Kwanini baadhi ya watanzania wanadharau elimu?

Kwanini baadhi ya watanzania wanadharau elimu?

Inawezekana kuna kundi kubwa halijua maana ya elimu ndio maana imekuwa ni kawaida sana kuisimanga, kuibagaza na kuishusha elimu. Elimu ni maarifa, elimu ni ujuzi, elimu ni mwanga, elimu ni silaha, elimu ni kio, elimu ni Pesa, elimu ni tiba, elimu ni kila kitu kwenye Maisha ya mwanadamu yoyote katika Dunia yoyote. Leo anatokea mtu anadharau badala ya kutoa maoni namna gani tutaunda na kuboresha elimu yetu.

Watanzania baadhi wanakera sana na bahati mbaya wengine wako bungeni kuibagaza elimu sijui inawezekana tumerogwa. Watu wanakalili wanafikili wasomi wanaweza kufanya miujiza wakihisi pengine msomi ni malaika hapana. Taifa letu lina wasomi wazuri ambao ujuzi wao unatumika vizuri kuliletea maendeleo na ustaarabu taifa, wapo serikalini na sector binafsi.

Inasikitisha sana maana hii laana imewashukia hata wasomi wenyewe kuweza kujidhalau na kushindwa kujiamini, kutetea mawazo, kupigania taaluma za kulinda hadhi na heshima ya utu wao. Hivi leo watu wanaita vyeti makaratasi kwa dhihaka hii ni laana sio bure. Kama kuna changamoto kwenye elimu yetu, tuiboreshe na sio kuibagaza inakera sana tunadhalau elimu huku tukipeleka watoto wetu shule
Elimu imejaa misingi ya kigeni kwa 98% Asili ya muafrika hata kiroho tu inagoma automatic na ndiyo maana ile spirit inalazimisha mioyo na akili na kinywa kuibagaza elimu ambayo kimsingi haimsaidii mtu mweusi
 
Wewe jamaa umenichekesha sana, kufanikiwa kimaisha wakati mwingine ni juhudi binafsi na kama kijana wako ni mvivu hataki kujitengeneza wakati mwingine ni tatizo lake yeye. Elimu haina mwisho, unapomaliza kusoma sio mwiso wa kujifunza unaweza ku compromise ukaanza kujifunza hata kitu kingine cha kuweza kuondesha maisha yako ndio maana ya kuelimika Mimi ni mwalimu lakini baada ya kukosa ajira Rasm nikaenda kusoma driving sasa hivi nasukuma mchuma kutoka dar mpaka Kigali kwa Kagame.
 
Shida ni yaliyomo kwenye mitaala yetu hayaendani na mahitaji ya sasa
Wewe nadhani umejibu kifupi sana lakini umeelewa vyema contexts ya mjadala huu , watu wapo busy huko
Wewe ndio hujui elimu ndio maana unaelezea elimu katika angle moja ya vitu lakini unasahau kuwa kupitia elimu ndio tunamtengeneza kijana kuwa principle member wa jamii na taifa husika hivyo tunavitu vingi vya kumfundisha. Unachokiongea ni changamoto za elimu yetu lakini sio tatizo la elimu yenyewe, tukiwa elimu Boro, tunapata wakulima Bora, watafiti Bora, wachumi, ma engineer, madoctor Bora wa kuchunga afya zetu. Pesa na utajiri ni juhudi za mtu binafsi.
Mzee kitu kikubwa unacho takiwa kujua ni kwamba Elimu hii unayo ipigia chapuo wewe ndiyo inayo kufanya uwe tegemezi kiteknolojia, kiuzalishaji ,kibiashara nk

Nimepitia education scheme ya china baada ya kujiuliza sana ni kwanini china ina high local industry development ? Kuliko karibu nchi zote na Asia na Africa na hata European countries kwa ujumla ?

Baada ya kupitia pia forums zao mbali mbali nikaja kubaini kwamba wenzetu wale ndio wanaiishi elimu katika mazingira yao halisi kabisa sio hii ya kwetu ya kulazimishwa kuimeza
 
Kadiri tunavyokataa elimu yetu, yaani elimu ya Kiafrika iliyofundishwa kwa karne na karne kwa vitendo, ndivyo tunavyojichimbia shimoni. Shimo tulilomo. Binafsi, sina mengi ya kuongeza hapa isipokuwa kushauri kwamba, tukienda kujadili Elimu tusiondoe mawazo ya Kiafrika, -School of thought- mawazo fikra n.k.....au kuondoa lugha za Kiafrika, vilevile usiondoe falsafa ya Kiafrika, usiondoe mwafrika na utamaduni wake. Kwa kufanya hivi utakuwa unajifanyia upendeleo mkubwa badala ya kujichimba shimo.
 
Ulifanya vizuri kumsomesha, Mungu anajua kesho ya kila mmoja Wala usijutie, huyo mwanao si sawa na ambae hajasoma, kupata au kukosa kila mtu atapitia bila kujali Elimu aliyonayo au ujuzi... mshukru Mungu tu kwa uzima. Namuombea kwa Mungu mafanikio
Sio kwamba namchukia huyo gharasa, nimemshauri na anetafutiwa fundi simu na yeye aa ze kujifunza.
Kujifunzia kwa mdogo wake tumeona sio poa watu wanamjua hawatakuja kumwamini kwa haraka .
Akajifunzie mbalu arudi akishaanza kuelewa basics
 
Labda kwasabu hawajapata wenye PhD/masters wengi wakuwa challenge, Mimi nakwambia siku sifa ya mbunge ikiwa ni masters/PhD hayo majiz hata bungeni yasingeruhusiwa wangenyang'anywa na ubunge kabisa. Kungekuwa na mjadala mkubwa sana
Kwanza ondokaneni na hizo PhD Arrogances vichwani mwenu mkiamini hizo ndio zinazo faa kuongoza, tambua kwanza uongozi ni inborn skills, halafu kanuni na taratibu ndizo zinafundishwa kulingana na mazingira husika, kuna PhD nyingi serikalini humo zimefanya nini katika taifa hili till to date? Taufa linalalamika ukosefu wa maji na umeme miaka yote ,elimu mbovu miaka yote , hizo PhD zimekuja na suluhu gani?

Tena taifa liliendelea kwa speed nzuri sana likiwa chini ya viongozi wa kawaida kabisa
 
Kwanza ondokaneni na hizo PhD Arrogances vichwani mwenu mkiamini hizo ndio zinazo faa kuongoza, tambua kwanza uongozi ni inborn skills, halafu kanuni na taratibu ndizo zinafundishwa kulingana na mazingira husika, kuna PhD nyingi serikalini humo zimefanya nini katika taifa hili till to date? Taufa linalalamika ukosefu wa maji na umeme miaka yote ,elimu mbovu miaka yote , hizo PhD zimekuja na suluhu gani?

Tena taifa liliendelea kwa speed nzuri sana likiwa chini ya viongozi wa kawaida kabisa
Elimu inamfanya mtu kuwa na kujiamini usiidharau, huwezi kujua PhD zimefanya Nini Kwasababu huna Elimu ya kiwango hicho na unauono wa mazingira ya hapo ulipo tu kuwa kwasabu hapana maji ndo ulalamikie PhD.
 
Ngoja Niwaite Hawa
BAKITA (BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA)
BAKIZA (BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR)
Mkuu hilo litakuwa ni jambo jema sana. Bila tafsiri ya"Elimu" ambayo wote tunaweza kukubaliana hatutaweza, nadhani, kufika popote pale.

Hoja ni nyepesi mno.
 
Hilohlo yakufuta ujinga ndo lamhm Sana, chamsingi tusipinge elimu mpaka kupelekea kuwanyima watoto wetu elimu.
Kwa mfumo wa elimu ya nchi hii hata mtoto akinyimwa haina madhara ila ajue KKK na lugha ya biashara (English) hiyo ndiyo msingi mkuu kwake kwa sasa baada ya hapo mtoto apate skill za maisha halisi yanayo endana na mazingira yake.

Huu ujinga wa mzazi anauza mashamba ,anauza mifugo eti mtoto asome halafu badae wote wanabaki maskini wanaanza kukodi mashamba tena na mtoto ana Bachelor Degree in mass communication na ana 4.8GPA HAPANA!!!
Na wapo wote hapo Baba na mtoto wana pambana na kulaumiana hawana mashamba wala mifugo yote waliuza ili mtoto asome hii HAPANA

Huu ujinga ufe kabisa shit! Na wazazi waelimishwe sana hapa tusitiane umaskini kipumbavu namna hii wakati mwanga ulisha kuwepo
 
Elimu inamfanya mtu kuwa na kujiamini usiidharau, huwezi kujua PhD zimefanya Nini Kwasababu huna Elimu ya kiwango hicho na unauono wa mazingira ya hapo ulipo tu kuwa kwasabu hapana maji ndo ulalamikie PhD.
Acha uongo na kukalili , PESA ndio humfanya mtu ajiamini, unaweza kuwa na elimu na huna pesa hata kupaombele kwenye vikao vya jamii huwezi pata mzee ,tafuta PESA ndiyo heshima usijidanganye kujaza ma vyeti ndani ili kutafuta heshima wakati huna PESA utaonekana wa hovyo tu.
 
Elimu inamfanya mtu kuwa na kujiamini usiidharau, huwezi kujua PhD zimefanya Nini Kwasababu huna Elimu ya kiwango hicho na unauono wa mazingira ya hapo ulipo tu kuwa kwasabu hapana maji ndo ulalamikie PhD.
swala la kujua nina elimu gani hilo halikuhusu sana mzee yawezekaka ulisha kuwa mwanafunzi wangu chuo X, hebu nikuombe acha kwanza personal attack, tuujadili na tuujengee hoja mjadala huu mzuri kabisa uliopo mezani hapa bwashee
 
Elimu katika nini? Mzee hebu elewa kwanz context ya mjadala kabla hujafura hasira kutetea kukalili kwako theories za wengine kwani unaweza nambia hayo unayo yasoma leo kwenye masters yametoka wapi na yaliandaliwa na nani?
Usishupaze shingo,elimu ni ufunguo wa maisha.ukibisha na hili,basi tena
 
Acha uongo na kukalili , PESA ndio humfanya mtu ajiamini, unaweza kuwa na elimu na huna pesa hata kupaombele kwenye vikao vya jamii huwezi pata mzee ,tafuta PESA ndiyo heshima usijidanganye kujaza ma vyeti ndani ili kutafuta heshima wakati huna PESA utaonekana wa hovyo tu.
Sawa mkuu.
 
Usishupaze shingo,elimu ni ufunguo wa maisha.ukibisha na hili,basi tena
Hahahaaa ndio nyie mnadanganya wazazi wanauza mashamba na mifugo halafu badae wanabaki na umaskini na vyeti vya mtoto wao kwenye sanduku, eti elimu ni ufunguo wa maisha!

Dhana ya elimu ni pana sana mzee hebu achana na hizo mythical historical Tems, ambazo hutumika kupumbaza watu na ndio maana hata hao wasomi wameamua wahamie upande wa pili......SIASA

Naipenda elimu ila sio elimu katika mifumo hii tuliyo nayo sisi na mchi nyingi za Africa ......HAPANA
 
Udadisi na kujifunza ndio huleta elimu ila elimu haiwezi kuleta haya niliyotaja.
Ukiona mtanzania anaidharau elimu ya hapa nchini, basi jua amefanya udadisi na akajifunza mwisho akaelimika kwamba bora apambane na mambo mengine ila sio elimu ya mchongo ambayo mtu hujifunza namna ya kuajiriwa badala ya kujiajiri.

Unakaa darasani karibu miaka 20 ukijifunza namna ya kuajiriwa alafu ukitoka humo serikali yako inakwambia ukajiajiri 😊
Elimu lazima imlettee mwanafunzi mabadiliko chanya katika maisha (fikra, uwezo wa kutenda, maongezi n.k).
Siyo lazima iwe ya mfumo wa kukaa darasani miaka mingi na kuambulia vyeti tu.
Changamoto ni kwamba watu wengi wanataka kuona mabadiliko haraka.
 
Imepitwa na wakati!

Nyakati zetu hazihitaji elimu za kukariri principle bali elimu tendaji ile ya field inayozaa kitu cha kuonekana na kutengeneza pesa halisi!!

Elimu hii iliopo ni ya kurithi toka kwa mkoloni yaani kuandaa watumishi wa serikali sasa watumishi wametosha na kuzidi inapaswa ibadilike ghafla na kuwa ya kujitegemea na ubunifu ukitumia nature kutatua changamoto!

Juzi nimeenda seminar ya sayansi ya walimu wa secondary nikaona ujinga uleule unapakwa rangi tu!hakuna cha maana ambacho kitaleta fedha baada ya mtoto kuhitimu yaani tunaandaliwa kufundisha jinsi vijana wajibu maswali ya competence based yaani kujiandaa kwa mitihani badala ya maisha halisi!huo ni ujinga hatari sana!

Niliwaambia haya ni mapokeo hayana majibu kwa vijana kuhusu kujiajiri na kujitegemea wakabaki wananishaangaaa tu eti naenda kinyume na wakufunzi!

Elimu ya sasa ujinga mtupu!

Jua HIVYO!!
Uko sahihi kabisa, tunataka elimu inayotoa ujuzi, sio elimu ya kukariri mambo kwa lugha kiingereza, kisha kuja kutishia wasio na elimu ya darasani. Mimi kwenye kazi zangu naheshimu mwenye ujuzi, sio mwenye cheti cha chuo.
 
Back
Top Bottom