Kwa hotuba hii ya Rais, Tujiandae na mgomo mkubwa wa madaktari

Hivi iwapo wanachi watawachukia madaktari kutokana na maneno ya kikwete, halafu madakari wakawajibu kuwa kama mnamuamini Kikwete basi nendeni kwake akawatibu, ni nani atakeyumia katika mvutano huo?

Mawaziri wetu wanatembea na dola elfu nne kama vijisenti vya kujikimu, wakati serikali hiyo haitaki kuwalipa madakatri kiasi hicho kwa kazi yao ngumu ya kuendeleza uhai wa taifa hili; je wa kulaumiwa awe nani? Ningekuwa dakatri ningerudisha hiyo stethoscope yangu mfukoni ili tuzungumze tena na Kikwete nimuulize alikotoa hiyo jeuri ya kutangaza kuwa madakatari ni waongo. Iwapo madakatari wangekuwa ni waongo, kila prescription wanayioandika ingekuwa inaua mtu!
 
mm nashangaa sana, jk amekaa muda wote akizungumza juu ya madaktari wakati kuna mambo mengi ambayo angepaswa kuzungumza. Tena karudi yale yale yaliyokuwa yanaongelewa.

Ndio kilichotegemewa. Ukiasikia rais anaongea na wazee wa kijiweni, basi ujue ni majungu matupu.:eek:
 
Kama kutatokea mgomo wa madaktari basi viongozi watakuwa si kina Ulimboka na wenzake walioenda Ikulu.

Waliongea tu hakuna zaidi, lakini jamani, usitake kuwa nabii wakati unajijuwa kuwa una dhambi!

Hawarudii tena na wala hawatoongelea tena, nasema labda wawe viongozi wengine wa madaktari na si wale walioenda Ikulu. Kama mnabisha tazameni kama hata wataongelea zaidi, pengine kwa sasa hata mikutano hawaitishi tena. Mkisikia Serikali ina "mkono mrefu" kama hamjui maana yake muulizeni Dokta Ulimboka.
 
Moderators, halafu hii habari ya madaktari ni siasa? kwanini haipelekwi jukwaa la kazi? mimi nnachoona ni mfanya kazi alimgomea mwajiri wake kwa kutaka maslahi bora, au kuna kingine?
 
Hayo ndo matokeo ya kuongozwa na rais asiye na hekima.

Ila the guy ni disaster kwelikweli. Inashangaza sana kwamba hajui hata nyakati tulizonazo, kwamba anashangaa madaktari kuomba majibu ya waziri mkuu yawe kwenye maandishi? Ameniacha hoi kweli kwenye hili kwani cha ajabu ni ninin hapa? Inaonesha anapenda kweli mambo yaishie jukwaani then basi. Halafu kwanini yeye anajiona kama Mungu vile? Eti aliyemweka waziri ndiye aliyemwekea naibu kwani huyo mtu yuko mbinguni mpaka anashindwa kuwaondoa hao watu kiasi kwamba watu inabidi waendelee kufa tu? Halafu kwa kuwa mawaziri ni wapitaji so waendelee tu kutuulia watu wetu na sisi tuwaache kwa kuwa ni wapitaji kwenye wizara? jk when will you be serious with the lives of poor tanzanians?
 
Mkuu, hiyo siyo win-win style, bali ni Win-lose management conflict!

Hivi Presida hata kama haya maongezi yake anaandikiwa (alkikuwa akisoma) si anaweza kuona kama kilichoandikwa si kizuri akakiacha na kusema aaminicho kinatakiwa? Ninauliza tuu kwa wajuao
 
Ila the guy ni disaster kwelikweli. Inashangaza sana kwamba hajui hata nyakati tulizonazo, kwamba anashangaa madaktari kuomba majibu ya waziri mkuu yawe kwenye maandishi? Ameniacha hoi kweli kwenye hili kwani cha ajabu ni ninin hapa? Inaonesha anapenda kweli mambo yaishie jukwaani then basi. Halafu kwanini yeye anajiona kama Mungu vile? Eti aliyemweka waziri ndiye aliyemwekea naibu kwani huyo mtu yuko mbinguni mpaka anashindwa kuwaondoa hao watu kiasi kwamba watu inabidi waendelee kufa tu? Halafu kwa kuwa mawaziri ni wapitaji so waendelee tu kutuulia watu wetu na sisi tuwaache kwa kuwa ni wapitaji kwenye wizara? jk when will you be serious with the lives of poor tanzanians?

Huna zaidi? JMK ndio kaongea na kaelezea kilichojiri, sasa madaktari wafanye ujeuri, mbona walipotoka Ikulu waliacha mgomo? kama huna zaidi ya ufataani ni bora ukae kimya.
 
Hivi Presida hata kama haya maongezi yake anaandikiwa (alkikuwa akisoma) si anaweza kuona kama kilichoandikwa si kizuri akakiacha na kusema aaminicho kinatakiwa? Ninauliza tuu kwa wajuao

Ulimuona alipokuwa akiongea? alikuwa hasomi hotuba, alikuwa akisoma notes.

Ni kipi hujakipenda. Kaelezea migomo mitatu iliyoungana, kaelezea baadhi ya madaktari kubadili masharti kila wanapopewa fursa ya kuongea na wawakilishi wa Serikali, kaweka wazi kila kitu. Nini hujakipenda?

Alipokuwa kimya, kila mmoja wenu, mwenye chuki tu kwa Kikwete, alikuwa analalamika yupo kimya, baada ya kuweka mambo sawa na kuudhibiti mgomo, kawaita wazee kuwaelezea kupitia kwao, nalo kwako pia ni kosa. Ulitaka akae kimya? ulitaka aongee? ulitaka mgomo uendelee? maana haya ndio yale? "hatumtaki" kwa tuhuma zipi? kimyaa!
 
Kama kutatokea mgomo wa madaktari basi viongozi watakuwa si kina Ulimboka na wenzake walioenda Ikulu.

Waliongea tu hakuna zaidi, lakini jamani, usitake kuwa nabii wakati unajijuwa kuwa una dhambi!

Hawarudii tena na wala hawatoongelea tena, nasema labda wawe viongozi wengine wa madaktari na si wale walioenda Ikulu. Kama mnabisha tazameni kama hata wataongelea zaidi, pengine kwa sasa hata mikutano hawaitishi tena. Mkisikia Serikali ina "mkono mrefu" kama hamjui maana yake muulizeni Dokta Ulimboka.

Nakubaliana na ww kwamba ma-Drs hawatagoma, simply bcz wamejiridhisha kuwa mtu wa mwisho wa madai yao ana upeo finyu sana tena sana, so even if ma-drs,manesi na wafamasia wote wa govt na private wakagoma; na 1/2 watz wakafa, bado jk atawaita wazee wake wa dar akamwaga ut...bo wake with no solution. Hivyo bila shaka akina ulimboka walibaini hilo na kuahirisha mgomo na madai yao until next govt phase, pia naamini hawatakaa meza moja kwa sasa badala yake wataachia 'self equilbrium adjustments' ishughulikie mgogoro huu kwa sasa. Iko fahamu Faiza Foxy!!?
 
binafsi sikufanikiwa kuisikiliza yote ila kwa maneno machache niliyoweza kuyasikia kwenye hotuba yake ni kwamba atazungumza na madaktari, wakati nilitegemea atasema atafanya mchakato wa kutimiza matakwa ya madaktari hata kama siyo yote ila kwa asilimia kubwa atatimiza. haya mazungumzo mpaka lini tunataka vitendo now.
 
WanaJF
Nimesikiliza kwa kituo hotuba ya JK. Naamini ilikuwa na malengo yafuatayo:

1. Kuwadhalilisha madaktari kuwa hawana uzalendo kwa kudai mishahara isiyowezekana (Sh Milioni 7 na milioni 17 kwa mwezi)

2. Kuwagombanisha madaktari na wananchi ili jamii iwaone kama watu wasiofaa ndani ya jamii.

3. Kuwashuhudia uongo madaktari kwa kueleza na kupotosha historia nzima ya mgomo na kudai watendaji wake akiwemo katibu mkuu waliwajibika ipasavyo. Mfano sakata la interns kudai eti waliondolewa muhimbili kwa sababu kulikuwa kumejaa wakati si kweli, na mengine mengi

4. Kuwageuka madaktari ambao walirejea kazini kwa kuelezea kuwa na imani na Rais baada ya mazungumzo yao, lakini leo amekuja kuwachambua na kuwasemea mbovu mbele ya wananchi na hata kupoteza dhana nzima ya makubaliano yaliyofanyika Ikulu last weekend.

5. Kumshambulia Dr Ulimboka kama alivyomshambulia Mgaya personally mwaka 2010. Hata hivyo ameshindwa kujua kuwa MAT ni chama cha madaktari Tanzania na sio chama cha madaktari wa serikali.

Katika maelezo yake yote hakuna hata sehemu moja ambapo JK ameelezea namna alivyosuluhisha ama atakavyosuluhisha na kutekeleza madai ya madaktari na hasa dai la kuwawajibisha waziri na naibu wake ili mazungumzo yaweze kuendelea baina ya pande mbili zinazoaminiana. Kutokana na hali hiyo, tutarajie yafuatayo muda wowote kuanzia sasa:

1. Madaktari kuitisha mkutano na wanahabari kuelezea uongo ulioshuhudiwa na Rais kuhusu chanzo cha mgomo.

2. Madaktari kuelezea ukweli juu ya makubaliano yaliyofikiwa Ikulu ambayo yalifanya mgomo usitishwe.

3. Madaktari kuelezea kutokuwa na imani na Rais siku mbili baada ya kuongea naye na baada ya kuwageuka na hivyo kuitisha mgomo mkubwa zaidi ya yote iliyotangulia.

4. Na mengineyo meeengi pia......//

Matatizo yote haya chanzo ni hotuba yake ya leo. Madaktari wasilaumiwe kwa hatua yoyote watakayoichukua sababu Rais wetu ameonyesha kutokuwajali wananchi kwa namna yoyote.

Hata hivyo, sitashangaa kama madaktari wakiamua kuchukua uamuzi wa kuudhihirisha uongo wa JK na kisha wakampuuza na kuendelea na majukumu yao.
BUSARA IMEKOSEKANA KATIKA HOTUBA YA JK.Hotuba ya Rais tulitemea mambo mawili kuvunja baraza la mawaziri au kuwafukuza waziri wa afya na makamu wake.Kuwashambulia Wanaharakati na Madaktari ni matusi kwani ni wao waliomzindua usingizini na kujua nini kinachoendelea katika wizara ya afya,hali ambayo iko katika wizara zote na taasisi za umma na serikali.Inaeleweka ya kua amesita kuchukua hatua za kuwafukuza waziri na naibu wa waziri wa afya kwa sababu yangezuka maeneo mengine.Je Wizara ya nishati na madini mambo,ulinzi,maliasili n.k.hali shwali?Kwa hotuba ya Rais nimefikia CONCLUSION MAWAZIRI NA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI NA MASHIRIKA YA UMMA REFLECTION AU KIOO CHA UTAWALA NA RAIS MWENYEWE JK.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
hata mimi sikuipenda hotuba yake yenye zarau nyingi na majigambo,
yenye kuwazalilisha hata wana harakati,
siwezi kukataa maneno ya mwl. nyerere kuwa mkulu bado ana umri mdogo
kuweza kuwa president.
 
Ukweli mimi ningekuwa ni Dr. Ulimboka, basi ninetoa ama\ri moja tu kuwa madakatari wote waweke chini manati yao (Stethoscopes). Mwanasiasa kumchezea dakatri ni kuhatarisha sana uhai wa taifa hili; wamezowea kuwachezea waalimu na kufanikiwa kujenga taifa la watu wajinga kiasi kuwa kazi za siasa zimebaki kuwa zao na familia zao, sasa iwapo wanataka kuahamisha mchezo huo na kuwachezea madakatri basi watajenga taifa la maiti kwa kufuta watu wote ambao siyo wa koo zao. Na hilo wengi hatutalikubali, kwani hatuwezi kuacha ndugu zetu wafutike kwa vile tu hatuna madaraka ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom