Ndiyo hivyo mwaya! Sifa na Utukufu apewe Bwana! Unajua nimekuwa nikitafali Neno la Mungu pale palipoandikwa "Mume na Mke wasiachane isipokuwa Kwa Habari ya Uasherati " nikaelewa Mungu ni Mkuu sana, alijua kuna nyakati Kama hizi kutakuwa na magonjwa yasiyo na tiba wala kinga ambayo Kwa sehemu kubwa hupatikana kupitia Uasherati , Kwa hiyo Mungu ikabidi aingilie kati aruhusu Talaka pale tu itakapothibitika pasina Shaka kuwa mmoja wa wana ndoa Au wote wamefanya uasherati hapo Talaka ruksa! Sasa nimekuwa nikiwauliza wachungaji wachache Kwenye semina mbalimbali za ndoa kuwa kwanini ninyi huwa mnadiscourage Watu kupeana Talaka wakati maandiko yako wazi na Kama ni swala la uasherati limethibitika na pengine Kama ni mtoto ameshazaliwa nje ya ndoa? Wakasema inabidi kusameheana, nikawaambia sawa lakini kusameheana kupo na swala la kuachana ni lingine na Kama ni hivyo ingeandikwa mojamoja kuwa Watu wasemeheane wasiachane !
Swali zuri umeuliza lakin hakuna kitu ambacho Mungu anachukia kama kuachana,
Mungu anachukia kuachana
Mungu anachukia kuachana
Ukibase kwenye Bible katika upande mmoja, unaweza ona Bible inajichanganya lakini sivyo
Ukitakata kuelewa Bible kuwa vizur inabidi utulivu na Roho Mtakatifu ndani yake akufundishe
Mungu aliumba mke na mume( Hii ni taasisi)
Ndio maana shetani anaipiga vita kwa kuleta kuachana,
Hilo andiko lipo lakin usi egemee Mungu karuhusu kuachana
Mwanamke/mwanaume ataacha wazazi wake ataambatana na mume/mke wake
Na alicho kiunganisha mtu binadamu asikitenganishe, ni kifo tuuuu ni cha kutenganisha
Kama huko kuachana watu wengi wangeachana katika hizi ndoa, cha muhimu jua nini position yako katika ndoa, ukijua nini position yako katika ulimwengu wa roho na nini nguvu yako katika nafasi kama mwanamke kamwe huto tetereka
Sio kuwa huto face vita katika ndoa, vita vipo lakini Biblia niisomayo inanianiambia Hazitafanikiwa, isaya 54:17
Ila know ua position, know your position,
Jua jinsi ya kuitumia, jua jinsi ya kuitumia
Ukijua jinsi ya kuitumia talaka haitokuwa kwenye kinywa cha mwanamke,
Mwanamke mmoja ni jeshi kubwa mnooo
Sasa kama mwanamke hajui kama yeye ni jeshi lazima adui aingilie kati
Usipo jua haki zako lazima shetani akukamate, lazima akuletee na andiko watu wasiachane ila kwa uzinzi
Unajua shetani anajua Bible yote, na Biblia Yangu inaniambia andiko huua lakini neno huhuisha hivyo shika Neno na sio andiko
Neno linakuja na Roho Mtakatifu ndani yake na lina uzima na pumzi ndani yake kama neno ni uzima haliwez ua kitu cha Mungu, anaye ua ni shetani ambalo ni andiko linakuja kama Hadithi jins lilivyo halina nguvu ndani yake na mtu analibeba tuu,
(2corinth 3:6a) si wa andiko, bali wa roho, kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha
Mungu anaposema mwanamke atamlinda mume wake, ni katika vitu vingi mno, na kwa njia ya maombi,
Wewe ni Jeshi kubwa
Mungu anapo kupa mume nina uhakika uliomba, na Mungu akakupa huyu ndiye kama ni mume Mungu kakupa, Mungu sio dhalimu akupe mume ambaye baadaye anasema wataachana
Huyo sio Mungu tunaye mtumikia, huyo siyo Mungu tunaye muambudu aseme uongo Mungu wetu ni mkweli wala sio Muongo
Nina uhakika ulipo omba mume lazima alikupa jibu ndio ama siye , shida inakuja hapa kwetu sisi wamama au wadada kuolewa na waume ambao sio wetu
Ni hivi Mungu anapo sema nitakupa wa kufanana naye ina maana anakupa mtu ambaye utakuwa tayari kubeba udhaifu wake na yeye kubeba udhaifu wako,
Na kama unaona huwez beba udhaifu wa mwenzio huyo sio mume wako,
Mungu sio dhalimu narudia tena Mungu sio dhalimu
Hawez kukupa ndoa leo na baada ya mwaka ikavunjika sio Mungu tunaye mtumikia.
Mungu anatuwazia mema na wala si mabaya yeremia 29:11
[emoji115] [emoji115] kama anatuwazia mema hawez kutuachilia tuachane au uachane na mume wako
Unless otherwise hukumsikia Mungu wakati wa kuolewa ama ulimsikia na ukalazimisha kuolewa hata kama mlipendana na Mungu akaona huto dumu sababu sio match yako
Shida nyingi ni kutomsikia Mungu au kuweka kama husikii kama Mungu kakuambia sio mume wako subiria sababu Biblia inaniambia kuwa yeye anaujua mwanzo hadi mwisho, nina uhakika aliona hii ndoa itaishia nusu hivyo akatumia njia hadi ya ndoto kukuonya lakin unaamka unasema ndoto tuu
Lakin si ndoto ni Mungu anajaribu kukuambia
Udhaifu hatubebi tuu ila tuna ubeba katika kiti cha neema kwa maombi hadi mtu atakapo kaa sawa
Sasa ukiona huwez beba udhaifu wa mume kwa maombi hujui nini position yako as a praying woman
Au hakuwa mume wako uliingiia tu
Kiti cha Neema na Rehema ndipo tunapo pata mahitaji yetu na udhaifu wetu unashughulikiwa hapo
Mwanamke ni mlinzi kwa njia ya maombi, unaweza amua kuwa mke as mke au kuwa mke mlinzi sababu sio kila mke ni mlinzi, lakini kuna mke +mlinzi pia
Ukikaa katika hiyo position ya ulinzi na mke pia kila challenge inayokuja katika ndoa yako utajua tu kuna gap niliacha wazi ndio maana hichi kikapita
Yesu alipo mwambia Petro rudi nyuma ewe shetani
[emoji115] [emoji115]
Kwanini asimkemee Petro au amtoe Petro katika wanafunzi wake
Kwanini alimkemea shetani aliye ndani ya Petro?
Alijua kuwa sio Petro, ni shetani kamvaa Petro hivyo haku mpush away Petro ila alimkemea shetani aliye ndani ya Petro lakini Petro alibaki kuwa mwanafunzi wake
Hivyo unapo kutana na shida lazima ujue Petro sio wa kumfukuza ila shetani aliye ndani ya Petro ili Petro abaki atimize kusudi la Mungu.
Na unaona alicho ambiwa aliambiwa wewe ndiwe Petro juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu halitalishinda,
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni...
Mathayo 16:18-19
Huyo huyo Petro aliyevaliwa na shetani bado alipewa mamlaka kuu
In ua Presence Jesus is where I belong