. Uchumi wa chini:
Kundi bila Mtaji Wala Uzoefu. Hawa wanastrugle kila iitwayo leo kufanya kazi apate pesa ya kula siku ile. Ikitokea kapata zaidi, atajitahidi juu chini aimalize ili kesho akatafute nyingine. Mara nyingi hawajifunzi kwa wengine, na cheo maarufu wanachopenda kujipa hujiita Maskini jeuri. Yaani mfano ana smartphone na bando, kwenye group atajibizana na yoyote na hachukui mawazo mapya, huamini watu wote sawa tu kimaarifa. Uzuri wao hawa watu ni hard worker mnoo, ila kwenye u-smartworking ndo usiwahesabie.

2. Uchumi wa Kati
Kundi la uzoefu na maarifa. Hawa silaha yao kubwa ilowavusha uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati ni kupenda kujifunza vitu vipya na kuvifanyia kazi. Japo wengi hutoka familia maskini, lakini hutumia muda wao kujielekeza mambo ya msingi. Nakumbuka nilipoanza kujifunza kozi za Kiarabu, kichina na kifaransa, baadhi ya wana-circle wangu waliona napoteza muda na fedha. Lakini miaka 5 baadaye hivi sasa nishawaongoza wafanyabiashara wakubwa kwenda Dubai na China kama mkalimani wao.

Kundi hili unaweza kuwa hawamiliki asset, ila wanamiliki maarifa wanayo -yaupdate kila mwaka ili yaweze kuendana na mazingira.

Kundi hili hutumia kila fursa wapatayo kukikuza kile kidogo. Miaka 5 nyuma nilianza mradi wa kutengeneza vipodozi asilia , kwa level ya kuanzia tu ,hasa ushauri. Lakini kila nchi niloenda nilitafuta wazalisha vipodozi asilia na kujifunza kwao, hatimaye nikagundua tiba za magonjwa ya ngozi karibu yote na kuanza kuandaa bidhaa zake kutatua shida hizo.

Kingine zamani nilikuwa naogopa partnership nikijua anakuja kukuibia mawazo yako na ujuzi, Lakini baada ya kujifunza biashara kwa takwimu nikagundua soko la watanzania milioni 60 halijai (Unsaturated Market) hivyo nikajitengenezea sera ya kukaribisha partner ambaye mikataba yetu ya muda mfupi kati ya miezi 3 hadi 6 awe kasharudisha mtaji wake na faida ,pia kashajifunza uzalishaji na masoko. Kwanini mmizei 3 hadi 6? Kwa sababu kila miezi 3 tunabuni au kuboresha bidhaa, hivyo anakuwa na nafasi ya kuamua kuingia awamu ya pili au kutoendelea.

Faida ya kuwa kuwa uchumi wa kati ni kuwa japo haumiliki asset kama nyumba au gari au unamiliki asset za bei nafuu, lakini faida kubwa unakuwa unakutana kiurahisi na watu wa uchumi wa juu na kuweza kujifunza mbinu mpya. Changamoto la kundi hili , linahitaji hukubali kupitwa na starehe kama mechi za mipira, kuangalia TV na movie kupitiliza, kuijali sana afya yako kwa mazoezi na mlo kamili ili kuhimili ufanyaji kazi hadi usiku mwingi plus weekend.

Uchumi wa juu:
Kundi la wenye mtaji.Hawa ni aidha walianzia chini , wakafight hadi kati na hatimaye wakafika juu. Pia wapo walioanzia kati wakaja juu mfano karithi n.k.

Uimara wa kundi hili wana mtaji ambao hurahisisha mchakato wa kukuza utajiri wao. Kipimo cha utajiri wao ni pamoja na kumiliki asset za bei ghari na uhuru wa kusafiri kwenda kona wapendayo ya dunia ndani ya muda wapendao. Changamoto ya kundi hili , wanakua hawana maarifa ya kutosha kama kuhusu lugha za mataifa mengine au ttamaduni zao hivyo wanahitaji wasaidizi ambao hutoka kundi la kati.

Jitahidi ukishindwa kuwa daraja la juu, uwe daraja la kati. Na mtaji wa kuanzia ni hiyo akili timamu ulojaaliwa pamoja na masaa 24 unayopewa kila siku


Dr.Mussa Zaganza,
0713 039 875
Kibaha Maili moja,Pwani
 
mada muruwa kama hizi hauoni wachangiaji. ila wamejaa tele MMU kuchangia upupu wa hapa na pale wakitoka uko mbio wanalalama ajira hakuna.
 
Back
Top Bottom