Je, matatizo ya Mwanamke ni fursa kwa baadhi ya Wanaume?

Je, matatizo ya Mwanamke ni fursa kwa baadhi ya Wanaume?

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
12,920
Reaction score
29,621
Hey guys,

Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza kuhusu utafutaji wa kazi na fursa mbalimbali kati ya mwanaume na mwanamke.

Mara nyingi naona kuna tofauti kubwa sana.

Mwanaume anaweza kwenda kutafuta kazi au kujifunza kitu fulani, na majibu anayopata huwa ni mawili tu: kazi ipo au haipo.

Mambo yanakuwa ya moja kwa moja.

Changamoto kubwa naiona kwa baadhi ya wanawake, hasa wanapokutana na HR au manager ambaye ni mwanaume.

Badala ya mazungumzo kubaki kwenye kazi au fursa husika, mara nyingine mtu huanza kutengeneza mazingira ya mazoea, stori za karibu, na hatimaye kutongoza.

Niseme wazi, si ofisi zote ziko hivyo, si sehemu zote unaweza kukutana na hali hii, na si wanaume wote wana tabia hiyo(msisitizo).

Lakini ni jambo ambalo linaonekana kujirudia mara kwa mara kiasi cha kuibua maswali.

Najaribu kujiuliza, hawa wanaume wa aina hii huwa wana shida gani?🤔

Kwa nini umtengenezee ugumu mtu anayehitaji kazi au fursa mpaka ahisi kuna masharti ya ziada?
Kwa nini msaada au uwajibikaji uwe na matarajio ya malipo ya kimapenzi?😞

Mfano, mimi binafsi nilikuwa nimepanga nyumba kwa mmiliki ambaye ni mwanaume, ana familia na ni mtu ana ndoa.

Siku moja niliona mambo yangu hayajakaa sawa kifedha, hivyo nikampigia simu kabla hata muda wa kodi haujaisha nikamwambia.

"
Shikamoo mzee, najua tarehe ya kodi imekaribia lakini naona mambo yangu hayaja tik vizuri ikifika ukaona kimya naomba unipe muda kidogo kwa sababu hali yangu bado haijakaa sawa.

Akanijibu kwa upole sana na kuniambia watu wa aina yangu ni waaminifu na makini.

Nikasema sawa, labda ni mtu mwenye uelewa.
Lakini ilipofika muda wa kodi na kuona bado sijalipa, akanipigia simu tena na kusema.

Binti, nimekaa nikafikiria nikakuonea huruma.
Naweza nikakuacha ukae hapo hata miezi sita bila kulipa, au nikakupa sehemu nyingine kwa sababu nina nyumba nyingi🤔

Nikadhani labda ananisaidia kwa ubinadamu.
Kumbe baada ya hapo akaanza kusema jinsi anavyonipenda na maneno mengine mengi ya kimapenzi ( longo longo nyigi in Sugu voice).

Nikajiuliza, inawezekanaje mtu aanze kunipenda mara tu baada ya kujua nina shida? Noma sana.

Nilielewa haraka anachotaka, nikamwambia asijali nitatafuta namna ya kulipa, na kweli nililipa kama nilivyoahidi.

Sasa huwa najiuliza, tatizo huwa ni nini kwa baadhi ya wanaume kutaka kutumia matatizo ya wanawake kama fursa ya kupata mahusiano ya kimapenzi? Kwa nini wakiona mwanamke yuko kwenye hali ngumu, badala ya kusaidia kwa ubinadamu, wao huona huo kama mwanya wa kutimiza matamanio yao?

Au ni matumizi mabaya ya mamlaka na nafasi walizonazo?
Wewe unaonaje? Umewahi kushuhudia au kukutana na hali kama hii? 🤔💭

ShesRise_1 🖐
 
Mwanaume huongozwa zaidi na tamaa, na pengine ukaribu wa mwanamke mwenye changamoto zake huweza pelekea mwanaume anaemsaidia atamani kumuweka..😜
Ukiona mwanaume anae furahia matatizo ya mwanamke, basi tambua huyo mwanamke hajakamilika.
Lakini wapenzi wanapo achana kwa ubaya basi basi kiasili hua hakuna anae tamani kuona Ex wake akifanikiwa kwa namna yeyote.
 
matatizo ya mwanamke huwa ni fursa kwa baadhi ya wanaume. Katika jamii na mahusiano, wanaume wenye nia tofauti hutumia changamoto za kihemko, kifedha, au kisaikolojia za wanawake kujinufaisha wao wenyewe.
Vivyo hivyo kwa wanawake hii inacheza pande zote 2 sio wanaume tu na wanawake pia hufanya vivyo hivyo unaweza sema hakuna mimi nakwambia wapo
 
1779863559350.jpg
 
Hey guys,

Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza kuhusu utafutaji wa kazi na fursa mbalimbali kati ya mwanaume na mwanamke

Mara nyingi naona kuna tofauti kubwa sana

Mwanaume anaweza kwenda kutafuta kazi au kujifunza kitu fulani, na majibu anayopata huwa ni mawili tu: kazi ipo au haipo

Mambo yanakuwa ya moja kwa moja.

Changamoto kubwa naiona kwa baadhi ya wanawake, hasa wanapokutana na HR au manager ambaye ni mwanaume

Badala ya mazungumzo kubaki kwenye kazi au fursa husika, mara nyingine mtu huanza kutengeneza mazingira ya mazoea, stori za karibu, na hatimaye kutongoza

Niseme wazi, si ofisi zote ziko hivyo, si sehemu zote unaweza kukutana na hali hii, na si wanaume wote wana tabia hiyo(msisitizo )

Lakini ni jambo ambalo linaonekana kujirudia mara kwa mara kiasi cha kuibua maswali

Najaribu kujiuliza, hawa wanaume wa aina hii huwa wana shida gani?🤔

Kwa nini umtengenezee ugumu mtu anayehitaji kazi au fursa mpaka ahisi kuna masharti ya ziada?
Kwa nini msaada au uwajibikaji uwe na matarajio ya malipo ya kimapenzi?😞

Mfano, mimi binafsi nilikuwa nimepanga nyumba kwa mmiliki ambaye ni mwanaume, ana familia na ni mtu ana ndoa
Siku moja niliona mambo yangu hayajakaa sawa kifedha, hivyo nikampigia simu kabla hata muda wa kodi haujaisha nikamwambia

"
Shikamoo mzee, najua tarehe ya kodi imekaribia lakini naona mambo yangu hayaja tik vizuri ikifika ukaona kimya naomba unipe muda kidogo kwa sababu hali yangu bado haijakaa sawa

Akanijibu kwa upole sana na kuniambia watu wa aina yangu ni waaminifu na makini

Nikasema sawa, labda ni mtu mwenye uelewa
Lakini ilipofika muda wa kodi na kuona bado sijalipa, akanipigia simu tena na kusema

Binti, nimekaa nikafikiria nikakuonea huruma
Naweza nikakuacha ukae hapo hata miezi sita bila kulipa, au nikakupa sehemu nyingine kwa sababu nina nyumba nyingi🤔

Nikadhani labda ananisaidia kwa ubinadamu
Kumbe baada ya hapo akaanza kusema jinsi anavyonipenda na maneno mengine mengi ya kimapenzi ( longo longo nyigi in Sugu voice)

Nikajiuliza, inawezekanaje mtu aanze kunipenda mara tu baada ya kujua nina shida? Noma sana

Nilielewa haraka anachotaka, nikamwambia asijali nitatafuta namna ya kulipa, na kweli nililipa kama nilivyoahidi

Sasa huwa najiuliza, tatizo huwa ni nini kwa baadhi ya wanaume kutaka kutumia matatizo ya wanawake kama fursa ya kupata mahusiano ya kimapenzi? Kwa nini wakiona mwanamke yuko kwenye hali ngumu, badala ya kusaidia kwa ubinadamu, wao huona huo kama mwanya wa kutimiza matamanio yao?

Au ni matumizi mabaya ya mamlaka na nafasi walizonazo?
Wewe unaonaje? Umewahi kushuhudia au kukutana na hali kama hii? 🤔💭

ShesRise_1 🖐
ndugu mdau wa jf,
ni muhimu sana changamoto kama hizo zikupe hamasa na kuchochea nguvu zaidi ya kujizatiti katika kufanya kazi kwa bidii na maarifa, ili kujikomboa katika hali hiyo ya unyonge wa kiuchumi.

Uko sahihi kwamba,
watu wengi hutumia changamoto wanazopitia wengine kujifurahisha kimwili au kijinufaisha kiuchumi au kisiasa.

Kumbuka,
katika nyakati hizi za utandawazi, uovu mwingi umejificha katika wema.

Mshirikishe Mwenyezi Mungu akuvushe salama kwenye kwenye mtihani huo, na kukuvusha salama kwenye mto huo ambao umejaa mamba wengi ambao ni lazima kuuvuka 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Wanaume tujikite ktk kazi,tusitumie jinsia zetu kujinufaisha. Nataka niwaambie wanaume wenzangu wenye tabia hizi mbovu na ambazo hazikubaliki ktk jamii tuache mara moja,kwani licha ya kuwa zinakiuka miongozo,kanuni,taratibu na sheria za utumishi wa umma bali pia ni fedheha kuwa ipo siku moja utakamatwa,utawekwa zizuizini na utaadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Lazima watanzania hasa nyie watumishi wa umma mfanye kazi kwa weledi.
 
Back
Top Bottom