Kwa tabiri hizi, CCM tukiendelea kumchekea Rais Samia soon tutageuka kuwa wapinzani!

Mkuu kama ni unabii tu;-

Nabii Boniface victor anatabiri ccm itaendelea kutawala daima,na Rais anaefuata baada ya samiah ni Gwajima josephati sasa sijui tushike lipi!!!

Mi nadhani tuendelee kufanya kazi KWA bidii huku tukiomba amani iendelee kutawala nchini!!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yangu niipendayo SANA!!

Dr Samia Sululu Hassan ameletwa na Mwenyezi Mungu ili kuwakomboa Wa-Tanzania kutoka kwenye utawala wa JPM.
Mola ampe maisha marefu mama yetu.
 
Ipo hivi Samia karuhusu demokrasia kuvutia mabeberu na kutengeneza uhusiano bora na mabeberu, there was no way out, alijua akiendelea na siasa za JPM asingefika , anajielewa uwezo wake na anajua wazi pasipo misaada angekuwa rais mbovu kuwahi kutokea
Ni hulka yake tu, angeamua kuwachunia angewachunia na misaada ingeingia bila chenga.
 
Shaloom wana wema!
Nianze kwa nukuu hii ya Jakaya Kikwete, "Samia najua wewe ni zao la upinzani kwa hiyo haishangazi unavyowatendea wapinzani". Jakaya anakumbushia historia ya Samia kuwa anayo damu ya upinzani. Kwa kuwa ni Mzanzibari basi kama anayo hisia za upinzani basi tujue ni muumini wa Serikali tatu.

Pili tukumbuke Urais wa Samia haukuwahi kuwa programmed si na chama wala "ofisi nyeti" bali limetokana na Mungu kuamua ugomvi kati ya Watanzania na Bwana yuleee ikabidi Katiba ielekeze Samia kushika hatamu za uongozi. Hatua hii imewafurahisha mno Wazanzibari kuliko Watanganyika wakiamini kuwa Mungu amesikia kilio chao cha miaka mingi kwamba huu ndio wakati wa kuipata Zanzibar huru kutoka makucha ya Tanganyika. Itawezekana?

Tuanze na utabiri wa Shekh Yaya Hussein mwaka 2005 mwezi April. Yahya alisema, "Rais atakayeshinda Uchaguzi Mkuu atatokea Pwani na anayo sura ya kike. Atakayemfuata atakuwa ni mwanamume kutoka Bara lakini baada yake huyo atakuja Rais mwanamke. Huyo mwanamke atakabidhi kwa upinzani". Kweli, alishinda Jakaya Kikwete kutoka Pwani akiitwa handsome boy. Akafuatia Magufuli kutoka Bara. Kisha akaja Samia Suluhu Hassan (mwanamke). Je, utabiri huu utafika mwisho kwa Samia Suluhu Hassan kukabidhi nchi kwa upinzani? Time Will tell.

Mwaka juzi 2021 Askofu na Nabii Ndlovu wa Zimbabwe alitabiri kuwa ameoneshwa katika njozi kuwa mwaka 2022 kuna ndege itaanguka katika moja ya nchi za Afrika Mashariki. Na itaanguka ndani ya maji. Akasema ndege hiyo ikiua watu, basi chama kinachotawala kitaondoka madarakani lakini kwa kumwaga damu. Isipoua kitaondoka kwa Amani. Hapo maana yake ni kwamba ndege lazima ianguke. Alitumia maneno, "rulling system must quit". Alipuuzwa na spinning doctors". Mwaka Jana ndege ya Precision Air ikaanguka Ziwa Victoria na kuua watu 19. Je, unabii huu wa Ndlovu utafika mwisho na hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan kukabidhi nchi kwa upinzani?

Sasa tujenge hoja kwa uhuru wa kutoa maoni chini ya Ibara ya 18 ya Katiba.

Kinachoonekana ni Rais Samia Suluhu Hassan kurejesha demokrasia iliyokuwa imebinywa na mtangulizi wake JPM. Lakini ukweli ni kwamba ameenda mbali zaidi si tu kurejesha uhuru wa demokrasia lakini ameingia hata ndani ya vyama hivyo (Chadema) na kuwaimarisha kisiasa (rejea kauli ya JK hapo juu). Samia anakijenga Chadema hasa. Mwaka 2025 chama hiki kitavuna wabunge wengi sana sawa na hata nusu.

MUHIMU SANA: Katiba Mpya haitopatikana kabla ya 2025 kwa maana kwamba mtu yeyote asitegemee Uchaguzi 2025 utafanyika kwa Katiba Mpya, sahau maana inaweza kukiletea CCM shida kikaamua kumuondoa. Hivyo, msala huo atahakikisha 2026&7 Katiba Mpya inapatikana tayari upinzani ukiwa na nguvu kubwa. Hapo ndipo mpera-mpera wa Upinzani kuelekea 2030 utashika kasi naye hatowafanya kitu maana hatokuwa na cha kupoteza tena. Ifikapo 2030 upinzani utaweza kushinda lakini CCM itakubali kuachia Ikulu? Hapo ndipo ilipo unabii wa Nabii Ndlovu. Upinzani wakifanikisha hilo basi Serikali 3 haitokwepeka. CCM ikikataa kuondoka' Ikulu basi baada ya damu tutasuluhishwa na Jamii za Kimataifa ikiwezeka hata kugawana mkate. Mbowe analijua hili vizuri sana katika maongezi ya maridhiano. Lissu anaposema, "nasikia Kuna kugawana mkate" mueleweni.

Na ikumbukwe waliovujisha mkataba wa DP World ndio hao hao walio nyuma ya dili hili. Ndio walioshauri William Lukuvi na Abdalah Bulembo (maadui) wa Samia kisiasa kusogezwa Ikulu kufanikisha ajenda hii.

My Take: CCM kuweni makini mno na mahaba ya Samia kwa Upinzani kama bado mnataka kuitawala nchi hii. Mbowe si mjinga hata kidogo. Wajerumani, Wamarekani na EU are very smart in the deal. Kuweni macho kabla utabiri wa Nyerere nao kutimia, "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM". Hayo ndiyo yangu kwa Leo. Mkiona Kuna hoja chukueni mkiona ni upuuzi mnipuuze na kunitemea mate. Kwaherini!
Hoja yako sio dhaifu Sana, wenye akili tunaichukua na kuitafakari zaidi kadri muda unavyosonga!
 
Unajichosha Bure sana sana ukiendelea hivi unaweza usifike 2030
 
Samia najua wewe ni zao la upinzani kwa hiyo haishangazi unavyowatendea wapinzani". Jakaya anakumbushia historia ya Samia kuwa anayo damu ya upinzani. Kwa kuwa ni Mzanzibari basi kama anayo hisia za upinzani basi tujue ni muumini wa Serikali tatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kuna shida yoyote upinzani kushinda kihalali? Watanzania ndio wanapaswa kuamua chama kipi wakipe madaraka

Nchi hii iko mikononi mwa Mama Samia, tumuachie achape kazi. Najua hana roho mbaya kwa wapinzani. Iwapo wapinzani watashinda atawakabidhi nchi, ila wanaCCM hawataki.
TUMUOMBEE
 
Hapo ndipo ndege itaanguka na kumwaga damu
 
Cha msingi chadema waachane na lissu,wamtafute mgombea msukuma mwenye ushawishi mkubwa
Kwa udikteta, ugaidi na mauaji ya Yule BWANA, itachukua miaka 100 labda msukuma kuja kuongoza nchi hii, waTanzania wakimuona msukuma wanaona kivuli Cha Yule BWANA.
 
Menemene tekel na persin .
Nyerere alitabiri chama kisikilize watu wanasemaje ? Na chama kisiposikiliza anguko ni dhahiri !
Mwenye video na aitupie ya nyerere.
Utabiri wa JKN umetimia bado wa Lema.
Kwaheri ya kuonana chama cha mwaka 77.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom