Bi. Regia,
Mimi kusema kweli nimekusoma ktk hali ambao yanishangaza mimi kwamba wewe hukuyajua haya..Ni hali halisi ya sehemu kubwa ya Tanzania na inasikitisha zaidi pale Wabunge wetu waliopewa dhamana ya kupeleka maendeleo vijijini wanapata muda wa kuwalaghai wananchi kwa Takrima na fedha. Rostam anasifika Igunga kwa kutoa fedha kama vile masikini wanavyoweza kumsifia mtu anayewapa Tsh1,000 kila siku anaposimamisha gari lake...
Ningekuomba sana ulitazame swala hili kwa mapana zaidi kwa sababu Tanzania leo ni maskini kuliko hata wakati wa Uhuru na hesabu ya maskini inazidi kuongezeka kila siku. Kama nchi nzima asilimia 14 ndio wenye umeme tena wa mgao, tunayo maji lakini maji safi ni chini ya asilimia 10 au hakuna kabisa! Hatuna walimu na madktari wa kutosha shule na zahanati zilizojengwa ni sawa na magofu au kiwanda kisichozalisha. Kumbuka pia Wadanganyika wengi hawajaona maendeleo na wengi zaidi hawajui maendeleo zaidi ya yale wanayoyaona ktk maisha yao hivyo sii rahisi kabisa kumshawishi mwana Igunga akuelewe ktk muda mfupi kiasi hicho...
CCM walikuwa wanataka ku prove kitu hivyo msinde msishinde Igunga lazima waichukue. Hivyo kwa ujumla wa yote haya wananchi wa Igunga hawakutendewa haki hata kidogo. Kilichofanyika pale ni kupeleka fahgari wawili wakagombane wakati nyasi hao wanaIgunga ndio waathirika. Kweli Chadema kimeweza kujijenga, lakini hii kweli ni haki?..Kweli chama kinatakiwa kujijenga wakati wa uchaguzi ambao wananchi wake wana nafasi moja tu ktk miaka mitano kufanya maamuzi magumu.
Ushauri wangu kwenu, tembeleeni sana majimbo, vijiji mkajionee wenyewe jinsi nchi yetu ilivyokuwa nyuma ktk maendeleo kwani sii Igunga peke yake, sehemu kubwa ya Taifa letu ni Igunga ya Rostam. Mbunge anachaguliwa na kusifikia sii kwa kuwapelekea maendeleo bali kwa kutoa misaada na sadaka zaidi kama Taifa letu linavyoomba misaada nje...Ni Mataifa gani marafiki zetu zaidi kama sii yale yanayotupa misaada kuliko Wawekezaji waliokuja kutupa ajira na kuinvest nchini..