Mzungu wa Meli
JF-Expert Member
- Dec 23, 2018
- 215
- 273
Unarudi lini mkuuKuna wimbo unaitwa 6 foot 7 foot wa Lil Wayne kamshirikisha Corey Gunz. Corey Gunz katika vesi yake anasema '... Son of Sam, Son of Gun, you niggaz are sons of me...'
Son of Sam ni jamaa anaitwa David Berkowitz au .44 Caliber Killer. Katika barua alizotuma kwa wahanga, polisi na hata majirani zake David anasema kua Sam ni pepo na yeye ndiye anatakiwa kulilisha damu.
Baadaye alipata kusema kua alijihisi yeye ni askari wa ibilisi na jukumu lake ni kumpa damu. Anasema pia kelele za mbwa waliobweka usiku kucha na kumkosesha usingizi ulikua ni wito wa ibilisi kumtaka atimize majukumu yake ya kiaskari.
Hayo tutaongelea baadaye, saa hii tumuongelee mtu ambaye alishambulia watu (wanawake zaidi) zaidi ya 13 akaua 6 na kuwaacha wengine 7 wakiwa na makovu ya milele.
Wahanga wake wa kwanza waliojulikana ni Donna na Jody. These ladies wakiwa ndani ya gari wakiagana kabla Donna hajaingia ndani kwao David akatokea mbele yao na kuanza kupiga risasi, Donna ikampata ya shingo Jody ikampata ya mapajani.
Hata baada ya risasi 5 kuisha David aliendelea kubonyeza trigger, muda wote Jody analia kuomba msaada, baba Donna alipotoka nje hakumkuta mhusika isipokua maiti ya mwanae.
Wiki 3 mbele akashambulia mtu na mpenzi wake, hapa hakufa mtu ila mwanaume ambaye alitakiwa ajiunge na jeshi akabakishwa na ulemavu na jeshi likaishia hapo.
Wakaja marafiki wawili, wanawake, wakiwa wanatembea kurudi nyumbani David akawatokea kwa nyuma. Walipoamua kuongeza mwendo David akachomoa .44 caliber magnum akashuti, mmoja risasi ikapita pembeni kidogo ya uti wa mgongo, she was lucky, mwingine risasi ilivunja uti wa mgongo wote so she will live ila kwa kupooza milele.
Kisha Captain Borell akapokea barua hapo akajitambulisha yeye ni nani. Ingawa mwandiko ulikua mbaya na misspelling nyingi mfano Your badala ya You are na wemon badala ya women ila Borell aliielewa.
Akaelewa kua New York inadeal na kesi mpya ya psychopath, a cold blood killer who will strike again. So akaunda kikosi kazi alichokipa mission aliyoiita Operation Omega, kikosi kazi kikaitwa Omega Task Force. Wapelelezi wakakusanywa wakawekwa humo ili kumnasa David. Na wakajitoa haswa kwakua ilishafikia hatua kesi ya David ikawa ni ya kukupandisha cheo.
Kisha barua ikaenda kwa Cassara ikionyesha inatoka kwa Carr ikimtakia afya njema. Cassara akawasiliana na Carr, watu hawa hawakua wakijuana, Carr akataka waonane wajadili hiyo barua kwakua na yeye kuna barua kapokea. Isipokua yake ilizungumzia mbwa wake kushutiwa.
Mtoto wa Cassara akamtaja David mpangaji wao wa zamani ambaye alichukia mbwa anavyobweka.
Narudi...
Sent using Jamii Forums mobile app