Kwani ni lazima Serikali kufanya miradi mikubwa wakati kuna kampuni zinaweza kukaribishwa kufanya miradi hiyo ili pesa ikatumike sehemu nyingine

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,604
8,733
Dp world ni sawa kuja kuwekeza bandarini ila kinacho fanya watu kupigia kelele ni ili la mikata mibovu ambayo kila kukicha serikali ikidondokea pua na kuishia patupu.


Kweli hipo miradi ambayo zinafanya bila serikali kama ya uchimbaji madini lakini hakuna manaufaa kwa wananchi wake wala faida kwake sijui tuseme ndani ya serikali yenye kinyogo kupitia ccm wazidi kutumia kunywe uchaguzi.

Serikali imejikuta ikiingia kwenye miradi mikubwa ambayo mwisho wa siku ushindwa na kupoteza pesa nyingi.

Ukichunguza nchi nyingi zilizofanikiwa miradi mikubwa sio ya serikali ila serikali usimamie miradi hiyo ili kulinda uchumi wa nchi yake na sheria zake.

Mfano mzuri tutajifunza kwa Dubai ambaye ni ruhusa hata kuleta mradi gani kwake ili mradi usivunje sheria.

Nchi kama Japan inayoongoza kwa usafiri mzuri wa treni ila ina makampuni binafsi yamewekeza kwenye usafiri

Je, tunashindwa nini kufungua fursa hii ili njia za usafiri kila mkoa wakafanya wao.?

Kuna makampuni makubwa ambayo ukiweka list hapa yanaweza kufanya miradi mikubwa na Serikali ikanufaika kwa wananchi wake lakini wakiendelea kufanya wao kama wao kuamini sijui vita ya uchumi wakati umakini wa mikataba usiofuatiliwa tutaishia kuwa masikini.
 
Back
Top Bottom