Nimejifunza mechanics na kuijua gari vyema. Gari ikiwa na hitilafu yoyote najua shida iko sehemu gani na natatua mwenyewe. Pale ambapo sina nyenzo, namuita fundi namwambia fungua sehemu flani unirekebishie kitu flani. Awali mafundi walikuwa wananibambikia sana vitu kwasababu nilikuwa sijui chochote. Unakuta alternator ina tatizo, fundi anaanza kubuni na kukubambikia matatizo lukuki. Mara nimebadiliheadgasket, mara sijui hose pipe inayotoka wapi kwenda wapi, mara sijui nut flani na kitu flani ongezea na mwishowe unakuta gharama zimekuwa kubwa bila sababu ya msingi. Pia nimejifunza mengi kuhusu sayansi ya dunia, IT, uhandisi na hata medical fields.