Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Status
Not open for further replies.
Siku ukiwa ndani ya ndoa ndio utaelewa, unaelezea vitu vya chuo ukiwa o level, baya zaid ukute hujawahi kuishi na mwanaume at least 6month practically pakua pakia.
Hamna kitu kisichoeleweka duniani hapa just kila mtu a play part yake basi tu.
 
Muulize kwanza mwenyezi mungu ambae hakumuumba mwanamke, bali akamtoa tu ubavuni mwa mwanaume..

Yaani nikubebe katika uumbaji halafu uje unifanyie kiburi?

Haiwezekani
Kiburi kivipi?
Kwahiyo mimi kusimamia haki zangu ndio kiburi?
 
Hahaha feminist upuuzi mtupu, wanawake bila kubebwa hawafiki kokote.

Kwa mfano Tanzania waseme nafasi zote za uongozi zinagombewa hutoona sura ya kike popote.

Wanawake hupewa viti maalum ndiyo size yao, nani atamsikiliza huyo feminist na wapi, na anaongea nini, ili iweje?! Hata wanawake wenzao huwapuuza, sasa iweje walalamikie wanaume?!

Eti haki zake, upuuzi mtupu.

Wanawake mtuheshimu waume zenu, muwe wake zetu bora, achana na uropokaji you call it feminism, ni ujinga.

Kaombe jukwaa uongee hizo HAKI ZAKO tuzisikie, hata wewe utajiona mjinga.

Haki gani, umenyimwa au ume nyang'anywa na nani?!

Kwanza nani atakusikiliza ukiropoka kudai hizo you call HAKI?!

Unataka wanaume waache vitu vya maana wakusikilize unalialia?!
 
Akishajua hizo haki ajitolee mahari na kujioa, tokea enzi za kale wanaume tulipewa kazi ya kuwapenda wanawake nao wakapewa agizo la kututii basi..hizo haki unazosema ndizo huondoa utii na ndo maana nikikupa kazi ya kuniletea wenye kujua hizo haki ambao wameoleka hutaniletea.
Wewe mwanaume si una haki zako? Mbona haujioi mwenyewe na kujitolea mahari?
 
Hajazaliwa wa kunipiga aisee never kabisa, Mimi natoka na wanaume matured, na sio waliokulia mifumo dume, so huwa Niko makini Sana kwenye selection, wanaume suruali kwangu hawana nafasi
Wanaume suruali na wanaume wasiovumilia ujinga ni watu wasiofanana, unachanganya mambo mate.
 
Wanaume waoga na wasiojiamini ndio hupenda wanawake wawe chini. Inshort hao Ni insecure people wanaamini ili wawe wanaume kamili lazima wamnyanyase mwanamke, pia Mila na desturi nyingi bado ni tatizo hasa Africa.

Ukweli ni kwamba feminist wana maneno mengi ka radio ya mbao, na kila kitu hujiweka mbele na kuona wanastahili na kila mara wako sahihi na huwa hawakosei. Kwa haya yote, mwanamke mwenye hizi tabia tunamlebo mgomvi au mkorofi. Na Mithali 21:19 inasema "Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika, kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi".

Sasa mwanamke wa hivi wa nini?
 
Hajazaliwa wa kunipiga aisee never kabisa, Mimi natoka na wanaume matured, na sio waliokulia mifumo dume, so huwa Niko makini Sana kwenye selection, wanaume suruali kwangu hawana nafasi

Hujapenda na kuoza bado. Usitakane mamba kabla hujavuka mto.
 
Feminism inatafsiriwa vibaya sana, maana mtu wa jinsia yoyote ile anaweza akawa ni Feminist. Bahati mbaya sana wanawake wengi wanaofuata hii falsafa hawafahamu hata undani wake ukoje. Kuwa muhanga wa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hakukufanyi kuwa Feminist. Mimi binafsi ni muumini mzuri kabisa wa Falsafa ya Feminism: Naamini inaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii nzima.

Sasa huwa tunachanganya mambo: Kuna wale wanawake wenye hasira ya maisha na wamekata tamaa na kuaamua kuwa na hasira ya kushambulia jinsia ya kiume ndiyo huwa wanajiita Feminist au tunawaita ni Feminists (This is very Incorrect). Mtu kazalishwa na mwanaume huko na akaachwa ,akaanza kuwa na hasira na wanaume wote anajiita Feminist AU mtu kalelewa na baba aliyemfanyia ukatili utotoni sasa amekuwa anachukia wanaume anajiita Feminist.

Inabidi tukae tufundishane nini maana ya Feminism: Maana wanawake wengi ambao wana kazi nzuri, elimu nzuri na kipato kikubwa (Independent Women) hujidhania kuwa wao ni Feminists. Hawa humu jukwaani ndiyo wako wengi mno na wanakera sana.

Nijuavyo mimi Falsafa ya Feminism ni zaidi ya mwanamke kuelimika au kuwa na pesa ili kupambana na jinsia ya kiume ambayo wengi hudhani ni kandamizi kiasili (Repressive and Evil in Nature). Pia ndani ya Falsafa ya Feminism kuna makundi makubwa mawili ambayo ni Radical Feminists na Moderate Feminists: Ukiwauliza hawa wanaojiita Feminists wako kwenye kundi gani hawawezi kukupa majibu, hata wewe mtoa mada Sheillah Sheillah huwezi kunipa jawabu.

NB: Hakuna mwanaume mwenye akili timamu ambaye atamchukia mwanamke Feminist. Ila tu huwa tunachukia wale wanawake wenye hasira na jinsia ya kiume kwasababu zao binafsi halafu wanavaa sura ya Feminism. Wengi wenu ni akili fupi sana na mnatukera sana(Wanaume na wanawake tunaofahamu haswa nini maana ya Feminism)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom