Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.



Nawasilisha!

Dada Regia kama hayo mambo umeyaona Igunga tu na huamini kama yapo sehemu zingine basi inaonekana hujaizungukia Tanzania, Jaribu kupita mikoa yote japo wilaya mbili tu kwa kila mkoa na na tarafa mbili kwa kila wilaya utakayofika, na upitie kata mbili kwa kila tarafa utakayofika na mwisho kabisa vijiji viwili kwa kila kata halafu baadaye uje useme kama Igunga ina tofauti na sehemu zingine.
 
wajemeni shida hizo ziko kila mahali hata kule karatu. Rostam alikuwa mbunge tu, kazi ya kuondoa kero hizo ni ya serikali.... aghh!
Huwezi kulinganisha kazi aliyoifanya Dr. Slaa Karatu na hali ya Igunga chini ya Rostum. Nenda Karatu kajionee mwenyewe au waulize watu wanaotoka huko.
 
Utashauri nini wakati Watanzania hawako tayari kubadilika? Kwa mfano, Rostam Aziz ndiye Mbunge aliyekuwa na ushiriki mdogo zaidi kati ya wabunge wa kawaida. Rostam ndiye mbunge pekee ambaye hakuchangia kwa namna yoyote ile kaika kipindi chake chote cha miaka mitano bungeni lililopita. Kama maendeleo uliyoghusia ndio hayo, wapiga kura wake walishawahi kumshikilia bango? Pia wabunge wa kuchaguliwa ndio wanaongoza kwa ushiriki zaidi ya wale wa kuteuliwa. Don't take personally, b'se this is in according to utafiti uliofanywa.

Nilichoongelea hakiwezi kubadilika mpaka pale Watanzania kwa ujumla watakapoamua kubadilika. Otherwise ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Hata hivyo, kila chama cha siasa na kwa kila Mbunge inabidi kufafanua zaidi ni kwa namna gani wamekuwa wakitumika kwa maslahi ya majimbo yao. Mijadala ya wazi ni muhimu kwa kukuza sio tuu demokrasia bali pia uwajibikaji. "Wabunge" wachache sana ni wabunge Tanzania. Hakuwa na hatakuwa Rostam tuu. Hili ni tatizo la kitaifa na sio tatizo la Igunga tuu.
Mkuu sikubaliani kabisa unapodai eti hao wananchi hawataki kubadilika.At least kwasababu uchaguzi umeshakamilika na matokeo ya idadi za kura umeyaona.Then tatizo haliwezi kuwa eti hawataki kubadilika.Mkuu weka maanani pia namba ya wale ambao walinyimwa fursa ya kupiga kura,na wale ambao walishindwa kwenda kupiga kura kwa sababu mbali mbali siwezi kuzitaja hapa zote.Tizama idadi ya wananchi walioipigia ccm kura uchaguzi huu na zile zilizopita.Its just a matter of time wananchi watafunguka macho kwa wingi zaidi.Wewe umepewa hadi ukweli kuwa hata vijana wadogo hawajui kusoma.Sasa hapo ndipo penye shida hata kama ni kweli wamekataa kubadilika,ukweli ni kwamba uelewa wao ni mdogo na solution si kusema tu hawataki kubadilika.Bali kuwasaidia kwa kuwapa elimu na pia ile ya uraia.Na pia kwa sababu ya uelewa wao mdogo,ndio maana bado idadi ya wapiga kura ni ndogo sana kulinganisha na population kwa ujumla.Kuhusiana na wabunge wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa sina comment kwa sasa.Pia sikubaliana na generalisation yako ambayo intention yake ni ku neutralise hoja.Hata kama tatizo ni la kitaifa na si la RA kama unavyodai.Bado RA ndiyo ametokea kuoneka onekana kama Fisadi papa lao.From sijui Kagoda to EPA to Richmond yumo.Sasa at least angewaonea huruma wananchi masikini.Kuongoza TZ inahitaji huruma nilishasema mara nyingi tu hapo nyuma.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Regia dadangu kwani hujui kwamba UMASIKINI na ELIMU DUNI ni mtaji mzuri sana wa CCM na CCM-B??

Wanapokuwa masikini zaidi ndo inapokuwa rahisi hata kuwadanganya au unawapa kitu kidogo tu tayari umeshawachota akili zote.

Check huo Ubwabwa kwa maharage au kwa mchuzi na nyama moja. Regia wewe huutamani huo ubwabwa?!!
 
Pole sana ndugu yangu naona kauli zako ni za mtu aliyekata tamaa. Chama na watu wa kuleta mabadiliko wapo.

Yawezekana nimekata tamaa,...lakini yawezekana wewe ndo umekata tamaa
na hutaki kuamini hivo.
Kila mtu anajua kipimo cha moyo wake ni vipi ana jiona kuhusu hali fulani.
Point yangu ni kwamba hakuna chama chenye kusimamia kinayo amini,....

Hapa ndipo unapo kuja umuhimu wa nguvu ya umma,...nguvu ya umma sio chadema
wala chama chochote,nguvu ya umma ni wananchi wenyewe.

Kazi ni je,wananchi hawa walio ibiwa miaka nenda rudi usiku na mchana,ni nani
ata waamsha wasi muone kwamba ni "sawa na wale"?

Hebu jiulize:-
CCM wametumia zaidi ya bilioni 3
CHADEMA wametumia zaidi ya 400 milioni
CUF wametumia zaidi ya 200 milioni
Wengine wametumia kama 10 milioni,....

kwa hesabu za kitoto ni kama 3.6 bilioni hivi.
Zote hizi zimetumika katika jimbo moja tu la Igunga,...jimbo lisilo kuwa na maji
na elimu mbofu mbofu.

Inashindikana nini kwa vyama hivi ambavyo vyote vinajidai kuipenda sana igunga
kutoa hela sawa na walizo tumia kwenye kampeni kuwachimbia wana Igunga visima vya maji?

Damn,....nisije pewa ban mie.
 
Ulishawahi kujaribu kubadilisha behaviour ya mtu mzima ambaye hana nia kabisa ya kutaka kubadilika? If so, how much luck did you have with your attempts to change them? Ulishajaribu kuchange behaviour ya spouse, partner or parent who had no interest in changing? How did that work out for you? My guess is that if you have tried, you have been consistently unsuccessful. In fact, you may have even alienated the person you were trying to enlighten. If they don't care do not waste your time.

Suala sio Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani? Suala hapa ni kama Watanzania wanataka kubadilika. Kama wanataka kubadilika wala haitachukua mwezi kubadilika. Kwani iliwachukua muda gani kwa Watunisia na Wamisri kubadilika? Hakuna aliyewabadilisha Watunisia au Wamisri. Ni wao wenyewe waliamua kutaka mabadiliko. Walipofikia uamuzi wa kubadilika wala haikuwachukua muda kupata haya mabadiliko.

Kimsingi, huwezi kumbadilisha mtu mzima ambaye hataki kubadilika. Ni mpaka pale atakapoamua yeye mwenye kuwa anataka kubadilika ndiyo unaweza kumsadia kubadilika. Research on coaching is clear and consistent. Coaching is most successful when applied to people with potential who want to improve, not when applied to people who have no interest in changing. Same applies to politics. So, the question is not when Tanzanian will change and who will change them but whether they have a willing to change.
Mkuu mfano wako ni mzuri lakini ni irrelevant hapa.Wananchi wa Tanzania siyo watu wazima peke yao.Unless utuambie mtu mzima ni nani kwenye definition yako?Unapozungumzia Tz unazungumzia pia na vijana.Kama na wao umewaweka kwenye kundi la "Utu uzima" basi niwie radhi.Kwenye hiyo research ya coaching factors za umri ziliwekwa?Given the fact that umetaja "utu uzima" kama kigezo.
 
Mkuu sababu ulizotoa za watu kujitokeza kupiga kura si za kweli!Jamani tusitumie hisia zetu katika masuala yanayopaswa kufanyiwa utafiti..Sababu za turn out kuwa ndogo hiyo yako haipo..
Haya tupe sababu mlozifanyia utafiti maana unapopinga unakuwa na jibu tayari.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
mheshimiwa mimi naona matatizo tanzania yanafanana tu ispokuwa baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi ambapo viongozi wao waliiba rasilimali za nchi mapema na wakanufaisha maeneo yao.

matatizo uliyoyazungumza hata Kirombero yapo na wewe ndiyo mbunge kivuli wa jimbo la Kirombero kama alivyo Kashindye katika Jimbo la Igunga hivyo ni vyema ukaanza na huko kwanza kabla ya kunyooshea kidole Igunga; mfano Kirombero nyaya za umeme zinapita juu ya nyumba za wananchi kuelekea mijini huku wananchi hao wakiwa gizani; Kirombero ardhi inagawiwa kama pipi tu!

