Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

kapicha haka kidogo nilie lo ni kitu gani hiki eeee MUNGU wa mbinguni, hivi kweli ccm hawamwogopi hata MUNGU.

2wqy4jl.jpg
 
Binafsi napenda nilingalie hili kwa jicho la tofauti,...tatizo sio rostam,...tatizo ni sera za chama chake.
Hakuna jimbo katika tanzania hii utaenda ukose kuyaona uliyo yaona Igunga,..haijalishi jimbo
hilo linaongozwa na mbunge tajiri wa ccm au mbunge maskini wa chama cha upinzani,...kote hali ni sawa kabisa.

Nimeona picha hapo juu ya watoto wakiwa darasani wamekaa chini wanajifunza kuandika....
Well,hainishtui hata kidogo,...trust me.

Nimesoma shule za serikali,kwanzia vidudu hadi chuo kikuu.
Nasoma UDSM,lakini hakuna tofauti ha hayo unayo yaona kwa watoto kukaa chini.
Labda tofauti tu ni kwamba udsm wanaosoma ni watu wazima kwahiyo hata wakikaa chini watakaa katika
hali ya ku-maintain usafi na unadhifu wao.
Lakini ukweli ni kwamba hata chuo kikuu na kikongwe kabisa Tanzania wasomi wake wanakaa chini wakiwa
wana sikiliza lecture.
(Nikipata nafasi nitatoa picha hapa siku moja)

Sasa kama chuo kikuu katika Tanzania kiko hivo unategemea nini kwa watoto wa shule ya msingi
walio vijijini kabisa?
Ni kawaida kabisa.

Mjini hapa watu wengi wamepanga,wapo wenye hela lakini hazitoshi kujenga,...
tatizo ni sera mbovu za ccm zinazo sababisha bei za bidhaa ya ujenzi kuwa juu.

Tofauti kati ya hawa wa mjini walio panga (nikiwemo mimi) na wale wa vijijini wanao onekana
kanika nyumba za tembe ni kwamba wao wameweza kujenga zao kutokana na kipato chao
hata kama tunaziita mbovu na sisi tumeshindwa kujenga ingawa tunawazidi kipato.

Chimbuko la haya yote ni sera mbovu za CCM,...lakini swali ni je,....
Kuna chama chenye sera nzuri za kuleta maisha mazuri kwa watanzania kweli?
Sidhani

Kama unahisi hakuna chama mbadala wa CCM then tubinafsishe hii nchi, maana haina maana sisi kuendelea kuishi maisha haya ya shida kwa sababu ya wanasiasa.
 
Idadi kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika Igunga imeachwa makusudi ili ccm ipite kiurahisi, watu wanaambiwa mgombea wa CHADEMA kajiondoa wanakubali because they are intellecualy blind.
Huyo bwana mwenye choo kile juenda ndo kwanza aliwahamasisha wenzie kukipigia CCM.batahi nzuri mradi wa shule za kanyaga twende(kata) ni bomu ambalo litawalipukia CCM even before 2015.
ROSTAM alitumia pesa zake kusilence hoja,hata aliweza kukodi watu kulia waakati anajiuzulu, na ccm ni kama mbwa anaekula matapishi yake walimtapika RA then wakamtafuna tena
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga wa mtu mlingajishie sanamu na kitu halisi,atachagua sanamu.
Naamini, kura za wanaigunga walizopigia ccm,zitawanyoosha kwa mateso ya miaka 4 ijazo.haikuhitaji Elimu kujua yaliyoshindikana miaka 17 yanawezekanaje miaka 4 wakati wachezaji ni wale wale?
'Watu wangu wanaangamia kwa Kukosa maarifa" vimenena vitabu vya dini
Dada ragia umekumbuka Tiketi wakati basi limeshapita.So sad
 
Dada Regia,

Kwanza nawapeni pole kwa kazi kubwa ya kwaelimisha Watanzania ili waeweze elewa haki na wajibu wao katika taifa hili, haya uliyoyaorozesha hapa ni hali halisi ya taifa letu Tanzania katika sehemu nyingi hasa vijijini ila yanazidiana kutokana na jamii ya sehemu husika, sehemu ambayo kuna elimu duni matatizo yanakuwa makubwa zaidi na hili wala sio kosa la wananchi ni tatizo la utawala uliopo madarakani, wamewanyima watu elimu na kuwafanya washindwe kujitambua na huo ndio mtaji wa ccm na kamwe hawatakaa watoe elimu bora kwa wana wa nchi hii ili waendelee kuwa na mawazo duni na fikira pofu ili wasione kwamba tatizo ni ccm kuendelea kuwa madarakani,

Tazama picha ya hao wanafunzi walio darasani; yani nakwambia ni ghara ya landcuser V8 moja tu kuboresha shule yote hiyo, lakini watu wanaona waziri, naibu waziri, katibu, mkurugenzi na....na.....na..... ni bora watembelee magari hayo ya kifahari na hawa watoto ambao ndio viongozi wa baadae wakae chini, kwa sisi wengine ambao tumetembea nchi hii yote; tumeshuhudia makubwa kuliko hayo ya igunga, kuna sehemu ukifika unaweza kulia, so kwa ujumla bado tuna kazi kubwa sana ya kufanya na tena nyie ambao ni wabunge wa Chadema mnatakiwa mtushirikishe sisi wadau na wenye uchungu wa kweli wa nchi hii ili tuwe na mikakati na mipango bora ili tusijefika 2015 tukaanza tena hadithi za 2020, wakati wa ccm kutoka madarakani ni 2015 na wala sio wakati mwingine, ccm kundelea kuongoza ni sawa na kusema tulikuja duniani kupoteza muda na wala sio kuishi na kufurahia maisha ambao ndio mpango wa muumba wetu.

Natoa ombi kwa kila mwananchi wa tanzania mwenye uchungu wa kweli wa nchi hii kuikataa ccm kuanzia sasa na kusaidia katika kuelimisha ndugu zetu waliokosa elimu, na kwa kila kijana, mzee, mtu wa makamu kuhakikisha unajiandikisha kupiga kura 2015 na unakwenda kupiga kura na unalinda kura uliyopigwa, hima watanzania bila kujali wewe ni askari, usalama wa taifa, mgambo, machinga tuungane kwa pamoja kuikomboa nchi hii, bila ccm kutoka katika madaraka sahau maendeleo ya nchi inayoitwa Tanzania, yaani sahau kabisaa, ccm ndiyo tatizo na mwanzo wa matatizo yote yanayoikumba nchi hii ya maziwa na asali. tuwaelimshe pia waishio vijijini wasiuze shahada za kupigia kura na hili ndilo tatizo kubwa sana.

Kwa pamoja tutafika na ipo siku tutaikomboa nchi hii.
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

Unajua chadema ni mabingwa waku exagerate vitu, km hali ndio iko hivyo kwa nn wananchi wameichagua CCM na kuwaacha nyie km kweli hayo mliyokuwa mnayasema ni ya kweli ? . Dada maelezo yako yanatia mashaka isije kuwa watafuta umaarufu tu wa kisiasa humu ndani km kawaida yenu
 
Nilimwona Mzee CD Msuya kwenye Mlimani TV jana akisisitiza hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya mafisadi na ufisadi. Ana wa kumsikiliza?
 
Idadi kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika Igunga imeachwa makusudi ili ccm ipite kiurahisi, watu wanaambiwa mgombea wa CHADEMA kajiondoa wanakubali because they are intellecualy blind.
Huyo bwana mwenye choo kile juenda ndo kwanza aliwahamasisha wenzie kukipigia CCM.batahi nzuri mradi wa shule za kanyaga twende(kata) ni bomu ambalo litawalipukia CCM even before 2015.
ROSTAM alitumia pesa zake kusilence hoja,hata aliweza kukodi watu kulia waakati anajiuzulu, na ccm ni kama mbwa anaekula matapishi yake walimtapika RA then wakamtafuna tena
Ukitaka kupima kiwango cha ujinga wa mtu mlingajishie sanamu na kitu halisi,atachagua sanamu.
Naamini, kura za wanaigunga walizopigia ccm,zitawanyoosha kwa mateso ya miaka 4 ijazo.haikuhitaji Elimu kujua yaliyoshindikana miaka 17 yanawezekanaje miaka 4 wakati wachezaji ni wale wale?
'Watu wangu wanaangamia kwa Kukosa maarifa" vimenena vitabu vya dini
Dada ragia umekumbuka Tiketi wakati basi limeshapita.So sad

