Boonabaana
JF-Expert Member
- Oct 22, 2011
- 255
- 105
Hatimae tumefikia kwenye win win na mgogoro umeisha. Msitake kuchochea mambo yaliyoisha.
Mkuu, hiyo siyo win-win style, bali ni Win-lose management conflict!
Hatimae tumefikia kwenye win win na mgogoro umeisha. Msitake kuchochea mambo yaliyoisha.
madaktari wanatakiwa kutoa ufafanuzi ili jamii isinywe sumu ambayo imetolewa na JK
dk ulimboka na wenzako msihofu kitu chochote,jipangeni vizuri ili kuhakikisha serikali inapata somo. Hii nchi imeoza.
mm nashangaa sana, jk amekaa muda wote akizungumza juu ya madaktari wakati kuna mambo mengi ambayo angepaswa kuzungumza. Tena karudi yale yale yaliyokuwa yanaongelewa.
Hayo ndo matokeo ya kuongozwa na rais asiye na hekima.
Mkuu, hiyo siyo win-win style, bali ni Win-lose management conflict!
Ila the guy ni disaster kwelikweli. Inashangaza sana kwamba hajui hata nyakati tulizonazo, kwamba anashangaa madaktari kuomba majibu ya waziri mkuu yawe kwenye maandishi? Ameniacha hoi kweli kwenye hili kwani cha ajabu ni ninin hapa? Inaonesha anapenda kweli mambo yaishie jukwaani then basi. Halafu kwanini yeye anajiona kama Mungu vile? Eti aliyemweka waziri ndiye aliyemwekea naibu kwani huyo mtu yuko mbinguni mpaka anashindwa kuwaondoa hao watu kiasi kwamba watu inabidi waendelee kufa tu? Halafu kwa kuwa mawaziri ni wapitaji so waendelee tu kutuulia watu wetu na sisi tuwaache kwa kuwa ni wapitaji kwenye wizara? jk when will you be serious with the lives of poor tanzanians?
Hivi Presida hata kama haya maongezi yake anaandikiwa (alkikuwa akisoma) si anaweza kuona kama kilichoandikwa si kizuri akakiacha na kusema aaminicho kinatakiwa? Ninauliza tuu kwa wajuao
Sasa ndio nimepata majibu ya kwanini nchi sasa inaenda mrama!! Mkuu ni tatizo!
Kama kutatokea mgomo wa madaktari basi viongozi watakuwa si kina Ulimboka na wenzake walioenda Ikulu.
Waliongea tu hakuna zaidi, lakini jamani, usitake kuwa nabii wakati unajijuwa kuwa una dhambi!
Hawarudii tena na wala hawatoongelea tena, nasema labda wawe viongozi wengine wa madaktari na si wale walioenda Ikulu. Kama mnabisha tazameni kama hata wataongelea zaidi, pengine kwa sasa hata mikutano hawaitishi tena. Mkisikia Serikali ina "mkono mrefu" kama hamjui maana yake muulizeni Dokta Ulimboka.
BUSARA IMEKOSEKANA KATIKA HOTUBA YA JK.Hotuba ya Rais tulitemea mambo mawili kuvunja baraza la mawaziri au kuwafukuza waziri wa afya na makamu wake.Kuwashambulia Wanaharakati na Madaktari ni matusi kwani ni wao waliomzindua usingizini na kujua nini kinachoendelea katika wizara ya afya,hali ambayo iko katika wizara zote na taasisi za umma na serikali.Inaeleweka ya kua amesita kuchukua hatua za kuwafukuza waziri na naibu wa waziri wa afya kwa sababu yangezuka maeneo mengine.Je Wizara ya nishati na madini mambo,ulinzi,maliasili n.k.hali shwali?Kwa hotuba ya Rais nimefikia CONCLUSION MAWAZIRI NA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI NA MASHIRIKA YA UMMA REFLECTION AU KIOO CHA UTAWALA NA RAIS MWENYEWE JK.MUNGU IBARIKI TANZANIA.WanaJF
Nimesikiliza kwa kituo hotuba ya JK. Naamini ilikuwa na malengo yafuatayo:
1. Kuwadhalilisha madaktari kuwa hawana uzalendo kwa kudai mishahara isiyowezekana (Sh Milioni 7 na milioni 17 kwa mwezi)
2. Kuwagombanisha madaktari na wananchi ili jamii iwaone kama watu wasiofaa ndani ya jamii.
3. Kuwashuhudia uongo madaktari kwa kueleza na kupotosha historia nzima ya mgomo na kudai watendaji wake akiwemo katibu mkuu waliwajibika ipasavyo. Mfano sakata la interns kudai eti waliondolewa muhimbili kwa sababu kulikuwa kumejaa wakati si kweli, na mengine mengi
4. Kuwageuka madaktari ambao walirejea kazini kwa kuelezea kuwa na imani na Rais baada ya mazungumzo yao, lakini leo amekuja kuwachambua na kuwasemea mbovu mbele ya wananchi na hata kupoteza dhana nzima ya makubaliano yaliyofanyika Ikulu last weekend.
5. Kumshambulia Dr Ulimboka kama alivyomshambulia Mgaya personally mwaka 2010. Hata hivyo ameshindwa kujua kuwa MAT ni chama cha madaktari Tanzania na sio chama cha madaktari wa serikali.
Katika maelezo yake yote hakuna hata sehemu moja ambapo JK ameelezea namna alivyosuluhisha ama atakavyosuluhisha na kutekeleza madai ya madaktari na hasa dai la kuwawajibisha waziri na naibu wake ili mazungumzo yaweze kuendelea baina ya pande mbili zinazoaminiana. Kutokana na hali hiyo, tutarajie yafuatayo muda wowote kuanzia sasa:
1. Madaktari kuitisha mkutano na wanahabari kuelezea uongo ulioshuhudiwa na Rais kuhusu chanzo cha mgomo.
2. Madaktari kuelezea ukweli juu ya makubaliano yaliyofikiwa Ikulu ambayo yalifanya mgomo usitishwe.
3. Madaktari kuelezea kutokuwa na imani na Rais siku mbili baada ya kuongea naye na baada ya kuwageuka na hivyo kuitisha mgomo mkubwa zaidi ya yote iliyotangulia.
4. Na mengineyo meeengi pia......//
Matatizo yote haya chanzo ni hotuba yake ya leo. Madaktari wasilaumiwe kwa hatua yoyote watakayoichukua sababu Rais wetu ameonyesha kutokuwajali wananchi kwa namna yoyote.
Hata hivyo, sitashangaa kama madaktari wakiamua kuchukua uamuzi wa kuudhihirisha uongo wa JK na kisha wakampuuza na kuendelea na majukumu yao.