Membe akalia 200bn za Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe akalia 200bn za Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Aug 5, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Written by CCM-ASP Zanzibar // 05/08/2012 // ZenjiLikiz // 12 Comments

  [​IMG]
  Kumbe zipo sababu nyingi kuwasikia wajumbe wetu wa BLW wanasema kwa ukali, ghazab na jazba wanapozungumzia haki ya Zanzibar ndani ya Muungano; dhulma inayofanyiwa Zanzibar ndani ya Muungano – na kelele zinapokuwa nyingi, zinaundwa kamati. Mpaka sasa zimeundwa kamati 200 kutatua kero (KARO) za Muungano; karo hazijasafika.
  Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na "Ushirikiano wa Kimataifa" amekalia pesa za Zanzibar zipatazo 200bn/= zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuipa Zanzibar kuendeleza/kufufua specifically zile EPZ, maeneo huru ya kiuchumi Zanzibar.
  Waliotoa pesa hizi wakiwemo UAE/Rasil Khemah – ambao viongozi wetu wote watatu (Shein, Seif-1 na Seif-2) wamekuwa kiguu na njia kutafuta misaada. Imepatikana Membe – laatul laah amezuia, just kutia saini tu ili pesa ziwe released.
  Kipengelea kimoja kinachomfanya Membe ndiye atiwe saini/pesa za misaada, mikopo, zawadi n.k zinapoingia katika foreign currency au misaada kama hiyo – Zanzibar hairuhusiwi kusaini, kwa sababu ‘si nchi' inatakaiwa TZ ndio imwage wino.
  Huu ni mwezi wa pili, Membe amekalia barua yetu na pesa zetu, halali yetu. Baadaye wanakuja Zanzibar eti kujiliza baada ya meli kuzama.
  Hiyo ndio TZ, na huo ndio Muungano wetu uliodumu miaka 48 kwa Bara kuidhulumu Zanzibar.
  * Plus, jana tu Abubakar alikuwa anasema ndani ya BLW kuwa hao hao akina Membe wameinyima Zanzibar fursa ya kuhudhuria vikao muhimu vya kimataifa kwa kuwanyima wajumbe wake visa, just kwa sababu wao watanganyika hawakwenda au hawakutakiwa kuwemo.
  Ushauri wangu: MAMBO YA NCHI Z ANJE IONDOSHWE KABISA KATIKA LIST YA MUUNGANO (GET ME RIGHT PLEASE, SIO SUALA LA KUGAWANA MABALOZI, LA HASHA). ONDOA FOREIGN AFFAIRS KATIKA LIST HIYO FOR GOOD.
  Mbaya zaiid katika sakata hili la Membe kuzuia pesa zetu, naibu wake anaitwa Mahadhi Juma Maalim – mzanzibari wa Muyuni/na Mungoni (huyu ni kambi ya NO vote katika referendum, na ndiye group la akina Samia, Haroun, Shamsi, Perera Ame Silima – wanachochea watu wa kusini wasema NO serikali tatu au muungano wa mkataba). Mahadhi, Kazi ya uzinzi haifai na kutafuta wanawake kuowa. Kuwa na akili wewe, nchi yako inazamishwa.
  Hizi habari za Membe kukalia 200bn/= zimeigusa BLW na cabinet ya Zanzibar – ni habari zilizoleta ghazab sana, maana hili si la mwaka 1968 au 1980s au 1970s – it's only two months ago or less (jana na leo).
  Naomba wana-mzalendo tujadili mada hii kwa kina na tuone impact yake. La kama mtaona abdisalum porojo – sawa. Maana huko nyuma nilisema mengi – mkaona ahhhh….huyu haipendi CCM + CUF na haitakai GNU tu. Leo akina Moyo, Jussa, Hamza, Mansour – wanasema hayo hayo niliyosema mimi long time ago.
  Mfano niliwahi kusema katika ukumbi huu kuwa ‘ushirikiano wa kimataifa' limeingizwa baada ya zahma ya Zanzibar kutaka kujiunga na OIC; awali ilikuwa haimo. Mzalendo walipinga baadhi yao – juzi Moyo amelisema, na ameonekana ‘champion/hero'.
  Hii ya membe sijui kama haitopingwa, lakini ulizeni wana-cabinet wa SMZ , muulizeni Mahadhi na huyo bosi wake Membe – kweli si kweli?
  Kidumu Chama Cha Mapinduzi – Udumu Muungano wa Serikali Mbili kuelekea MOJA TUUUU….!


  Related Posts

  TAIFA SATAR, KUWA BWAGA WAPINZANI,JANA 5-3


  Wikileak:Kikwete achukua rushwa, Sakata la Kempiski Zanzibar


  [​IMG]
  Zenjileak:Biwot company to get Zanzibar road tender?
  Doc:Mkataba wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar


  [​IMG]
  GNU na Mafisadi Vyeo Vya Juu  12 Comments on "TETEZI:MEMBE AKALIA 200BN/= ZA ZANZIBAR"
  1. mas-albimany 05/08/2012 kwa 8:54 mu · Ingia kujibu
   aaa hii kali ya mwaka, nampongeza sana alieandika makala hii yenye ufundi na ustadi wa hali ya juu, hawa viongozi wetu wa mrengo wa shoto hawajaliona hili? Na jee wana ccm maslahi hawayajui haya.


  2. zamko 05/08/2012 kwa 9:17 mu · Ingia kujibu
   @ CCM-ASP
   Kwani zile visa hazijatolewa kwa wale Wazanzibari Officials waliotakiwa kuhudhuria Mikutano ya Miradi ya Maendeleo?… Basi hii hakua dhulma tu nikumyima mtu haki yake ya free movement, kwani kuwanyima Wazanzibari Visa siojambo la busara. Mkutano ni wa Wazanzibari kwasababu wao ndio waliokua kiguu na njia kutafuta Misaada ya Zanzibar.
   Na hapa Tanganyika au Tanzania haitakiwi ingilie kati kwani hayo ni mambo ya Zanzibar na sio ya Muungano. Maskini Mh.Omar Yusuf, Maalim Seif Sharif, Hamadi Massoud na DR. Shein mbio zao zote zile zimeishia ukingoni.. Kwasababu Wafalme Weusi wameona Wazanzibari Officials wakihudhuria mikutano hii Zanzibar itafunguka .
   Kwani Miradi yote ile yakuanzisha Shirika letu la ndege na kua na ndege zetu wenyewe imo katika Mipango hii ya Vitega uchumi. Upanuaji wa Bandari, Airport ya Unguja na Pemba na Ujenzi wa Hospitali kubwa Univercity na maabara za utafiti pia zimo katika safari hizi.
   Kama alivyosema muandishi kwamba pesa zimekubaliwa lakini wakizitoa nilazima ziingie kwenye Tanganyika/ Tanzania foregn currency. Halafu ati watu hawa wanawadanganya akina Waziri Ramadhani Abdallah Shaaban kwamba Ombi la Eneo la Mafuta nikuwaombea Zanzibar.
   Hivyo kama wanatupenda kweli kwanini wasiruhusu hii misaada ambayo imetafutwa na Wazanzibari wenyewe? Pesa sio yao ni just kutia saini au kutoa viza kwa Viongozi wetu kwenda ku-demonstrate utumiaji wa fedha hiyo na faida zake. Lakini pia wamekataa kutoa visa kwasababu Tanganyika haimo.
   Huu ndio Muungano na huyu ndie Mfalme wetu JETA,kama Serikali ya Tanganyika ingeweza kuziba riski na kutoa basi nafikiri Wazanzibari tungekua hatupo tena katika visiwa hivi.
   Hawa ndio (ati) ndugu zetu, hawa ati ndio wanatupenda… Tuyajue haya natupiganie Nchi yetu..


  3. zamko 05/08/2012 kwa 9:49 mu · Ingia kujibu wazalendo Wazanzibari wa ndani na nje..
   Baada yakuwasiliana na jaamaa wanaojua sakata hili linavyoendelea nikwamba.. Serikali ya Tanganyika(Tanzania) inataka pesa zote ziingizwe kwenye Account ya Foregn Currency kama alivyosema Muandishi. Lakini hizo nchi zilizokusudia kutoa misaada na zawadi ya fedha au ndege kwa Zanzibar wamekataa .
   Kwanini walmekataa kuziingiza fedha hizo ndani ya Tanganyika Tanzania foregn currency kwasababu mikata yote iliosainiwa na Zanzibaris Officialls nikwamba fedha ni za Zanzibar na sio za Muungano na hayo yalikua makubaliano baina ya doners Countries na Zanzibar.
   Hivi juzi tu nasikia Mh. Ali Mohamedi Sheni aliitwa kukubaliana na ST -Membe kwamba serikali yake ikubali fedha hizo ziingizwe humo na watapewa wenyewe. Lakini nasikia Maalim Alikataa kata kata akisaidiwa na cabinet yote ya Mawaziri na MBLW. Sasa hivi fedha hizo hazijaingizwa na Ugomvi wa Mke mwenza unaendelea.
   Watu wanamshutumu DR. Ali Mohamedi Sheni akisaidiwa na akina wahafidhuna (Jidawi, shamuhuna, Seif Ali Iddi, na Waziri wa Nishati watafanikisha Mpango huo) Lakini nasikia Dole gumba ambalo linatoka kwa Private Intelligent wa Kizanzibari wameashatuma ujumbe ktk donners countries.
   Kuna habari hizi za uamini usiamini, nasikia (ati), akina Benad Membe wanafanya hivi makusudu kuikomoa Zanzibar katika kuongezeka kwa eneo la Bahari na Uchimbaji mafuta. Hivyo hata kama wamekwenda New York tayari kuna PI-wakizanzibari wameshatuma docc. nyengine ambazo zinachambua baadhi ya Mam,bo yasio ya Muungano ambayo yameingizwa katika Muungano bila ya concept ya Wazanzibari au MBL… Nasikia hivi jaamma wemekua wanachuana chini kwa chini.
   Maoni:
   Safari nindefu na Jini hili Mapembe (muungano) limeshajua kama Chano cha mara hii ni kikubwa ambacho kitamfanya Mganga alitoe Jini hili kama kutakua na Ushiriano na Muwele (mgonjwa).. Hivyo kuna kama kukomoana baina ya ST na SMZ-SUK… Kwamba nyinyi mumejifanya munaweza kupata misaada kutoka Nje sasa wapi hiyo misaada yenu itaingilia?
   Hivyo tunatakiwa tupige campeni ya habari hizi kule Muyunu (kwenye embe Tamu) na tuwajuvye watu jinsi ya hali ya hatari. Uongo Wazee dawa hata kama kuna watu watakua wanampendelea Mahadhi Juma lakini wanaweza wakatizama na manufaa ya Nchi yao. Kuhusu suala hili tusilizungumzie hapa tu nilazima kuenezwe habari kwa vijana wote kwamba kuna uhaini huu wakuzuia fedha yetu ambayo imetafutwa na viongozi wetu wa SUK kwa ajili ya maendeleo ya Viwanda, kilimo, biashara, Airport n.k lakini zimekaliwa na Benard Membe. Sasa watu wataendelea kuwa invigilant.


  4. Ashakh (Kiongozi) 05/08/2012 kwa 10:14 mu · Ingia kujibu
   uzuri ni kupata muongozo wa nini kifanyike. Tunapokuwa na wito mmoja inakuwa rahisi kwani hapatikani mwengine kuzungumza kitu kisichoeleweka.
   Bw Abdu hebu tupatie mwongozo nini tufanye, kwa pande mbili:
   1) GNU
   2) Hao watanganyika
   Tatizo letu jengine ni huu usiri wa viongozi wetu. Bado wanashindwa kuvikabili vyombo vya habari na kuwajuvya wananchi nini kinaendelea. Hapo tungeweza kwa kiasikikubwa kuwasaidia kwa kutia pressure na kuutangaza ubaya wa Watanganyika kila kona ya dunia.
   Viongozi jitoweni na mutueleze juu ya kadhia hii


  5. Said-Said 05/08/2012 kwa 10:21 mu · Ingia kujibu
   Kila jambo linalokwamisha maendleo ya Zanzibar nyuma yake kuna Muungano, mimi nadhani serikali ya SUK ikizembea mpaka wao hawa viongozi wataambiwa wende waktiwe kwenye hizo account za Tanganyika.
   Msaada anapewa Zanzibar; Tanganyika anakwamisha kwa malengo gani??????Mbona jamani hawa mabwana wanatupeleka kwenye vita mwisho wake tupigane na tuhasiminae wala sio lengo letu.
   WAZO LANGU:
   Serikali ya SUK isiangalie katiba wala nini irudishe Benki kuu yake na mapema ili haya yaishe; ili kuanzia mwakani haya mambo ya misaada na fedha tuyacontrol wenyewe vyenginevyo hakuna liwalo tutabaki kupiga kelele za bure na hawa watanganyika wala wahashughuliki na zogo letu wakishaona pesa huwa hawana akili tena na hasa kama za Zanzibar hutamani tusipewe hata senti.
   Muungano gani huu, ndio mana UAMSHO yupo katika njia ya sawasawa hizi shotcut za mkataba na mengine tutarudi palepale.


  6. abdisalum 05/08/2012 kwa 11:08 mu · Ingia kujibu
   Bwana Ashak – mimi sera yangu iko wazi: Muongozo wangu ni kama ufuatavyo:
   Plan A: BLW wapotishe /wafanye private bill ya kujiondoa ndani ya Muungano kabla ya hata kuundwa katiba mpya/timeline: December 2012. BLW wafanye haraka tujitoe sisi ili kama tutakufa maskini nje ya muungano ni SAWA kuliko kubaki na tamaa ya fisi.
   Plan B:SMZ iorosheshe assets zake zipi zao na zipi za muungano – na zipi mchanganyiko, mfano BoT – hii ni yetu sote, therefore apatikane mtu atupigie hesabu Zanzibar zao ni nganpi na kipi na kipi+ Tanganyika zao ni nini na nini na kipi?
   Plan C: let's make it very clear, kuwa foreign affairs na currency ziwe ni pure Zanzibar 100% zanzibaris. Kuna mifano hai ya jana na leo, mawaziri wa SMZ waliponyimwa visa just kwa sababu wafalme akina Membe (Pembe) hawakupenda sisi tuende huko.
   Plan D: Tuachiwe TUPUMUEEEEEE (wewe ashak bingwa, so hizo ideas pia zitengenezee action plan with time line – I can help you sir) usijali.
   Plan E: Shein aingilie kati privately (yeye na Kikwete) kwa maana kuwa wakati wa Karume mambo yakizidi mno, alikuwa direct anampigia simu JK na kumwambia kuwa ‘tupatieni kiasi kadha ya dola", na JK hakuwa na ujanja wala kusema NO – akitoa tu. Ushauri wangu – Shein ajikaze kidogo, amkabili JK n aamwambie Membe atoe pesa zetu hizo. Mwizi wahed!
   Hii imetokezea katika mifano – mradi wa umeme Pemba-Tanga – Tanganyika wlaitoa pesa kutaka wasitake, na Karume alimpigia simu tu Kikwete, kadhalika na mambo mengine ya pesa.
   Hawa watanganyika bila kuwapiga rungu kali shingoni hawakubali sulhu ya kirahisi – hawa genes zao kama zimechanganyika na damu ya punda au mbuzi kwa ukaidi.
   Plan F: Isome dua kesho, na kafara – tujue moja tunaomba M/Mungu atutakabalie hiyo hiyo kesho – tunataka tuone watu wapaparike kama kuku hadharani inshallaaaahhh.
   Ama kuhusu GNU hapo sijui niseme nini – maana ni bad governance na haijawez aku-prove efficiency yake kama ilivyotarajiwa.
   Kubwa zaidi imejenga himaya ya CCM ndani ya serikali, na ubaguzi wa watu ndani ya serikali – hupati kazi kama sio mtoto wa fulani; hupati kusoma kama sio mtoto wa fulani, uwe unatoka makunduchi au kizimkazi kwao abdulhamid yahya mzee; hupati hata mkopo wa saccos kama sio mwana fulani. Hiyo ndio GNU yetu.
   Perfomance katika public service is at zero point, na arrogance ya mawaziri – look haruna, Shamhuna, Sira Ubwa Mwamboya, ex-hamad massoud, hawa wote ni arrogant na watu jeuri sana, wanaishi katika impunity - bila kujali. Almuradi GNU kwa Zanzibar ni mess!


  7. Bosco 05/08/2012 kwa 11:25 mu · Ingia kujibu Ahsante sana CCM-ASP kumbe weye ndie abdu salum. Unapokuja kwa jina la CCM-ASP unakua na mada nzuri sana kuliko ukija kwa jina la abdu salum.
   Hapa mimi naungana na ashakh kuwambia viongozi wavunje ukimya waweke mambo hadharani tuanike ushenzi wa watanganyika.
   Tunaposema kua watanganyika ni wabaya kwetu wao wanaona tunawasingizia haya sasa yaoneni. Tsh bilion 200 ni burget ya wizara kama 2 hivi za tanganyika na kwa zanzibar hiyo pesa ni kubwa sana ikitumika vizui.


  8. ole 05/08/2012 kwa 11:27 mu · Ingia kujibu
   Namshukuru muandishi kwa kugema habari hizi ila napata wasi wasi kwamba hizi habari ni za kweli au vipi ? Nasema hivi kwa sababu sisi mara nyingi tunakuwa ni redio kifua,tunachoongea wakati mwengine inakuwa ni tetesi tu bila ushahidi.Hivi kweli katika kipindi kama hichi cha mapambano litokee tokeo kama hili lisuzungumzwe likaeleweka kwa wote ? Mimi nahisi kama kweli hili jambo lipo basi kwa nini wawakilishi na wabunge wetu wasilizungumze hili bungeni? Kwa sababu hili ni jambo kubwa tulifanyiieni kazi kwa sote.Halafu pia kwa sasa Uamsho ndie mtetezi wa Wazanzibar mbona kimya tuseme hawalijui hili,wakalitangaza Visiwani.


  9. Mrfroasty (Ufundi) 05/08/2012 kwa 12:05 um · Ingia kujibu
   Sheikh Abdi shukurani kwa kutunyofoloa hayo, lakini nadhani ukweli utabakia pale pale kuwa wengi wa wazalendo na wananchi kwa ujumla hawawezi kuhakikisha ukweli wa habari kama hizi.Sio kwasababu zimetoka kwako au kwa mzalendo yeyote mwengine, bali kwa kukosekana nyaraka au ushahidi wa kuthibitisha hio habari yenyewe.
   Labda kwa mtu kama mie ningeliona copi za barua hizo zilizoganda kwenye desk ya Membe au angalau hao viongozi wetu wangelizungumza hili la kuona misaada inakwama kwa waziri wa mambo ya nje.Kwa bahati mbaya, sijawahi kuwasikia kulalamikia hilo (pengine wana sababu zao binafsi [​IMG] ).
   Mwisho
   Vyovyote iwavyo, nadhani nakubaliana nawe kwa 100% kuwa muungano ni sawa na gonjwa sugu.Tiba pekee ni kujitoa na kusonga mbele na taifa la watu wa Zanzibar kama ilivyokuwa awali.
   Hili la kusonga mbele na taifa huru la Zanzibar, sijaona kama ni suala jepesi kama litavyofikiriwa na wengi ikiwamo na mimi mwenyewe.Kunahitajika ujasiri wa viongozi na wananchi kushikamana kwa ujumla.Tusikubali kutishwa tishwa na propaganda za hapa na pale, kuwa hatuwezi mara usultani utarudi!.Hayo ya usultani kurudi, siyasemi mie nadhani kila habari inayoandikwa na NIPASHE, imekuwa ndio ajenda na propaganda yao kuu.
   Wasalaam,
   mrfroasty


  10. Mrfroasty (Ufundi) 05/08/2012 kwa 12:07 um · Ingia kujibu
   Kwa kuongezea, wanaojaribu kutonesha kuwa nje ya muungano Zanzibar itakuwa na Mapinduzi na vita ya wenyewe kwa wenyewe pia niliwahi kuyasoma kutoka kwenye kinywa kichafu cha Mh.Shamsi Vuai Nahodha.


  11. Ghalib 05/08/2012 kwa 12:31 um · Ingia kujibu
   Dah nakuna utosi,hizi 200bilion ni dola au shilingi !
   Ngoja nitafakari,wakati huo huo nipo kwenye mstari na front line muungano tuuvunje haraka tuondoe kinaga ubaga.
   Wajumbe wa baraza la wakilishi watamke tu muungano hakuna,mwanasheria mkuu amekiri hilo na hajui hata auite vipi huu muungano.
   Cha msingi hapa kufanyike privacy katika hili,watoke wajumbe kimya kimya mpaka UN,hapo ndio agenda itwangwazwe,lakini kama tutaendelea kuchanganua uwanjani,mahafizuna watazua baa.


  12. rasmi 05/08/2012 kwa 12:53 um · Ingia kujibu
   Serikali ya Watanganyika si ya watu wa kuaminika kwetu sisi tu, bali kwa yoyote; hivi sasa wana ugomvi na Malawi pia wanataka kuwaibia lake Nyasa. Habari zimejaa kwenye Jamii forum na kwa kiburi chao eti watawapelekea hata Majeshi ikibidi! Kama wanavyotufanyia sisi wanapoona mambo yanawabadilikia katika kutimiza malengo yao ya hadaa.
   Wamalawi nao wamejibu mapigo kwa kudai lake Nyasa ni lao lote na hawatoi hata inchi moja kuwapa Tanzania (Tanganyika), na wanawatukana vibaya kwa kuwaambia wanamwabudu Mungu wao Nyerere aliewabadilisha akili na kuwa misukule.
   Kumbe hata Wamalawi wanajua kwamba hawa jamaa ni hatari kwa udanganyifu, ufujaji, wizi wa mali za Umma za watu – hata watu wao wenyewe pia wanawaibia! Na wanajua kwamba sisi Wazanzibari tuna matatizo nao kwa tabia zao hizi – angalia jamii forum kwenye hilo sakata linaloendelea. Wanatukanwa kwamba wanaongoza kwa mismanagement/Wizi wa Mali asili zao wenyewe na hawatosheki na walichonacho!
   Kwetu sisi wamegonga ukuta hivi sasa; hapachimbiki wala hakitoki tena kitu hapa. Muungano ni kiini macho cha kuendeleza wizi na hadaa.
   Na wahafidhina watoe vilivyo vyao; vya Wazanzibari hawana haki hizo…
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkuu umeshusha nondo nzito sana hapa wasiwasi wangu hawa Mods wataziondoa naomba unitumie kwenye email yangu
  manyanza@jamiiforums.com
   
 3. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Siujui muungano no comments!
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni nchi, Zanzibar si nchi, ni lini hawa watu watakiri kuwa kujiita tu nchi hakufanyi shehemu mojawapo ya Jamhuri ya Tanzania kutambuliwa kama nchi, sasa je hao wanaotembeza bakuli kutoka Zanzibar wanafanya hivyo kwa niaba ya nchi au kwa niaba ya eneo linaloitwa Zanzibar? huku wataka na kule wataka....yote umekosa! You guys, you cant eat your cake and still have it...hivi hamkujifunza chochote toka ule wakati mlipotolewa mkuku OIC kwa sababu ya kukosa sifa ya nchi?

  Hii hoja ingekuwa na maana kama ingesema tetesi ni Membe akalia 200bn/= za Tanzania na si za Zanzibar...ngojeni kwanza muwe nchi kwani ukweli mchungu ni kuwa Zanzibar si nchi, period.
   
 5. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Natetemeka sana
   
 6. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 7. b

  bdo JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  kaa chini kwanza kama umesimama, ila hata mie natetemeka hivi Membe ndiye anayetoa VISA?
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  It only takes a fool to believe in this asinine and wild allegation. Hivi kama hali ingekuwa hivi na Zanzibar wakawa wana haki na hicho kinachozungumzwa hali ingekuwa shwari hivi? Hakuna hata wakati mmoja ambao misaada imewahi kutolewa kwa jina la zanzibar ikapitia kwa serikali ya muungano. Watu wamejiunga na kukutanishwa na matatizo yao na sasa wanaamua kutaka kusingizia matatizo yao kwa Membe. Ndiyo wale wale wanaotuhumiwa kuwa na kampuni iliyosajili meli za Iran na sasa wanatunga uongo ambao hata mtoto wa chekechekea hawezi kuuamini.

  Sasa wanawashambulia wale ambao ni voice of reason na walioonyesha objectivity kuhusu muungano kwa kuwaita wasaliti. Wakitaka kuondoka waondoke salama badala ya kutafuta visingizio vya kijinga!
   
 9. chairman mao

  chairman mao Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr shein kakaa kimya,maalim seif karidhika,balozi seif kaona sawa.
  Wewe peke yako ndio umeona Mh. Membe tatizo.
  Iko shida hapa
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Membe na watanganyika wote wanaweza kuwa watu wabaya sana na wasio watakia mema Zanzibar. Vipi kuhusu Naibu waziri wa mambo ya nje Mh Mahadhi Maalim, Makamu wa rais Dr Bilali, Shamsi Vuai nao hao ni watanganyika? Kwa nini wanafanya mambo kama watanganyika?
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Si nchi maana hakuna nchi isiyo na vyombo vya dola! hakuna nchi isiyo na kiti UN.

  Hawa watu ni waajabu sana, wamesahau kuwa mishahara ya Rais wa ZNZ hadi mfagiaji inatoka hazina Dar.
  Wamesahau kuwa gharama za wabunge 50 zinatoka hazina.
  Wamesahau kuwa si Ikulu wa maskani wanalipa umeme
  Wameshau kuwa Spika na BWL wote ni wafaidika wa mishahara na mafao ya Tanganyika
  Wamesahau kuwa Gharibu Bilal amepewa Bilioni 32 kwa ajili ya ZNZ
  Wamesahau kuwa hawana bajeti ya jeshi wala polisi
  Wamesahau kuwa viongozi wao wote wastaafu wanalipwa na Tanganyika


  LET ZNZ GO! Hawa watu uwezo wao wa kufikiri unatisha! uchoyo na umimi umewajaa sana!
  Sidhani kuwa wanahitaji ZNZ huru, wanachohitaji ni elimu kumwekea kila mznz huru.
   
 12. J

  JeanPrierre Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii kali, Zanzibar siyo Nchi tena!!!!!!!:israel:, na kelele zenu zote hizo
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  Hela zenyewe mkopo, mnapozitaka mnajua kulipa nyie? Tanesco tu mmeshindwa kulipa.....

  Hebu tanganyika waacheni wazanzibari waende jamani khaaaa
   
 14. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu Membe inaonesha ana nguvu kuliko Rais wa Zanzibar,makamu wote hadi baraza la wawakilishi.
  Na nguvu yake imefanya mje kulalamika hapa badala ya kum face.
  Kazi mnayo.
   
 15. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Duh wapemba bwana. Mnapenda kuota ndoto za mchana. Tangu lini mikataba ya fedha ikasainiwa na waziri wa mambo ya nje? Hapo ndipo ninapotilia shaka ukweli wa porojo hii
   
 16. m

  mkataba Senior Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ni wasaliti tuu kwa Wazanzibari, ndo maana Wazenji hawadili nao, ni maslahi binafsi tuuu wanajulikana huko Zenji.
   
 17. m

  mkataba Senior Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hata wawakilishi wao wanalipwa kutoka Tanganyika
  au ......???
   
 18. siralola

  siralola Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Viongozi wa zanzibar ndani ya muungano hawalioni hili au ndo wakipakea mishahara wanakaa kimya.
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,813
  Likes Received: 36,903
  Trophy Points: 280
  Free zanzibar!

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 20. D

  Don Draper Senior Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli ZNZ walipewa 200 billion?

  na je ni kweli Membe hajatia signature?

  kwani hizi pesa za bilateral zinatakiwa kutiwa sign na Membe au waziri wa Fedha?

  Protocol inasemaje?

  Kama ni za development projects kwa nini serikali ya UAE isiingize direct kwenye miradi ya maendeleo huko ZNZ kama wanavyofanya waChina?
   
Loading...