Wakati unaandika haya mlikuwa maliwatoni au wapi ? nyie hizo pesa hata km mngeshinda mngezitoa wapi za kutekeleza hizo ahadi zenu? tunarudi kule kule ni serikali ya ccm ndio ingewapa na tena kwa kuwapigia magoti na kuomba wawatekelezee hizo ahadi zenu
 
Unajua chadema ni mabingwa waku exagerate vitu, km hali ndio iko hivyo kwa nn wananchi wameichagua CCM na kuwaacha nyie km kweli hayo mliyokuwa mnayasema ni ya kweli ? . Dada maelezo yako yanatia mashaka isije kuwa watafuta umaarufu tu wa kisiasa humu ndani km kawaida yenu
Sasa GB kuna jipya kweli hapa! Hali hii ndio halisi sio kwa Igunga tu. Ni Tanzania nzima na bado CCM inachaguliwa tu. Watanzania walio wengi wanadhani ndio MAISHA na hakuna wa kuyabadili haya. Tuendelee tu kuigharamia kijinga SIASA na wanasiasa.
 
hebu angakieni na hii video ya hao WATATURU
 
Last edited by a moderator:
Binafsi napenda nilingalie hili kwa jicho la tofauti,...tatizo sio rostam,...tatizo ni sera za chama chake.
Hakuna jimbo katika tanzania hii utaenda ukose kuyaona uliyo yaona Igunga,..haijalishi jimbo
hilo linaongozwa na mbunge tajiri wa ccm au mbunge maskini wa chama cha upinzani,...kote hali ni sawa kabisa.

Nimeona picha hapo juu ya watoto wakiwa darasani wamekaa chini wanajifunza kuandika....
Well,hainishtui hata kidogo,...trust me.

Nimesoma shule za serikali,kwanzia vidudu hadi chuo kikuu.
Nasoma UDSM,lakini hakuna tofauti ha hayo unayo yaona kwa watoto kukaa chini.
Labda tofauti tu ni kwamba udsm wanaosoma ni watu wazima kwahiyo hata wakikaa chini watakaa katika
hali ya ku-maintain usafi na unadhifu wao.
Lakini ukweli ni kwamba hata chuo kikuu na kikongwe kabisa Tanzania wasomi wake wanakaa chini wakiwa
wana sikiliza lecture.
(Nikipata nafasi nitatoa picha hapa siku moja)

Sasa kama chuo kikuu katika Tanzania kiko hivo unategemea nini kwa watoto wa shule ya msingi
walio vijijini kabisa?
Ni kawaida kabisa.

Mjini hapa watu wengi wamepanga,wapo wenye hela lakini hazitoshi kujenga,...
tatizo ni sera mbovu za ccm zinazo sababisha bei za bidhaa ya ujenzi kuwa juu.

Tofauti kati ya hawa wa mjini walio panga (nikiwemo mimi) na wale wa vijijini wanao onekana
kanika nyumba za tembe ni kwamba wao wameweza kujenga zao kutokana na kipato chao
hata kama tunaziita mbovu na sisi tumeshindwa kujenga ingawa tunawazidi kipato.

Chimbuko la haya yote ni sera mbovu za CCM,...lakini swali ni je,....
Kuna chama chenye sera nzuri za kuleta maisha mazuri kwa watanzania kweli?
Sidhani

Pole sana ndugu yangu naona kauli zako ni za mtu aliyekata tamaa. Chama na watu wa kuleta mabadiliko wapo.
 
Unajua chadema ni mabingwa waku exagerate vitu, km hali ndio iko hivyo kwa nn wananchi wameichagua CCM na kuwaacha nyie km kweli hayo mliyokuwa mnayasema ni ya kweli ? . Dada maelezo yako yanatia mashaka isije kuwa watafuta umaarufu tu wa kisiasa humu ndani km kawaida yenu

Natamani Kama Ningekujua Hata Kwa Sura, Si Haba!! Kwa hali yote hii ccm wanavyorubuni Watu kutokana na kutokujua na Umasikini Wao!! Na kulirudisha Hili Taifa Nyuma kama Mungu ametuumba bila uwezo wa Kufikiri bado Unasimama na Kuchangia Hoja!! Kweli Huna Huruma na Watu Wenzako na Mungu Akulaani wewe Hadi Utakapokuwa na Huruma na Binadamu Wenzako!! Ni bora kukaa kimya Kuliko Kushabikia Ujinga
 
Laana huwa inaenda kwa wale waongo na wazandiki , na hili liko wazi ni cdm
 
Labda nimuulize tena Dada Regia,
Ikiwa hali ya WATANZANIA walio wengi ndio hiyo ulioiona hapo Igunga, kuna haja ya:
1. Kuwa na BUNGE kubwa namna hii lenye hadi VITI MAALUM kama cha kwako? Mbona Igunga Mbunge ni mmoja wilaya nzima?
2.Kuwa na RUZUKU kwa vyama vya SIASA ya kuchezea kwa kiwango hiki kama ilvyofanyika Igunga?
 
Unajua chadema ni mabingwa waku exagerate vitu, km hali ndio iko hivyo kwa nn wananchi wameichagua CCM na kuwaacha nyie km kweli hayo mliyokuwa mnayasema ni ya kweli ? . Dada maelezo yako yanatia mashaka isije kuwa watafuta umaarufu tu wa kisiasa humu ndani km kawaida yenu

Unataka kubisha?
 
Najiuliza hivi wana-Igunga wamerogwa na nani?? haiwezekani bana!!
 
Labda nimuulize tena Dada Regia,
Ikiwa hali ya WATANZANIA walio wengi ndio hiyo ulioiona hapo Igunga, kuna haja ya:
1. Kuwa na BUNGE kubwa namna hii lenye hadi VITI MAALUM kama cha kwako? Mbona Igunga Mbunge ni mmoja wilaya nzima?
2.Kuwa na RUZUKU kwa vyama vya SIASA ya kuchezea kwa kiwango hiki kama ilvyofanyika Igunga?

WC,kwanza nashukuru kwa comments zako zote,ni very positive zenye lengo la kusaidia nchi..
Katika post yako hii labda nami nikuulize unadhani nchi yetu tatizo ni kukosekana kwa fedha?Unafikiri Bunge likiwa dogo ndio haya matatizo yatakwisha?unadhani hili ndio primary solution,nifafanulie and then tujadiliane kwa kina!
 
hayo ndio maisha watanzania tuliyojitakia,kama wana igunga wanayaelewa matatizo yao inakuwaaje bado wanakiweka madarakani chama ama mgombea asiweza kuwasaidia na je serikali haiyaoni hayo ama ndio hiyo makusudi ili waendelee kushika dola

umefikia wakati sasa tubadilike na kile tukipendacho kufanyiwa basi ni vyema tuwafanyie na wenzetu,vitu kama zahanati na shule hata madawati ni mambo ambayo yalitakiwa yafanyiwe kazi na bwana RA katika miaka yote 17 aliyokuwepo madarakani mbona tunaona mifano kama moshi ya ndesamburo ama kilosa ya mkulo mbona angalau kuna vitu vinaonekana?

tusiwafanye wananchi ni mtaji wa kisiasa na mwisho wa siku hatuwafanyii kile wanachokihitaji,

hata kama sijafika igunga lakini picha tu zaonyesha kuwa huko sio shwari,angalia malinyi ulanga ni mbali na mkoa wa morogoro mbugani huko hata redio hazishiki lakini mda wa jioni watu wanauziwa umeme wa jenereta,simu zipo,zahanati zote zimewekwa solar kuna hospitali kubwa ya lugara shule nzuri za secondari kama Tumaini,kipingo na maisha huwezi kuyafananisha na hayo ya igunga alikokuwa tajiri namba moja Tanzania,nampongeza sana mzee ngasongwa alifanya kazi kubwa

huu ni wakati wa kubadilika na sio kuwafanya wananchi kama mtaji wa kisiasa na ku-take advantage ya ujinga walionao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom