Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Status
Not open for further replies.
Huijui hata kidogo historia ya dunia.
Vita na matatizo makubwa duniani kati ya mataifa yamesababishwa na watawala wa kiume.Ni nadra sana kumpata mwanamke mtawala aina ya Adolf Hitler,Iddi Amin,n.k
Wanawake ni wazuri sana kusimamia na kuepusha ajali kwa familia zao na mataifa yao lakini sio familia za wenzao na mataifa ya wenzao!

Siku dunia ikiwa taifa moja hapo sawa kumpa mwanamke madaraka yale ya juu kabisa ila sio sasa mataifa na falme nyingi kuna kutoelewana.

Fikiria ukute rais wa jirani ni mwanamke na huku nchini kwetu ukute ni mwanamke alafu kuwe na chuki kati yao! Amini nakwambia vita lazima iibuke tu hata Yesu aje kuwapatanisha sio rahisi[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]

Ahueni tunayoiona duniani leo ni matokeo ya vifua na makoromeo ya wanaume sababu ungekuta ni wanawake wanatawala wangeshaangamizana kitambo sana.
 
Mimi sihitaji kusaidiwa kufikiria maana hapo tu yenyewe uko nje ya mada ingekuwa mtihani ungeshapata zero yako
Nachela sana, huku umenileta wewe, na mimi kuonyesha wapi unakosea na siko nje ya mada sababu ninacho kiandika hapa ni matokeo ya kuwa ndani ya mada.

Watoto wa kike kujadili mambo kielimu huwa hamuwezi kabisa, zaidi ya kuleta hisia mbele ya elimu, lazima uonekane kituko.
 
Daah, kwahiyo unanikana siyo ?

Nikajua umeniita kwa nia nzuri nije kupata faida, kumbe ni kinyume chake ?

Ngoja nimuite mrembo mwingine, aje kulisadikisha hili, kama kweli mimi ni mbishi au la !
Nimekuita kwa nia nzuri kabisa. Si unaona sasa hivi unavyofurahi unabishana hadi mwenyewe unapenda.
Nisingekuita mida hii ungekuwa umepoa sana.
 
Huijui hata kidogo historia ya dunia.
Vita na matatizo makubwa duniani kati ya mataifa yamesababishwa na watawala wa kiume.Ni nadra sana kumpata mwanamke mtawala aina ya Adolf Hitler,Iddi Amin,n.k
kuna waziri mkuu wa Israel alikua mwanamke mtata sana anaitwa golder meir
 
Nimekuita kwa nia nzuri kabisa. Si unaona sasa hivi unavyofurahi unabishana hadi mwenyewe unapenda.
Nisingekuita mida hii ungekuwa umepoa sana.
Unaweza kuthibitisha kwamba nafurahi ? Au nafurahia hiki ninacho kifanya muda huu ?
 
Feminism inatafsiriwa vibaya sana, maana mtu wa jinsia yoyote ile anaweza akawa ni Feminist. Bahati mbaya sana wanawake wengi wanaofuata hii falsafa hawafahamu hata undani wake ukoje. Kuwa muhanga wa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hakukufanyi kuwa Feminist. Mimi binafsi ni muumini mzuri kabisa wa Falsafa ya Feminism: Naamini inaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii nzima.

Sasa huwa tunachanganya mambo: Kuna wale wanawake wenye hasira ya maisha na wamekata tamaa na kuaamua kuwa na hasira ya kushambulia jinsia ya kiume ndiyo huwa wanajiita Feminist au tunawaita ni Feminists (This is very Incorrect). Mtu kazalishwa na mwanaume huko na akaachwa ,akaanza kuwa na hasira na wanaume wote anajiita Feminist AU mtu kalelewa na baba aliyemfanyia ukatili utotoni sasa amekuwa anachukia wanaume anajiita Feminist.

Inabidi tukae tufundishane nini maana ya Feminism: Maana wanawake wengi ambao wana kazi nzuri, elimu nzuri na kipato kikubwa (Independent Women) hujidhania kuwa wao ni Feminists. Hawa humu jukwaani ndiyo wako wengi mno na wanakera sana.

Nijuavyo mimi Falsafa ya Feminism ni zaidi ya mwanamke kuelimika au kuwa na pesa ili kupambana na jinsia ya kiume ambayo wengi hudhani ni kandamizi kiasili (Repressive and Evil in Nature). Pia ndani ya Falsafa ya Feminism kuna makundi makubwa mawili ambayo ni Radical Feminists na Moderate Feminists: Ukiwauliza hawa wanaojiita Feminists wako kwenye kundi gani hawawezi kukupa majibu, hata wewe mtoa mada Sheillah Sheillah huwezi kunipa jawabu.

NB: Hakuna mwanaume mwenye akili timamu ambaye atamchukia mwanamke Feminist. Ila tu huwa tunachukia wale wanawake wenye hasira na jinsia ya kiume kwasababu zao binafsi halafu wanavaa sura ya Feminism. Wengi wenu ni akili fupi sana na mnatukera sana(Wanaume na wanawake tunaofahamu haswa nini maana ya Feminism)
Thread Closed!
I second you comrade Cato nadhani maelezo yako yamemaliza kila kitu hapa, na feminist wengine need to see this.




Let's meet at the top, cheers 🥂
mkuu kuna social experiment naifanya

Well n good chief! 👊


Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom