Kwa kweli Marekani ni model wa Demokrasia duniani.

Kwa kweli Marekani ni model wa Demokrasia duniani.

econonist

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
25,836
Reaction score
41,354
Kwa kweli Marekani ni model wa demokrasia duniani. Uchaguzi imefanyika ndani ya masaa sita washindi washajulikana na walioshindwa wamekubali kushindwa na maisha yanasogea. Hadi Rais kichaa Trump kakubali kushindwa na kuahidi kufanya kazi na democrats.

Kwa marekani usipotekeleza sera zako ulizohaidi utapigwa chini. Sio huku mtu anahaidi katiba mpya kumbe Hana mpango wa Katiba mpya. Anamfukuza Makamu wa Rais kisa kanadi sera yake ya Katiba mpya. Ingekuwa marekani tayari umeshakizamisha chama chako. Kwa kweli sijui lini tutapata demokrasia kama ya marekani ambapo wananchi hawaingiliwi kwenye maamuzi yao.

Pamoja na madhaifu yake, marekani kajitahidi kusimamia demokrasia. Kubali maamuzi ya wananchi. Huku Tanzania, Tume ndio inayopiga kura na hata wakaurugenzi wa tume hugombea kupitia CCM ( kumbuka Mahera). Serikali ipo tayari kuua watu ili ibakie madarakani. Tume ndio inapiga kura na kutangaza mshindi. Haijalishi ulipiga kura au la, tume itakupigia kura.

Utashangaa hapa Bongo tumefanya uchaguzi mdogo hapo Chamwino sidhani hata kama Kuna mtu anajua matokeo ya uchaguzi na nani kashinda. Matokeo ni Siri ya tume na CCM yake. Inasikitisha sana.
 
Ila democrats wanawaruhusu mpaka watu wa upinde... sipendi mimi.
 
Ila democrats wanawaruhusu mpaka watu wa upinde... sipendi mimi.

Unadhani raia wa marekani wanajali hilo, wanavipaombele vya msingi zaidi

Mambo ya upinde ni nyie wabongo ndio mnapigia kelele
 
Marekani wana demonstrate jinsi taasis huru zenye misingi zinavyoweza kuamua future ya nchi, tofauti na nchi ya maelekezo ya mtu mmoja
 
Back
Top Bottom