baloziwamitaa_
Member
- Aug 21, 2018
- 32
- 27
Takribani miaka 30 ya muziki wa Bongofleva, imekuwa wazi kwamba muziki, maisha na safari huenda sambamba. Nyimbo hutengeneza kumbukumbu za kipekee zinazohusishwa na maeneo, hali ya hewa, mandhari na matukio tuliyokutana nayo safarini. Zinapounganishwa na hisia zetu za kuona na kunusa, huacha alama ya kipekee akilini mwetu — kama vile alama za vidole.
Kama huamini, jaribu kukumbuka mojawapo ya nyimbo unazozipenda. Mara moja, akili yako itakurudisha mahali ulipoisikia kwa mara ya kwanza, mazingira yaliyokuzunguka, au hisia ulizokuwa nazo wakati huo. Hivyo ndivyo ubongo wetu unavyounganisha muziki na kumbukumbu.
Na hapo ndipo lengo la orodha hii linapoanzia.
Hizi ni nyimbo tano zinazobeba hisia za kusafiri au nguvu za kipekee zinazoweza kuwa sauti ya safari zetu — iwe ni safari halisi au safari ya maisha. Zinaufanya uzoefu wetu kuwa wa kina zaidi na kukamilisha muunganiko wa wewe, muziki na safari.
1. Darassa — Usikate Tamaa (Ft. Ben Paul)
Kama kuna wimbo unaokupa hisia za kutembea kwa kujiamini katikati ya jiji lenye pilikapilika bila kujali chochote, basi ni huu. Katika video yake, Darassa anatembea barabarani na kikundi cha watu akipita bila kujali huku akiimba:
“Tembea ujionee, Dunia imebeba Mengi
Tamaa sio kizazi, mzazi wivu haujengi
Kila siku tuko mtaani sio good life hatupendi
Sina mi nakaa siwezagi kujipretendi
Stay true be real daima nita stay real
Mitaa inajua nigekuwa nani kama mziki usingekuwa deal
I’m ill life ishanipotezeaga akili
Kwenu neighbour wanagombana
Kwetu killer got killed…”
Wimbo huu unaelezea maisha kama tamthilia yenye uchungu na utamu. Tunahangaika kutafuta riziki, tunakuwa watumwa wa pesa, halafu siku moja maisha yanaisha.
Lakini pia una ujumbe wa kufuata njia ambayo moyo wako unakuonyesha. Na kutokana na ujasiri anaouonyesha kwenye video, inaonekana ameridhika na safari yake ya maisha.
2. Appy — Watu Feki
Filamu za madawa ya kulevya ni kazi za kipekee na mara nyingi hazipati sifa inayostahili. Gomorrah ni filamu ya Italia, iliyoongozwa na Matteo Garrone inasemekana inatokea katika kitabu cha ukweli (non-fiction) kilichoandikwa na mwandishi Roberto Saviano, ambaye alifichua siri za shirika la uhalifu la Camorra — genge kubwa la mafia huko Naples na Caserta, kusini mwa Italia. Binafsi nimeiangalia series ya Gomorrah mwaka 2023 nikiwa kwenye duka langu la mangi ambako kuna rafiki yangu nilimlengesha akapata fremu inayofuata karibu yangu.
Kipindi nyimbo hii inatoka tulikuwa na ugomvi mkubwa na mshikaji wangu niliyemleta kashirikiana na majirani zangu wakinituhumu mchawi napata wateja mimi tu wenyewe hawauzi. Ujumbe wake ni rahisi lakini mzito:
Shukrani ya Mapunda Mateke. Wahusika wakuu ni Genny na Ciro kwenye muvi ya Gomorrah, Ciro alikuwa mentor wake Genny. Lakini mwisho wa siku wote wawili wanataka kuonyesha kuwa nani mfalme wa eneo hilo. Yaani mtu umempambania ukamfundisha biashara na namna ya kutengeneza fedha halafu anaungana na washindani wako. Siku moja niliamua liwalo na liwe nikaweka wimbo huu wa appy kwenye repeat asubuhi mpaka jioni.
Ilikuwa kila ninapokuja kufungua duka kama sijaanza nao namaliza nao kwa kuurudia sana, hadi mshikaji wangu alijishtukia akaja kuniomba msamaha. Kila nikiusikia huu wimbo huwa namkumbuka na ninakumbuka sehemu ile, maisha ya kuangalia sana muvi za madawa ya kulevya unaiba mbinu za kibiashara, jinsi ya kusovu migogoro, wizi wa reja reja na vitu kama hivyo.
3. Jah Prayzah — Mandionei
Huu ni wimbo wa lugha ya Kishona. Kama hujawahi kusikiliza muziki wa lugha hiyo, basi huu ni mwanzo mzuri sana.
“Kana muchi mhanya masara sei?
Kama wewe ni mwepesi vipi umeachwa nyuma?
Mamirirei?
Umeacha nini? / Kwa nini umesimama?
Kundishora mandionei?
Unanikosoa, umeona nini kwangu?
Mmm mandionei?
Mmm umeona nini kwangu?
Zvamunoreva zvinondipei?
Unachosema kinanipa nini?
Chamakandi vengera ndakaiteiko?
Unanichukia, lakini nimefanya nini?
Munongo nongedza pandiri sei?
Unaonyesha kila mahali ninapoenda?
Mmm mandionei?
Mmm umeona nini kwangu?
Zvamunoreva zvinondipei?
Unachosema kinanipa nini?
Chamakandi vengera ndakaiteiko?
Unanichukia, lakini nimefanya nini?
Munongo nongedza pandiri sei?
Unaonyesha kila mahali ninapoenda?
Mmm mandionei…!?
Mmm umeona nini kwangu…!?”
Nilipomsikia kwa mara ya kwanza Jah Prayzah ilikuwa mwaka 2016 wakati anashirikiana na Diamond Platnumz kwenye wimbo wa Watora Mari, nyimbo za Jah Prayzah zimekuwa sehemu ya kila orodha yangu ya nyimbo za safari.
Mandionei ni wimbo wa kwanza kwa mwaka 2025 wa msanii huyu wa Zimbabwe, Jah PrayZah. Wimbo huu ni Afrobeats wenye hisia za kutafakarisha, unaozungumzia kukosolewa na watu ambao pengine hawana cha kukuzidi, muda mwingine wamepoteana kwa upande wao na kusahau asili yao. Aina ya watu ambao wanataka kushirikiana na wewe kwa faida zao binafsi tu, huku wakikuonea wivu.
Muziki uliotumika kwenye huu wimbo una uwezo wa kugusa hisia kwa namna ya pekee kila unapokuwa safarini. Ala inayotumika kwenye sehemu kuu ya wimbo huamsha kumbukumbu za zamani na hisia za kupambana no matter what.
4. Benpaul — Jikubali
“ Unaweza kuwa doctor, unaweza kuwa Star
Unataka kuwa Linah, unaweza kuwa shaa
Kipaji mali yako, elimu ngao yako
Usiache jambo kati kwenye maisha yako
Unaweza kuwa Diamond, unaweza kuwa Jay
Unaweza kuwa JB, unaweza kuwa Ray
Mi nakuasa it’s your time
Huwezi kuwa chini you’ve got somethin’ special
Unampenda Lady Jay dee unamzimia Zitto
Trust me iko siku utatimiza ndoto yako
You can be a Boss, you can be a lawyer
You can be the President
You’ll be successful…”
Huu ni mojawapo ya nyimbo maarufu zaidi za Insipiration.
Kuanzia vesi ya kwanza tu, unapata hamu ya kuondoka na kwenda kutafuta mishemishe yako mwenyewe ya kujitegemea.
Ni wimbo unaofaa sana unapokuwa unaendesha gari kwenye barabara ndefu yenye ukimya, huku pande zote kukiwa na mandhari ya wazi.
Na bila shaka, kiitikio chake cha:
“ Wakati wako ndio leo (leo)
Kutimiza malengo yako
Nakusihi Anza sasa (sasa)
Jishughulishe utapata
Wakati wako ndio leo (leo)
Kutimiza malengo yako
Nakusihi anza sasa (sasa)
Jishughulishe utapata…”
Ni sehemu ambayo kila mtu hujikuta akiimba kwa hisia huku akikunja ngumi.
5. Kala Jeremiah — America (Ft. Zest)
“ Usinifuate, acha!
Mi nataka kwenda America, acha!
Mi nataka kwenda usinifuate, acha!
Mi nataka kwenda America, acha!
Mi nataka kwenda…”
Huu ni mmoja wa nyimbo zenye kiitikio kinachogusa hisia kwa nguvu sana.
Kila ninapousikia, hunifanya nijisikie mwenye furaha na huzuni kwa wakati mmoja — hisia ambazo ni vigumu kuzielezea. Mfano, kuna hisia umekaa kitambo sana hujarudi nyumbani — miaka miwili mitatu hujarudi unakuwa unashauku ya Kwenda. Yeyote atakayetaka kukwambia usiende ni kama unamjibu kama Zest kwenye wimbo huu acha!.
Ukiwa safarini, kuna muda hisia zinakuja kana kwamba hakuna sababu ya msingi kwenda wakati huo, unaweza geuza ukaahirisha usipokuwa makini. Athari ya huu wimbo ndio huwa naiyona hapo, nasema moyoni acha!….Nataka Kwenda America!! (Nikimaanisha Nyumbani moyoni). Muziki unakupeleka mahali pengine kabisa na kuifanya safari yako iwe ya kukumbukwa milele.
Hitimisho
Nyimbo hizi zimevuka mipaka ya aina zao za muziki na maana zake za kawaida.
Zinapounganishwa na safari na matukio ya maisha, zinapata maana mpya kabisa. Zinazifanya safari zetu kuwa za kipekee, zinatupa mtazamo mpya wa maisha na kubadilisha kumbukumbu nzuri kuwa hazina ya milele.
P.S. Wakati mwingine wimbo uliodhani ni wa kawaida au umezoeleka unaweza kuwa wimbo unaobadilisha maisha yako.
Ndivyo ilivyokuwa kwa “Nilipe” ya Click Master, ambayo imepata umaarufu kwa sababu huyu jamaa hatengenezi muziki wa kufikiria sana. Anatambua kuwa siri ya Bongo Flava ya kweli ipo mtaani. Kwa kuchanganya mirindimo ya beat inayochochea nishati ya mwili, na mashairi ya kawaida yanayogusa mifuko, madeni, na tabia za watu wetu wa kila siku, anakuwa sio msanii tu, bali ni msemaji wa burudani wa mwananchi wa kawaida. “Sherehe” ni uthibitisho tosha kuwa vibe lake bado liko juu!
P.S. Kama umefurahia makala hii au umejifunza jambo jipya, usisite kusema chochote — ningependa kusikia mtazamo wako
Nifuatilie pia instagram ili kuunga mkono kazi yangu, na MEDIUM kama umefurahia makala hii.
Uwe na siku njema.
Mungu akubari