Kwanini Dr. Mpango asijiuzulu au kutimuliwa?

Kwanini Dr. Mpango asijiuzulu au kutimuliwa?

Ingeongezwa TAX yoyote Ile ni lazima imguse mwananchi. Hakuna kodi inayoligusa shirika au taasisi.

Tanzania wigo wa kodi si halisia, kutoza kodi kubwa haimaanishi kukusanya kodi nyingi.

Watungaji wa wigo wa ukusanyaji kodi wangeenda kujifunza biashara za Bakhresa, biashara zake ni kubwa sana lakini ndogo ndogo, ndogo ndogo kwa maana zinamgusa kila mtu na kwa bei ambazo ni vigumu kulalamika.

Kodi inatakiwa iwe vivyo hivyo, pana sana lakini ndogo kiasi ambacho mwananchi halalamiki.

Mpango akajifunze mipango ya Bakhresa atashinda.
 
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...

Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....

Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi

Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...

Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi

Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?

Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?

Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....
Mkuu ulitaka Corporate Tax iongezwe toka 30% mpaka Ngap???...Huoni huo mzigo pia ungemshukia final consumer?.Literaly Bank Industry ya Tanzania ina faida kubwa sana kutokana na hakuna Tax nyingi Compared to Kenya or Uganda. Ndo Maana unakuta Tanzania kuna Bank Nyingi sana Compared to any East African Country ihali watu wanaotumia huduma za Kibanki ni ndogo kuliko hata Kenya na Uganda.
 
Hii kitu hata BOT na TRA maelezo yao yalikua yanapishana km mnakumbuka waliochokieleza BOT ndo hiki knachotokea sasa but kwa kpnd kile TRA na serikali walikua wabishi sasa cha kujiuliza ina maana wizara ya fedha walikua hawajui hz gharama ztalipwa na customers au mabenk?
Ilikuwa zuga kwa BONGOLALAZ ili wasishtukie...siunaona hata humu IPO mijitu inayotumia miguu kufikiri..inafurahia ukamhmuaji huo...so..Serikali sikwamba haikujua inachofanya!
 
Kwa mfano wewe unataka kadi mpya ya ATM.
Benki ikakutoza shilingi 1000/-.
Hapo wewe umeshalipa VAT ya kutengeneza hiyo ATM card.

Yaani gharama zote za na kodi zote zilizohusika katika kutengeneza hiyo ATM card zimekuangukia wewe tayari.

Benki haikufanya kazi ya kanisa, wewe ndiye uliyelipa VAT zote zilizohusika. Yaani input VAT zimekuangukia wewe kama mteja wa mwisho.

Sasa, Serikali inataka 18% Katika hiyo fee ya shilingi 1000/- ambayo itakuwa 180/-.

Serikali haitozi VAT kwenye interest rate ambayo ni faida ya benki, na benki katika accounts zao huweka gharama Kama hizi za kureplace ATM cards Kama input costs. Yaani gharama za kuendesha benki.. Hizo gharama actually wewe ndiye ulizoingia. Wao benki hawakuingia hizo gharama.

Concept inakuja kuwa, serikali haikupata "cut" yake (Value Added Tax). Kwa sababu VAT imekuwa carried forward to you, ila kwa kupitia mgongo wa "No VAT on financial services" jamaa walikuwa wanapiga hela ndefu na serikali haipati kitu.

Sasa serikali inataka 18% ya hiyo 1000/-, yaani hela ambayo wewe umeshaitoa kwa kuilipa benki.

Kumbuka kwamba unapojaza fomu, kalamu ya benki, mihuri, wino na karatasi uliyotumia, kampuni Kama mgololo wametozwa VAT kuzitengeneza na wewe umesakiziwa na umeshalipa kwa kupitia fee uliyolipa benki. Sasa benki ndiyo inatakiwa iwakilishe hiyo VAT kwa serikali.

Kama benki haikuchaji fee, basi haitadaiwa kwa sababu wewe hujailipa hiyo kodi, wao ndiyo wameilipa na mgololo ndiyo wataiwakilisha.

Serikali ipo right conceptually, na benki hazina haja ya kuzidisha gharama.
Kiongozi wewe Dr mpango..nini hebu tuambie nini Maana ya Kodi ya VAT....mnapiga maneno humu wakati huku Mtaani tunataabika nahiyo mliyotuletea! Kwanini mnawadharau watanganyika kwa Kiasi hiki...yaani mnawaona hawana uwezo kabisa wakujua Jema na Baya!
 
Yaani haijawahi kutokea
kodi inayopaswa kuchajiwa makampuni inawashukia wananchi
na hakuna mtu wa kuwajibishwa
na kosa linafanyika kwa kutokuwa na uelewa tu wa aina ipi ya kodi wapandishe
Mpaka miaka 10 PhD atawakomesha[emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Naona hii VAT ya 18% sasa imewekwa kila sehemu. Hivi inawezekana ilikuwepo tangu zamani ila utekelezaji wake ulikuwa hafifu? Juzi naenda kurenew comprehensive insurance nakuta kitu kimepanda kutoka laki 8 na ushee mpka Milioni. Kisa? Eti sasa wanakata na 18% ya ile 3% ya valuation ya gari.
 
