Rais Samia, 4Rs Bila Sheria Haitafika Popote

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,553
41,061
Mlengo wowote ambao nchi inataka kwenda, ifanikiwe ni lazima kuwepo na sheria ya kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa. Bila ya sheria, jambo hilo haliwezi kufika popote. Baadhi watalifanyia dhihaka, wengine watalipuuza na wengine watalihujumu, na huwi na namna ya kuwaadhibu.

Ndiyo maana kulipoanzishwa Azimio la Arusha, sheria nyingi zilibadilishwa. Kulipoanzishwa Azimio la Iringa la siasa ni kilimo, zipo sheria zilitungwa na nyingine kubadilishwa. Ndiyo maana ilikuwa ukikiuka misingi ya Azimio la Arusha, unaweza kukamatwa na ukashtakiwa.

Sasa, kama Mh. Rais Samia yupo serious na 4Rs, na ana dhamira nchi iende huko, ni lazima baadhi ya sheria zitungwe na nyingine zibadilishwe, ili wale wanaoenda kinyume na nchi inakotaka kwenda waweze kukamatwa, kushtakiwa, na kuhukumiwa.

Mathalani ama kingekuwa na sheria inayotamka wazi kuwa mtu yeyote lama atatumia nafasi yake ya uongozi kuleta fikra za kisasi, kuwakomoa watu au kuwabagua watu au kutoa kauli za kuwabagua watu kwa msingi wowote ule katika kuwapa huduma wananchi, atakuwa amevunja sheria inayomtaka kila kiongozi kuhamasisha umoja, basi kiongozi huyo atafutwa uongozi mara moja, atafikishwa mahakamani, na akithibitika kutenda kosa hilo, atafungwa jela bila nafasi ya faini kwa muda usiopungua miezi 6, tungekuwa na sheria kama hiyo, au inayofanana na hiyo, yule mhuni Sabaya, mwenyekiti wa CCM Arusha aliyesema kuwa watu wakimchagua kiongozi ambaye siyo mwanaCCM watanyimwa huduma, na hakuna mkuu wa mkoa atakayeenda kuwatembelea kusikiliza matatizo yao, leo hii hii angekuwa mikononi mwa Polisi, tayari kwaajili ya kufikishwa mahakamani na kisha jela.

Tunaomba Rais Samia ipanue falsafa yako ya 4Rs, ili iwe ndiyo msimamo wa nchi, na kisha itungiwe sheria ili tuwadhibiti wahuni ambao kila siku wanapalilia utengano, na kutumia nafasi za uongozi kuwagawa wananchi au kuwafanyia uonevu kwa sababu ya kukosa uvumilivu.
 
Mlengo wowote ambao nchi inataka kwenda, ifanikiwe ni lazima kuwepo na sheria ya kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa. Bila ya sheria, jambo hilo haliwezi kufika popote. Baadhi watalifanyia dhihaka, wengine watalipuuza na wengine watalihujumu, na huwi na namna ya kuwaadhibu...
Samahani mkuu, kwani 4Rs ni nini
 
Back
Top Bottom