Kwa mimi youtube ni zaidi ya chuo kikuu

Kwa mimi youtube ni zaidi ya chuo kikuu

Nimejifunza techniques nyingi mfano where should I apply od button, mpangilio wa rangi kwenye nyumba yangu, pia imenisaidia mambo mengi katika ku sort out my career on accounting problems. Wala sinaga mtu wa kumuuliza mi nazama zangu yutyub mambo yanajipa tu mchawi bando.
Naomba link ya kupangilia chumba.
 
Ngoja nkaanzishe ka page niite Youtube University [emoji1550][emoji1550]
 
Mimi nimejifunza Graphic designing, sijasomea mambo ya IT lakini hii ni taaluma yangu ya ziada kupitia University of YOUTUBE
Mkuu ebu nipe mbinu ulizotumia kujifunza graphic designing,nataka nijifunze hii kitu aisee but mi sio mtaalamu wa IT
 
Yaani mimi nilikuwa nikienda Home Kijijini smartphone yangu haina Network kabisa hakuna Mawasiliano au mara nyingine nikirudi chuo unakuta Geto ninalokaa hamna network ya Internet kwahio unakuta ni mpaka nitoke nje Usiku ndio ni download au niperuzi mtandao lakini Kupitia Youtube nilijifunza namna rahisi ya Kutengeneza Kamtambo ka Kuboost na Kuvuta mawimbi ya Network kwa mazingira Yoyote
Yaani saivi ni Full raha niende Kokote TZ hata mtandao wowote mimi network ni full 3G/4G hata nikiwa Geto ni mwendo wa 3G/4G cha mihimu niwe na Bundle Langu tuu bass
Duh,, mkuu kwahyo hako kamtambo unako??
 
Kweli Youtube ni nomaa,, na mkumbuke kuna watu kibao wanaingiza zaidi ya dola 500 kwa siku kupitia Youtube
 
Binafsi napenda sana music production YouTube imekua mkombozi mkubwa sana kunifanikishia hitaji langu japokua vifaa vimekua ni changamoto lakini kwa hivi ambavyo ninavyo Nina uwezo wa kutengeneza beat mtu akaimba vizuri na mambo yakaenda mwake

YouTube ni zaidi ya shule
 
Kwa hiyo wote mliosoma chuo kikuu mnakili kabisa YouTube ni zaidi ya chuo kikuu???real???
Mnasahau ya kuwa hayo madude yamewekwa na wenzenu waliosoma kama nyinyi?? YouTube haijajiwekea material kuna watu walipata elimu ya darasani wakafanya beyond kazi kwenu.
 
YouTube haiwezi kuwa zaidi ya shule hata siku moja ndugu yangu. Hizo contents unazo ziona ndio zimekusaidia kuliko mkufunzi wako chuo kuuu, zimewekwa na mtu aliye kwenda shule na kufahamu kama mwanafunzi anatakiwa afanye nini.
Hivyo mnavyovisifia havijajiweka YouTube, vimewekwa na binadamu mwenye maumbile na ubongo kama wako tofauti ni kwamba yeye alijua anapaswa kufanya nini zaidi ya pale anapoishia mwalimu wakati wewe ulipokuwa chuo alipokuwa anaishia mwalimu wewe uliishia nyuma yake kidogo.

Hivi unadhani Mmilikiwa Facebook alifundishwa chuoni namna ya kutengeneza facebook? ama muanzilishi wa YouTube alifundishwa darasani namna ya kutengeneza hicho unachokiona ni bora!
Ndicho ulicho jifunza YouTube...???
 
Yaani mimi nilikuwa nikienda Home Kijijini smartphone yangu haina Network kabisa hakuna Mawasiliano au mara nyingine nikirudi chuo unakuta Geto ninalokaa hamna network ya Internet kwahio unakuta ni mpaka nitoke nje Usiku ndio ni download au niperuzi mtandao lakini Kupitia Youtube nilijifunza namna rahisi ya Kutengeneza Kamtambo ka Kuboost na Kuvuta mawimbi ya Network kwa mazingira Yoyote
Yaani saivi ni Full raha niende Kokote TZ hata mtandao wowote mimi network ni full 3G/4G hata nikiwa Geto ni mwendo wa 3G/4G cha mihimu niwe na Bundle Langu tuu bass
Hetu tupia huo Uzi au link ya YouTube nasi tujifunze bro
 
Back
Top Bottom