Kwanini hawa wana pesa sana lakini hawajasoma?

Kwanini hawa wana pesa sana lakini hawajasoma?

Look at the big picture uelewe mambo

Kwa wastani watu waliopata elimu wengi wanamaisha nafuu kuliko waliokosa kabisa.

Hao matajiri wacheche isiwe kigezo kudhani elimu haina umuhimu. Ukidhani hivyo unajidanganya tu
Elimu ni muhimu maradufu, ispokuwa wale ambao wameikosa wasikate tamaa, wapambane mpaka kieleweke.
 
-Wasomi wengi waoga,wao wanaamini Mivyeti na PHD ndio maisha,wanaishia kujenga nyumba na kumiliki gari na milioni 5 bank tu basi.
-Oneni BASHITE ndani ya mda mfupi anajenga ghorofa 5 Mwanza.
-Wengi wanapata pesa kwa ujanja ujanja aka ushanta mfano King Msukuma utajri wake ulitokana na Utapeli wa Madini.
-Top 5 ya matajiri wa bongo utajiri wao umetokana na kuidhulumu serikali na wizi eg Wengi wamedhulumu viwanda vya serikali,Mashamba ya Mkonge,Kuiba Nyara za serikali meno ya tembo,Kupewa tenda za kuprint nyaraka za serikali kiujanja ujanja,Kuyafirisi Ma-Bank na mashirika ya umma.....
Na wewe jaribu kufanya hayo kama hujasahaulika. wenzako wamejituma wewe umebaki na hasira zako!!!
 
Kufanikiwa kwa wapumbavu kutawaangamiza..

Kuwa na hela na kuwa tajiri sio shida. Pale utajiri unapokujia na huna hekima (kuwa mpumbavu) jua wazi hizo hela au huo utajiri utakutawala.. na eventually utayaendea maangamizo.

Akili ya kupata hela sio akili ya kuzi control.. hapo unahitaji hekima ya tofauti kabisa, kutoka kwa Mungu.

Ndio maana matajiri wanashauriwa kwenda shule.. maana kuajiri msomi akusaidie ku control hela haitoshi..

Bakhresa na Dewji walipeleka watoto wao shule na watoto wao ndio wana control pesa zao.. unaona wazi makubwa wanayofanya...

In short elimu ni muhimu sana katika utajiri.. ukiwa na hela huna elimu.. hizo hela zitakupanda kichwani.

Ila wengi huwa hawajiulizi, source ya utajiri wao ni ipi.. hiyo ni mada ya siku nyingine.
Umeandika vizuri mkuu
 
1. Wavuvu. Samaki wana pesa ile mbya. Wengi utajir wamepata ziwani.

2.migodi ya madini. Gold na diamond ni madini yanayoongoza katika soko la dunia ila yanapatkana mikoa waliopo wasukuma hapa tanzania ukitoa kule Arusha

3. Biashara. Wasukuma wanawafatia wachaga kwa kufanya biashara hasa za maduka ya jumla na nafaka.

4. Kilimo. Hasa pamba, mchele na mahind ndyo yamewatajirisha weng wasukuma.
Kuna tajir mmoja msukuma anaexploit wasukuma wenzie. Yeye hununua nafaka kipindi cha mavuno kwa bei ya chini na kutunza kwenye godown zake. Huuza pale bei zinapopanda. Kwa mfano mwaka jana mwezi wa nne alinunua zaidi ya gunia 8000 za mahnd kwa bei chin ya 40000. Sasa anauza gunia kwa 100000. Yani 60% profit.

5. Ufugaji wa ngombe. Wasukuma wanajitahid kufuga ngombe kibiashara. Sio kama wamasai anamiliki ngombe elf 10 ila analia njaa na anaishi kwenye nyumba iliyoezekwa kwa nyasi.

6. Utapeli na ujanjaujanja i.e Bashite.

Ivyo vyote apo juu. Mtu anayejidai amesoma hawezi kufanya. Wenyewe walisoma wakae ofisini kwenye kiti kinachozunguka huku akisubiri mafao ya uzeeni.
Ukienda wilaya ya Misungwi vijijini kuna Wasukuma kibao wanamiliki vitalu vya migodi huko vijijini na kila utakapopita utakuta marundo ya mchanga/udongo ambao huchekecha na wanamitambo midogomidogo huo mchanga hulindwa sana na kuzungushiwa fensi na ulinzi wa uhakika,hela ya huo mchanga ndio inajenga ''Mabugando'' ya Mwanza na ndio hununua hizo VX,ila huko vijijini kuna dhuruma kubwa hasa kutapeliwa kwa wanavijiji na hao vibopa vijana na bado wenyeji ni masikini wanaonufaika ni hawa matajiri wajanja wachache.
 
Waarabu wa Tanzania wengi wao hawasomi kabisa lakini wanaongoza mabasi ya abiria na mali nyingine nyingi
 
Waarabu wa Tanzania wengi wao hawasomi kabisa lakini wanaongoza mabasi ya abiria na mali nyingine nyingi hasa ktk mikoa ya pwani
 
Bro. Ukianza kutafta pesa ukiwa na miaka 11. Ukifikisha miaka 50. Ukamrithisha mwanao anaeanzia kwa miaka 11 na yeye akifikisha miaka 50. 100 years doing business. Lazma na wewe utafikia hapo.

Chakufanya anza mapema.
 
Mwsho wa siku watu wengi waliosoma wana pesa kuliko wengi wasiosoma hata la sio pesa ka ya Dewji ila waliosoma wengi wana unafuu kuliko wasiosoma.....

Matajiri wachache wasiosoma wasiwadanganye kuwa shule haina umuhimu....

Mi nimesoma sina pesa ya kunita tajiri ila sehemu zote nilizofanya kazi wasiosoma wanalipwa mishahara duni sana ......

Tajiri mmoja asiesoma anaajiri wafanyakazi 40....
30 hawajasoma anawalipa laki na nusu kwa mwezi..

10 wamesoma anawalipa milion kwa mwezi....

Sasa hapo bosi mmja kwa waajiriwa 40 afu mnaidharau shule!
 
Kwanini watu hawa wana pesa nyingi sana wakati hata shule hawajaenda pesa hizi wanazitoa wapi?

Kwa mfano mabas yote ya mwanza bukoba ni yao ukitoa machache ya warabu

Mabasi yote ya mwanza mbeya ni yao na hawajaenda hata shule wanatoa wapi pesa hizo

Wanapata wapi hela za kujenga maghorofa na kumiliki mitaa iliyojaa maghorofa mfano mzuri kwa mkoa wa mwanza kuna mzee shinyanga anamiliki mtaa wa uhuru uliojaa maghorofa yake pekee

Wanatoa wapi ujanja wa kumiliki hospitali zao binafisi mfano makoye hospital wakati hata shule hajaenda

Wako wengi sana ngoja nikutajie wachache uweze kunambia wanatoa wapi pesa hizo,
John bina, ncheye, king msukuma, midimu, luhuye, batco, super samy, super shemu, katagi expres, masaba, njiwa pori,ndege sera bila kumusahau bwana mdogo frester naye siku hizi ni hatari ni moto mwingine ule hata kuna yule dogo anayemiliki kumbi za harusi pale sinza kwa remy kalibu na mori ndo hawo hawo kumbi hizo zinaitwa kwalalumpa hao nimekujia wachache tena ambao hawajasoma bado kariako nako wamejaa

Swali wanapataje pesa hizo?
Kuna tofauti kati ya kusoma na utajiri, kwanza wakati wewe unaumiza kichwa kufanya asaiment za chuo mwenzako anaumiza kichwa afanye mradi gani wa kumuingizia pesa. Na kumbuka kuna hakili za darasani na hakili za maisha. Sasa wewe kama umepewa hakili za darasani wewe soma tu na mwenzako aliyepewa akili za maisha mwache afanye uwekezaji wake.
 
mfano we msomi unatumia mda mwingi kuchunguza maisha ya watu kingine nyie wasomi ni waogo sana kwa kujalibu frs mnawaza kuajiriwa mtaendelea kuwadis hawa wasio soma sana
 
Na wewe jaribu kufanya hayo kama hujasahaulika. wenzako wamejituma wewe umebaki na hasira zako!!!
Mkuu Two Wrongs Don't Make it Right...Huo Ndio Ukweli wala Haubadiliki...Matajiri wengi wa Kitanzania Utajiri wao ni wa Kimagumashi sana,Walifanya hizo issue miaka ya giza.

Matajiri wengi wa bongo utajiri wao upo kwenye categories below:-

1.Ngada Hapa Wapo Wengi.
2.Ufisadi(Rushwa,10%,Kugeana Tenda Kindugu,Kampuni Hewa,Wafanyakazi Hewa) Hapa anafall Mafurushi
3.Utapeli...Dhulumati..Janja Janja.....Hapa anafall King Msukuma
4.Wizi----Kuzidisha Sifuri,Kuchoma Docs,Kuchora Rackets hapa anafall Dr. Machache
5.Kuiba Nyara/Mali za serikali hapa Anafall MO na SSB.
6.Ndele,Ngende,Punje hapo wengi wa Nyanda za Juu kusini na Kusini.

Kwa Nchi za wenzetu Utajiri wao upo Straight mfano mtu kama Mmiliki wa FB unaona alipoanza na kuibuka sio hawa watu ambao wamedhulumu mashamba ya katani ya serikali kisha na viwanda vya serikali kisha unasema ni bilionea wakati ni mwizi tu.
 
Mara nyingi wasomi katika kufanya biashara au kilimo hutanguliza hasara kwanza tofauti na wasio wasomi. Ila amini usiamini 98% ya utajiri uliopo kwa baadhi ya watu tunaowaona wamefanikiwa si wa halali.Unaweza kuwa umetokana na biashara haramu kama unga, ( cocaine), rushwa, wizi, magendo na ushirikina kwa kutoa kafara Watoto, au wazazi.
 
Hela ikishikwa na asiyesoma inayeyuka??? Babu na bibi zetu hawakwenda shule fedha walikuwa hawana? Silly question
 
Ukiamua kusoma kweli kweli utaishia kuwa mhadhiri wa vyuo vikuu na maslahi yako kipesa utayapata huko ingawa sio utajiri. Ukiamua kuwa tajiri ukainamia kusaka pesa mapema shule ukaweka pembeni, kama hutatumia pesa unayoipata hovyo ni lazima utakuwa tajiri tu.
 
utajiri woote unaoujua wew unatoka kwa shetani. ndio unaweza ukatajirika kwa bahati yako mwenyew ila, ili utajiri wako uendelee kusimama lazima utakwenda kutafuta kinga kwashetani(waganga) matajiri wanasiri kubwa, Mimi na wew hatujui
 
Back
Top Bottom