HA ha ha a ha ha ha ha ha ha ha ww ukisikia TAMKO kaa tu KIMYA usiumize KICHWA vp BEI ya SUKARI ilikuwaje leo tunanunuaje????
 
Cha ajabu zaidi ni kuwa kuna watanzania wanaojiona wana akili timamu wataendelea kusifia na kusema "Wacha atunyooshe"....Hahahahah....Dah...Mi nakasirika mpaka nacheka sana....
Wengi wa namna hii ndo unakuta kila siku wanapiga mizinga au kuomba mikopo.
 
Ingeongezwa TAX yoyote Ile ni lazima imguse mwananchi. Hakuna kodi inayoligusa shirika au taasisi.

Tanzania wigo wa kodi si halisia, kutoza kodi kubwa haimaanishi kukusanya kodi nyingi.

Watungaji wa wigo wa ukusanyaji kodi wangeenda kujifunza biashara za Bakhresa, biashara zake ni kubwa sana lakini ndogo ndogo, ndogo ndogo kwa maana zinamgusa kila mtu na kwa bei ambazo ni vigumu kulalamika.

Kodi inatakiwa iwe vivyo hivyo, pana sana lakini ndogo kiasi ambacho mwananchi halalamiki.

Mpango akajifunze mipango ya Bakhresa atashinda.
Kuna kipindi unakuwaga na michango mizuri sana...Inakuwaje usiwashauri mapema kabla hawajatulea majanga mtaani? Dr..Mpango anaamini katika kukamua Ng'ombe hadi atoke Damu badala ya Maziwa kisha wanaitisha Mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili yakutaja namba za mapato bila kujua kwa kiasi gani watu wanaumia...Hakuna MTU hapendi kulipa Kodi ila lazima iwe na kiasi ukinikamua hadi nikashindwa kuenda Biashara yangu...Utapata wapi Kodi..Nch hii bado tuna safari ndefu sana tatizo wanaongoza kwa kutaka kusifiwa!
 
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...

Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....

Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi

Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...

Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi

Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?

Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?

Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....
Akili mbovu kabisa wewe ulitaka nani alipe kodi kama sio mwananchi? hizi akili za kufikiri wakati umeshikilia ukuta bure kabisa!
 
Kuna kipindi unakuwaga na michango mizuri sana...Inakuwaje usiwashauri mapema kabla hawajatulea majanga mtaani? Dr..Mpango anaamini katika kukamua Ng'ombe hadi atoke Damu badala ya Maziwa kisha wanaitisha Mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili yakutaja namba za mapato bila kujua kwa kiasi gani watu wanaumia...Hakuna MTU hapendi kulipa Kodi ila lazima iwe na kiasi ukinikamua hadi nikashindwa kuenda Biashara yangu...Utapata wapi Kodi..Nch hii bado tuna safari ndefu sana tatizo wanaongoza kwa kutaka kusifiwa!

Nilishauri zamani sana na ndiyo maana Kikwete akaanza kushusha the, kutokea 20% kuja 18% na akaanzisha mpango wa kushusha PAYE kutoka tarakimu mbili kushusha hadi tarakimu moja.

Na bado tutaendeleza kushauri.
 
Huo ndiyo ukweli halisi Mkuu, hakuna la kuongeza.
kijana wewe mwenye akili ulimtukana Lowasa akiwa CCM leo kahamia chadema unamuabudu,bure kabisa! mnapewa bando la intaneti kama malipo ya kutukana watu na ninyi mmeridhika hovyo kabisa.
 
wabunge hawajui vat unategemea nini?
eti benk ndo watakatwa vat?
sasa akikatwa bank hyo itaitwaje vat?
hawa ukawa nao bure kabisa

Mkuu wakati bajeti ya serikali inapitishwa haikupitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania bali ilipitishwa na kikao cha ccm katika ukumbi wa bunge ndio maana unaona maumivu haya kwa wananchi.Usiwalaumu ukawa hawakushiriki kupitisha najisi hii.
 
kijana wewe mwenye akili ulimtukana Lowasa akiwa CCM leo kahamia chadema unamuabudu,bure kabisa! mnapewa bando la intaneti kama malipo ya kutukana watu na ninyi mmeridhika hovyo kabisa.
Hebu changia huu mjadala nani anatakiwa kulipa 18% kwenye miamala ya Fedha
 
Labda 'taasisi' inaona faida ni kubwa kuliko hasara
lakini nna wasiwasi mno na Inflation...
tunaweza kuamka tukajikuta tuko Zimbabwe ingine....
leo hadi 'uzazi wa mpango' unafutwa kimasiharamasihara tu
Hutaki kufyatua wewe eeh??????
 
Back
Top Bottom