Kwanini konyagi huwa inalazwa?

Kwanini konyagi huwa inalazwa?

Ile sio mbwembwe ile ni physics Mkuu, Henry's law,the solubility of a gas in a liquid is proportional to the partial pressure of that gas above the liquid.

Ile paaah!, inafanya inakuwa rahisi zaidi kukifungua kifuniko kwa zenye mifuniko ile. Kumbuka.sio chupa zote zinafanana viuniko ndio maana bado sio zote zinapigwa chini.

Hiyo ni worldwide sio bongo tu.
Ni kweli
Alaf Bro Yoda najua wewe sio mnywaji..
 
Kulazwa kwa Konyagi mezani ni tamaduni ya mtaani iliyojaa maana ya kiheshima, ukali wa kinywaji, au ubabe wa wanywaji.

Ni style tu ya kuonyesha upekee kwamba msije mkamuangusha huyu mwamba ngoja tumlaze - Ni street culture, si lazima iwe na maana rasmi.
Umeeongea vema ila kuna kitu hakijagusiwa. Kwanini inapigwa kitakoni kwa Kofi wakati wa kuifungua.

Na nadhani watu wakikuona unakunywa konyagi sijui wanakutafsiri vipi maana unaonekana umekubuhu
 
"Si kila anywapo amelegea, wala si kila mnywaji amepotea; maana kuna wanaokunywa kwa akili kama vile mto upitavyo maji bila mafuriko". - Mstoiki5:3 😅
Ukitaka kujua ulevi ni ugonjwa some AA pombe ni kitu kibaya sana ni vile tu kimehalalishwa. Embu angalia vijana wa Arusha wale wadudu walivyo.

Ile sio bangi sababu bang haileweshi mtu akayumba zile ni pombe zimewafanya watu wanaongea ujinga na kufanya mambo ya ajabu ajabu tu.
 
Bado hujui matatizo ya pombe
 
Wanaoshabikia pombe ni mby hali ya kiwa ameona kwa nje namshangaa sana. Uliza aliyepitia humo. Ukiongelea ubaya wake na hufafanui ni umbea
 
Sawa.
Kwahiyo kinywaji cha Kulaza tu ni Konyagi , na inakubid kwakuwa sio maamuzi yako binafsi?.

Hard Liquors nying hulazwa kwasababu ya Muundo wa chupa, hakuna cha ubabe , utamaduni wala ukali wa Kinywaji.
Usiniquote vibaya Sijasema kwamba kinywaji cha kulaza ni konyagi tu, Nimejibu hoja iliyoulizwa, nisingeweza kuzungumzia vinywaji vingine ambavyo havijaulizwa!!

Uko sahihi, Hard liquors mara nyingi huja katika muundo wa chupa ndefu nyembamba hivyo hulazimu kuilaza au kuiweka kwenye dish kisha kusave kidogo kidogo kwenye glass.

Konyagi kulazwa si kwa sababu haiwezi kusimama — inasimama vizuri sana. Hii ni lugha ya mtaa na tafsiri ya utamaduni wa unywaji, si hitaji la kimuundo.

Watu wanailaza konyagi hata sehemu zenye utulivu, wengine hata wakiwa pekee yao home 😅
 
Kwasababu ni pombe ya kimaskini hivyo wengi huwa wanailaza kama kuificha isionekane ili wasionekane ni watu wenye hadhi ya chini.
 
Umeeongea vema ila kuna kitu hakijagusiwa. Kwanini inapigwa kitakoni kwa Kofi wakati wa kuifungua.

Na nadhani watu wakikuona unakunywa konyagi sijui wanakutafsiri vipi maana unaonekana umekubuhu
Huaminika kusaidia ifunguke kirahisi [Sijajua kitaalamu imekaaje].

Saa nyingine ni kama Ishara ya kusema “Tunanza kazi”.

Lakini pia ni kama vile Style fulani ya mkongwe/Mzoefu.

Kuonyesha wewe si mgeni kwenye meza. 😂
 
Ukitaka kujua ulevi ni ugonjwa some AA pombe ni kitu kibaya sana ni vile tu kimehalalishwa. Embu angalia vijana wa Arusha wale wadudu walivyo.

Ile sio bangi sababu bang haileweshi mtu akayumba zile ni pombe zimewafanya watu wanaongea ujinga na kufanya mambo ya ajabu ajabu tu.
Ni kweli ulevi ni ugonjwa, lakini si kila unywaji ni ulevi, Kuna tofauti kati ya mnywaji wa kawaida na mlevi sugu.

Pombe ina madhara ikizidi, lakini sasa kwanini ipo?
Mbona imehalalishwa?
Mbona hutumika kihalali katika matukio ya kijamii kama Sherehe na vikao?

Si kila kinachotumika vibaya ni kibaya kiasili ila anayetumia vibaya ndiye mbaya mwenyewe.

Wadudu wa Arusha wame develop tabia mbovu.
Tabia hutokana na mazingira na watu waliokuzunguka.

Bangi na pombe zote huathiri fahamu. Bangi haijidhihirishi kwa kuonekana wazi kama pombe ila zote ni addiction zatakiwa kuepukwa.

Waitre niletee nyingine 😂
 
Ni physics tu imetumika hapo,, pembeni ni kupana,kitako ni chembamba,hivyo ni vyema lile bapa sehemu pana ilazwe,ili ipate tulia,hata meza ikitingishwa isiwe rahisi kudondoka.
 
Salaam alyekum,

wakati sosho media zimejaa taarifa zisizo na tija sijui gwaji boy, sijui gen z binafsi naona ni kama kelele za chura ambazo hazimzuiii kuendelea na kazi huo ulikuwa utangulizi lakini swali langu ni kwanini konyagi huwa inalazwa? …..ukizingia kwenye comment principle yangu ni ile ile “ntakutafuta ntakupata na nitakufurahisha”
hujui kwa nn inaitwaga 'Kasichana' au 'kisichana'?
 
Ni kweli ulevi ni ugonjwa, lakini si kila unywaji ni ulevi, Kuna tofauti kati ya mnywaji wa kawaida na mlevi sugu.

Pombe ina madhara ikizidi, lakini sasa kwanini ipo? mbona imehalalishwa? Mbona hutumika kihalali katika matukio ya kijamii kama Sherehe na vikao?

Si kila kinachotumika vibaya ni kibaya kiasili — anayetumia vibaya ndiye mbaya mwenyewe.

Wadudu wa Arusha wame develop tabia mbovu, Tabia hutokana na mazingira na watu waliokuzunguka na si kileo maana Ulevi ni tabia pia.

Bangi na pombe zote huathiri fahamu. Bangi haijidhihirishi kwa kuonekana wazi kama pombe — zote ni addiction zatakiwa kuepukwa.

Waitre niletee nyingine 😇😅
Kiasi nakubaliana na wewe kiongozi, ila kwa wadudu niamini mimi ule ni ulevi unawawehusha vijana. Fikiria hii kombo (mirungi+visungura+bangi+ugoro/pariki) alafu ni mtu anajidunga muda wote.

Kuna siku wamepata ajali kama pikipiki 4 kwa mpigo vijana 8 wakakata moto palepale hao wawili ukiwaona ni swala la muda tu alafu wanayoongea unaona.hawa washapagawa.
 
Hatari sana mkuu, Unafikiri ni hatua ipi inatakuwa ichukuliwe?
 
Back
Top Bottom