Kwanini baadhi ya watanzania wanadharau elimu?

Kwanini baadhi ya watanzania wanadharau elimu?

Inawezekana kuna kundi kubwa halijua maana ya elimu ndio maana imekuwa ni kawaida sana kuisimanga, kuibagaza na kuishusha elimu. Elimu ni maarifa, elimu ni ujuzi, elimu ni mwanga, elimu ni silaha, elimu ni kio, elimu ni Pesa, elimu ni tiba, elimu ni kila kitu kwenye Maisha ya mwanadamu yoyote katika Dunia yoyote. Leo anatokea mtu anadharau badala ya kutoa maoni namna gani tutaunda na kuboresha elimu yetu.

Watanzania baadhi wanakera sana na bahati mbaya wengine wako bungeni kuibagaza elimu sijui inawezekana tumerogwa. Watu wanakalili wanafikili wasomi wanaweza kufanya miujiza wakihisi pengine msomi ni malaika hapana. Taifa letu lina wasomi wazuri ambao ujuzi wao unatumika vizuri kuliletea maendeleo na ustaarabu taifa, wapo serikalini na sector binafsi.

Inasikitisha sana maana hii laana imewashukia hata wasomi wenyewe kuweza kujidhalau na kushindwa kujiamini, kutetea mawazo, kupigania taaluma za kulinda hadhi na heshima ya utu wao. Hivi leo watu wanaita vyeti makaratasi kwa dhihaka hii ni laana sio bure. Kama kuna changamoto kwenye elimu yetu, tuiboreshe na sio kuibagaza inakera sana tunadhalau elimu huku tukipeleka watoto wetu shule
Sababu ni hizi;

1. Kuna masikini waliokwenda shule, na wasiokwenda shule. Hivyo kutofautisha mwenye shule na asiye nayo huku wote ni masikini ni ngumu.

2. Kuna wasio na shule ni matajiri na huku wapo waliokwenda shule lakini ni masikini.

3. Wengi wa waliokuwa wanaonekana wana akili mashuleni eidha washaharibikiwa mtaani au wapo hoi.

4. Wasio na shele, wengi hujivunia connections. Sasa kama mtu ana connections zinazompa anachopata mwenye shule, what is that shule for..!??

etc
 
Elimu ninini? Acheni kuaminisha watu kwamba kukalili theories za watu wengine na kuzilazimisha zikae kichwani mwako ndio elimu sahihi!

Tambua dhana ya elimu ni pana sana tofauti kabisa na sisi hasa waafrica tunavyo ipokea na kuiamini .

Na ndio maana unaweza ukawa umeweza kukalili theories za wazungu hadi level ya PhD lakini problems analysis and solution zikaja kutolewa kwa usahihi na mtu ambaye hana hata certificate ila ni great thinker.

Kwenye elimu kinacho badilisha watu ni ile socialization kutoka kwa watu tofauti na misimamo pamoja mitazamo aliyo ikuta wakati anazaliwa.

Ndio maana mtu anaweza akawa hana elimu hiyo ya darasani lakini kajikita kwenye maswala ya dini na ana socialize na watu tofauti kwa upande huo naye atakuwa na ustaarabu kama ulio nao wewe mwenye PhD na mnaweza mkakaa same meeting na wote mkatoa hoja za msingi kabisa na pengine Ukazidiwa mbali kabisa.
Wewe mbona ulisoma?
Kama elimu si kitu, rudisha vyeti.
 
Mawazo yako yameegemea eneo moja ndugu, wewe unawaza kuwa the fundamental end of education is materialism. Elimu ni zaidi ya vitu brother, kuna vitu vingi vya kijana unamfundishi kuadopt cultural complexities, value development, collaboration and cooperation. Elimu ni maisha hizo theories zikifundishwa under good pedagogical manner tukaboresha maabara zetu, wataalamu wetu tunapata vijana wazuri wakuweza kulisaidia taifa acha hizo wewe ndugu usiwaze vitu tu.
Mmekazana elimu elimu elimu na mnajenga hoja kutetea kukaa darasani na kukalilishwa theories walizo fanya wenzenu ndio na nyie mpo busy kuzimeza ,

Maana ya elimu unaijua lakini mzee?
What is Education? In a very simple,well known and understandable definition?
 
Nimekwambia mdogo wangu wa like ni fundi simu na electronics kibao, kaishia form four.
Nilimpeleka akakaa na fundi ....hii ni elimu informal.hana cheti.
Anakimbiza mjini.

Mdogo mwingine ana procurement degree analelewa na huyu fundi simu
Hongera Sana kwa kusomesha, mtu akishakuwa na Elimu tu kijamii ni zaidi ya ajira, hawezi kurubuniwa kirahisirahisi.
 
Elimu inaongeza life expectancy isipuuzwe..na mara zote wanaoipuuza ni wale walioikosa, chamsingi serikali ionyeshe kuwa education is matter kwa kufanya yafuatayo...
1. Ili mtu kugombea ubunge awe na Shahada ya Pili.
2. Cheo chochote kuanzia ngazi ya kata iwe ni kuanzia Elimu ya masters degree.
3 waitambue Shahada ya Pili kwenye mishahara ya watumishi.
4. Nk
Hizo kelele za kuidharau Elimu zitapotea automatically, mf. huwezi ukawa unapinga ukatili wa kijinzia huku unaidharau Elimu hyo haileti mantik
Hujui hawahawa wanaoidharau elimu ndio wabunge na watunga sheria?
 
Yes lazima! kichwa changu sio cha kujaza matakataka yasiyo na tija kwa sasa na hasa baada ya kuona uhalisia wa the so called elimu
Kichwani mwangu kitu ambacho hakina practical results za kimtaa sikiingizi wala sikisomi.
Nikae kukariri Archimedes principle...a body can float ujinga ujinga flani.
 
Elimu ni zaidi ya ajira...mfano hizi kauli zakusema "siwezi kula pipi na maganda yake" zimemaliza vijana wengi Sana Ila kwasasa vijana wanajar afya zao, nimesoma uzi mmoja hapa mzaz analalamika kuona kondom kwenye beji la mwanae anayesoma sek. Hyo ni ishara njema kwa mtoto kiafya
Kwahiyo shule ulienda kusomea namna ya kutumia condom sio?
 
Mfumo wetu wa elimu haumsaidii mhitimu kuyatawala mazingira yake, bora tuurudie mfumo wa zamani wa elimu wa kikoloni.
 
Ubovu wa Elimu ya Tanzania unaonekana kwa wahitimu wanapo Anza kufanyia kazi walicho jifunza, na wasomi wa Tanzania wengi ni wajinga yani hawana tofauti na ambao hawaja enda shule au yawezekana hata ambao hawaja enda shule Wana afadhali, watu wana fundishwa wanakalili ili wajibu mitihani sio kuelimika
 
Siku Hawa mnaowaita watunga Sheria za nchi watakapoanza kuingia mjengoni na minimum qualification ya masters degree ndio itakuwa mwarobaini wa kuithamini elimu....
Sasa wewe jiulize watunga Sheria za nchi wanatakiwa wajue kusoma na kuandika tu basi...nani ataithamini elimu??...Leo maprofesa wa udsm wanazidiwa mshahara na msukuma😀😀 serious???
 
Shida ni yaliyomo kwenye mitaala yetu hayaendani na mahitaji ya sasa
 
Wewe mbona ulisoma?
Kama elimu si kitu, rudisha vyeti.
Baada ya kusoma nakuona mambo ninayo yajaza kichwani hayana tija kwa mustakabali wa maisha halisi nikaona nisipoteze tena wanagu huko

Wanangu leo anauwezo wa kutengezeza pesa katika umri wake wa miaka 24 kuliko hata ange poteza muda kuhangaika hayo ma theories

Nilicho fanya nimehakikisha wanajua KKK ambao ndio msingi mkuu wa mawasiliano kimaandishi na kimazungumzo wamesoma lugha muhimu hasa kingereza kwa ajili ya mawasiliamo maana lazima hilo nilikubali na baada ya hapo nimewaweka site huko wana uhakika wa kula na kunywa kwa fedha zao wenyewe
 
Hongera Sana kwa kusomesha, mtu akishakuwa na Elimu tu kijamii ni zaidi ya ajira, hawezi kurubuniwa kirahisirahisi.
Nimesomesha gharasa....tasa mpaka University kwa kwa miaka saba zaidi .
Ametoka yupo kitaa, hata mxhumba kamkimbia kwan wanaume siku hizi hamtaki dada asiye na kazi.

Nimempa informal education mdogo wake chini ya miaka miwili, leo ni fundi simu anamlea dada yake.

Mkubwa huyu wa procurement sasa ndio anaanza na yeye kujifunza ufundi simu baada ya mim dada yake kumshauri sana. Nilimshauri mpaka nikawa nalia....
Joyce, Joyce sahau Hilo licheti nitakupe ukajifunzie ufundi simu mbali kidogo kama unaona aibu hapa watu wanakujua
 
Mmekazana elimu elimu elimu na mnajenga hoja kutetea kukaa darasani na kukalilishwa theories walizo fanya wenzenu ndio na nyie mpo busy kuzimeza ,

Maana ya elimu unaijua lakini mzee?
What is Education? In a very simple,well known and understandable definition?
Wewe ndio hujui elimu ndio maana unaelezea elimu katika angle moja ya vitu lakini unasahau kuwa kupitia elimu ndio tunamtengeneza kijana kuwa principle member wa jamii na taifa husika hivyo tunavitu vingi vya kumfundisha. Unachokiongea ni changamoto za elimu yetu lakini sio tatizo la elimu yenyewe, tukiwa elimu Boro, tunapata wakulima Bora, watafiti Bora, wachumi, ma engineer, madoctor Bora wa kuchunga afya zetu. Pesa na utajiri ni juhudi za mtu binafsi.
 
Nimesomesha gharasa....tasa mpaka University kwa kwa miaka saba zaidi .
Ametoka yupo kitaa, hata mxhumba kamkimbia kwan wanaume siku hizi hamtaki dada asiye na kazi.

Nimempa informal education mdogo wake chini ya miaka miwili, leo ni fundi simu anamlea dada yake.

Mkubwa huyu wa procurement sasa ndio anaanza na yeye kujifunza ufundi simu baada ya mim dada yake kumshauri sana. Nilimshauri mpaka nikawa nalia....
Joyce, Joyce sahau Hilo licheti nitakupe ukajifunzie ufundi simu mbali kidogo kama unaona aibu hapa watu wanakujua
Ulifanya vizuri kumsomesha, Mungu anajua kesho ya kila mmoja Wala usijutie, huyo mwanao si sawa na ambae hajasoma, kupata au kukosa kila mtu atapitia bila kujali Elimu aliyonayo au ujuzi... mshukru Mungu tu kwa uzima. Namuombea kwa Mungu mafanikio
 
Mmekazana elimu elimu elimu na mnajenga hoja kutetea kukaa darasani na kukalilishwa theories walizo fanya wenzenu ndio na nyie mpo busy kuzimeza ,

Maana ya elimu unaijua lakini mzee?
What is Education? In a very simple,well known and understandable definition?
Elimu ni kuitengeneza/ kuifanya akili iweze kufikiri vizuri... Hapo vipi?
 
Hawa mawaziri wanaoboronga sio Masters na pHD
Labda kwasabu hawajapata wenye PhD/masters wengi wakuwa challenge, Mimi nakwambia siku sifa ya mbunge ikiwa ni masters/PhD hayo majiz hata bungeni yasingeruhusiwa wangenyang'anywa na ubunge kabisa. Kungekuwa na mjadala mkubwa sana
 
Back
Top Bottom