Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 9,285
- 9,048
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...
Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....
Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi
Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...
Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi
Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?
Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?
Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....
Kwa mfano wewe unataka kadi mpya ya ATM.
Benki ikakutoza shilingi 1000/-.
Hapo wewe umeshalipa VAT ya kutengeneza hiyo ATM card.
Yaani gharama zote za na kodi zote zilizohusika katika kutengeneza hiyo ATM card zimekuangukia wewe tayari.
Benki haikufanya kazi ya kanisa, wewe ndiye uliyelipa VAT zote zilizohusika. Yaani input VAT zimekuangukia wewe kama mteja wa mwisho.
Sasa, Serikali inataka 18% Katika hiyo fee ya shilingi 1000/- ambayo itakuwa 180/-.
Serikali haitozi VAT kwenye interest rate ambayo ni faida ya benki, na benki katika accounts zao huweka gharama Kama hizi za kureplace ATM cards Kama input costs. Yaani gharama za kuendesha benki.. Hizo gharama actually wewe ndiye ulizoingia. Wao benki hawakuingia hizo gharama.
Concept inakuja kuwa, serikali haikupata "cut" yake (Value Added Tax). Kwa sababu VAT imekuwa carried forward to you, ila kwa kupitia mgongo wa "No VAT on financial services" jamaa walikuwa wanapiga hela ndefu na serikali haipati kitu.
Sasa serikali inataka 18% ya hiyo 1000/-, yaani hela ambayo wewe umeshaitoa kwa kuilipa benki.
Kumbuka kwamba unapojaza fomu, kalamu ya benki, mihuri, wino na karatasi uliyotumia, kampuni Kama mgololo wametozwa VAT kuzitengeneza na wewe umesakiziwa na umeshalipa kwa kupitia fee uliyolipa benki. Sasa benki ndiyo inatakiwa iwakilishe hiyo VAT kwa serikali.
Kama benki haikuchaji fee, basi haitadaiwa kwa sababu wewe hujailipa hiyo kodi, wao ndiyo wameilipa na mgololo ndiyo wataiwakilisha.
Serikali ipo right conceptually, na benki hazina haja ya kuzidisha gharama.