Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Mimi nadhani huu ndio wakati muafaka kawa mwanasiasa wa kweli, kwenye kampeni husemi mtu, rostam kwa sasa ni mwanacham tu, haikuwa sahihi kuyasema haya akiwa kule
Dada yote unayosema hapa ni kweli kabisa lakini mbona hamkuyasema wakati mkiwa Igunga?
 
EMT unafikiri hao Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani?

Utashauri nini wakati Watanzania hawako tayari kubadilika? Kwa mfano, Rostam Aziz ndiye Mbunge aliy

ekuwa na ushiriki mdogo zaidi kati ya wabunge wa kawaida. Rostam ndiye mbunge pekee ambaye hakuchangia kwa namna yoyote ile kaika kipindi chake chote cha miaka mitano bungeni lililopita. Kama maendeleo uliyoghusia ndio hayo, wapiga kura wake walishawahi kumshikilia bango? Pia wabunge wa kuchaguliwa ndio wanaongoza kwa ushiriki zaidi ya wale wa kuteuliwa. Don't take personally, b'se this is in according to utafiti uliofanywa.

Nilichoongelea hakiwezi kubadilika mpaka pale Watanzania kwa ujumla watakapoamua kubadilika. Otherwise ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Hata hivyo, kila chama cha siasa na kwa kila Mbunge inabidi kufafanua zaidi ni kwa namna gani wamekuwa wakitumika kwa maslahi ya majimbo yao. Mijadala ya wazi ni muhimu kwa kukuza sio tuu demokrasia bali pia uwajibikaji. "Wabunge" wachache sana ni wabunge Tanzania. Hakuwa na hatakuwa Rostam tuu. Hili ni tatizo la kitaifa na sio tatizo la Igunga tuu.
 
Waache wafu wazike wafu wenziwe.
Rais mwenyewe hajui kwa nini Nchi yake ni maskini so ni ngumu sana pia watu wa IGUNGA kujua kwa nini wao ni maskini na ndo maana wameichagua CCM kwa mara nyingine.
 
...........Tatizo watu ni wabinafsi sana, Kama si selfish nini hasa!!! Rostam utajiri aliokuwa nao angeweza kabisa kuboresha jimbo lake.
 
UWEZO TUNAO,
Mkuu hakika wewe ndio umeitoa picha halisi ya TANZANIA yetu, hii sii Igunga tu bali sehemu kubwa ya nchi yetu iko hivi.. tazama darasa hili ukitazama madawati mawili tu unapata wanafunzi 45 na zaidi halafu kuna mwalimu mmoja!.. Hapa kweli tutajisifia kwa ujenzi wa shule wakati hili darasa lilitakiwa kuhudumiwa na walimu 5 ktk madarasa tofauti!.

Ebu jamani watazameni hawa vijana wetu, kesho wakianza fujo kwa viongozi wetu tunapiga makelele kuwa ni wahuni, hali hakuna kati yetu anaweza kuishi ktk hali hii hata kwa siku moja..Mimi ningeomba wenye TV wafanye mchezo wa kuwaweka wabunge na mawaziri wetu ktk mazingira haya kwa mwezi mmoja tu halafu tupate kuona nani kati yao atakuwa na ujasiri wa kumaliza muda huo.
 
EMT unafikiri hao Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani?
Watanzania watabadilika siku ukiwaweka ktk mazingira ya kubadilika. Sisi wengine tumetoka vijijini na tumebadilika kwa kila hatua ya maisha tuloikuta au maendeleo tuloyaona. Tulijisaidia machakani bila kuona aibu wala noma, tukaenda mijini tukakuta mambo tofauti na ndio kujifunza kwetu kumetokana zaidi na yale tuloyaona ama kuyakuta.

Inasikitisha sana kumsoma Rostam ambaye alikuwa right handman wa JK hakuwafanyia kitu wananchi wake zaidi ya kuwagawia fedha za mlo mmoja, lakini ndivyo walivyo wabunge na viongozi wetu wengi sana. Dar ni mji unaopanuka sana lakini tazama basi hauna mifereji (sewerage system) wala hatujengi toka chini kuhakikisha kama kutatokea mafuriko maji hayatakaa!.. nyumba zinajengwa kiholela, visima vya maji kila nyumba kama matayarisho ya makaburi yetu wenyewe..Kifupi sioni la kusifia utawala huu maana nakumbuka mimi miaka 45 iliyopita nilikuwa Kibara, Mwibara kulikuwa na maji safi tukinywa maji toka ktk bomba. Leo Kibara ile ya miaka ya 60 huipati ktk wilaya nyingi za Tanzania...
 
EMT unafikiri hao Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani?

Ulishawahi kujaribu kubadilisha behaviour ya mtu mzima ambaye hana nia kabisa ya kutaka kubadilika? If so, how much luck did you have with your attempts to change them? Ulishajaribu kuchange behaviour ya spouse, partner or parent who had no interest in changing? How did that work out for you? My guess is that if you have tried, you have been consistently unsuccessful. In fact, you may have even alienated the person you were trying to enlighten. If they don't care do not waste your time.

Suala sio Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani? Suala hapa ni kama Watanzania wanataka kubadilika. Kama wanataka kubadilika wala haitachukua mwezi kubadilika. Kwani iliwachukua muda gani kwa Watunisia na Wamisri kubadilika? Hakuna aliyewabadilisha Watunisia au Wamisri. Ni wao wenyewe waliamua kutaka mabadiliko. Walipofikia uamuzi wa kubadilika wala haikuwachukua muda kupata haya mabadiliko.

Kimsingi, huwezi kumbadilisha mtu mzima ambaye hataki kubadilika. Ni mpaka pale atakapoamua yeye mwenye kuwa anataka kubadilika ndiyo unaweza kumsadia kubadilika. Research on coaching is clear and consistent. Coaching is most successful when applied to people with potential who want to improve, not when applied to people who have no interest in changing. Same applies to politics. So, the question is not when Tanzanian will change and who will change them but whether they have a willing to change.
 
Dah! hii habari imenishtua sana, pia siwezi kushangaa kwani siyo Igunga peke yake ukitembelea baadhi ya majimbo kadhaa utakutana na hali kama hii... Hii hali haikupaswa kuwa sehemu ambayo tajiri mkubwa na kifisadi wa kimataifa Rostam anatoka, nilitegemea wananchi wa huko wangekuwa na maendeleo kwa kiasi flani hivi....

Kwenye hii dunia ya sasa ukiwa hauna elimu ni taabu sana, sasa sipati picha hao vijana na watoto wasiyo jua kusoma wala kuandika hatima yao itakuwa je? Hizi lawama pia serikali inahusika moja kwa moja, maana kwa kushindwa kuwapa wananchi wake haki zao muhimu kama elimu na Afya...

Hii mdio miaka 50 ya uhuru tunajivunia? hakika tumepiga hatua kubwa kwa kufanya wananchi wake mbumbumbu..... Ili tatizo alitoisha kama wananchi wenyewe hatuta amka na kuwapigania wenzitu ambao wanakandamizwa kwa kuto kujua haki zao.

DSC_0491.jpg
Nimependa sana hii hoteli ya kitalii
 
Ulishawahi kujaribu kubadilisha behaviour ya mtu mzima ambaye hana nia kabisa ya kutaka kubadilika? If so, how much luck did you have with your attempts to change them? Ulishajaribu kuchange behaviour ya spouse, partner or parent who had no interest in changing? How did that work out for you? My guess is that if you have tried, you have been consistently unsuccessful. In fact, you may have even alienated the person you were trying to enlighten. If they don't care do not waste your time.

Suala sio Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani? Suala hapa ni kama Watanzania wanataka kubadilika. Kama wanataka kubadilika wala haitachukua mwezi kubadilika. Kwani iliwachukua muda gani kwa Watunisia na Wamisri kubadilika? Hakuna aliyewabadilisha Watunisia au Wamisri. Ni wao wenyewe waliamua kutaka mabadiliko. Walipofikia uamuzi wa kubadilika wala haikuwachukua muda kupata haya mabadiliko.

Kimsingi, huwezi kumbadilisha mtu mzima ambaye hataki kubadilika. Ni mpaka pale atakapoamua yeye mwenye kuwa anataka kubadilika ndiyo unaweza kumsadia kubadilika. Research on coaching is clear and consistent. Coaching is most successful when applied to people with potential who want to improve, not when applied to people who have no interest in changing. So, the question is not when Tanzanian will change and who will change them but whether they have a willing to change.
Mkuu wangu, ktk hili nadhani mnakosea sana kufikiria ktk ufinyu huo. Binadamu anabadilika sana tu. Na sii mtu anayembadilisha mwenzake isipokuwa mazingira yaliyopo yatakulazimu ubadilike.

Yapo maswala ambayo yanamhusu mtu mmoja mmoja na yapo ya kijamii, hivyo maendeleo ya jamii ndiyo tunayozungumzia na kama utayaweka mazijngira ktk hali fulani lazima watu watabadilika. Kama leo kuna barabara ya magari sidhani kama watu watashindwa kununua magari wakaendelea kusafiri na Punda. Sema mazoea yana taabu sana. kama watu wamezoea kuomba omba sii rahisi kuwashawishi wafanye kazi ili kujipatia maisha bora lakini kama mazingira yatawalazimu kutafuta kazi na miaya ya ombaomba akaondolewa basi wengi wao watalazimika kutafuta na kufanya kazi..

Hivyo kubadilisha mazingira ili kuwawezesha wananchi kufuata mkondo wa matayarisho hayo ndio kazi ya serikali inapojenga miundombinu, na sera zinazo walazimu wananchi wake kuchukua mkondo mpya ktk maendeleo yao. Leo hii bila elimu hupati ajira itabidi uende shule na vijana wengi wanakimbilia shule siku hizi, lakini lazima pia ajira zenyewe lazima ziwepo na ziwe na malipo ya kumwezesha maisha bora zaidi ya yale alokuwa nayo. Hii ndio kazi ya viongozi na wasomi wetu kuandaa mazingira haya kwa wananchi wake.

Binadamu hubadilika kulingana na mazingira yaliyopo, leo hii tupo hapa JF kutokana na utaalam wa tovuti ktk mawasiliano. Yale maswala ya kuandika barua za salaam sana ama baada ya salaam umekwisha - Tumebadilika!
 
Dada Mtema!
Ukweli ni kwamba sehemu zote wanaposhinda ccm raia wake wana walakani!! nlowakwaza kwa hili wanisamehe buuuuuure!! Lakini huu ndiyo ukweli!

Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
 
WC,unafikiri haya unayoyapendekeza yakifanyika,matatizo haya tunayoyapigia kelele yataondoka?kimsingi nakubaliana na hoja yako ila najaribu kutafakari kwa kina,kwamba leo nchi yetu ikiamua kupunguza ukubwa wa Bunge,Serikali n.k.Je hali tuliyonayo sasa ya umaskini itapungua kwa kiasi gani?

Nadhani hajji sahihi Mkuu. Kila mwaka Bunge hupitisha Bajeti ya Wizara mbalimbali kwaajili ya Miradi mbalimbali hapa nchini lakini swali la kujiuliza je miradi hii hukamilika yote?na je fedha zinazotengwa huenda wapi?na je kama tukipunguza ukubwa wa Bunge na Serikali je fedha hizi zitatumika vizuri?accountability ya fedha itabadilika?kupunguza- ukubwa wa Bunge na Serikali ni unafikiri ni suluhisho la awali?tatizo la nchi yetu sio uwajibikaji?

Politician will always be politician.....dada unasema nini na unakataa nini?

Kutatua matatizo ya wananchi sio kwa njia moja tu, ziko nyingi na anazo sema Wilcard ni njia mojawapo, unabisha nini?

Topic yako nzuri sana kwa juuu juu, ila inasikitisha kumbe kuna sehemu mnajua matatizo mpaka mfike!

Ulichosema kuhusu Igunga ni sehemu kubwa ya nchi hii iko hivyo! nenda Ludewa kwetu, nenda ileje mbeya, nenda uvinza kigoma, nenda xxxx! ni Tanzania yetu.

kinachonihuzunisha mpaka kupelekea kuandika haya, ni kuwa unamaanisha ikitokea sehemu Mbunge wa CCM kafanya unayoyasema wewe basi aendelee kukaa madarakani! ndio maana sehemu za mafisadi waliowaletea maendeleo wananchi wao basi kwako wewe ni sawa! au je ulivyokuwa unaenda huko igunga ulifikiri ikoje hasa? maana mshtuko wako unaonyesha unaweza kuwa Pinda au Kikwete pindi ukija kuwa rais!

sisi wana sosholojia tunasababu ya kwa nini maeneo hayo hayo watu wanawaweka hao hao mnaosema wabaya! simply ushindi ni strategy kusema sema fulani hivi fulani vile haisaidii sana kwenye siasa, mnatakiwa kuwa na strategy ambazo kwa chama chenu hamna ,hazipo na huwa hamtaki kuambiwa wala kukosolewa.
 
THE NEW ROSTAM AZIZ AND THE IMAGINERY GOAL IN BARTER TRADE WITH CCM TODAY AND ON

Da Regia, what Rostam are you talking about here?? You must understand that at no time did Rostam Aziz go to parliament for the benifit of Tanzanians in Igunga.

Na sio Rostam tuu. Ubunge siku hizi umekuwa dili Tanzania. Unakuta mtu msomi na Ph.D au uprofessa anaacha fani yake na kukimbilia ubunge. Why? Kwa nini asitumie taaluma yake kusaidia taifa? Tatizo akishaingia kwenye siasa na contribution ya taaluma yake kwa taifa inapotea kabisa. Pia huu mtindo wa wafanyabiasha wakubwa kuingia kwenye politics umeharibu kabisa maana halisi ya ubunge.

This has unscheduled expectations from the voters of treating their MP as a provider of financial assistance. As Pius Msekwa once said: For as the old adage goes, ‘members of parliament are men and women of high rank, [but] they have nothing in the bank!". Wabunge wetu wana kiasi gani cha fedha benki? Tena tulishamwuliza Regia Mtema wanalipwa kiasi gani akasepa on the ground that kanuni za bunge zinamzuia kusema mshaharana marupurupu yake. How ridiculous it is that an employer does't even know how much they pay their employer?

Huyu jamaa hata ukimlaumu haisaidii sana,
Kwanza amepitia chaguzi za 1994, 1995, 2000,2005 & 2010 na wananchi wamempa kura,
Hapa bana wa kuwalaumu ni wana-Igunga wenyewe.
Hawa jamaa utafikiri walilishwa limbwata na huyu tapeli,
Cha ajabu anawawekea mtu na bado wanamchagua.
Hawa wana Igunga hawasaidiki kabisa,
Mungu aliamua kuwasaidia kuwakomboa but inawezekana wameshazoea shida wakaamua warudishe matatizo,
Hakuna haja ya kuwasemea na shauri zao wenyewe na huyo dalali wao,
Wacha awadalalie hata kidogo walichonacho!!
 
Ulishawahi kujaribu kubadilisha behaviour ya mtu mzima ambaye hana nia kabisa ya kutaka kubadilika? If so, how much luck did you have with your attempts to change them? Ulishajaribu kuchange behaviour ya spouse, partner or parent who had no interest in changing? How did that work out for you? My guess is that if you have tried, you have been consistently unsuccessful. In fact, you may have even alienated the person you were trying to enlighten. If they don't care do not waste your time.

Suala sio Watanzania wababadilika lini na watabadilishwa na nani? Suala hapa ni kama Watanzania wanataka kubadilika. Kama wanataka kubadilika wala haitachukua mwezi kubadilika. Kwani iliwachukua muda gani kwa Watunisia na Wamisri kubadilika? Hakuna aliyewabadilisha Watunisia au Wamisri. Ni wao wenyewe waliamua kutaka mabadiliko. Walipofikia uamuzi wa kubadilika wala haikuwachukua muda kupata haya mabadiliko.

Kimsingi, huwezi kumbadilisha mtu mzima ambaye hataki kubadilika. Ni mpaka pale atakapoamua yeye mwenye kuwa anataka kubadilika ndiyo unaweza kumsadia kubadilika. Research on coaching is clear and consistent. Coaching is most successful when applied to people with potential who want to improve, not when applied to people who have no interest in changing. Same applies to politics. So, the question is not when Tanzanian will change and who will change them but whether they have a willing to change.

Oh! yes you have made my day,

But let me put this foward with a very positive note..........you may change anybody, whether s/he like or not! but you need something extra to achieve that..you need convicing power!

Siasa za chadema haziwezi kumbadilisha mtu mzima, hatuna convicing people hatuna hakuna mtikila wale wa enzi hizo.... tunajua kutukana, kurusha makombora ya ufisadi na kulazimisha hoja iende tutakavyo..kwa nini mtu aisende kupata urabu wake na aendeleena umaskini wake!!

Is high time this party should employ expert in dealing with Tanzanians, ama sivyo unaweza ukawa kichaa bure...hivi chadema huwa wanafanya tafiti? za nini ? lini na wapi? Tanzania hii mtu anaweza kuibiwa mke na bado akampa kura aliyemuibia mke! something is very very wrong!

mwisho...mafanikio ya chadema ndio imekuwa barrier ya chama hiki kutokwenda mbele..complacent kills!

haya wakubwa nipo nipo tu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nadhani hujanielewa kaka,nisome vizuri tafadhali!

Politician will always be politician.....dada unasema nini na unakataa nini?

Kutatua matatizo ya wananchi sio kwa njia moja tu, ziko nyingi na anazo sema Wilcard ni njia mojawapo, unabisha nini?

Topic yako nzuri sana kwa juuu juu, ila inasikitisha kumbe kuna sehemu mnajua matatizo mpaka mfike!

Ulichosema kuhusu Igunga ni sehemu kubwa ya nchi hii iko hivyo! nenda Ludewa kwetu, nenda ileje mbeya, nenda uvinza kigoma, nenda xxxx! ni Tanzania yetu.

kinachonihuzunisha mpaka kupelekea kuandika haya, ni kuwa unamaanisha ikitokea sehemu Mbunge wa CCM kafanya unayoyasema wewe basi aendelee kukaa madarakani! ndio maana sehemu za mafisadi waliowaletea maendeleo wananchi wao basi kwako wewe ni sawa! au je ulivyokuwa unaenda huko igunga ulifikiri ikoje hasa? maana mshtuko wako unaonyesha unaweza kuwa Pinda au Kikwete pindi ukija kuwa rais!

sisi wana sosholojia tunasababu ya kwa nini maeneo hayo hayo watu wanawaweka hao hao mnaosema wabaya! simply ushindi ni strategy kusema sema fulani hivi fulani vile haisaidii sana kwenye siasa, mnatakiwa kuwa na strategy ambazo kwa chama chenu hamna ,hazipo na huwa hamtaki kuambiwa wala kukosolewa.
 
Hakika kijiji chetu kimekosa umeme tu,lakini kila kitu kipo in place na kila baada ya miaka mitano lazima tuwe na mbunge mpya,hatutaki mambo ya akina R.A,nilikuwa naona kwetu kuna shida kumbe wengine ni zaidi.Suala la maji ni yanamwagika kijiji kizima ukipenda unalipia unaingiza nyumbani kwako.
 
Politician will always be politician.....dada unasema nini na unakataa nini?

Kutatua matatizo ya wananchi sio kwa njia moja tu, ziko nyingi na anazo sema Wilcard ni njia mojawapo, unabisha nini?

Topic yako nzuri sana kwa juuu juu, ila inasikitisha kumbe kuna sehemu mnajua matatizo mpaka mfike!

Ulichosema kuhusu Igunga ni sehemu kubwa ya nchi hii iko hivyo! nenda Ludewa kwetu, nenda ileje mbeya, nenda uvinza kigoma, nenda xxxx! ni Tanzania yetu.

kinachonihuzunisha mpaka kupelekea kuandika haya, ni kuwa unamaanisha ikitokea sehemu Mbunge wa CCM kafanya unayoyasema wewe basi aendelee kukaa madarakani! ndio maana sehemu za mafisadi waliowaletea maendeleo wananchi wao basi kwako wewe ni sawa! au je ulivyokuwa unaenda huko igunga ulifikiri ikoje hasa? maana mshtuko wako unaonyesha unaweza kuwa Pinda au Kikwete pindi ukija kuwa rais!

sisi wana sosholojia tunasababu ya kwa nini maeneo hayo hayo watu wanawaweka hao hao mnaosema wabaya! simply ushindi ni strategy kusema sema fulani hivi fulani vile haisaidii sana kwenye siasa, mnatakiwa kuwa na strategy ambazo kwa chama chenu hamna ,hazipo na huwa hamtaki kuambiwa wala kukosolewa.
Mkuu wangu nimeipenda hii sana! Nawaomba sana sasa hivi tuweke nguvu kubwa ya kuwasukuma hawa viongozi wa Chadema, wachukie wasichukie ni kazi tunawakabidhi. Tuyaseme yote mabaya, makosa, machungu na yenye kuwakereketa ili wapate kuifanya kazi tunavyotaka sisi wananchi.

Nina hakika umefika wakati tuanze tena kuwalima kama tulivyofanya miaka ya nyuma..Tumewabeba sana na hakuna sababu ya kuelendelea kuwabeba ikiwa sisi ndio tunaoumizwa kila siku, wao wakifaidika na mishahara minono na posho ambazo hawaruhusiwi kuzisema kwa waajiri wao sisi wananchi. Na kama sikosei wakati ule Dr.Slaa na wengine wengi walishinda hapa JF kusikia vilio vya wananchi na tuendelee kuwakosoa wote hasa hiki chama cha Chadema kwa sababu ndio tumaini letu kama chama.

Na nina hakika watayafanyia kazi mengi tu, kwani huko nyuma mengi mloyasema kuhusu viongozi wake, mwelekeo wake ndio yaliwawezesha Chadema kufanya mabadiliko makubwa na hata leo kushika nafasi ya pili. Uwakilishi wa malalamiko yetu ndiko kutakowawezesha zaidi kuwakilisha iwe ndani ya chama au kitaifa. Nimeandika mengi sana ktk mada ya - Ichaguzi Igunga:- TUMEJIFUNZA NINI? na sasa naelekeza zaidi nguvu zangu kukikosoa chama na viongozi wake pale napoona makosa... Lengo sii kukivuruga chama bali kukielekeza chama kwa wananchi na sii wananchi kukifuata chama.
 
Huyu jamaa hata ukimlaumu haisaidii sana,
Kwanza amepitia chaguzi za 1994, 1995, 2000,2005 & 2010 na wananchi wamempa kura,
Hapa bana wa kuwalaumu ni wana-Igunga wenyewe.
Hawa jamaa utafikiri walilishwa limbwata na huyu tapeli,
Cha ajabu anawawekea mtu na bado wanamchagua.
Hawa wana Igunga hawasaidiki kabisa,
Mungu aliamua kuwasaidia kuwakomboa but inawezekana wameshazoea shida wakaamua warudishe matatizo,
Hakuna haja ya kuwasemea na shauri zao wenyewe na huyo dalali wao,
Wacha awadalalie hata kidogo walichonacho!!
Hapana mkuu wangu wala usiwalaumu wana Igunga, sema sisi tumejifunza kipi. Tanzania tuna tatizo moja kubwa sana la Uongozi. WATU hawaaminiki, hatuna kiongozi ambaye tunaweza kuweka imani zetu kwamba ana lengo na nia nzuri ya maendeleo yao hivyo wananchi wanamchagua Zimwi likujualo -halikuli likakwisha yaani pale walipofikia ndio maendeleo yao hawatataka kuona Igunga inarudi nyuma zaidi ya hapo..Wana Igunga 120,000 kutopiga kura inatuonyesha kwamba hawana imani na siasa zetu, hawana imani ya uchaguzi wala wagombea wake kwa sababu wanajua hapatakuwepo na mabadiliko yoyote. Igunga itabakia Igunga ile ya toka Uhuru.

Mwafrika bado kabisa kujenga ustaarabu wa kuaminika. Sisi ni Wapuuza, Walafi na Wabinafsi kiasi kwamba hata hatuwezi kuaminiwa na wazazi wetu wenyewe ingawa wana mapenzi makubwa juu yetu lakini huwawezi kutuamini. Na katika tabia ya kutoaminiana ndio maana mirathi ni janga kubwa sana, mzee hadi anakufa hajamrithisha mtoto wake hata mmoja kwa sababu anajua akimwachia urithi wake hao watoto wengine ndio wamekosa kila kitu.

Kusema kweli Igunga nna hakika Chadema wameshinda kwa kushindwa. tayari wananchi wamepata mwanga mkubwa sana hasa vijana ambao joto la jiwe limewawakia kwa miaka yote ya ujana wao. CCM imeshinda kutokana na wazee na kinamama ambao tulifaidika sana na mfumo wa mwalimu Nyerere. Shule bure, Hospital bure na waliweza kujenga maisha yao leo hii ni wastaafu wakiwa na mashamba yao ya kilimo. Ni maisha waliyoyazoea na hawatasahau hisani (ingawa ilikuwa right yao) ya CCM ktk makuzi yao.
 
ROSTAM AZIZI AKITUPORA KODI ZETU KULE BENKI KUU DAR ES SALAAM MAANA YAKE NI KWAMBA YEYE PAMOJA NA CCM WANATUAMBIA WATANZANIA TULIOKO VIJIJINI KWAMBA MSOTO NI HAKI YETU

Siri ya utajiri wa 'kijinga' wa Rostamu Aziz ni jasho la Wa-Tanzania wakiwemo hao nuvu kazi wa Igunga wanashindwa kutwa mzima wakisaka wasafiri wa kwenye Boda Boda kwenda huko madongo kuinama kusikofikika na chombo chochote kingine.

Nasema kwamba ni utajiri wa KIJINGA kwa sababu unaponenepesha mfuko wako wewe tu katika bahari kubwa kama vijana hao kwenye picha ambao nao wanatamani maisha mazuri, ni dhahiri kwamba mpaka hapo Roastamu anafanikiwa kuweka maisha yake rehani bure maana vijana hao watafika mahali watajiuliza kwamba huyu kapata toka wapi na sisi kwa nini tukose?????????????

Kama kuna mtu bado haamini kwamba hawa akina makapuku wenzetu ndio wanaomtajirisha Fisadi Rostam Aziz basi ukaanze tu kufikiria tozo za gali sana wanazotozwa kila wanapompigia mteja simu kwamba wanaenda kuchukua na baiskeli; kitu wasichokielewa vijana wengi ni kwamba Rostam anazo senti 50 kwa kila kicheko unachokipitisha kwa mwenzio kupitia ama simu za VODACOM au AIRTEL.

Wengine mnakumbuka nguvu iliotumika kumsukuma pembeni Prof Msolla alipotaka kutupunguzia kodi ya mawasiliano kwenye simu za viganjani.

Akina mama wakilima mtama kijijini hapo wakienda kuuza sokoni basi hutozwa kodi ambazo Wa-Tanzania tumekubaliana kwa pamoja tukazihifadhi kwenye Majenga Mapacha aka Majengo ya Balali pale Magogoni Dar es Salaam.

Fedha hizo zilizotokana na mkulima wa Igunga, kijana wa Boda Boda, mchimba madini wa Mererani, Mtanzania mlima kahawa Moshi na Bukoba (ambao siku hizi hawaitwi walipakodi bali ni WACHAGGA, CHUSA, SUKUMA na WAHAYA wakati wa kampeni za kisiasa) zote zikijumlishwa kwa pamoja pale Benki Kuu ya Taifa ndizo tunazommegea Dr Magufuli (heshima mbele) kujawajengeeni daraja la MBUTU iliomshinda Rostam Aziz

Hivyo ni vema Wana-Igunga wakaelewa kwamba ujezi wa daraja ni tangu mauzo yao ya mtama na uwele vijijini, kubeba watu kwenye Boda Boda, tozo HATARI kwenye simu tunazopiga ... wala wasije wakadhani kwamba kuna chama chochote nchini kikiwemo CCM kinachoweza kujigambia ujenzi wa kitu chochote nchini.

Kila kilicho chema unachokiona iwe ni barabara ya lami, maji safi na salam, tiba za kuaminika, nyumba nzuri za waalimu na mishahara yao hadi mishahara ya Rais Kikwete, ni mimi na wewe ndio tunaowalipa.

Sasa pale ambapo unasikia kwamba Wa-Tanzania tunawakaba koo viongozi wetu wa serikali si kwamba tuna hila bali ni kwamba Rostam Aziz akisaidiwa na maafisa wetu kutuibia pale tulikojihifadhia fedha zetu za kodi Benki Kuu maana yake ndio kama hivo wizi wa Rostam unawaelekeza watoto hao hapo juu wakae kwenye vumbi.

Ni kwamba watoto wetu wanakosa elimu bora huku Rostam Azizi yeye anapeleka mtoto wake aende akasome Ulaya na badala yake huyo naye hujigeuza taahira wa kutumia hela za masikini kupondea raha na mtoto wa Mugabe na darasani ziii!!!

Ndio, nasema maana maana ya maendeleo duni kabisa tunaoona huko Igunga ni kwamba kodi za wazazi wao hao watoto hapo juu tayari wamekamata wajanja wasiokua na utu wala huruma kwa maendeleo yetu, kwa ajili ya kununulia ukubwa na shahada za wapiga kura...

... kukodishia CUF Chombo-Cha- Mawinguni kwenye kampeni kama ilivyotokea Igunga huku baadhi ya wahariri wa vyombo mbali mbali nchini wakihongwa safari ya kwenda kuulizana New York maswali ambayo wangejiuliza wakiwa hapa hapa nchini.

Wana-Igunga, sehemu tu ya kero za Wa-Tanzania wenzenu kila pembe ya nchi ndio hayo. Wala sio siri kwamba ufisadi unapotokea maisha hugeuka kuwa magumu zaidi kwa walala hoi.

Na hapo ndipo Fisadi Rostam anapowaambia Wana-Igunga kwa hela zao anaziponda kwa raha zake na kwamba ni sharti waende hizo kilometa 13 kusaka maji, tiba, shule na mahitaji mengine mengi ambayo laiti Rostam Aziz na CCM wasingefanya ujambazi kama huo kila kitu kingekua bora, jirani zaidi na bila kulazimika kujikomba kwa mtu yeyote yule.

NB: Unapomaliza kusoma taarifa hii sasa kiambie mwenyewe kwamba 'TANGU SASA NI JUKUMU LANGU MWENYEWE KUWA CHACHU WA MABADILIKO YA KULETA AHUENI NCHINI NA KWAMBA KAMWE SITOUNGA MKONO UFISADI WOWOTE DHIDI YA MASIKINI WENZANGU NCHINI'.

Sasa nenda ukawaelimishe walau watu kumi zaidi kila siku, mijini na vijiji, ndipo mabadiliko yatakapopatikana Hii kazi si ya akina wale; ni jukumu la kila mtu nchini kwani mtaji mkubwa kwa CCM miaka yote ni UMBUMBUMBU wetu.

...........Tatizo watu ni wabinafsi sana, Kama si selfish nini hasa!!! Rostam utajiri aliokuwa nao angeweza kabisa kuboresha jimbo lake.
 
Mkuu sababu ulizotoa za watu kujitokeza kupiga kura si za kweli!Jamani tusitumie hisia zetu katika masuala yanayopaswa kufanyiwa utafiti..Sababu za turn out kuwa ndogo hiyo yako haipo..

QUOTE=Mkandara;2599663]Hapana mkuu wangu wala usiwalaumu wana Igunga, sema sisi tumejifunza kipi. Tanzania tuna tatizo moja kubwa sana la Uongozi. WATU hawaaminiki, hatuna kiongozi ambaye tunaweza kuweka imani zetu kwamba ana lengo na nia nzuri ya maendeleo yao hivyo wananchi wanamchagua Zimwi likujualo -halikuli likakwisha yaani pale walipofikia ndio maendeleo yao hawatataka kuona Igunga inarudi nyuma zaidi ya hapo..Wana Igunga 120,000 kutopiga kura inatuonyesha kwamba hawana imani na siasa zetu, hawana imani ya uchaguzi wala wagombea wake kwa sababu wanajua hapatakuwepo na mabadiliko yoyote. Igunga itabakia Igunga ile ya toka Uhuru.

Mwafrika bado kabisa kujenga ustaarabu wa kuaminika. Sisi ni Wapuuza, Walafi na Wabinafsi kiasi kwamba hata hatuwezi kuaminiwa na wazazi wetu wenyewe ingawa wana mapenzi makubwa juu yetu lakini huwawezi kutuamini. Na katika tabia ya kutoaminiana ndio maana mirathi ni janga kubwa sana, mzee hadi anakufa hajamrithisha mtoto wake hata mmoja kwa sababu anajua akimwachia urithi wake hao watoto wengine ndio wamekosa kila kitu.

Kusema kweli Igunga nna hakika Chadema wameshinda kwa kushindwa. tayari wananchi wamepata mwanga mkubwa sana hasa vijana ambao joto la jiwe limewawakia kwa miaka yote ya ujana wao. CCM imeshinda kutokana na wazee na kinamama ambao tulifaidika sana na mfumo wa mwalimu Nyerere. Shule bure, Hospital bure na waliweza kujenga maisha yao leo hii ni wastaafu wakiwa na mashamba yao ya kilimo. Ni maisha waliyoyazoea na hawatasahau hisani (ingawa ilikuwa right yao) ya CCM ktk makuzi yao.[/QUOTE]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom