Kwa wapenzi wa mambo ya mauaji tu

Interesting
Albert Fish.

Edward Budd aliweka tangazo kwenye gazeti kua anatafuta kazi. Akataja anwani aliyopo na kwamba yupo radhi kufanya kazi kokote. Baada ya muda wakapokea mgeni, Albert Fish.

Muonekano wa kitajiri, umri umesogea kidogo, nywele zenye mvi, nadhifu na alitembea na pesa nyingi mfukoni. Usingeweza wazia kingine.

Akakaribishwa ndani akaeleza kua ameona tangazo na amekuja kukutana na kijana mwenyewe, Edward akaitwa, akaja ila alikua na kijana mwingine, Willie. Albert akasema amependa kama angeweza kuondoka nao wote.

Akakubaliwa.

Wakawa wamekaa wanapiga stori akiwaelezea maisha ya mjini. Stori zikiwa zinaendelea akaingia binti wa miaka 10, ilikua Jumapili Gracie alikua akitokea kanisani. Kumuona tu Albert akatoa pesa na kumtania "Hesabu nikuone" Gracie akahesabu na kumtajia kiasi sahihi, Albert akampa pesa akamwambia akanunue pipi.

Kisha akawapa pesa kidogo Edward na Willie. Akaomba udhuru kwa wazazi wao akisema anaenda kwenye birthday ya mtoto wa dada yake siyo mbali na hapo, sherehe ikiisha angewapitia Edward na Willie na kuondoka nao.

Wazazi wakakubali.

Albert akapendekeza aende na Gracie.

Wazazi wakakubali.

Wakataka wambadilishe nguo angalau akalingane na wenzake huko kwenye sherehe. Albert akasema yupo sawa hivyo alivyo wasitie shaka hivyo wao wanaenda.

Wakaondoka. Muda ukayoyoma si Albert wala Gracie aliyerudi. Wakaifuata anwani aliyowatajia hawakukuta jengo na ilkua ni anwani feki, badala yake walikuta pagale.
Kwa maelezo ya Albert ni kwamba huo muda alimpotezesha fahamu Gracie kisha akamficha humo yeye akaenda matembezini akitarajia arudi usiku aondoke naye.

Lakini waliomtafuta Gracie pengine walikua na kihoro hata hawakuingia kwenye lile pagale.

Hiyo ikawa Jumapili ya mwisho ya wazazi, na kaka zake Willie na Edward kumuona Gracie. Hawakuweza muona hata akiwa mfu kwakua Albert alimla Gracie.

Familia ya Gracie ikapokea barua. Barua ilitoka kwa Albert Fish, safari hii alitaja jina lake la kweli na akaelezea tukio zima kuanzia kumuacha Gracie kwenye pagale kumrudia usiku na kwenda naye kwake. Hakuacha kitu. Alielezea ni jinsi gani alimkata vipande vidogo vidogo kumpika na kumla, anadai alikula mwili wa Gracie kwa zaidi ya siku 10.

Hii barua ikafikishwa polisi. Ikaanza kufuatiliwa ilipotokea, ikaja kukutwa orijin yake ni huko mjini wakajikuta ana kwa ana na kijana wa kiume ambaye akakiri kua ni kweli ile anwani ni yake lakini hajawahi kuandika barua na kuituma kwenda kwa anwani ya Budd.

Hii inamaanisha ili kumkamata ilitakiwa atume tena barua ila safari hii ofisi za posta ziwe na maafisa watakaokua wakiangalia kila anayetuma barua. Tatizo likawa vipi kama asipotuma tena? Ingekua anwani ni ya kweli wangeweza kumtumia na yeye ili aijibu ila haiko hivyo, so what next?

Kitu kimoja kuhusu serial killers hua wanajihisi wao ni miungu, wanatamani kusujudiwa, kuonyeshwa kua umuhimu wao ni mkubwa. Hivyo ukiweza kucheza na akili ya muuaji wa aina hii una % nzuri za kumkamata.

Maaskari wakaipublish barua kwenye gazeti kisha wakasema kila kilichokua mule ni uongo mtupu, wakasema kua rangi ya gauni iliyotajwa mule ni uongo, ni uongo pia kwamba Albert Fish alikua ndiye kinara ile siku yupo kwa Kina Gracie. Wakasema alikua ni mzee muoga, dhaifu ambaye hakuonyesha kuana nguvu.

Kilichofuaa ITV? Albert akatuma tena barua, tena safari hii akawatumia na polisi, shenzi kabisa mnasema mi muongo? Hahaha hiyo sehemu ya tusi nimetunga.

Anyway, akawa amejitia kitanzini. Ile barua ya kwanza na ya pili ilielezea mauaji kinaga ubaga kiasi ilikua na details ambazo ni muuaji tu angeweza kuzijua.

.....ok sikumbuki vizuri kama alikutwa na hatia au walisema kua jamaa ni insane but there is that.
 
Kwa wale wapenzi wanaopenda kufuatilia visa vya mauwaji, uchunguzi hadi kupatikana kwa Wauthumiwa karibuni tu-share na kufurahi pamoja. we learn something out of this. Hii noi mauwaji tu na theories zake.

Binafsi napenda sana kufuatilia hizi issues hasa kwa wale wanaofuatilia "serial killers'. Hapa unajifunza sababu zinazopelekea mtu kuwa serial killer, anaanzaje, anakuaje, anapata hamu gani ya kuendelea kuuwa, adhabu wanazopewa na maneno ya mwisho wakati wananyongwa.

Lengo ni kujifunza jinsi ya kujilinda na sio kujifunza kuuwa!! Asanteni
Every crime has a motive, Blood murders, True Crime, Blood relatives, Swamp murders, .... ugonjwa wangu
 
Every crime has a motive, Blood murders, True Crime, Blood relatives, Swamp murders, .... ugonjwa wangu
Tupia hapa jukwani, Napenda sana ila Last Wordsa of Serial Killers! Napenda sana jamaa aliwauwa wanawake karibia kumi na tano makahaba! Alikua ana deal na wanawake tu. Kumbe aliwahi kuzinguliwa
 
Tupia hapa jukwani, Napenda sana ila Last Wordsa of Serial Killers! Napenda sana jamaa aliwauwa wanawake karibia kumi na tano makahaba! Alikua ana deal na wanawake tu. Kumbe aliwahi kuzinguliwa
Napenda FBI profiling jinsi wanavyoweza kujua serial killer ni mtu wa namna gani mfano kuna jamaa alikua anaua kila mwaka aliwasumbua sana polis marekan kwa zaidi ya miaka kumi FBI waliwambia atakuwa mtu mwenye familia mpole na anapendwa na kuheshimikana jamii na walipomkamata alikuwa sawa na walivyosema
 
Napenda FBI profiling jinsi wanavyoweza kujua serial killer ni mtu wa namna gani mfano kuna jamaa alikua anaua kila mwaka aliwasumbua sana polis marekan kwa zaidi ya miaka kumi FBI waliwambia atakuwa mtu mwenye familia mpole na anapendwa na kuheshimikana jamii na walipomkamata alikuwa sawa na walivyosema
Dah yule mmoja yeye alikua na silaha yenye Silencer na alikua akiwauwa kutokea kwenye gari yake! Ukizoea hizi mambo zina utamu Wake.

Sasa hivi inayotamba ni ile ya The Mind of the Murderer
 
Back
Top Bottom