Kwanini Dr. Mpango asijiuzulu au kutimuliwa?

Kwanini Dr. Mpango asijiuzulu au kutimuliwa?

Tatizo ni kwamba waandaaji wa huu muswada WALISAHAU kwamba banks zote na kampuni za simu nyingi zinaendeshwa na sekta binafsi.Wao waliilenga ile service charge kana kwamba wanaipanga wao na haitabadilika na ndiomaana walikuwa wanacalculate kabisa na kodi yenyewe itakayolipwa na banks.Mfumo huu usingeleta madhara kama ungelenga tozo za Ewura,Tcra na Sumatra kwa sababu upangaji wake uwahusisha WADAU wote so Dr Mpango alikuwa sahihi because kodi hii ililenga TOZO ambayo TAYARI IMEPOKELEWA na bank na kwa maana hiyo bank anakuwa last consumer kwa mujibu wa VAT Act
Hakuna kitu kama hicho hapo, mnalazimisha mambo tu, VAT ni properly kwa end consumers, sasa bank hawezi hata siku moja wakawa end consumers, ni nadharia zisizokuwa na uelekeo
 
Mada nzuri, lakini imejadiliwa kindezi sana. Ni kama vile watu wapo kijiweni wanakunywa kahawa, nilidhani kwa mada kama hizi watu watajadili kwa facts, figures lakini ni porojo za mkahawani tu.
Uchofanya wewe mwenyewe hapo ni undezi mtupu at least ungekuja na hizo points to differentiate lakini yale yale (wabongo bhana )
 
Hakuna kitu kama hicho hapo, mnalazimisha mambo tu, VAT ni properly kwa end consumers, sasa bank hawezi hata siku moja wakawa end consumers, ni nadharia zisizokuwa na uelekeo
Labda unisaidie kidogo, unapotumia huduma ya UMOJA ATM kati ya Wewe na Bank nani anakuwa last consumer as far as VAT act is concerned halafu tutaendelea
 
Kinachofanyika ndicho kilichopaswa kufanyika dk anajua maana ya vat na alijua nini anafanya kwa kusaidiana na hayo makampuni
Kifupi wanakula wote na makato yamekuwa ya hovyo hata hujui unashangaa hela inapungua
Naamini kilichowapa ujasiri ni uelewa mdogo kabisa kama punje wa wananchi kuhusu haya mambo na ndio bado unawapa ujasiri
Binafsi nilijaribu kumuelewesha Dada mmoja hatari ya hilo jambo akafanya muamala akakatwa akaniambia wala sio mbaya maana kaongezeko kenyewe mbona kadogo nikaona basi nikae kimya tu mpaka "usiku utakapokwisha"
 
Kinachofanyika ndicho kilichopaswa kufanyika dk anajua maana ya vat na alijua nini anafanya kwa kusaidiana na hayo makampuni
Kifupi wanakula wote na makato yamekuwa ya hovyo hata hujui unashangaa hela inapungua
Naamini kilichowapa ujasiri ni uelewa mdogo kabisa kama punje wa wananchi kuhusu haya mambo na ndio bado unawapa ujasiri
Binafsi nilijaribu kumuelewesha Dada mmoja hatari ya hilo jambo akafanya muamala akakatwa akaniambia wala sio mbaya maana kaongezeko kenyewe mbona kadogo nikaona basi nikae kimya tu mpaka "usiku utakapokwisha"
 
Wananchi weng Tanzania hawajijui,maadam wengi hawalalamiki huku wakihofia ubabe wa mkuu wa kaya,serikali nayo imekaa kimya,uko wapi unafuu wa maisha kwa maskin ktk awamu hii ya tano?Yuko wapi aliyejipiga kifua na kupiga push up huku akitudanganya yuko katka kuwasaidia maskin!
 
Aliyekwambia mimi namuabudu Lowassa nani!?
Acha kukurupuka na kuandika uzushi. Usiandike kitu ambacho huwezi kutoa uthibitisho hata chembe.

kijana wewe mwenye akili ulimtukana Lowasa akiwa CCM leo kahamia chadema unamuabudu,bure kabisa! mnapewa bando la intaneti kama malipo ya kutukana watu na ninyi mmeridhika hovyo kabisa.
 
Mimi as last consumer
Ok, kwa mfano wewe ni mteja wa Azania au Akiba bank umefanya drawings kupitia Umoja ATM ukalipa Service charge kwa bank yako na halafu BANK nayo ikalipa service charge kwa Kampuni ya UMOJA kwa transaction hiyohiyo moja,Je bado wewe utakuwa last consumer, kama ndiyo swali ni kwanini uwe wewe na siyo Bank halafu tutaendelea
 
Mada nzuri, lakini imejadiliwa kindezi sana. Ni kama vile watu wapo kijiweni wanakunywa kahawa, nilidhani kwa mada kama hizi watu watajadili kwa facts, figures lakini ni porojo za mkahawani tu.
Hahah leta facts basi ili tuuone utofauti wako mkuu
 
Ok, kwa mfano wewe ni mteja wa Azania au Akiba bank umefanya drawings kupitia Umoja ATM ukalipa Service charge kwa bank yako na halafu BANK nayo ikalipa service charge kwa Kampuni ya UMOJA kwa transaction hiyohiyo moja,Je bado wewe utakuwa last consumer, kama ndiyo swali ni kwanini uwe wewe na siyo Bank halafu tutaendelea
Ndiyo ni mimi na si bank, kwa kuwa kiuhalisia mimi ndiyo mtumia wa mwisho wa huduma hiyo ya miamala, bank ni facilitator tu ili huduma inifikie na VAT itachajiwa kwangu na si bank.
 
Kila mtu anaona ukweli wa kilichotokea baada ya serikali kuweka VAT kwa mabenki na makampuni ya simu kwenye huduma za pesa..kutoa na kuweka na kutuma...nini kimetokea...

Hatimae gharama hizo zimemshukia mwananchi wa kawaida...tofauti na lengo la serikali
mwanzo walifikiri watazi charge taasisi hizo za fedha.....

Inawezekana aliobuni kodi hii hakujua hata maana ya VAT....na wala hakujua hii itamshukia mwananchi

Kama alitaka kodi kwa mabenki walipaswa kuongeza 'corporate tax' na sio VAT...

Sasa kama Dr Mpango ambae ndo in charge wa masuala yote ya fedha,uchumi na kodi Tanzania
hajui tofauti ya 'corporate Tax' na VAT na alikuwa hajui hii kodi itamshukia mwananchi

Hivi kwa nini asijiuzulu? why Magufuli hamtiimui?

Sasa kama hili tu hakuwa na uelewa nalo wa kutosha hadi kuleta confusion iliyotokea
na badala yake wananchi ndo 'waathirika wakubwa' why tumuamini 'atatufaa'?

Hii kodi ni kelelezo kidogo tu ya 'wananchi' watakavyoumia kwa maamuzi yenye kuonesha
'uelewa mdogo' wa mambo wa viongozi....
..wewe mbona hijajiuzuru?
 
Mimi huwa siamini kuwa nchi hii itafikia uchumi wa kati kama CCM itaendelea kuwa madarakani. Kama Albert Einstein alivyowahi kusema "Problems cannot be solved by the same persons who created the problems". Matatizo ya nchi hii yameletwa na CCM tangu enzi hizo ikiitwa TANU! Watu hawa wa CCM wamekuwepo madarakani tangu uhuru, how do you expect kuwa wataweza kutatua matatizo yaliyowashinda for more than 50 years now?

Matatizo ya nchi hii ni ya kimfumo. Namna recruitment inavyofanyika (refer uteuzi wa nafasi mbalimbali uliofanywa na Rais Magufuli hivi karibuni including wakurugenzi wa Halmashuri) haufanyiki kwa weledi badala yake inaingizwa siasa ya kuchagua makada wa chama into a very sensitive position kama hiyo ambayo to me ndiyo muhimili wa kusimamia ukuaji wa uchumi katika local level. Katika nafasi kama hiyo unahitaji kuajiri watalaamu wenye weledi wa hali ya juu na wanaoweza kubuni na kusimamia fursa zilizopo katika ngazi ya halmashauri badala ya kutegemea subsidies from central governments. Kwa list ya wakurugenzi walioteuliwa na Mhe. Raisi hivi karibuni very few wanasifa hizo.

Ukiweza kuwa na wataalamu wenye sifa katika local level (waliopatikana kihalali - in a competitive basis) watakaoweza kuzibadili Halmashuri kuwa autonomous with viable and sustainable income sources, TRA kazi yao ya kubuni vyanzo mbadala vya mapato itakuwa simple na hawatakuwa wanakurupuka kutafuta vyanzo mbadala vya mapato kwa sababu watakuwa wanafanya kazi yao professionally including kuconduct studies and research na kuwahusisha wadau katika vyanzo vipya vya mapato. Kwa sababu ya kukosa weledi hivi sasa TRA inafanya kazi ya kubuni vyanzo vya mapato bila hata ya kuwa na taarifa sahihi zilizofanyiwa utafiti wa kutosha na ndiyo maana hata waliingiza VAT kwenye biashara ya utalii kwa kigezo eti Kenya inacharge kodi kama hiyo, Seriously? Mimi namwonea huruma sana mkurugenzi wa TRA coz kama nchi inaendeshwa kwa kufuata weledi jukumu la TRA ngekuwa kubuni vyanzo vikubwa vya mapato ambavyo vingekutumika kwenye mipango mikubwa ya uwekezaji ikiwemo kutekeleza hilo wazo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Sasa badala yake wamebebeshwa jukumu la kukusanya mapato ya mpaka OC za underperforming local government authority. Inanchekesha ukienda kwenye baadhi ya halmashauri kuna baadhi ya watalaamu kwa mwaka hawajawahi kutembelea clients wao at village level kwa sababu hakuna fedha ya OC iliyopokelewa toka serikali kuu. Very shame!

Unafortunately sasa na Mkuu wetu wa nchi ameamua kuishi katika kisiwa hataki ushauri wala kukoselewa eti akiamini anawatendaji wachapakazi kumbe timu yake na hasa at regional and local level amezungukwa na vilaza ambao nao wanapayuka tu ili kumlizisha yeye while in actual fact hakuna ubunifu wowote wa kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi na kipato cha mwananchi mmoja mmoja. For sure juhudi zake yeye peke yake hazitasaidia coz would not be sustainable and come 2020 maneno haya yatakuwa kumbumbuku nzuri tu!. Bahati mbaya zaidi anawazuia hata wapizani wake wasikosea while angewaacha waseme ingemsaidia sana kufanya self assessment na hivyo angeadjust accordingly. Wewe jiulize kwenye hili suala la VAT, bungeni kama wapinzani wangeshiriki kikamilifu kwa watu dizaini ya Zitto Kabwe mapungufu ya hii VAT kwenye miamala ya Bank na Mitandao ya simu yangeonekana na hivyo isingekuwa rahisi mzigo huu kuachwa uwaumize wananchi kama ilivyotokea sasa kwenye bunge la Dr Tulia na wachangiaji kina Job Lusinde!

Any ways Mungu ibariki Tanzania, ingawa for the next five years ni maumivu tu mengine!
 
Serikali ya maprofesa isiyojua tofauti za kodi!
Na haya matamko yao ya majukwaani ndio kabisa yanakwenda kuuzika uchumi wetu kwani hayatoi majibu ya wapi fedha za miradi yao ya viwanda itakakopatikana.
Niishangae serikali ya maprofesa juu ya bajeti kiduchu ya wizara ya kilimo huku ikijinasibu kujenga viwanda. Ni uchumi wa nchi ipi uliojengwa nje ya malighafi kutoka mashambani? Labda wa Saudia wa mafuta. Hii haiingii akilini kuondoa kodi za mazao na kuongeza za miamala. Ni bora kodi za mazao ni za msimu kuliko hizi za miamala za kila uchao. Mkulu umebugi parefu mno! Nafikiri mmelewa sifa na au mnapowaona wananchi wakiwa meno nje msifikiri wanatabasamu, hiyo ni ishara ya mtu aliye na hasira kali ya ndani kwa ndani.
Kikwete sijui nikushukuruje kwa hili kwani hatukuistahili zawadi hii adhimu. Sijui nilikuudhi wapi, ni bora ungeniambia ili nikuombe msamaha kuliko ulikonichunia huku unatabasamu kumbe ulikuwa na la kunikomesha! Hewala bwana japo yangu imeshindwa.
 
Aliyekwambia mimi namuabudu Lowassa nani!?
Acha kukurupuka na kuandika uzushi. Usiandike kitu ambacho huwezi kutoa uthibitisho hata chembe.
Hii JF ina kumbukumbu zako tele jinsi ulivyo kinyonga
 
Weka ile ambayo mimi niliandika kuonyesha kwamba namuabudu Lowassa au kufurahia ujio wako CHADEMA ili uonyeshe huo ukinyonga wangu. Acha kukurupuka kuandika vitu ambavyo havipo. Ushahidi ushahidi ushahidi!

Hii JF ina kumbukumbu zako tele jinsi ulivyo kinyonga
 
Mimi nimechoka na unafiki wa waTanzania. Hapa nyinyi ndo mlikuwa mnampigia debe Magufuli......mkiponda vyama vya upinzani. Mkituaminisha kwamba Upinzani hawana experience ya uongozi.

Leo mnataka kutuaminisha kwamba Magufuli ni dictator! Hata mwaka wa uongozi bado... What a shame! Wenyewe wanasema: USIPIME KINA CHA MAJI KWA KUWEKA MIGUU!

Akina Mange Kimambi wanashinda kwenye mitandao wakitukana eti Magufuli ni dictator yet juzi ndo walikuwa wanaimba mapambio kuisifia CCM na Magufuli. Mimi nasema wacha waTanzania wengi tuumie tumezidi kwa unafiki.

Ngoja tuisome Number. Labda next time watu wakipewa nafasi ya kufanya maamuzi watakuwa wanafikiria kwanza kabla ya kutenda. Kama ulimpigia kura Magufuli. Support him! Ni wewe ulimpa kura. Unless ulimpa kura ya kinafiki kusudi upate mwanya wa kupiga pesa! Na hilo amelikataa.

Mimi leo ukiniuliza, nasema Tanzania haijawahi kupata Rais mchapakazi na mwenye uchungu na taifa hili kama Mh. John Pombe Magufuli. Udictator wake siuoni. Maamuzi ya kukurupuka siyaoni. Magufuli ni yule yule. Hajawahi kubadilika. Na tunaomba asibadilike.
 
Back
Top Bottom