Tatu sisi wana Igunga tunampenda sana Rostam kwa ucheshi wake ambao unaleta amani utulivu; hatupendi viongozi wanaotoka kwenye vyama vya kumwagiana Tindikali na kuvua watu hijabu, hivyo ROSTAM hata kama angegombea tena katika uchaguzi ulioisha juzi bado tungempa asilimia 80 ya kura zote na huyo mgombea wenu asingepata hata asilimia 5.
 
The root cause ni sisi wenyewe Watanzania.

Politicians use us for their own benefits because we Tanzania don't really bother anymore. Ili mradi tunaenda haja kubwa, that's what matter to us now. Our future generation tumeisahau kabisa. And we will be punished for this. Asha Dii alianzisha thread moja muhimu sana juu ya trend ya African Politics (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-politics-historia-itajirudia-tanzania-5.html) ambapo nilisema: We create problems, which in turn we use them to buy votes from voters. Whether wangeshinda Chadema, CUF au walivyoshinda CCM, by 2015 hali mbaya ya maendeleo jimbo la Igunga itaendelea kuwa vile vile. Trust me on this.

Our political game is based on manipulating the poor and illiterate. We create opportunities of dependency to the government and this way the poor always put the same leader, leadership style in power. We the people make our leaders whether new or old what they are. Our leaders in a large measure a reflection of the totality of our attitude to everything. Leadership is sustained by fellowship.

I agree with you completely...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Haya tupe sababu mlozifanyia utafiti maana unapopinga unakuwa na jibu tayari.

Zipo nyingi Mkuu,nitazitaja chache

1. Vituo vya kupitia kura vimewekwa mbali mno,mtu anatembea hadi 13kms kufuata kupiga kura.
2. Wengine unakuta familia nzima hawajui kusoma na kuandika hivyo anaona tabu kutafuta msaada wa kusaidiwa kupiga kura
3. Wapo wengi waliotoa malalamiko ya kupoteza shahada zao na hawakupata msaada.
4. Wapo waliuza shahada zao sababu ya fedha ndogo
5. Siku ile ya kupiga kura kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na shughuli nyingine kama vile minada hivyo wengine wala na bora wajitafutie chochote kuliko kwenda kupiga kura.
6. Si wote waliojiandikisha lengo lao lilikuwa ni kupiga kura,wengi walijiandikisha kwa lengo la kuwa na kitambulisho kitakachowasadia katika shughuli zao nyingine,hivyo kupiga kura kwao ni subsidiary kwakuwa hajui faida wala hasara za kupiga kura.
 
mheshimiwa mimi naona matatizo tanzania yanafanana tu ispokuwa baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi ambapo viongozi wao waliiba rasilimali za nchi mapema na wakanufaisha maeneo yao.

matatizo uliyoyazungumza hata Kilosa yapo na wewe ndiyo mbunge kivuli wa jimbo la Kilosa kama alivyo Kashindye katika Jimbo la Igunga hivyo ni vyema ukaanza na huko kwanza kabla ya kunyooshea kidole Igunga

Tatu sisi wana Igunga tunampenda sana Rostam kwa ucheshi wake ambao unaleta amani utulivu; hatupendi viongozi wanaotoka kwenye vyama vya kumwagiana Tindikali na kuvua watu hijabu, hivyo ROSTAM hata kama angegombea tena katika uchaguzi ulioisha juzi bado tungempa asilimia 80 ya kura zote na huyo mgombea wenu asingepata hata asilimia 5.

Am from Kilombero,not Kilosa!
 
Rostam na alaaniwe kwa kuwadidimiza na kuwakandamiza watanzania wa Igunga. Ipo wana-Igunga watapata ufahamu na atahama Igunga kwa hiari yake arudi Iran. Silaha yake ya kuwatawala ilikuwa ni kuhakikisha hawapati elimu wala taarifa tofauti na propaganda zake. Ndo maana akawahonga simu mabalozi. Mungu wape wana-Igunga ufahamu mapema kabla ya 2014, wawaadhibu magamba kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
 
Huwezi kulinganisha kazi aliyoifanya Dr. Slaa Karatu na hali ya Igunga chini ya Rostum. Nenda Karatu kajionee mwenyewe au waulize watu wanaotoka huko.

Hawezi kukuelewa huyo na inaonekana anaongelea ndani ya chupa ya chai......nimekaa Karatu na naifahamu na Igunga naifahamu japo kidogo kwa kupita mara nyingi kwenye shughuli zangu na huwezi linganisha maeneo haya mawili..

Kanikera sana kudhalilisha ukweni na kupalinganisha na kwa Rost Hamu............
 
Zipo nyingi Mkuu,nitazitaja chache

1. Vituo vya kupitia kura vimewekwa mbali mno,mtu anatembea hadi 13kms kufuata kupiga kura.
2. Wengine unakuta familia nzima hawajui kusoma na kuandika hivyo anaona tabu kutafuta msaada wa kusaidiwa kupiga kura
3. Wapo wengi waliotoa malalamiko ya kupoteza shahada zao na hawakupata msaada.
4. Wapo waliuza shahada zao sababu ya fedha ndogo
5. Siku ile ya kupiga kura kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na shughuli nyingine kama vile minada hivyo wengine wala na bora wajitafutie chochote kuliko kwenda kupiga kura.
6. Si wote waliojiandikisha lengo lao lilikuwa ni kupiga kura,wengi walijiandikisha kwa lengo la kuwa na kitambulisho kitakachowasadia katika shughuli zao nyingine,hivyo kupiga kura kwao ni subsidiary kwakuwa hajui faida wala hasara za kupiga kura.
Bibie,hilo la sita ulloandika hapo ndilo linameza habari nyingine zote.. Kama watu wamejiandikisha kupiga kura ili wapate vitambulisho vya mambo mengine ina maana wamechoka na upigaji kura kwa sababu hawana imani na siasa zetu na sii kwamba hawajui faida na hasara zake - wanajua hakuna FAIDA! Huu ndio ukweli, haya maswala la gulio na kadhalika hayawezi kuwa na maana kwao kama wanajua kutakuwepo na mabadiliko wakiwachagua wabunge wao iwe CCM au Chadema tena kwa kumsimamisha mbunge ambaye maisha yake ni hohehahe kama wao. Akili zao zinawatuma kwamba wanamjengea maisha bora mtu huyo mbunge na sii wao (Of which it's true)..Yale yale ya kutoaminiana.

Kwa hiyo umeona umuhimu wa kitambulisho, kitambulisho kinaweza kubadilisha maisha yao ktk sehemu zinginezo na sii kupiga kura na ndiko ukweli ulikosimama. Acha Igunga, mimi nina hakika majority ya Watanzania wamejiandikisha kupiga kura kwa sababu hii wapate kitambulisho cha kupiga kura kama ID ya makazi na uraia wao na umuhimu wake wanaujua wao, lakini basi nyie Wabunge wetu mnapinga kutolewa kwa vitambulisho vya Kitaifa na kuviona havina maana wakati mahitaji yake ni makubwa sana kuliko maelezo kwa raia kina sisi tusokuwa na majina.
 
K4C:
Tukitaka kuchangia mfuko huo tufanyeje? japokuwa mimi ni mwana igunga lakini kuna ndugu zangu wengi sana wanaishi kirombero!
 
Yawezekana nimekata tamaa,...lakini yawezekana wewe ndo umekata tamaa
na hutaki kuamini hivo.
Kila mtu anajua kipimo cha moyo wake ni vipi ana jiona kuhusu hali fulani.
Point yangu ni kwamba hakuna chama chenye kusimamia kinayo amini,....

Hapa ndipo unapo kuja umuhimu wa nguvu ya umma,...nguvu ya umma sio chadema
wala chama chochote,nguvu ya umma ni wananchi wenyewe.

Kazi ni je,wananchi hawa walio ibiwa miaka nenda rudi usiku na mchana,ni nani
ata waamsha wasi muone kwamba ni "sawa na wale"?

Hebu jiulize:-
CCM wametumia zaidi ya bilioni 3
CHADEMA wametumia zaidi ya 400 milioni
CUF wametumia zaidi ya 200 milioni
Wengine wametumia kama 10 milioni,....

kwa hesabu za kitoto ni kama 3.6 bilioni hivi.
Zote hizi zimetumika katika jimbo moja tu la Igunga,...jimbo lisilo kuwa na maji
na elimu mbofu mbofu.

Inashindikana nini kwa vyama hivi ambavyo vyote vinajidai kuipenda sana igunga
kutoa hela sawa na walizo tumia kwenye kampeni kuwachimbia wana Igunga visima vya maji?

Damn,....nisije pewa ban mie.

you got a point.

lakini, hapo kwenye nyekundu hapo, mh.......pananikumbusha dilemma ya kuchagua "kula yai au kusubiri atotolewe kuku?" ama ile nyingine ya kuchagua "kula gunia la mbegu au kupanda mbegu ili uje upate mavuno yake?".

hizi dilemma nyingine.....kaazi kwelikweli!
 
Mkuu wangu, ktk hili nadhani mnakosea sana kufikiria ktk ufinyu huo. Binadamu anabadilika sana tu. Na sii mtu anayembadilisha mwenzake isipokuwa mazingira yaliyopo yatakulazimu ubadilike.

Yapo maswala ambayo yanamhusu mtu mmoja mmoja na yapo ya kijamii, hivyo maendeleo ya jamii ndiyo tunayozungumzia na kama utayaweka mazijngira ktk hali fulani lazima watu watabadilika. Kama leo kuna barabara ya magari sidhani kama watu watashindwa kununua magari wakaendelea kusafiri na Punda. Sema mazoea yana taabu sana. kama watu wamezoea kuomba omba sii rahisi kuwashawishi wafanye kazi ili kujipatia maisha bora lakini kama mazingira yatawalazimu kutafuta kazi na miaya ya ombaomba akaondolewa basi wengi wao watalazimika kutafuta na kufanya kazi..

Hivyo kubadilisha mazingira ili kuwawezesha wananchi kufuata mkondo wa matayarisho hayo ndio kazi ya serikali inapojenga miundombinu, na sera zinazo walazimu wananchi wake kuchukua mkondo mpya ktk maendeleo yao. Leo hii bila elimu hupati ajira itabidi uende shule na vijana wengi wanakimbilia shule siku hizi, lakini lazima pia ajira zenyewe lazima ziwepo na ziwe na malipo ya kumwezesha maisha bora zaidi ya yale alokuwa nayo. Hii ndio kazi ya viongozi na wasomi wetu kuandaa mazingira haya kwa wananchi wake.

Binadamu hubadilika kulingana na mazingira yaliyopo, leo hii tupo hapa JF kutokana na utaalam wa tovuti ktk mawasiliano. Yale maswala ya kuandika barua za salaam sana ama baada ya salaam umekwisha - Tumebadilika!

Mkuu sikatai kama binadamu habadiliki. Suala kubwa ni willingness ya binadamu kubadilika. Kama binadamu hana willingness ya kubadilika hata ukicreate mazingira ya kubadilika itakuwa ngumu kumbadilisha. On the other hand, unaweza kuweka mazingira katika hali fulani ku influence watu kubadilika. Lakini kama nilivyosema mwanzoni our political game is based on manipulating the poor and illiterate. We create opportunities of dependency to the government and this way the poor always put the same leader, leadership style in power. Politicians wanajua wazi kuwa waki create mazingira ya watu kubadilika hawatakaa madarakani. Umeona yaliyomkuta Mubarak na policy yake ya kuhakikisha kuwa kila nyuma ina at least one computer na internet connection?
 
Dada yote unayosema hapa ni kweli kabisa lakini mbona hamkuyasema wakati mkiwa Igunga?
Kwa kweli katika kampeni ile ya Igunga hakuna neno ambalo CDM haikuwaeleza wana Igunga, yote haya si tu walielezwa bali wanayaona wao wenyewe pale Igunga, lakini sijui ni wapi wanaIgunga hawakuelewa hadi wakaipa CCM kura 26,000, kwa kweli huitaji kufika hata darasa la kwanza kujua kama CCM ni wababaishaji, lakini wapi bwana!!!. Mimi inafikiaga level nasema ngoja tu waonje gharama za kufanya uamuzi mbovu, ili baadae iwe rahisi kuwakumbusha walipojikwaa. Miaka mitano sio mingi.

Kuna ambao mwaka 2010 waliwapigia kura CCM sasa hivi wanatoa milio ya kila aina huku mtaani, mana kwanza elimu ndogo, ajira hakuna, hata ukipata ajira mshahara kiduchu, inflation rate ni balaa, mahitaji ya muhimu bei juu, petrol haishikiki, umeme ndo hivyo. kwa kweli hakuna rangi ambayo hawaioni sasa hivi. I believe, 2015 wote tutakuwa tunaongea lugha moja.
 
Mkuu sikatai kama binadamu habadiliki. Suala kubwa ni willingness ya binadamu kubadilika. Kama binadamu hana willingness ya kubadilika hata ukicreate mazingira ya kubadilika itakuwa ngumu kumbadilisha. On the other hand, unaweza kuweka mazingira katika hali fulani ku influence watu kubadilika. Lakini kama nilivyosema mwanzoni our political game is based on manipulating the poor and illiterate. We create opportunities of dependency to the government and this way the poor always put the same leader, leadership style in power. Politicians wanajua wazi kuwa waki create mazingira ya watu kubadilika hawatakaa madarakani. Umeona yaliyomkuta Mubarak na policy yake ya kuhakikisha kuwa kila nyuma ina at least one computer na internet connection?
Mkuu wangu hakuna kitu willingness mahala kuna serikali. Kazi ya serikali ni kuhakikisha binadamu anabadilika ili kupata maendeleo. Kweli wapo wanaokataa na kupingana na serikali ili kusetiri tamaduni zao lakini leo hii wanahesabika. Makosa makubwa ya hawa jamaa zetu ni kwamba wanafanya usanii kwa kuweka ahadi badala ya kujenga matumaini ktk mabadiliko yao.

Na ndio maana tunashindwa kuwaamini na hakika ukiniuliza mimi niseme ukweli kama nawaamini Chadema nitakwambia siwaamini baadhi ya WATU, but it worth a try kuliko kuendelea na CCM japo kuwa sitaki kufanya majaribio ktk maisha ya watu... Hivyo kinachonisukuma ni kukubali kumpa nafasi Chadema na nauona urahisi wa kumwondoa Chadema akivurunda kuliko kumwachia CCM ambaye kwa kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanavyozidi kupata nguvu ya shetani kusimika nguzo zao.

Amini maneno yangu mkuu sii kweli kwamba Watanzania hawataki mabadiliko isipokuwa hawana FAITH na siasa zetu na pasipo imani kwa uhakika trust, hope na belief zinaondoka. Bahati mbaya viongozi wetu wameshindwa kujenga imani za watu, historia inatufundisha mengi ya kutoaminiana, usanii umechukua nafasi kubwa ya maisha yetu yaani hata Utajiri mtu anaupata kwa kuchonga misheni..Kwa hiyo sii rahisi mkuu wangu kunishawishi hata mimi leo ktk jambo jema bila mimi kukuwekea mashaka wewe...Na wewe utakuwa mtu wa kukuchunga zaidi ya shughuli unayoifanya. Hivyo mimi nakua sifanyi kazi isipokuwa kukuchunga na kupoteza muda wa kujiendeleza. Na nikiacha kukuchunga utaniacha mataani!... MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO.
 
Mkuu sababu ulizotoa za watu kujitokeza kupiga kura si za kweli!Jamani tusitumie hisia zetu katika masuala yanayopaswa kufanyiwa utafiti..Sababu za turn out kuwa ndogo hiyo yako haipo..

..Wana Igunga 120,000 kutopiga kura inatuonyesha kwamba hawana imani na siasa zetu, hawana imani ya uchaguzi wala wagombea wake kwa sababu wanajua hapatakuwepo na mabadiliko yoyote. Igunga itabakia Igunga ile ya toka Uhuru.

Kama kwenye huo utafiti hii sababu haipo, basi huo utafiti kautupe tu kwa sababu utakuwa either umepikwa au walioufanya utafiti ni "magarasa" tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom