Kwa hotuba hii ya Rais, Tujiandae na mgomo mkubwa wa madaktari

Ama kweli siasa ni mchezo mchafu jamaa kawatanguliza madaktari jana kwa baiskeli ya mbao yeye kaja na vogue..... kweli kama mtu makini hotuba ya leo ilikuwa ni matusi na dharau kwa madaktari. Nachelea kusema wawakilishi wa madaktari walioongea faragha na mkuu pengine wamewasaliti wenzao kwa kula mbivu na kuwaachia mbichi wengine...... Mhhhhh hii ni balaaaa.
 
Kikwete no MTAWALA siyo KIONGOZI. Angekuwa ni kiongozi asingezungumzia sana mgogoro wa serikali na madaktari zaidi ya kusema kwamba amekaa nao na kuna mambo ya msingi serikali yake inashughulikia. Kilichonichefua, ni ile staili yake ya kuongea kana kwamba yeye ndiye mshindi na kwa kweli kwa mtizamo wangu ni kama amewatukana madaktari mbele ya wananchi. Ushauri wangu ni kwamba kuna haja ya madaktari kutoa maelezo kuhusu maneno ya rais ili nao wajisafishe mbele ya wananchi. Wasipofanya hivyo, itakuwa kama watoto wa shule tu wanaodanganywa kwa chips mayai.
 
WanaJF
Nimesikiliza kwa kituo hotuba ya JK. Naamini ilikuwa na malengo yafuatayo:

1. Kuwadhalilisha madaktari kuwa hawana uzalendo kwa kudai mishahara isiyowezekana (Sh Milioni 7 na milioni 17 kwa mwezi)

2. Kuwagombanisha madaktari na wananchi ili jamii iwaone kama watu wasiofaa ndani ya jamii.

3. Kuwashuhudia uongo madaktari kwa kueleza na kupotosha historia nzima ya mgomo na kudai watendaji wake akiwemo katibu mkuu waliwajibika ipasavyo. Mfano sakata la interns kudai eti waliondolewa muhimbili kwa sababu kulikuwa kumejaa wakati si kweli, na mengine mengi

4. Kuwageuka madaktari ambao walirejea kazini kwa kuelezea kuwa na imani na Rais baada ya mazungumzo yao, lakini leo amekuja kuwachambua na kuwasemea mbovu mbele ya wananchi na hata kupoteza dhana nzima ya makubaliano yaliyofanyika Ikulu last weekend.

5. Kumshambulia Dr Ulimboka kama alivyomshambulia Mgaya personally mwaka 2010. Hata hivyo ameshindwa kujua kuwa MAT ni chama cha madaktari Tanzania na sio chama cha madaktari wa serikali.

Katika maelezo yake yote hakuna hata sehemu moja ambapo JK ameelezea namna alivyosuluhisha ama atakavyosuluhisha na kutekeleza madai ya madaktari na hasa dai la kuwawajibisha waziri na naibu wake ili mazungumzo yaweze kuendelea baina ya pande mbili zinazoaminiana. Kutokana na hali hiyo, tutarajie yafuatayo muda wowote kuanzia sasa:

1. Madaktari kuitisha mkutano na wanahabari kuelezea uongo ulioshuhudiwa na Rais kuhusu chanzo cha mgomo.

2. Madaktari kuelezea ukweli juu ya makubaliano yaliyofikiwa Ikulu ambayo yalifanya mgomo usitishwe.

3. Madaktari kuelezea kutokuwa na imani na Rais siku mbili baada ya kuongea naye na baada ya kuwageuka na hivyo kuitisha mgomo mkubwa zaidi ya yote iliyotangulia.

4. Na mengineyo meeengi pia......//

Matatizo yote haya chanzo ni hotuba yake ya leo. Madaktari wasilaumiwe kwa hatua yoyote watakayoichukua sababu Rais wetu ameonyesha kutokuwajali wananchi kwa namna yoyote.

Hata hivyo, sitashangaa kama madaktari wakiamua kuchukua uamuzi wa kuudhihirisha uongo wa JK na kisha wakampuuza na kuendelea na majukumu yao.

Hizi post zenu kwa mliobahatika kushiriki ktk hio hotuba mnatuchanganya kwani report zenu zinakinzana na kuashiria ushabiki wa kisiasa!
 
Hatimae tumefikia kwenye win win na mgogoro umeisha. Msitake kuchochea mambo yaliyoisha.
 
JK mshenzi sana. anafikiri kuwa kila kitu kinaweza kumalizwa kisiasa. Hiyo ndiyo hasara ya kuwa na raisi ambaye upeo wa akili zake ni kama za bata. Kuwatanguliza wanae mbele yeye kubaki nyuma huku akijidai kuwalinda ilihali hatari nyingi hutokea mbele kuliko nyuma. Shenzi zake kabisa. anatoa matusi ya kipuuzi kwa kutumia misemo ya kikwere, amenikasirisha sana, samahani kama lugha itawa......anaboa sana huyu mpu......!!!!
 
Ma-Dk walitakiwa baada tu ya mkutano wao na Rais ambao kimsingi haukuwa umepangwa, ulikuja kwa kustukiza tu; walitakiwa mara baada ya kikao kile waitishe mkutano wa wana habari na kufunguka ni nini yaliyojiri Ikulu lakini wao wakatoka huko wakamsifi Rais ni mwenye busara na msikivu. sasa usikivu na hekima ndiyo hii tuloisikia leo?

Hivi hao ma dokta hawakusoma alama za kwa nini JK aliahirisha ghafla kukutana na wazee kabla hajakutana nao? Sasa sijui watakuja na hoja gani maana mkulu keshameza hoja zao zote.

Kweli akili sio ujanja.
 
Hapa Serikalii Kupitia Kwa Rais ndo wanaleta Siasa Kwenye swala la Msingi!kaongea na madaktari alafu anawageuka Kwa Wananchi kwa Kudanganya,Mimi naamini serikali hii tiatia maji sana!!Tunaongozwa na watu Bogazzzz sijapata Kuona!!!Kwa ili simuungi Mkono hata Kidogo JK washauri wake wanafiki sana!!

Sasa kitakacho tokea Mtaona Madaktari tupo tayari Kufukuzwa kwaajili ya Kutetea haki zetu,Hiii serikali bwana ipo ipo tuuuuu!!Huyuuuu anasema hili yule anasema lile!!
 
Nalikumbuka vizuri tangazo la Madaktari kurudi kazini. walisema kwakuwa final ni Rais na wamempa live. wanamwamini na wanajua hawezi kuwaangusha hivyo wakarudi kazini bila masharti. Yani leo ndo nimegundua ukubwa wa tatizo. Isue umeishaimaliza hata kama hutekelezi ungekaa kimya. jamaa katia mafuta motoni. bahati mbaya huu mgomo wabongo wengi wanaujua kiundani sana hakukuwa na sbb ya historia pale. alitakiwa kuwaomba radhi waathirika na kuwatakia afya njema, kisha akatoa porojo za kuboresha mwisho kama mkuu wa dola angepiga bit la mgomo ulikuwa ilegal na ikitokea kuna isue awasihi wakae mezani la hatavumilia tena ilegality.mwisho porojo kidogo then wale wazee wa ccm unawatia mpunga unasepa. option 2 ilikuwa akae kimya. sasa kalikoroga tena.
 
Ma-Dk walitakiwa baada tu ya mkutano wao na Rais ambao kimsingi haukuwa umepangwa, ulikuja kwa kustukiza tu; walitakiwa mara baada ya kikao kile waitishe mkutano wa wana habari na kufunguka ni nini yaliyojiri Ikulu lakini wao wakatoka huko wakamsifi Rais ni mwenye busara na msikivu. sasa usikivu na hekima ndiyo hii tuloisikia leo?

Hivi hao ma dokta hawakusoma alama za kwa nini JK aliahirisha ghafla kukutana na wazee kabla hajakutana nao? Sasa sijui watakuja na hoja gani maana mkulu keshameza hoja zao zote.

Kweli akili sio ujanja.

Kama JK aliweza kuidhinisha posho na kisha akamgeuka waziri mkuu wake na spika kuwa hajaidhinisha, anashindwa nini kuwageuka madaktari???
 
Nalikumbuka vizuri tangazo la Madaktari kurudi kazini. walisema kwakuwa final ni Rais na wamempa live. wanamwamini na wanajua hawezi kuwaangusha hivyo wakarudi kazini bila masharti. Yani leo ndo nimegundua ukubwa wa tatizo. Isue umeishaimaliza hata kama hutekelezi ungekaa kimya. jamaa katia mafuta motoni. bahati mbaya huu mgomo wabongo wengi wanaujua kiundani sana hakukuwa na sbb ya historia pale. alitakiwa kuwaomba radhi waathirika na kuwatakia afya njema, kisha akatoa porojo za kuboresha mwisho kama mkuu wa dola angepiga bit la mgomo ulikuwa ilegal na ikitokea kuna isue awasihi wakae mezani la hatavumilia tena ilegality.mwisho porojo kidogo then wale wazee wa ccm unawatia mpunga unasepa. option 2 ilikuwa akae kimya. sasa kalikoroga tena.

mkuu hapo umenichekesha sana lol, ingawa point zako zote hapo juu ni valid
 
Back
Top Bottom