Kwanini Dr. Mpango asijiuzulu au kutimuliwa?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,667
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...

Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....

Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi

Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...

Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi

Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?

Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?

Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....
 
Yaani umeniwahi kidogo tu mkuu! Hii mada nilitaka kuishusha baada ya muda mfupi. Kwakweli hawa walioitwa wanyonge wa hali ya chini wanaumia sana.Makapuni ya simu na mabenki hayana makosa yeyote kisheria, viongozi wetu kwa kukosa weledi wametuumiza hivi hivi. Hawa ndio tunaambiwa wajenzi wa Tanzania ya uchumi wa viwanda duh.
 
Yaani haijawahi kutokea
kodi inayopaswa kuchajiwa makampuni inawashukia wananchi
na hakuna mtu wa kuwajibishwa
na kosa linafanyika kwa kutokuwa na uelewa tu wa aina ipi ya kodi wapandishe
 
Si mpenzi wa siasa lakini. nakumbuka aliyasema sana haya mambo ZZK tupampuuzilia mbali na kumwona hajui asemalo. Sasa tumeumbuka. Dr Mpango alituondoa hofu kumbe ni "Funika kombe...." Samahani sana Zito, naliona wazi wazi, lile kombe laooooo
 
Huyu Mpango hata VAT inawezekana haijui ni kodi ya aina gani hasa
 
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...

Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....

Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi

Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...

Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi

Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?

Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?
Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....

Ni bahati mbaya kwa serikali kwamba jambo hili lilichukua mjadala mkubwa katika maeneo mengi; kwenye mainstream media, social media, mitaani; nakadhalika. Ninachokiona hapa ni kwamba serikali huwa inafanya mambo kwa kujua kwamba inaweza kukabiliwa na upinzani wa jambo husika kwa muda tu, halafu mambo yanaendelea kama kawaida. Kwamba serikali inafahamu wananchi walioipa mamlaka hawana shida-lolote ukiwaambia poa tu! Kwa nchi ambazo wananchi "wanajitambua" jambo hili lingeibua "mshikemshike".

Ni kweli mkuu The Boss, mambo ambayo serikali ilielezwa kwamba yanaenda kuwakamua wananchi lakini ikatumia nguvu kubwa kubisha ndio yanatokea-kwenye miamala ya simu na mabenki tumeanza kupigizwa kimyakimya!
 
Sio kwamba hawajui tofauti ya VAT na Corporate Tax ila ulikuwa ni mpango maalumu tu na ndio maana upinzani ulifanyiwa figisu figisu sana Bunge lililopita walijua tu wabunge watahoji....

Bunge liliendeshwa kisanii ili kupitisha mipango ovu!
 
Si yeye tu, Serikali nzima ya Magufuli kwa maneno na matendo yao inadhihirisha wazi ni weupe mno vichwani na inasikitisha eti ndio brains za kuifikisha TZ kwenye uchumi wa kati!!!!!

YETU MACHO!!!

Walitoa matamko kabisa ya kuzipiga mikwara benki zisiongeze kodi
sasa kumbe kodi zimeshaongezwa
na wao wako kiimya kabisa.....aibu sana
 
Cha ajabu zaidi ni kuwa kuna watanzania wanaojiona wana akili timamu wataendelea kusifia na kusema "Wacha atunyooshe"....Hahahahah....Dah...Mi nakasirika mpaka nacheka sana yani akili za watanzania

Na hili ni jambo moja tuliloliona waziwazi impact yake
tujiulize ambayo impact itakuja miaka mingi baadae
kama denil la Taifa
 
Yaani haijawahi kutokea
kodi inayopaswa kuchajiwa makampuni inawashukia wananchi
na hakuna mtu wa kuwajibishwa
na kosa linafanyika kwa kutokuwa na uelewa tu wa aina ipi ya kodi wapandishe
Eeehee nchi yangu! Wachumi waliwatahadharisha mapema lakini wao wakajiita ndio serika. Gharama mpya za miamala ya simu mabango yake mapya yalishatolewa na kufanya kazi.
 
Nchi yetu ni kichwa cha mwendawazimu Mkuu. Hata mwendawazimu akikuita na kukwambia njoo nikunyoe hushtuki unampelekea kichwa chako ili akunyoe huku ukiwa umetulia tuliii. Inasikitisha sana hii hali ya nchi yetu.

Back
Top Bottom