Kwa hotuba hii ya Rais, Tujiandae na mgomo mkubwa wa madaktari

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
WanaJF
Nimesikiliza kwa kituo hotuba ya JK. Naamini ilikuwa na malengo yafuatayo:

1. Kuwadhalilisha madaktari kuwa hawana uzalendo kwa kudai mishahara isiyowezekana (Sh Milioni 7 na milioni 17 kwa mwezi)

2. Kuwagombanisha madaktari na wananchi ili jamii iwaone kama watu wasiofaa ndani ya jamii.

3. Kuwashuhudia uongo madaktari kwa kueleza na kupotosha historia nzima ya mgomo na kudai watendaji wake akiwemo katibu mkuu waliwajibika ipasavyo. Mfano sakata la interns kudai eti waliondolewa muhimbili kwa sababu kulikuwa kumejaa wakati si kweli, na mengine mengi

4. Kuwageuka madaktari ambao walirejea kazini kwa kuelezea kuwa na imani na Rais baada ya mazungumzo yao, lakini leo amekuja kuwachambua na kuwasemea mbovu mbele ya wananchi na hata kupoteza dhana nzima ya makubaliano yaliyofanyika Ikulu last weekend.

5. Kumshambulia Dr Ulimboka kama alivyomshambulia Mgaya personally mwaka 2010. Hata hivyo ameshindwa kujua kuwa MAT ni chama cha madaktari Tanzania na sio chama cha madaktari wa serikali.

Katika maelezo yake yote hakuna hata sehemu moja ambapo JK ameelezea namna alivyosuluhisha ama atakavyosuluhisha na kutekeleza madai ya madaktari na hasa dai la kuwawajibisha waziri na naibu wake ili mazungumzo yaweze kuendelea baina ya pande mbili zinazoaminiana. Kutokana na hali hiyo, tutarajie yafuatayo muda wowote kuanzia sasa:

1. Madaktari kuitisha mkutano na wanahabari kuelezea uongo ulioshuhudiwa na Rais kuhusu chanzo cha mgomo.

2. Madaktari kuelezea ukweli juu ya makubaliano yaliyofikiwa Ikulu ambayo yalifanya mgomo usitishwe.

3. Madaktari kuelezea kutokuwa na imani na Rais siku mbili baada ya kuongea naye na baada ya kuwageuka na hivyo kuitisha mgomo mkubwa zaidi ya yote iliyotangulia.

4. Na mengineyo meeengi pia......//

Matatizo yote haya chanzo ni hotuba yake ya leo. Madaktari wasilaumiwe kwa hatua yoyote watakayoichukua sababu Rais wetu ameonyesha kutokuwajali wananchi kwa namna yoyote.

Hata hivyo, sitashangaa kama madaktari wakiamua kuchukua uamuzi wa kuudhihirisha uongo wa JK na kisha wakampuuza na kuendelea na majukumu yao.
 
Kwa njisi mgomo wa pili ulivyoisha, sitarajii mgomo mwingine mkubwa zaid ya ulw wa kwanza.
 
Uyo ndiyo JK mnaongea vizuri mnapatana alafu anakubadilikia kama akujui.
Kwani Mmesaau Matukio mengi anayo fanya? Uyo si wakumuamini atakidogo.
poleni Madaktari. iyo ndiyo bongo bana.
 
akili zao wachanganye na za mbayuwayu mkuu! vasco dagama kawapiga goli la kisigino mkuu......
 
....5. Kumshambulia Dr Ulimboka kama alivyomshambulia Mgaya personally mwaka 2010. Hata hivyo ameshindwa kujua kuwa MAT ni chama cha madaktari Tanzania na sio chama cha madaktari wa serikali.....
Hapo kwenye Red sikushanga maana namjua vyema mk..were aliwahi kusema kuwa hajui nn chanzo cha umaskini wa watanzania! kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa hajui MAT ni chama cha madokta Tanzania.
 
mm nashangaa sana, jk amekaa muda wote akizungumza juu ya madaktari wakati kuna mambo mengi ambayo angepaswa kuzungumza. Tena karudi yale yale yaliyokuwa yanaongelewa.
 
Sisi wa Tz ndivyo tulivyo, tunadanganywa na tabasamu kisha tunapiga makofi ili tuonekena tunaelewa kumbe holaa.
 
JK kawachokoza madaktari kabisa.Tutarajie mgomo mkubwa sasa.

Hakuna mgomo tena Mnyisanzu. Baada ya hotuba hii mawazo yamegawanyika. Daktari atakayeamua tutamshangaa sana kwasababu pamoja na nia yao njema hawana haki ya kuua. Kudai maslahi kwa kumwaga damu za watu ni laana. Hekima iwatawale waöne hii ni changamoto ktk kazi na maisha yao. Hakuna haja ya kutunishia musuli ugali ulio usonga wewe mwenyewe.
 
Kwa kuwa hawa watu walishakubali kurudi kazini naona hasingesema tena kuhusu mgomo. Naona kama kalikoroga tena.
 
Wacheni ujinga wenu hamna uwezo wa kugoma nyie. Madai yenu ni kijingajinga tu utafikiri hamkusoma hata vidato!
 
dk ulimboka na wenzako msihofu kitu chochote,jipangeni vizuri ili kuhakikisha serikali inapata somo. Hii nchi imeoza.
Watafute njia nyingine hii ya kuipasomo serikali kwa ndugu zetu sisi masikini kupoteza maisha tumeichaka.
 
Jamani alichoongea JK ni siasa, ukweli ni kwamba makubaliano ya kimsingi ya JK na Ma-Dk upo pale pale!
Ameongea kujisafisha kama kiongozi wa nchi asidharaulike ukweli ni kwamba hy ni propaganda kwa wa-tz kupitia wazee wa dsm!
 
JK kawachokoza madaktari kabisa.Tutarajie mgomo mkubwa sasa.

Labda siku wanajeshi wakigoma ndio tunaweza kuona mabadiliko ya kweli madaktari walimu na wafanyakazi wengine migomo yao ni migomo mbuzi tu wala haina tija.Madktari walikuja na msimamo mkali hawatajadili chochote wakati mponda na Nkya wapo ofisini, ghafla wakabadilika hao magogoni wakiwa kule wakarudi wakatutangazia mgomo kwisha wanachapa kazi na wana imani na rais, hawakutoa details za majadiliano, sasa huyohuyo waliyemsifu wana imani nae kawanyea! Najua hawatathubutu kugoma tena ila wataendelea kutoa huduma duni chini ya mgomo baridi amabao ni mbaya sana maana wataumia wananchi wa kawaida na ni kinyume cha weledi wao wanatakiwa wawe wazi wamegoma kuliko kuumiza watu kimyakimya,. madokta wameenda shule ngumu sana na miongoni mwa cream ta taifa lakini kwa hili inabidi tuanze kuwafikiria vinginevyo, hawakuwa na strategies au plans b c hata d???
 
Tulitaraji hotuba ya kipuuzi kutoka kwa Mk...were. Tunamjua. Ila kitaeleweka tu, u dr ni taaluma sana.
 
Back
Top Bottom