Kwa wapenzi wa mambo ya mauaji tu

Kwa wapenzi wa mambo ya mauaji tu

Hawa jamaa wana roho nzuri sana, kwa huku Africa ni kama wale wachawi wanaotuchukuaga misukule na kwenda kututesa bila ya wao kufaidika na chochote.
Hahahaha Mkuu nimecheka kwa sauti hadi abiria hapa kastuka, alidhani nacheka wigi lake
 
Huu uzi hata nami nilisoma, jina tu limenitoka..
Yap ishu za mauaji zilizofanywa kwa weledi especially majasusi, nadhani ndio kusudio lako

Kuna siku nilisoma bandiko fulani hapa jf sikumbuki alipost nani, ila nililipenda. Lilikua linausu mjasusi kutoka CIA aliyejiengua na ujasusi. Alikutwa amekufa akiwa yupo ndani ya begi lililofungwa kwa zipu za ndani ya hilo begi.

Security camera hazikuweza kunasa tukio lolote likionesha ni namna gani aliweza kuingia mle kwenye begi wala hakukua na alama za fingerprint zenye kuonesha nani aliyemuingiza kwenye begi.

Daktari mmoja ambaye alikua anamwili sawa na yule marehemu alijaribu kuingia kwenye lile begi huku akisaidiana na wenzake lakini hakuweza kuenea, jambo ambalo liliwaacha watu mdomo wazi

Ni mauaji ambayo mpaka sasa hayajatafutiwa suluhu kua nini kilichomuua haswa yule victim. Vipimo vyote vilichukuliwa ili kubaini nini kilichosababisha afe lakini hola. Mwili ulipimwa ili kubaini kua pengine alikufa kwa kuishiwa pumzi lakini hola, walicheki mwili kama unasumu yeyote ile lakini hawakukuta na tatizo lolote lile kwenye mwili ule ambalo ingewasaidia kujua nini sababu ya kifo cha huyo jasusi



Sent using unknown device

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Albert Fish.

Edward Budd aliweka tangazo kwenye gazeti kua anatafuta kazi. Akataja anwani aliyopo na kwamba yupo radhi kufanya kazi kokote. Baada ya muda wakapokea mgeni, Albert Fish.

Muonekano wa kitajiri, umri umesogea kidogo, nywele zenye mvi, nadhifu na alitembea na pesa nyingi mfukoni. Usingeweza wazia kingine.

Akakaribishwa ndani akaeleza kua ameona tangazo na amekuja kukutana na kijana mwenyewe, Edward akaitwa, akaja ila alikua na kijana mwingine, Willie. Albert akasema amependa kama angeweza kuondoka nao wote.

Akakubaliwa.

Wakawa wamekaa wanapiga stori akiwaelezea maisha ya mjini. Stori zikiwa zinaendelea akaingia binti wa miaka 10, ilikua Jumapili Gracie alikua akitokea kanisani. Kumuona tu Albert akatoa pesa na kumtania "Hesabu nikuone" Gracie akahesabu na kumtajia kiasi sahihi, Albert akampa pesa akamwambia akanunue pipi.

Kisha akawapa pesa kidogo Edward na Willie. Akaomba udhuru kwa wazazi wao akisema anaenda kwenye birthday ya mtoto wa dada yake siyo mbali na hapo, sherehe ikiisha angewapitia Edward na Willie na kuondoka nao.

Wazazi wakakubali.

Albert akapendekeza aende na Gracie.

Wazazi wakakubali.

Wakataka wambadilishe nguo angalau akalingane na wenzake huko kwenye sherehe. Albert akasema yupo sawa hivyo alivyo wasitie shaka hivyo wao wanaenda.

Wakaondoka. Muda ukayoyoma si Albert wala Gracie aliyerudi. Wakaifuata anwani aliyowatajia hawakukuta jengo na ilkua ni anwani feki, badala yake walikuta pagale.
Kwa maelezo ya Albert ni kwamba huo muda alimpotezesha fahamu Gracie kisha akamficha humo yeye akaenda matembezini akitarajia arudi usiku aondoke naye.

Lakini waliomtafuta Gracie pengine walikua na kihoro hata hawakuingia kwenye lile pagale.

Hiyo ikawa Jumapili ya mwisho ya wazazi, na kaka zake Willie na Edward kumuona Gracie. Hawakuweza muona hata akiwa mfu kwakua Albert alimla Gracie.

Familia ya Gracie ikapokea barua. Barua ilitoka kwa Albert Fish, safari hii alitaja jina lake la kweli na akaelezea tukio zima kuanzia kumuacha Gracie kwenye pagale kumrudia usiku na kwenda naye kwake. Hakuacha kitu. Alielezea ni jinsi gani alimkata vipande vidogo vidogo kumpika na kumla, anadai alikula mwili wa Gracie kwa zaidi ya siku 10.

Hii barua ikafikishwa polisi. Ikaanza kufuatiliwa ilipotokea, ikaja kukutwa orijin yake ni huko mjini wakajikuta ana kwa ana na kijana wa kiume ambaye akakiri kua ni kweli ile anwani ni yake lakini hajawahi kuandika barua na kuituma kwenda kwa anwani ya Budd.

Hii inamaanisha ili kumkamata ilitakiwa atume tena barua ila safari hii ofisi za posta ziwe na maafisa watakaokua wakiangalia kila anayetuma barua. Tatizo likawa vipi kama asipotuma tena? Ingekua anwani ni ya kweli wangeweza kumtumia na yeye ili aijibu ila haiko hivyo, so what next?

Kitu kimoja kuhusu serial killers hua wanajihisi wao ni miungu, wanatamani kusujudiwa, kuonyeshwa kua umuhimu wao ni mkubwa. Hivyo ukiweza kucheza na akili ya muuaji wa aina hii una % nzuri za kumkamata.

Maaskari wakaipublish barua kwenye gazeti kisha wakasema kila kilichokua mule ni uongo mtupu, wakasema kua rangi ya gauni iliyotajwa mule ni uongo, ni uongo pia kwamba Albert Fish alikua ndiye kinara ile siku yupo kwa Kina Gracie. Wakasema alikua ni mzee muoga, dhaifu ambaye hakuonyesha kuana nguvu.

Kilichofuaa ITV? Albert akatuma tena barua, tena safari hii akawatumia na polisi, shenzi kabisa mnasema mi muongo? Hahaha hiyo sehemu ya tusi nimetunga.

Anyway, akawa amejitia kitanzini. Ile barua ya kwanza na ya pili ilielezea mauaji kinaga ubaga kiasi ilikua na details ambazo ni muuaji tu angeweza kuzijua.

.....ok sikumbuki vizuri kama alikutwa na hatia au walisema kua jamaa ni insane but there is that.
Electric chair ilimuhusu huyu mshenzi, kwa maelezo yake mwenyewe alidai aliwafanyia ushenzi zaidi ya watoto 100.
 
Duuu........ Nimepitia uzi nimestaajabu sn kusikia kua kuua ni Hobbie kwa baadhi ya watu hasa hawa serial killers......
Ila nimeburudika na kuelimika na visa mbali bali very interesting.....
 
Duuu........ Nimepitia uzi nimestaajabu sn kusikia kua kuua ni Hobbie kwa baadhi ya watu hasa hawa serial killers......
Ila nimeburudika na kuelimika na visa mbali bali very interesting.....
Hahahahaha that's life Mpwa
 
Najua wengi. Wengine hadi nimewasahau majina kwakua nilikua nawasoma stori zao kwenye website moja hivi ambayo imefungiwa nahisi tangu 2015. Ilikua inaitwa Tru Tv Crime Library.

Kuna Ted Bundy. Mwanasheria mtanashati aliyeachwa na mpenzi wake, akiwa na huo msongo akaanza kuua wanawake ambao walifanana na mpenzi wake.

Wahanga wake walikua ni wanawake waliofanana maumbo, nywele na wengine mpaka macho. Kuanzia mwaka 1974 mpaka 1978 Ted Bundy alizunguka majimbo saba ya Marekani akitimiza nia yake ovu kwa kila mwenye bahati mbaya ya kumuamini.

Nani asingemwamini? Mwanasheria mtanashati, mkono mmoja una POP (Hogo) anakuomba binti umsaidie kubeba vitabu kuviingiza kwenye gari. Kimojawapo kitakusukuma uende kama siyo utanashati basi ni roho ya huruma.

Kwa mbinu hii alinasa wengi. Yeye anasema ameua wanawake 30, lakini ripoti nyingine zinasema inaweza kua zaidi, nyingine zimesema wahanga ni 50 lakini ripoti rasmi haijathibitisha idadi yake. Hii inamaanisha wahanga wanaweza kua wengi kuliko alivyojitahidi kukumbuka.

Kwake kuua ilikua ni namna ya kulipiza kutendwa. Baadaye hali ikawa mbaya akawa akiua anakaa na maiti zaidi ya wiki akiziingilia, akipiga punyeto na kuzimwagia, ilimridhisha kwakua alijiona yeye ni mmiliki wa huu mwili ambao ataamua aufanye nini na muda gani. Ted akawa amenasa kwenye 'necrophilia' yaani kupenda kufanya mapenzi au kuvutiwa kimapenzi na maiti.

Mhanga wa kwanza mara nyingi humsumbua muuaji, hujikuta anaoverkill au kutumia njia nyingi baada ya muda hufuzu, huweza jua wapi akigusa ataua kwa haraka. Ted alijiamini, idadi kubwa ya wahanga ilimaanisha ameexcel kumdhibiti mtu, especially mwanamke, lakini hapana. Siku nyingine tena kama kawaida Ted akiwa na P.O.P feki akamuomba mdada amsaidie kuingiza vitabu kwenye gari.

Mdada akakubali wakiwa kwenye gari Ted akampiga na chuma kichwani, binti akaonekana kuzimia gari likawashwa safari ikaanza. Kati kati ya safari binti akazinduka na kufungua mlango akajitupa nje. Huyu ni mhanga pekee aliyepona kutokea mikononi kwa Ted (Nimemsahau jina)

Akaja akakamatwa. Akafunguliwa mashtaka, akaomba awe anajiwakilisha mwenyewe kwakua na yeye ni wakili. Hii ilimaanisha apewe muda wa kwenda maktaba kupitia kesi zingine, ila hii pia ilimaanisha anaweza kutoroka.

Hivyo akatoroka.

Akakamatwa tena. Safari hii ulinzi ukaimarishwa, Ted akiwa anajitetea ilimaanisha anatakiwa aji-cross examine. Hivyo muda wa kuji-cross examine ulipofika Ted akawa anatumia sauti mbili.

Moja ndogo ndogo ya yeye kama upande wa utetezi na nyingine yenye mamlaka kama wakili. Isingeweza saidia, hii iliwadhihirishia wazee wa baraza kua huyu mtu hayupo sawa kichwani, ingawa hata yeye alitaka aachiwe kwa kuonekana hayupo sawa kichwani.

Mbinu yake ikagonga mwamba Ted akahukumiwa kifo.

Nimesahau vitu vingi, nahisi alitoroka mara mbili ila sikumbuki sawasawa.
Ted bundy alihukumiwa kifo cha umeme.

Siku ya hukumu ilipofika alikuwa anatia huruma na akaonyesha kuwa na hofu na kukosa amani kabisa ni kama hakuwa akiamini siku yake imefika. Wakati ulipofika maofisa wa kutoa hukumu walimuingiza chumba cha hukumu, akatolewa nguo za jela, askari wakamuingiza pamba eneo la njia ya haja kubwa kwa kuzisokomeza na kuzisindikiza na fimbo ili kuzuia asije kukata gogo na kuchafua hali ya hewa balaa likianza.

Alikuwa akilia kama mtoto mdogo, akafungwa katika kiti cha umeme na kuvalishwa mikanda ya kuzuia asitoke katika hicho kiti. Alikamuliwa maji sehemu zote ambapo umeme utashikishwa mwilini pake ikiwamo kichwani alipokuwa amenyolewa kipara kwa sasa ili akivalishwa kofia ya kiti kile cha umeme, kiweze kumcharaza shoti vema kabisa, akapewa nafasi ya maneno ya mwisho, na padre kumuombea kisha huku ikaanza, akachapwa shoti hadi kufa na mzoga wake ukatolewa kwaajiri ya maziko.

images%20(9).jpeg
images%20(10).jpeg
images%20(11).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ted bundy alihukumiwa kifo cha umeme.

Siku ya hukumu ilipofika alikuwa anatia huruma na akaonyesha kuwa na hofu na kukosa amani kabisa ni kama hakuwa akiamini siku yake imefika. Wakati ulipofika maofisa wa kutoa hukumu walimuingiza chumba cha hukumu, akatolewa nguo za jela, askari wakamuingiza pamba eneo la njia ya haja kubwa kwa kuzisokomeza na kuzisindikiza na fimbo ili kuzuia asije kukata gogo na kuchafua hali ya hewa balaa likianza.

Alikuwa akilia kama mtoto mdogo, akafungwa katika kiti cha umeme na kuvalishwa mikanda ya kuzuia asitoke katika hicho kiti. Alikamuliwa maji sehemu zote ambapo umeme utashikishwa mwilini pake ikiwamo kichwani alipokuwa amenyolewa kipara kwa sasa ili akivalishwa kofia ya kiti kile cha umeme, kiweze kumcharaza shoti vema kabisa, akapewa nafasi ya maneno ya mwisho, na padre kumuombea kisha huku ikaanza, akachapwa shoti hadi kufa na mzoga wake ukatolewa kwaajiri ya maziko.

View attachment 1418794View attachment 1418795View attachment 1418796

Sent using Jamii Forums mobile app
Wonderful narration! Asante kwa picha na taarifa kamili
 
Now Jack hana hata death toll kubwa. Ana wahanga watatu kama sikosei ila umaarufu wake ni kwavile ilikua jambo geni wa UK, wengine maarufu kwa haraka haraka ni Ed Gein, naye hana hata death toll kubwa ila kuna hadi movie ilitengenezwa kutokana na tukio lake. Kuna Jefrey Dahmer, John Wayne Gacy, Long River Ripper, hapa palitakiwa pawe sehemu ukiingia huchoki kusoma visa ila ndo vile.

Kweli kabisa
Na haya mauwaji wengi ni States na ndiko wanaouwa zaidi
Wote uliowataja nimewapitia kidogo ni balaa hao



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Nimeanza kupenda kufanya mauaji ghafla,.

Nahisi kama kuna pepo limeniingia baada ya kusoma huu uzi.

Msaada plz naona nashindwa kujizuia
(sijui kama siku ya leo itapita salama kwangu)
Hahaha kapimwe corona Mpwa! Itakua imekupanda kichwani
 
Back
Top Bottom