Hongera Rais Samia kwa Ph.D Nyingine ya Heshima, Akemee Kuitwa Dr? Kuna Haja TCU/MCT/Maelezo Kutoa Ufafanuzi/Muongozo kwa Media Kuita Watu Dr?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,077
115,350
Wanabodi, kama kawa, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa.

Mada ya leo ni pongezi kwa Rais Samia kwa kutunukiwa Ph.D nyingine ya heshima, Je wajua mtu kutunukiwa Ph.D ya heshima, hakumfanyi mtunukiwa kuitwa Dr. as an official title? Ila ni rukhsa kuitwa Dr. socially!. Je tumshauri Rais Samia akemee kuitwa Dr officially?

Pia je kuna haja kwa TCU kuutoa tena ule ufafanuzi kuhusu matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima za honoris causa, kama ulivyotolewa na Prof. Joseph Kironde kwenye moja ya majarida ya TCU?

20221202_183754.jpg

Na jee kuna haja kwa MCT, TEF, na Maelezo watoe muongozo kwa Media kuwaita au kuwaandika watu kwa title za Dr, watu ambao sio madakitari?

Udakitari ni title ya heshima, na uko udakitari wa aina kuu mbili ambao wanaitwa Dr as an official title, na udakitari wa 3 ni udakitari wa heshima, ambapo mtunukiwa haitwi Dr.

Hawa ni
1. Madaktari wa kusomea kitu chochote cha medical, iwe ni udakitari wa binadamu, mifugo, mimea etc.
2. Udakitari wa falsafa Ph. D ambao is earned kwa academic achievements.
3. Udakitari wa heshima ambao is not earned, but ni granted.

Kwanza nijiunge na Watanzania wengine kumpongeza Rais wetu Samia kwa ziara yake ya kiserikali nchini India, pongezi zangu za kwanza ni kwenda kwa ndege yetu ya ATCL, hakuna kitu kinakuza utalii kama uwepo wa direct flights, hivyo kitendo cha dege letu la Tanzania, kutua viwanja vikubwa vya kimataifa, ni sifa na heshima kubwa kwa nchi yetu.

Napongeza sana hili kwasababu ni moja ya mada zangu za nyuma, yenye kichwa cha habari, "Kwanini Rais Wetu Anaposafiri Nje ya Nchi, Apande Ndege za Wengine, Wakati Sisi Ndege hizo tunazo na uwezo huo tunao!. Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Nikashauri, gharama isiwe hoja, nikashauri aandamane na ujumbe wa wafanyabiashara watakao jilipia, Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York
hili limefanyika, hongera sana!.

La tatu ni lile nililoliibua kwenye ule mkutano wa Rais na vyombo vya habari wa mwaka 2016, niliposhauri rais wetu anapofanya ziara za Kitaifa nje ya nchi, aandamane na media, both public na private, na pia tuko waandishi wa kujitegemea wenye uwezo wa kujilipia, tushirikishwe. Ziara hii ya India local media zetu zimeshirikishwa kikamilifu, hongera Zuhura Yunus!.

Mada ya leo ni kuhusu shahada za heshima, honoris causa, jee mtunukiwa anapaswa kuitwa Daktari na kuandikwa Daktari?. Hapa pia nimpongeze Rais Samia kutunukiwa shahada ya pili ya heshima ya udakitari na moja ya vyuo vikuu vya India vyenye heshima kubwa sana duniani.

Japo Rais Nyerere, Mwinyi na Mkapa, walitunukiwa PhD za heshima za honoris causa lakini hawakuitwa kwa title za Dr. Lakini Rais Jakaya Kikwete na Mzee Reginald Mengi, baada ya kutunukiwa waliitwa Dr na kuandikwa Dr hadi na sisi media tuliwaandika hivyo.

Baada ya Rais Samia kununikiwa shahada ya heshima ya udakitari wa falsafa pia tumeanza kumuita Daktari na kumuandika Daktari.

Na juzi tena nchini India, Rais Samia kaheshinishwa tena kwa PhD nyingine ya heshima, hii sasa ni ya pili. hakuna ubishi kuhusu Rais Samia kustahili heshima hii anastahili kabisa.

Ila kiukweli shahada za heshima, yaani PhD za honoris causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa japo Jakaya Kikwete na Mzee Mengi walipopewa waljitwa Dr, kwa PhD ya honoris causa, haya yalikuwa ni makosa, tusiendeleze makosa haya kwa Rais Samia!

Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Joseph Kironde.

Naomba kwanza tutofautishe mtu kujiita Dr, Professa, tulikuwa na Profesa Matikisa, Profesa Singira, Profesa Maji Marefu, Dr. Manyaunyau, Dr. Ngwizukulu Jilala, Dr. Mwaka, rais wa Manzese, rais wa Wasafi, rais wa Yanga, hakuna ubaya wowote mtu kujiita vyovyote, na kuna kuitwa, sio wewe bali wanaokuita, Dr, Prof, rais au kuitwa vyovyote pia hakuna ubaya wowote mtu kuitwa vyovyote as long as ni informally, lakini unapoandika jina lako kwenye usajili wowote, rasmi, lazima utatumia majina rasmi na title rasmi.

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ametunukiwa Ph. D za heshima 14!, lakini huwezi kusikia popote akiitwa Dr au kuandikwa Dr.

Kwa vile huu utaratibu wa shahada za heshima, sio utaratibu wetu wa jadi zetu, viongozi wetu wanapotunukiwa Ph. D hizi, ni vyema tukaufuata utaratibu na utamaduni wa shahada hizo.

Wananchi, rukhsa kuwaida Daktari, na kwenye mikutano ya kawaida, ila kwa sisi media, na kuandikwa kama title, hili linahitaji Ufafanuzi wa TCU, na baada ya TCU kama ilivyofafanuliwa na Prof. Joseph Kironde kwenye jarida la TCU, kuna haja kwa TCU kulitolea ufafanuzi. Na baada ya TCU kulifafanua, MCT nayo ilitolee muongozo kwa vyombo vya habari kuhusu kuwataja au kuwaandika madaktari hawa wa heshima kwa titles za udakitari.

La mwisho, ni kwa madaktari wenyewe hao wa heshima.

Nakumbuka kwenye moja ya matukio yaliyokuwa yakitangazwa live Mubashara na TV zetu, mmoja wa viongozi aliteleza ulimi na kumuita Mkuu wa nchi "Mheshiwa Mungu" mbele ya Mkuu huyo wa nchi, Mkuu yule alicheka tuu kwa kujua mzungumzaji ni ameteleza tuu ulimi.

Yule aliyeita Mheshimiwa Mungu, hakuomba radhi, bali alirekebisha tuu na kuendelea,
View: https://youtu.be/6y3V86aZYf0?si=kJQf8vmFWBtauuAC
Mwingine akamwambia
View: https://www.instagram.com/p/CNew4kTgqg3/?igshid=NTc4MTIwNjQ2YQ==

Na Mkuu wa nchi alipokuja kuhutubia, aliendelea tuu na hotuba yake as if nothing blasphemous has happened!. Kikichokuja kutokea is now a history!, kwasababu hakuna ajuye sababu, this could have been kulichangia!.

Alichopaswa kufanya Mkuu wa nchi ni kukemea!. Huwezi kuitwa Mungu kimakosa radhi isiombwe na wewe kuendelea as if nothing happened!.

Hivyo kwenye hili la kuitana titles za udakitari wa heshima, kugeuzwa ni title rasmi, kitendo cha waitwa kutokemea, au kukaa kimya, tafsiri yake ni ama wanapuuza, ama wanaridhia, ama wanafurahia.

Kwasababu sio wao wanao jiita madaktari, na maadam ni title ya heshima, kuna ubaya gani mtu kuheshimika na kuitwa title ya heshima ya usomi ubobezi na ubobevu ili hali ni title ya heshima tuu?, hivyo kuitwa anahesabika kuridhia!, jee tuwashauri viongozi wetu wakemee?.

Kufuatia maendeleo ya utandawazi kumeibuka vyuo vikuu vya mtandaoni, online universities zinazouza shahada za kununua, bila hata kuingia darasani, vyuo vikuu hivi vya mtandaoni vina issues Ph. D za heshima kwa kulipia tuu tena ni dola 100 tuu!, hili lisipotolewa muongozo na ufafanuzi, utafikia wakati tutashindwa kutofautisha yupi ni Daktari wa kweli wa kusomea, Daktari wa heshima, na Daktari wa kununua makaratasi, tutakuja kuichanganya jamii yetu.

Mbona kwa wanasheria hili limewezekana ili mtu kuwa wakili, lazima uthibitishwe na Jaji Mkuu wa Tanzania na kusajiliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, hivyo TCU yenye jukumu la kutoa ithbati ya vyuo vikuu, hii madaktari wa heshima kuitwa madaktari na kuandikwa madaktari , kuna haja ya kulitolea ufafanuzi au tujiachie tuu kwasababu sini jina tuu?. What's a big deal kuhusu titles?. The rationale, tunapo puuza na kudharau vitu vidogo vidogo, ndio mwisho wa siku, tunadharau vikubwa, tunaishia kulia!.

Wasalaam
Paskali
 
Sasa kwani hata akiitwa nini kinabadilika..

Kwa Tz PhD hata hizo za kusomea zimesaidia nini taifa ukiacha angalao wanaofundisha, kufanya tafiti na kutibu binadamu au Wanyama na Mimea.?

Ukinitajia Dr yeyote kwenye siasa za Tz kwa sasa mwenye impact na kujali mambo yanavyoenda nintashukuru mno...

Dr Charles Kimei.. anahoroja tu bungeni.
Dr Kitila Mkumbo... Hola
Dr. Ndakidemi.. sijui hata yupo wap.
Dr. Tulia... Mlamba miguu wa executives.
Dr Kabudi.... yupo kweli
Dr. Bashiru...
Dr. Ryoba.. kaigeuza TBCC channel ya katuni
Dr. Jafo.. kaamua kuwa mpole.
Dr Biteko..😀.

Embu tuishie hapo.
 
Hao wanasiasa wanalazimisha kutumia title ya Dr, machawa huwambii kitu hata wenye elimu ya juu, ndio maana watu wengi wana mashaka na mfumo wa elimu yetu, unaozalisha wasomi wajinga
 
Huku kwetu kwenye bara la giza ndiyo tunahangaika na hizi title, huwezi kukutana na watu wa dunia ya kwanza akijitambulisha kwa kutanguliza title.....wenzetu wanafanya kila juhudu mtu mwenye PHD yake ilete impact kwenye jamii yake na Taifa lake.....huku kwetu masifa jambo la kwanza na la pili namna ya kupiga ufisadi bila kugundulika
 
Sasa kwani hata akiitwa nini kinabadilika..

Kwa Tz PhD hata hizo za kusomea zimesaidia nini taifa ukiacha angalao wanaofundisha, kufanya tafiti na kutibu binadamu au Wanyama na Mimea.?

Ukinitajia Dr yeyote kwenye siasa za Tz kwa sasa mwenye impact na kujali mambo yanavyoenda nintashukuru mno...

Dr Charles Kimei.. anahoroja tu bungeni.
Dr Kitila Mkumbo... Hola
Dr. Ndakidemi.. sijui hata yupo wap.
Dr. Tulia... Mlamba miguu wa executives.
Dr Kabudi.... yupo kweli
Dr. Bashiru...
Dr. Ryoba.. kaigeuza TBCC channel ya katuni
Dr. Jafo.. kaamua kuwa mpole.
Dr Biteko..😀.

Embu tuishie hapo.
Wakati mwingine ficha upeo wako mdogo, yaani hao ndo unataka ufanye iwe justification yako. Hao walioingia kwenye siasa ulitaka wafanye nini katika chama kilichojichokea wanachokitumikia.
 
Huku kwetu kwenye bara la giza ndiyo tunahangaika na hizi title, huwezi kukutana na watu wa dunia ya kwanza akijitambulisha kwa kutanguliza title.....wenzetu wanafanya kila juhudu mtu mwenye PHD yake ilete impact kwenye jamii yake na Taifa lake.....huku kwetu masifa jambo la kwanza na la pili namna ya kupiga ufisadi bila kugundulika
Kwa mazingira haya ya serikali kuitelekeza sayansi na teknolojia ulitaka walete impact gani zaidi ya wanayoleta kwa sasa.
 
Wanabodi, kama kawa, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa.

Mada ya leo ni pongezi kwa Rais Samia kwa kutunukiwa Ph.D nyingine ya heshima, Je wajua mtu kutunukiwa Ph.D ya heshima, hakumfanyi mtunukiwa kuitwa Dr. as an official title? Ila ni rukhsa kuitwa Dr. socially!. Je tumshauri Rais Samia akemee kuitwa Dr officially?

Pia je kuna haja kwa TCU kuutoa tena ule ufafanuzi kuhusu matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima za honoris causa, kama ulivyotolewa na Prof. Joseph Kironde kwenye moja ya majarida ya TCU?

View attachment 2780800

Na jee kuna haja kwa MCT, TEF, na Maelezo watoe muongozo kwa Media kuwaita au kuwaandika watu kwa title za Dr, watu ambao sio madakitari?

Udakitari ni title ya heshima, na uko udakitari wa aina kuu mbili ambao wanaitwa Dr as an official title, na udakitari wa 3 ni udakitari wa heshima, ambapo mtunukiwa haitwi Dr.

Hawa ni
1. Madaktari wa kusomea kitu chochote cha medical, iwe ni udakitari wa binadamu, mifugo, mimea etc.
2. Udakitari wa falsafa Ph. D ambao is earned kwa academic achievements.
3. Udakitari wa heshima ambao is not earned, but ni granted.

Kwanza nijiunge na Watanzania wengine kumpongeza Rais wetu Samia kwa ziara yake ya kiserikali nchini India, pongezi zangu za kwanza ni kwenda kwa ndege yetu ya ATCL, hakuna kitu kinakuza utalii kama uwepo wa direct flights, hivyo kitendo cha dege letu la Tanzania, kutua viwanja vikubwa vya kimataifa, ni sifa na heshima kubwa kwa nchi yetu.

Napongeza sana hili kwasababu ni moja ya mada zangu za nyuma, yenye kichwa cha habari, "Kwanini Rais Wetu Anaposafiri Nje ya Nchi, Apande Ndege za Wengine, Wakati Sisi Ndege hizo tunazo na uwezo huo tunao!. Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Nikashauri, gharama isiwe hoja, nikashauri aandamane na ujumbe wa wafanyabiashara watakao jilipia, Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York
hili limefanyika, hongera sana!.

La tatu ni lile nililoliibua kwenye ule mkutano wa Rais na vyombo vya habari wa mwaka 2016, niliposhauri rais wetu anapofanya ziara za Kitaifa nje ya nchi, aandamane na media, both public na private, na pia tuko waandishi wa kujitegemea wenye uwezo wa kujilipia, tushirikishwe. Ziara hii ya India local media zetu zimeshirikishwa kikamilifu, hongera Zuhura Yunus!.

Mada ya leo ni kuhusu shahada za heshima, honoris causa, jee mtunukiwa anapaswa kuitwa Daktari na kuandikwa Daktari?. Hapa pia nimpongeze Rais Samia kutunukiwa shahada ya pili ya heshima ya udakitari na moja ya vyuo vikuu vya India vyenye heshima kubwa sana duniani.

Japo Rais Nyerere, Mwinyi na Mkapa, walitunukiwa PhD za heshima za honoris causa lakini hawakuitwa kwa title za Dr. Lakini Rais Jakaya Kikwete na Mzee Reginald Mengi, baada ya kutunukiwa waliitwa Dr na kuandikwa Dr hadi na sisi media tuliwaandika hivyo.

Baada ya Rais Samia kununikiwa shahada ya heshima ya udakitari wa falsafa pia tumeanza kumuita Daktari na kumuandika Daktari.

Na juzi tena nchini India, Rais Samia kaheshinishwa tena kwa PhD nyingine ya heshima, hii sasa ni ya pili. hakuna ubishi kuhusu Rais Samia kustahili heshima hii anastahili kabisa.

Ila kiukweli shahada za heshima, yaani PhD za honoris causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa japo Jakaya Kikwete na Mzee Mengi walipopewa waljitwa Dr, kwa PhD ya honoris causa, haya yalikuwa ni makosa, tusiendeleze makosa haya kwa Rais Samia!

Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Joseph Kironde.

Naomba kwanza tutofautishe mtu kujiita Dr, Professa, tulikuwa na Profesa Matikisa, Profesa Singira, Profesa Maji Marefu, Dr. Manyaunyau, Dr. Ngwizukulu Jilala, Dr. Mwaka, rais wa Manzese, rais wa Wasafi, rais wa Yanga, hakuna ubaya wowote mtu kujiita vyovyote, na kuna kuitwa, sio wewe bali wanaokuita, Dr, Prof, rais au kuitwa vyovyote pia hakuna ubaya wowote mtu kuitwa vyovyote as long as ni informally, lakini unapoandika jina lako kwenye usajili wowote, rasmi, lazima utatumia majina rasmi na title rasmi.

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ametunukiwa Ph. D za heshima 14!, lakini huwezi kusikia popote akiitwa Dr au kuandikwa Dr.

Kwa vile huu utaratibu wa shahada za heshima, sio utaratibu wetu wa jadi zetu, viongozi wetu wanapotunukiwa Ph. D hizi, ni vyema tukaufuata utaratibu na utamaduni wa shahada hizo.

Wananchi, rukhsa kuwaida Daktari, na kwenye mikutano ya kawaida, ila kwa sisi media, na kuandikwa kama title, hili linahitaji Ufafanuzi wa TCU, na baada ya TCU kama ilivyofafanuliwa na Prof. Joseph Kironde kwenye jarida la TCU, kuna haja kwa TCU kulitolea ufafanuzi. Na baada ya TCU kulifafanua, MCT nayo ilitolee muongozo kwa vyombo vya habari kuhusu kuwataja au kuwaandika madaktari hawa wa heshima kwa titles za udakitari.

La mwisho, ni kwa madaktari wenyewe hao wa heshima.

Nakumbuka kwenye moja ya matukio yaliyokuwa yakitangazwa live Mubashara na TV zetu, mmoja wa viongozi aliteleza ulimi na kumuita Mkuu wa nchi "Mheshiwa Mungu" mbele ya Mkuu huyo wa nchi, Mkuu yule alicheka tuu kwa kujua mzungumzaji ni ameteleza tuu ulimi.

Yule aliyeita Mheshimiwa Mungu, hakuomba radhi, bali alirekebisha tuu na kuendelea,
View: https://youtu.be/6y3V86aZYf0?si=kJQf8vmFWBtauuAC

Na Mkuu wa nchi alipokuja kuhutubia, aliendelea tuu na hotuba yake as if nothing happened!. Kikichokuja kutokea is now a history!, kwasababu hakuna ajuye sababu, this could have been kulichangia!.

Alichopaswa kufanya Mkuu wa nchi ni kukemea!. Huwezi kuitwa Mungu kimakosa radhi isiombwe na wewe kuendelea as if nothing happened!.

Hivyo kwenye hili la kuitana titles za udakitari wa heshima, kugeuzwa ni title rasmi, kitendo cha waitwa kutokemea, au kukaa kimya, tafsiri yake ni ama wanapuuza, ama wanaridhia, ama wanafurahia.

Kwasababu sio wao wanao jiita madaktari, na maadam ni title ya heshima, kuna ubaya gani mtu kuheshimika na kuitwa title ya heshima ya usomi ubobezi na ubobevu ili hali ni title ya heshima tuu?, hivyo kuitwa anahesabika kuridhia!, jee tuwashauri viongozi wetu wakemee?.

Kufuatia maendeleo ya utandawazi kumeibuka vyuo vikuu vya mtandaoni, online universities zinazouza shahada za kununua, bila hata kuingia darasani, vyuo vikuu hivi vya mtandaoni vina issues Ph. D za heshima kwa kulipia tuu tena ni dola 100 tuu!, hili lisipotolewa muongozo na ufafanuzi, utafikia wakati tutashindwa kutofautisha yupi ni Daktari wa kweli wa kusomea, Daktari wa heshima, na Daktari wa kununua makaratasi, tutakuja kuichanganya jamii yetu.

Mbona kwa wanasheria hili limewezekana ili mtu kuwa wakili, lazima uthibitishwe na Jaji Mkuu wa Tanzania na kusajiliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, hivyo TCU yenye jukumu la kutoa ithbati ya vyuo vikuu, hii madaktari wa heshima kuitwa madaktari na kuandikwa madaktari , kuna haja ya kulitolea ufafanuzi au tujiachie tuu kwasababu sini jina tuu?. What's a big deal kuhusu titles?. The rationale, tunapo puuza na kudharau vitu vidogo vidogo, ndio mwisho wa siku, tunadharau vikubwa, tunaishia kulia!.

Wasalaam
Paskali

Tatizo waTZ uchawa na unafiki umetujaa. Wanaowaita hao waheshimiwa kwa title hiyo ya u-Dr wengine wanajua kabisa kwamba wanachofanya sio sahihi!
 
Sasa kwani hata akiitwa nini kinabadilika..

Kwa Tz PhD hata hizo za kusomea zimesaidia nini taifa ukiacha angalao wanaofundisha, kufanya tafiti na kutibu binadamu au Wanyama na Mimea.?

Ukinitajia Dr yeyote kwenye siasa za Tz kwa sasa mwenye impact na kujali mambo yanavyoenda nintashukuru mno...

Dr Charles Kimei.. anahoroja tu bungeni.
Dr Kitila Mkumbo... Hola
Dr. Ndakidemi.. sijui hata yupo wap.
Dr. Tulia... Mlamba miguu wa executives.
Dr Kabudi.... yupo kweli
Dr. Bashiru...
Dr. Ryoba.. kaigeuza TBCC channel ya katuni
Dr. Jafo.. kaamua kuwa mpole.
Dr Biteko..😀.

Embu tuishie hapo.

Dr. Taletale
Dr. Joseph Kasheku Msukuma.
 
Wanabodi, kama kawa, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa.

Mada ya leo ni pongezi kwa Rais Samia kwa kutunukiwa Ph.D nyingine ya heshima, Je wajua mtu kutunukiwa Ph.D ya heshima, hakumfanyi mtunukiwa kuitwa Dr. as an official title? Ila ni rukhsa kuitwa Dr. socially!. Je tumshauri Rais Samia akemee kuitwa Dr officially?

Pia je kuna haja kwa TCU kuutoa tena ule ufafanuzi kuhusu matumizi ya title ya Dr. kwa Ph.D za heshima za honoris causa, kama ulivyotolewa na Prof. Joseph Kironde kwenye moja ya majarida ya TCU?

View attachment 2780800

Na jee kuna haja kwa MCT, TEF, na Maelezo watoe muongozo kwa Media kuwaita au kuwaandika watu kwa title za Dr, watu ambao sio madakitari?

Udakitari ni title ya heshima, na uko udakitari wa aina kuu mbili ambao wanaitwa Dr as an official title, na udakitari wa 3 ni udakitari wa heshima, ambapo mtunukiwa haitwi Dr.

Hawa ni
1. Madaktari wa kusomea kitu chochote cha medical, iwe ni udakitari wa binadamu, mifugo, mimea etc.
2. Udakitari wa falsafa Ph. D ambao is earned kwa academic achievements.
3. Udakitari wa heshima ambao is not earned, but ni granted.

Kwanza nijiunge na Watanzania wengine kumpongeza Rais wetu Samia kwa ziara yake ya kiserikali nchini India, pongezi zangu za kwanza ni kwenda kwa ndege yetu ya ATCL, hakuna kitu kinakuza utalii kama uwepo wa direct flights, hivyo kitendo cha dege letu la Tanzania, kutua viwanja vikubwa vya kimataifa, ni sifa na heshima kubwa kwa nchi yetu.

Napongeza sana hili kwasababu ni moja ya mada zangu za nyuma, yenye kichwa cha habari, "Kwanini Rais Wetu Anaposafiri Nje ya Nchi, Apande Ndege za Wengine, Wakati Sisi Ndege hizo tunazo na uwezo huo tunao!. Je, Uzinduzi Royal Tour ungekuwa na maana kama Rais Samia angetua kwa Dreamliner & ATC kuzindua Direct Flights from DAR-JFK-DAR/JRO-JFK-JRO?

Nikashauri, gharama isiwe hoja, nikashauri aandamane na ujumbe wa wafanyabiashara watakao jilipia, Hongera Rais Samia, Kwenda US, Kuhutubia UN, Safari ya Kuzindua Filamu Yako ya Royal Tour, Tunaomba Tukusindikize, Dreamliner Yetu Itue New York
hili limefanyika, hongera sana!.

La tatu ni lile nililoliibua kwenye ule mkutano wa Rais na vyombo vya habari wa mwaka 2016, niliposhauri rais wetu anapofanya ziara za Kitaifa nje ya nchi, aandamane na media, both public na private, na pia tuko waandishi wa kujitegemea wenye uwezo wa kujilipia, tushirikishwe. Ziara hii ya India local media zetu zimeshirikishwa kikamilifu, hongera Zuhura Yunus!.

Mada ya leo ni kuhusu shahada za heshima, honoris causa, jee mtunukiwa anapaswa kuitwa Daktari na kuandikwa Daktari?. Hapa pia nimpongeze Rais Samia kutunukiwa shahada ya pili ya heshima ya udakitari na moja ya vyuo vikuu vya India vyenye heshima kubwa sana duniani.

Japo Rais Nyerere, Mwinyi na Mkapa, walitunukiwa PhD za heshima za honoris causa lakini hawakuitwa kwa title za Dr. Lakini Rais Jakaya Kikwete na Mzee Reginald Mengi, baada ya kutunukiwa waliitwa Dr na kuandikwa Dr hadi na sisi media tuliwaandika hivyo.

Baada ya Rais Samia kununikiwa shahada ya heshima ya udakitari wa falsafa pia tumeanza kumuita Daktari na kumuandika Daktari.

Na juzi tena nchini India, Rais Samia kaheshinishwa tena kwa PhD nyingine ya heshima, hii sasa ni ya pili. hakuna ubishi kuhusu Rais Samia kustahili heshima hii anastahili kabisa.

Ila kiukweli shahada za heshima, yaani PhD za honoris causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa japo Jakaya Kikwete na Mzee Mengi walipopewa waljitwa Dr, kwa PhD ya honoris causa, haya yalikuwa ni makosa, tusiendeleze makosa haya kwa Rais Samia!

Tuiombe TCU ilifafanue hili, kwa kuzingatia hoja ya Prof. Joseph Kironde.

Naomba kwanza tutofautishe mtu kujiita Dr, Professa, tulikuwa na Profesa Matikisa, Profesa Singira, Profesa Maji Marefu, Dr. Manyaunyau, Dr. Ngwizukulu Jilala, Dr. Mwaka, rais wa Manzese, rais wa Wasafi, rais wa Yanga, hakuna ubaya wowote mtu kujiita vyovyote, na kuna kuitwa, sio wewe bali wanaokuita, Dr, Prof, rais au kuitwa vyovyote pia hakuna ubaya wowote mtu kuitwa vyovyote as long as ni informally, lakini unapoandika jina lako kwenye usajili wowote, rasmi, lazima utatumia majina rasmi na title rasmi.

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama, ametunukiwa Ph. D za heshima 14!, lakini huwezi kusikia popote akiitwa Dr au kuandikwa Dr.

Kwa vile huu utaratibu wa shahada za heshima, sio utaratibu wetu wa jadi zetu, viongozi wetu wanapotunukiwa Ph. D hizi, ni vyema tukaufuata utaratibu na utamaduni wa shahada hizo.

Wananchi, rukhsa kuwaida Daktari, na kwenye mikutano ya kawaida, ila kwa sisi media, na kuandikwa kama title, hili linahitaji Ufafanuzi wa TCU, na baada ya TCU kama ilivyofafanuliwa na Prof. Joseph Kironde kwenye jarida la TCU, kuna haja kwa TCU kulitolea ufafanuzi. Na baada ya TCU kulifafanua, MCT nayo ilitolee muongozo kwa vyombo vya habari kuhusu kuwataja au kuwaandika madaktari hawa wa heshima kwa titles za udakitari.

La mwisho, ni kwa madaktari wenyewe hao wa heshima.

Nakumbuka kwenye moja ya matukio yaliyokuwa yakitangazwa live Mubashara na TV zetu, mmoja wa viongozi aliteleza ulimi na kumuita Mkuu wa nchi "Mheshiwa Mungu" mbele ya Mkuu huyo wa nchi, Mkuu yule alicheka tuu kwa kujua mzungumzaji ni ameteleza tuu ulimi.

Yule aliyeita Mheshimiwa Mungu, hakuomba radhi, bali alirekebisha tuu na kuendelea,
View: https://youtu.be/6y3V86aZYf0?si=kJQf8vmFWBtauuAC

Na Mkuu wa nchi alipokuja kuhutubia, aliendelea tuu na hotuba yake as if nothing happened!. Kikichokuja kutokea is now a history!, kwasababu hakuna ajuye sababu, this could have been kulichangia!.

Alichopaswa kufanya Mkuu wa nchi ni kukemea!. Huwezi kuitwa Mungu kimakosa radhi isiombwe na wewe kuendelea as if nothing happened!.

Hivyo kwenye hili la kuitana titles za udakitari wa heshima, kugeuzwa ni title rasmi, kitendo cha waitwa kutokemea, au kukaa kimya, tafsiri yake ni ama wanapuuza, ama wanaridhia, ama wanafurahia.

Kwasababu sio wao wanao jiita madaktari, na maadam ni title ya heshima, kuna ubaya gani mtu kuheshimika na kuitwa title ya heshima ya usomi ubobezi na ubobevu ili hali ni title ya heshima tuu?, hivyo kuitwa anahesabika kuridhia!, jee tuwashauri viongozi wetu wakemee?.

Kufuatia maendeleo ya utandawazi kumeibuka vyuo vikuu vya mtandaoni, online universities zinazouza shahada za kununua, bila hata kuingia darasani, vyuo vikuu hivi vya mtandaoni vina issues Ph. D za heshima kwa kulipia tuu tena ni dola 100 tuu!, hili lisipotolewa muongozo na ufafanuzi, utafikia wakati tutashindwa kutofautisha yupi ni Daktari wa kweli wa kusomea, Daktari wa heshima, na Daktari wa kununua makaratasi, tutakuja kuichanganya jamii yetu.

Mbona kwa wanasheria hili limewezekana ili mtu kuwa wakili, lazima uthibitishwe na Jaji Mkuu wa Tanzania na kusajiliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika, hivyo TCU yenye jukumu la kutoa ithbati ya vyuo vikuu, hii madaktari wa heshima kuitwa madaktari na kuandikwa madaktari , kuna haja ya kulitolea ufafanuzi au tujiachie tuu kwasababu sini jina tuu?. What's a big deal kuhusu titles?. The rationale, tunapo puuza na kudharau vitu vidogo vidogo, ndio mwisho wa siku, tunadharau vikubwa, tunaishia kulia!.

Wasalaam
Paskali

Ninashauri tarehe aliyopata digirii iwe siku ya mapumziko.
 
Hayati JPM aliwahi kusema, "Tulichezewa Mno".
Ngozi nyeupe huwa wanapiga hesabu kwanza kabla ya kufanya chochote.
Huenda tayari walishaona fursa!
 
Back
Top Bottom