Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Kwanini baadhi ya wanaume hamuwapendi Feminists?

Status
Not open for further replies.
Singo mom's mnajifariji sana ila mioyoni mwenu mnawaka moto,mimi nipo relaxed sina shida but ni vile hapa zinasomeka sentences zingekuwa zinasomeka hisia zenu pasingekalika humu na wengi wenu mpo humu mkijionyesha ni miamba ili wale ambao hawajaingia bado kwenye tasnia hiyo wachukulie ni kitu simple ili nao yawakute ila kiukweli mnateseka sana!

Kudanganyana tu na mkiendelea na viburi vyenu kujifanya vichwa ngumu kutokana na mna-make some money kwa kudanga kwa pimbi's wasiokuwa na malengo na vijikazi vyenu mnavyopewa kwa kuvuliwa nguo mtaachwa achwa hovyo mpaka akili ziwakae.

Na bado!!!
Hili povu vepee maana umeanza personal attack tu nyingi Mara single moms Mara kile na wewe si uwe single daddy, kavue boxa ili upewe kazi si una mtaji haya vua boxa upate kazi ujikwamue kiuchumi.
 
Feminism inatafsiriwa vibaya sana, maana mtu wa jinsia yoyote ile anaweza akawa ni Feminist. Bahati mbaya sana wanawake wengi wanaofuata hii falsafa hawafahamu hata undani wake ukoje. Kuwa muhanga wa unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hakukufanyi kuwa Feminist. Mimi binafsi ni muumini mzuri kabisa wa Falsafa ya Feminism: Naamini inaweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii nzima.

Sasa huwa tunachanganya mambo: Kuna wale wanawake wenye hasira ya maisha na wamekata tamaa na kuaamua kuwa na hasira ya kushambulia jinsia ya kiume ndiyo huwa wanajiita Feminist au tunawaita ni Feminists (This is very Incorrect). Mtu kazalishwa na mwanaume huko na akaachwa ,akaanza kuwa na hasira na wanaume wote anajiita Feminist AU mtu kalelewa na baba aliyemfanyia ukatili utotoni sasa amekuwa anachukia wanaume anajiita Feminist.

Inabidi tukae tufundishane nini maana ya Feminism: Maana wanawake wengi ambao wana kazi nzuri, elimu nzuri na kipato kikubwa (Independent Women) hujidhania kuwa wao ni Feminists. Hawa humu jukwaani ndiyo wako wengi mno na wanakera sana.

Nijuavyo mimi Falsafa ya Feminism ni zaidi ya mwanamke kuelimika au kuwa na pesa ili kupambana na jinsia ya kiume ambayo wengi hudhani ni kandamizi kiasili (Repressive and Evil in Nature). Pia ndani ya Falsafa ya Feminism kuna makundi makubwa mawili ambayo ni Radical Feminists na Moderate Feminists: Ukiwauliza hawa wanaojiita Feminists wako kwenye kundi gani hawawezi kukupa majibu, hata wewe mtoa mada Sheillah Sheillah huwezi kunipa jawabu.

NB: Hakuna mwanaume mwenye akili timamu ambaye atamchukia mwanamke Feminist. Ila tu huwa tunachukia wale wanawake wenye hasira na jinsia ya kiume kwasababu zao binafsi halafu wanavaa sura ya Feminism. Wengi wenu ni akili fupi sana na mnatukera sana(Wanaume na wanawake tunaofahamu haswa nini maana ya Feminism)

Asante mkuu! Wewe umeongea kile ambacho wengi huwa tunajaribu kukiongea ila tu huwa tunatafsiriwa vibaya yaani africa bado watu wengi hawajajua nini maana ya feminism hivyo mimi naona bora tuachane nayo tu tufuate tamaduni zetu kieleweke kimoja!

Eti africa feminism inatafsiriwa kuwa ni mwanamke kuwa juu ya mwanaume! Sasa sijui ni mwanamke gani huyo anayejielewa atataka kuwa juu ya mwanaume!
 
Empowering women is not a problem at all! The real problem is who is preparing these men to live with the empowered women!

Nafikiri hapa ndipo shida ilipo! Tuko busy kuwawezesha wanawake hadi tunasahau kuwaandaa wanaume namna ya kuishi na hao wanawake wanaowezeshwa tutaendelea kupiga kelele kila siku oo feminism feminism africa feminism bado sana!
Mimi nadhani zianzishwe movements za kusaidia wanaume hasa wa ki Africa maana now wanachangamoto nyingi Sana kijamii,na vile wamesahaulika basi Ni changamoto sana
 
Hawawezi kujuta kabisa kulelewa na strong mama like me Tena watanishukuru maana nitawafundisha life skills mbalimbali so hawata regret kamwe
Mfano rahisi tu angalia watoto wa nusu familia na familia kamili
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mikazo gani imekutisha mwanamke kuwa ndio mzee au kuwa kikondoo haimaanishi ni mke bora
Sawa ila mwanamke akiwa mtiifu mpole na mwerevu inapendeza sana,na hutoskia nyumba hiyo kukiwa na visa visa,ila wewe nakufananisha na wa moyo wangu,yaani ana misimamo flani ambayo sijui ka ntawezana.
 
Una shida sehemu best...!
Hauko sawa u needed deliverence.
Au la hauishi Bongo wewe..labda nikupe mfano hai ..
Mume ameajiriwa ..tuseme take hom ni 800k..tuna watoto wanne..wote wanasoma . Kila mtoto mhula inatakiwa 400k
Bado nyumba msosi uwepo ..
Bado Kuna emergence za hapa na pale. .
Bills zote zilipwe...
Hebu niambie Magu kapandisha lini mshahara? Sasa hivi mshahara ni 24 had 24th. No posho at all...alafu unasema nikae him kuja kufurahisha wewe..nikikuona laki tu unaanza kuruka Ruka Kama maharage. Maisha yamebadilika sio km zamani..saidianeni majukumu...we ukilipa Ada Mimi ntalipa bills zote na nitahakiksha msos hom unakuwepo!
C'moon men. ! Unataja kuishi maisha ya kimaskini siku mmoja akidondoka ndo mama aanze jifunza kupika bagia? Hapana badilika haraka sana iwezekanavyo ..tukija kwenr suala la malezi nadhani kila mtu na ulezi wake. Mfano mie nahakikisha saa 8 cmchana Niko home..ntarudi na watoto nitasimamia show ya homework n other stuffs . .nikichelewa kurudi inajulikana nimechelewa Kwasababu maalum..lakini sio nikae hom nikutegemee wewe tu kisa mie ke. .umefeli...!
Kwanza wanaume wanaowapa hela wake zao za matumizi wamebakia wa kuhesabu..maisha yamebadilika

nazumgumzia familia nyingi za kiaAfrica na duniani, Mwanamme ndio anabeba mzigo mkubwa wa majukumu kuliko mama na mwanaume ndio kwa kiasi kikubwa yuko expose kwenye mapambano na magumu na mtu huyu anarudi nyumbani usiku daily..mama upo nyumbani na haupo front kivilee zaidi ya vishughuli vidogo vya hapa na pale na mapema uko nyumbani utashindwa kumpikia mmeo, utashindwa kumfulia mumeo hata boxer kama hamna washing machine? kama ni maji yetu haya ya bomba utashindwa hata kumuandalia maji?

Naamini familia yenye mwanamke mpambanaji na mwanamme mpambanaji na wote ni watu wakuwepo nyumbani kwa muda mdogo au nadra sana huwa hakuna familia hapo wala mapenzi na hiyo ndoa haiendi popote...

Raha ya maisha ya familia na mambo yaende ni kwa mwanaume either kuwa busy sana au kuwa ndio solver wa magumu ya familia, na mama atleast awe anakuwepo kuwepo nyumbani sio busy saana kivile ili ailinde familia hapa unazungumzia responsibility za nyumbani kama mama..

sijaona bado umuhimu wa mke na mume kama wote mko busy na muda hamna, hapa mzigo unarudi kwa watoto kwa maana ya makuzi na malezi..tafsiri ya ndoa na maisha ya familia kwenye imani zote inazungumzia mwanamme kutoka jasho na mama kurelax, mama atoke jasho na mwanamme atoke jasho sidhani kama kuna familia hapo na sijui hiyo familia unaiendeshaje..
 
Wanjikweza Sana hapa hawana lolote mtu anajitutumuaaa ohh mke akae ndani mtu hata kumpa laki 2 Kama poket money huwez..Yanini Sasa kuleteana ufukara?
Kiukweli kipato Cha mwanaume hakiwezi lazima mufe maskini mushindwe kupeleka watoto shule nzuri na maisha yawashinde kiujumla. Mimi binafsi siwezi acha kutafta hela ili wanangu waishi vizuri kisa mwanaume Yani siwezi, nitapambana usiku na mchana
 
Jamani . What a massage. Nimesoma nikafika mwisho nikascroll kujua hii akili ni Nani?
Jamani Kuna wanaume hapa duniani...nilikua nimejilaza Ila nimejikuta nakaa kabisa...
Kuna kipindi fulani nilipitia situation km uliyoandika hapa..mie sipendi kbs mtu anaiambie swag za ajabu ajabu...mfano wanaume wanaamini 100% wenyewe ndo wenye final say .yaan akisema usimchallenge. .Mimi siko hivyo hata nukta. Ukiniambia hii ni nyeusi nna Haki ya kukuambia mie naona hii ni blue ...sio mie nisema ni blue uanze kulalamika sikusikilizi ..alafu aliyewadanganya nyie ndo final say ni nyau gani huyo?
Kwamba wanaume hawakosei...nyie ndo mna brilliant ideas ..kwamba sis wanawake tupo kwaajili ya kuwastrehesha tu....na kuzaa tu..hivi alowadanya haya maujinga?
Hivi ni wapi mmesoma kuwa wanawake hatuna mawazo mazuri?hatuna ushauri mzuri? Eti mtu anafikia gatua anasema ufalme wa mwanaume usiguswe...??? Ufalme huo ni upi ..kwamba hutaki kuwa challenged? Utaula wa chuya kwa Wangari aisee...
Msikilize mkeo ideas zake msapoti unavyoweza... Kubaki kukanywa...masuala ya kutishana tishana oh Mimi ndo mwanaume ndo hatuendelei .( Mie nitendee dhambi zote nitavumilia Ila sio kuniletea masuala ya ufalme wa juha nop sitaweza)
Mimi Uhuru wa kutoa maoni nimeupigania Sana Sana ndoani kwangu . Nna miaka miwili naona Uhuru wa kutoa maoni na mawazo kwa mapana nauona...yaani siwez ishi na mtu nifate anayosema yeye hata Kama ni wrong kisa mume! Hapana aisee..sikilizaneni kosoaneni mambo yatakaa sawa...!

Wewe kaka Mungu akupe pumzi...upate mke mwema mwenye positive ideas mtasonga mbele haraka sana !achana na mahawayani haya! Ngoja nikufollow moyo wangu itulie!💕
Hahahaa... kwahiyo uka-scroll hadi chini, unakuta "...kumbe Kajuma Nature kenyewe ndo haka; kabaayaaaaa!"

Joke aside, binafsi huwa nashangaa sana hizi mentality tunazitoa wapi though makuzi nayo nadhani yanachangia kwa kiasi kikubwa!! My mom, for instance, she's too tough na huwezi kumletea ujinga ujinga tu kwa kuona "...si mwanamama tu huyu, atanifanya nini", and I adore her!
 
Naona umeandika kinyume bibie, sisi wanaume tunao jiamini ndiyo tunataka wanawake wawe chini yetu, lakini hili siyo limekuja tu,bali hili ni jambo la kimaumbile, vipi maumbile yetu yawe tofauti halafu tunafanane kwa haki, hili halipo.

Lakini, mwanamke hajaumbwa kuwa juu ya mwanuame, na kuwa chini ya mwanaume siyo kunyanyaswa, bali hiyo ndiyo stahiki.

Maumbile ndiyo yanabainisha haki na majukumu.

Ufeministi ni uchizi wa kujitakia.
Mwanaume anayejiamini Hana mda mchafu wa kubishana na wanawake ili aonekane yeye kidume, kidume kinachojiamini kinaheshimu wanawake, na Wala hakijilinganishi maumbile yake ili kionekane Bora.
Halafu ukisema maumbile ndio ubora wa mwanaume how about sex toys dildo lenyeee ni mb... Ya kiume Ila haliongei Wala halina SAUTi kwahyo kisa umbile lake tayari ni mwanaume?
 
Kiukweli kipato Cha mwanaume hakiwezi lazima mufe maskini mushindwe kupeleka watoto shule nzuri na maisha yawashinde kiujumla. Mimi binafsi siwezi acha kutafta hela ili wanangu waishi vizuri kisa mwanaume Yani siwezi, nitapambana usiku na mchana
Tatizo tuna unafiki Sana. Hivi men akiishiwa Bora aende akakope hela kitaa kwa washikaji au bora mkopane humo ndani mfichiane Siri? Mie napenda ndoa ya kubebana...msaidiane. Mume amekwama elfu kumi mpe mumeo atatue shida zake ....siwez kaa ndani hata kidg
 
Sawa ila mwanamke akiwa mtiifu mpole na mwerevu inapendeza sana,na hutoskia nyumba hiyo kukiwa na visa visa,ila wewe nakufananisha na wa moyo wangu,yaani ana misimamo flani ambayo sijui ka ntawezana.
Wewe unataka mtu akutii je unajiheshimu, unajielewa are you responsible, matured enough kuheshimiwa kweli?
Ukiona unabishiwa Mambo jichunguze Mambo binafsi hata ka nakupenda ukiwa unafanya Jambo siyo na kupinga kwa nguvu zote utii wa kijinga ni hatari Sana.

[emoji23][emoji23][emoji23]Eti unanifananisha na wa moyo wako, eeeh tafta size yako, wanawake design yangu tunapenda wanaume walio timamu na waelewa maana tunapenda kuhoji kila Jambo na sio wale ndio mzee, ndio mzee
 
Huwezi amini nilitaka kumjibu Anne kuwa nahakika huyu chige hanywi pombe..hii sio akili ya pombe kbs .! Mungu akutangulie
😀😂🤣😆😂!!! Si bora basi hata ingekuwa taamu... manake wakati nipo stupid boy nilishawahi kuiba dawa ya kukohoa ya mtoto wa sista; unaambiwa ilikuwa tamu balaa!!

Ilivyoisha kutokana na mimi kuiba iba si nikajipeleka mwenyewe hospitali kujidai eti nakohoa nikidhani nami nitapewa kama dawa ya yule mtoto!

Yule daktari mtu mbaya sana, though miaka mingi sana imepita lakini sijasahau ile dawa yake aliyonipea dirishani ambayo nami bila kujua nikaibugia yoooote kwa funda moja... kumbe mkojo wa punda, na nilikuwa siijui!! Ni kama masihara but ni mkasa ambao sijausahau!!!!

Tukirudi kwenye pombe sasa! Back in the days jinsi inavyopendwa si nikadhani na yenyewe ni tamu!!! Kuja kuionja sasa.... aaaaaaaaaargh!!!!
 
Sperm collectors mtasanda tu ni mwendo wa kuwamwagia manii afu tunaeda kuoa wanawake wanaojua nafasi yao kama wanawake nyie ni makopo ya kutolea ugwadu tu m.*****
Wewe endelea kuwamwagia hao ambao mnaendana nao akili sisi smart woman hatudaganyiki tunajua kunusa Mambo mengi before even ur move, so ni ngumu Sana kutukamata tunajiamini oooh ka jike la Simba, maana tuna date kwa pleasure and we choose from the best
 
Nawe utakuwa unasumbuliwa na ushamba tu na wala si kingine!!

Ushamba unawafanya watu wadhani brutality ndio uanaume wakati huo ni ushamba tu!!

Ushamba ndo unawafanya watu waone mwanaume asiyepiga mwanamke ni dhaifu!!

Ushamba ndo unawafanya watu waone kupiga mwanamke ndo uanaume!!!

Ushamba ndo unawafanya watu wakatae kuoa wasomi eti kwa sababu "wasomi wanajifanya kujua sana"!!

Ushamba ndo unawafanya watu wadhani mwanaume anayemsikiliza wife/girlfriend wake huyo mwanaume ni dhaifu, na anapelekeshwa!!

Ushamba ndo unawafanya watu waone mwanamke akikubishia basi huyo ni jeuri hata kama ni kweli ulichofanya ni upumbavu lakini usipingwe eti kisa ni mwanaume!!!

Ushamba ndio unawafanya watu wadhani mwanamke hana sauti kwenye jamii!!

NI ushamba huu huu ndio unawafanya watu waamini wanaume ndio wanastahili kurithi na wanawake hawastahili!!!

Ushamba ndo unawafanya watu wadhani feminism ni ukorofi!!

My girlfriend or wife will always be MY BEST FRIEND!!

So, nitakuwa very stupid endapo nitataka my girlfriend or wife awe kama Msukule kwangu, anayekubali kila ninachosema au kutaka hata kama ni cha kipumbavu!!!

For me I'll feel blessed mwanamke akinikosoa, na nikiangalia nakubali kabisa kwamba she's right and I was not, kuliko unakuwa na mtu ambae mwanaume ukishatoa maamuzi hata kama ni ya kipumbavu, yanapita hivyo hivyo na kuja ku-backfire familia yako mwenyewe!!

Na nitakuwa very stupid nikianza kurusha ngumi kwa MY BEST FRIEND coz' kama alichofanya ni completely intolerable, my best option will always be to let her go, and trust me, she'll always be my best friend no matter what!!!

And guess what... am now in my 40's, lakini sijawahi kuachana na mwanamke kwa visa, and am proud of it coz' I know how to manage difficult situation!!!!

Na kama alivyosema cariha hapo juu, watu aina yenu mnasumbuliwa na insecurity and inferiority complex, na kwahiyo mnataka kutambulika kama wanaume not based on your responsibility as a man but by being physically TOO TOUGH over a woman... huo ni ushamba tu!!

I don't have to do anything stupid to prove my manhood which will always be judged based on my responsibility as a man!

Again, I love a feminist women, na sio mwanamke unayeweza kumpelekesha pelekesha tu kama msukule, na hajui hata haki zake!!

Na kama hajui haki zake, na hawezi kupigania haki zake at a family level, ni namna gani anaweza kupigania haki za familia wakati ambapo mumewe yupo kwenye mazingira yasiyomwezesha to stand for his family?!

Daah hii comment imenitoa chozi aisee
Mkuu Bwana Mungu akubariki na akuzidishie
 
Wewe unataka mtu akutii je unajiheshimu, unajielewa are you responsible, matured enough kuheshimiwa kweli?
Ukiona unabishiwa Mambo jichunguze Mambo binafsi hata ka nakupenda ukiwa unafanya Jambo siyo na kupinga kwa nguvu zote utii wa kijinga ni hatari Sana.

[emoji23][emoji23][emoji23]Eti unanifananisha na wa moyo wako, eeeh tafta size yako, wanawake design yangu tunapenda wanaume walio timamu na waelewa maana tunapenda kuhoji kila Jambo na sio wale ndio mzee, ndio mzee
Huyu saiz kabisa ndomana akijidai kuzira napiga kimya tu anakuja mwenyewe,alafu mwanamke jeur na mwenye misimamo sijui kwanini moyo ndo unamhitaji zaidi,hata chumbani dah! is so sweet.
 
Hahahaa... kwahiyo uka-scroll hadi chini, unakuta "...kumbe Kajuma Nature kenyewe ndo haka; kabaayaaaaa!"

Joke aside, binafsi huwa nashangaa izi mentality tunazitoa wapi though makuzi nayo nadhani yanachangia kwa kiasi kikubwa!! My mom, for instance, she's too tough na huwezi kumletea ujinga ujinga tu kwa kuona "...si mwanamama tu huyu, atanifanya nini", and I adore her!

Ndo maana kumbe wewe ni yai bora.kumbe Kuna mtu nyuma aliyekufanya uwe hapo ...jamani kina mama waleeni watoto wenu kwa usawa..Ila Bahati mbaya sana wanaume Kama we wanapataga wake majanga. Yaani
omba Sana Mungu akupe mke mnayeelewana!
Hakuna mwanamke hapa duniani asiyependwa kusikilizwa maoni yake na mumewe nasema hakuna .msikilize mkeo then mrekebishe. Mpe na ww idea yako fikieni conclusionpamoja ..hamtakufa kwa stress Kama mnavyodondoka Sasa hivi kwasababu ya kukifanya nyie ndo nyie...na mtakufa had mkome
 
Tatizo tuna unafiki Sana. Hivi men akiishiwa Bora aende akakope hela kitaa kwa washikaji au bora mkopane humo ndani mfichiane Siri? Mie napenda ndoa ya kubebana...msaidiane. Mume amekwama elfu kumi mpe mumeo atatue shida zake ....siwez kaa ndani hata kidg
Kwanza sikuhizi vyuma vilivobana unaenda kukopa kwa Nani akupe hela kiurahisi hivo zaidi ya kukopa penye riba kubwa Hadi ushangae.
Mapenzi ya kubebeana mzigo ni mazuri Sana mume umekwama hapa Mimi na support amount hyo inakuwa nzuri hata kwa watoto na stress zinapungua, imagine huna kitu mume Mambo yamekwama, au wanao subiri wanaume wawape kila kitu wasubirie tu Mimi siwezi
 
Pia zianzishwe movement za kuwapiga bomba "sperm banks" aka sperm collector aka makopo maana ni dhairi DNA tofauti tofauti zinavyovunda ndani mwao zinawafanya kua wendawazimu. Na ushahidi tunauona kwa huyu single mother hapa anavyobwata
Utapigaje bomba sperm kwetu wakati ndo zinatakiwa kwetu na Zina kazi nyingi mno na muhimu. Ni sawa useme watu wasishiriki Hilo tendo unafikiri population itaongezekaje Sasa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom