Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 34,629
- 59,769
Yeah most of serial killers ni wale wanaolipa visasi halafu wanajikuta wananogewa! Mmoja wakati anahojiwa alisema alikua anapenda vile Roho ya mtu inavyotoka! Na yale maneno kama don't kill me, etc!
Nakumbuka hapa kulikuwa na Dr mmoja anaitwa Shipman (UK)
Huyu jamaa alikuwa kwenye kitongoji kimoja akiwa na zahanati yake alipoanza kuuwa mmoja akanogewa akawa anawadunga sindano za sumu wazee huku akiwaangalia roho inavyotoka anaona raha
Unaweza kumsoma Dr Shipman
Alikuja kugundulika baada ya kugushi saini ya bibi kizee mmoja wa miaka zaidi ya 90 kuwa kamuachia urithi wa hela nyingi sana na nyumba
Lakini mtoto wa huyo mama ambae nae alikuwa na miaka kama 70 alikataa katu hiyo hoja na kusema haiwezekani mama yake kumrithisha kwani yeye ndio alikuwa anamtunza miaka yote na hakuwahi kuongelea mirathi
Ndipo siani ikaenda kuchunguzwa na mtaalamu mmoja akabaini imegushiwa
Hapo ikabidi wafukue kaburi kuona kwa uchunguzi
Wakabaini sumu
Ikawapelekea wafukue tena makaburi mengine
Walipofikisha 25 na zote zina sumu akahukumiwa kwa hizo 25 ingawa walisitisha maana inasemekana aliuwa zaidi ya 100
Mwingine anaitwa Fred West huyo nae alikuwa balaa wakishirikiana na mke wake
Walianza na mtoto wao wa kike na kumzika kwenye ukuta
Mauwaji yaliendelea sana kwa kualika watu nyumbani kwao na kuwauwa
Wengi wanaouwawa ni malaya ambao hata ndugu kuwatafuta inakuwa vigumu kwa kazi yao ilivyo
Malaya akifa ndugu ni vigumu kujua kwani wanajua yuko na mambo yake hata wenzake wanaona labda kapata buzi limempeleka mji mwingine
Dunia Ina mambo hii
Sent from my iPhone using Tapatalk