Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Faiza usibishane na huyu mbunge. Anatia aibu kila akiandika humu jamvini. Yaani hata sijui huwa anafikiria nini.Mbunge ni mtunga sheria na muhakikishaji wa ufanisi wa mawaziri.
Pia ni mjumbe wa halmashauri ya serikali za mitaa jimboni mwake, na akiwa mjumbe wa halmashauri, ana nguvu kama diwani tu. Bila kuilalamikia srikali ilete au itekeleze mradi fulani, atawasaidiaje wananchi?
Mbunge sio mleta maendeleo, siyo mtoa fedha au mjenga barabara. Ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo lake.
Mlikuwa Igunga na hamkutaja hata jina lake, leo ndio mnajifanya mna uchungu?
Huyu mbunge si alisema uchaguzi haumuhusu RA?... mpelekeni mahakamani, acheni kubwabwaja.
 
Kwa kuwa PhD UDSM sasa ni sawa tu na kugawa vitumbua hivo, nampendekeza Rostam Aziz naye akakirimiwe kwa kuleta UFISADI nchini na kuchangia sana kugusa maisha ya watu wengi nchini.
 
90% ya wabunge ccm ni maslahi binafsi ,,,,kwani hushangai mkuu wa mkoa anataka ubunge dr anataka, engineer anataka. kafumu cheo alicho nacho ni kikubwa kuliko ubunge lakini subiri tuone alichogombania kupata ubunge tutakiona muda sio mrefu

I predict Mzee Kiwete atampa Uwaziri wa NISHATI NA MADINI very soon kwenye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni ili aendelee kuwaibia Watanzania kupitia raslimali za madini. Ni lazima afanye hivo ili kulipa fadhila za waliomteua pamoja na kurudisha gharama alizotumia kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga.

Hiyo ndiyo aina ya Wanasiasa tulionao kwenye Chama Cha Magamba/Majambazi.
 
Matatizo hayapo Igunga tu karibu nchi nzima, badala ya kulalama ndani ya JF tumia nafasi yako ndani ya bunge kuleleta msisimko wa maendeleo kitaifa, Rostam inamponza zaidi rangi yake ukweli 90% ya wabunge wanafanana kimawazo na kiakili ndio maana taifa halisongi mbele.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Ok,basi kwenye kubadilika kati ya hao watu wazima,kuna vijana ambao wa kuanzia miaka 18 maybe hadi 30 or 35.Hao huwezi kuwajumuisha na hao watu wazima wasiotaka kubadilika.Ndio maana nikakuuliza kama umri ulikuwa kigezo zaidi tu ya utu uzima.Vijana ni more likely ku embrace new ideas na kutaka mabadiliko ama maendeleo.Hapo mwanzoni kabla ya jibu lako hili, niliwachukulia hao watu wazima wasiotaka kubadilika kama watu wazima haswa na siyo watu wazima wenye miaka 18 ambayo ni halali kupiga kura.

Kwa ujumla elimu ingewasaidia zaidi wananchi wote kwa ujumla wao.Kwani wakijuwa haki zao na kuijuwa connection kati ya well being yao ie umasikini, na uamuzi wao kwenye sanduku la kura.Kwamba wanaweza kuleta mabadiliko ie kuondokana na umasikini kwa kutumia sanduku la kura.Basi watabadilika.Hiyo connection ikishawaingia kwenye akili yao basi hakuna tabu.

Mkuu an adult person is a person who is 18 or above. Vijana kuanzia miaka 18 hadi 30 or 35 bado ni adult people na wanajumuishwa kama adult persons. Wapo vijana wenye umri wa miaka 18 kwenda juu na hawataki kubadilika. Yaani this is a naked fact. Nakubaliana na kuwa vijana are likely to embrace new ideas na kutaka mabadiliko au maendeleo lakini hili sio kwa vijana wote. Why? Wapo vijana wengi ambao ni well being na hawataki mabadiliko kabisa.

In deed, vijana ambao hawataki mabadiliko ni wale ambao ni well being. Wengi wa hawa vijana wanaogopa kuwa kukiwa na mabadiliko ya kisiasa yataadhiri yale ambayo wamenufaika au wanaendelea kunufaika kutokana na system ya sasa. Kweli inaweza kuwasaidia zaidi wananchi wote kwa ujumla wao lakini pia wapo watu wenye elimu nzuri tuu lakini simply hawako tayari kubadilika. Soma post ya Zing hapo juu watu walijengewa shule huko Maswa lakini walengwa wamesepa majengo yapo empty. Pamoja na kutengenezewa mazingira ya kujiendeleza wamesepa b'se bado hawataki kubadilika.
 
EMT,
mkuu hapa kidogo umenishtua kusikia Maswa imejengwa shule lakini haina wanafunzi na mnawalalamikia wananchi, hivi mmefanya utafiti kwa nini shule hizo hazina wanafunzi?. Maanake mimi naamini kabisa kwamba shule sii majengo na wanafunzi hufuata palipo na walimu. Pia lazima tutafute sababu nje ya hawa watu yawezekana pia kwamba Maswa hakuna ajira, wazazi wao pengine wamefariki au wamehama mji na kuwaacha watoto na bibi au shangazi zao (mila zetu) ambao hawana uwezo isipokuwa kutegemea watoto wao kuchunga mifugo na kazi nyingine za uzalishaji maanake umaskini jamani huja na mengi.

Soby,
Mkuu wangu maneno yako msumari na hakika ndivyo inavyotakiwa kuwa lakini kwa Tanzania yetu Mbungen ndiye mzazi, baba wa jimbo. Na kamanakumbuka Rostam mwenyewe alijisifia kwa kupeleka maendeleo Igunga akayataja yote makubwa alowafanyia hadi watu wakaingia uchungu na machozi kuwatoka, wengine walizimia na kumwagiwa maji, sasa Bi.Regia alipokwenda huko na kuyakuta aloyakuta hakuamini udanganyifu ule kwani hao wana Igunga maskini ya watu hawajui nini maendeleo na hawaelewi nini majukumu ya mbunge, hivyo sidhani kaa Regia anakosea kwa sababu alowacha ukumbi wazi kujadili maendeleo ya Igunga ni yeye mwenyewe Rostam...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
EMT,
mkuu hapa kidogo umenishtua kusikia Maswa imejengwa shule lakini haina wanafunzi na mnawalalamikia wananchi, hivi mmefanya utafiti kwa nini shule hizo hazina wanafunzi...........

Mkuu mkadara unawajua au umewai kuwasikia jamii ya watu wanaitwa watindiga au wamang'ati. Unapoogelea hizi jamii development kwao ina mtazamo tofauti na jamii nyingine. So miradi ya mendeeleo kwa hizi jamii inatakiwa itambue hilo. Jamii hizo zinahitaji zaidi miradi ya kulinda mistu na mapori wanayoishi kuliko hata shule na hospitali.

Sijui kama kuna mtua ana takwimu za Population ya watu hawa na area wanayocover kwa movement zao
 
  • Thanks
Reactions: Ame
EMT,
mkuu hapa kidogo umenishtua kusikia Maswa imejengwa shule lakini haina wanafunzi na mnawalalamikia wananchi, hivi mmefanya utafiti kwa nini shule hizo hazina wanafunzi?. Maanake mimi naamini kabisa kwamba shule sii majengo na wanafunzi hufuata palipo na walimu. Pia lazima tutafute sababu nje ya hawa watu yawezekana pia kwamba Maswa hakuna ajira, wazazi wao pengine wamefariki au wamehama mji na kuwaacha watoto na bibi au shangazi zao (mila zetu) ambao hawana uwezo isipokuwa kutegemea watoto wao kuchunga mifugo na kazi nyingine za uzalishaji maanake umaskini jamani huja na mengi.

Soby,
Mkuu wangu maneno yako msumari na hakika ndivyo inavyotakiwa kuwa lakini kwa Tanzania yetu Mbungen ndiye mzazi, baba wa jimbo. Na kamanakumbuka Rostam mwenyewe alijisifia kwa kupeleka maendeleo Igunga akayataja yote makubwa alowafanyia hadi watu wakaingia uchungu na machozi kuwatoka, wengine walizimia na kumwagiwa maji, sasa Bi.Regia alipokwenda huko na kuyakuta aloyakuta hakuamini udanganyifu ule kwani hao wana Igunga maskini ya watu hawajui nini maendeleo na hawaelewi nini majukumu ya mbunge, hivyo sidhani kaa Regia anakosea kwa sababu alowacha ukumbi wazi kujadili maendeleo ya Igunga ni yeye mwenyewe Rostam...

Mkuu inawezekana Kuna sababu nyingine zilizofanya wasepe lakini point yangu ni kwamba the only best way kumbadilisha mtu ni pale yeye mwenyewe anapokubali kubadilika. Unaweze ukajenga shule, ukajaza walimu na vitendea kazi bora lakini kama mwanafunzi hataki kusoma there is nothing you can do about it. Na kama wana priorties nyingine kama alizozungumzia Zing hapo juu ndio kabisaa.

Kuhusiana na post uliyomjibu Soby inawezekana Mh Regia Mtema pia hajui kazi za ubunge jimboni. Labda alitegemea kwa vile Rostam ni tajiri basi angetumia utajiri wake kuijenga Igunga. of course hii ni fikra kwa Watanzania wengi. Wanadhani majimbo yenye wabunge matajiri yananufaika zaidi. Mheshimiwa ana point lakini tatizo ni the way anavyotaka kui defend. Si umeona yule mbunge wa Ludewa wanadai katoa pesa zake binafsi kununua ambulance anavyo kuwa criticized. Kama unategemea mbunge ajenge hospitali, mashule, madaraja, n.k, serikali itafanya nini? Ni nini majukumu ya mbunge jimboni kwake?

Sawa Rostam alikuwa Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa. Mbona wabunge wengine hawapigi kelele?
Sawa alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake. Mbona kuna wabunge wengine wana ushawishi ndani ya vyama vyao lakini maendeleo majimboni mwao ni ovyo? Halafu what exactly does she mean anaposema kuwa Rostam angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake? Kwa hiyo Chadema ikuchukua madaraka, na Mh Mtema akiwa mbunge na mshawishi ndani ya chadema, atashauri mawaziri wapekele miradi jimboni kwake? Vipi wale wabunge ambao hawana ushawishi ndani ya vyama vyao lakini wako mstari wa mbele kuleta maendeleo jimboni?

Yes, alikuwa mbunge tajiri sana lakini nini kazi ya mbunge? Does she mean kuwa mbunge tajiri anastahili to do more than mbunge ambaye sio tajiri? If so, basi tuchague wabunge ambao ni matajiri because they can do more majiomboni mwetu? Mkuu sio kwamba namfagilia Rostam. Point yangu ni kwamba kama ilivyokuwa kwa Rostam wabunge wengi sana hawawatumikii wananchi wao majimboni. Point yangu ni kwamba hili ni tatizo la kitaifa. Kama tunachukulia hili kama tatizo la Rostam tuu then, hatutatua tatizo. Hayo mambo 11 Mheshimiwa aliyoodheresha hapo yako almost Tanzania na sio Igunga tuu.

Most of MPs are not performing their duties as MPs in their constituencies. Hata waki perform wanakuwa wanafanya kazi ambazo zina belong to the executive kama kununulia wananchi ambulances. Mkuu utakumbuka tulijadili hii issue sana kwenye ile thread iliyokuwa inamshutumu Mh Zitto Kabwe kuandika proposal ya kuomba mabati ya shule Barrick Gold.
 
Umeandika makala ndefu lakini bahati mbaya ni pumba tupu.nlitegemea utakuwa objective kumbe unaendeleza umaskini wako wa mawazo.apa tupo ht tusio na vyama.vp yule kiongoz wa kanisa alosema wana igunga wachague chadema..vp kule sumbawanga ambapo waumini walitengwa na kanisa..vp kule arusha ambapo kiongoz mkuu wa kanisa tena wa kanda nzima aliposema wazi kuwa waumini wake wachague Chaga Development Manifesto.vp mw'kiti wa cdm alipompiga kofi mwangalizi wa uchaguzi wa kiislam kule hai...mi sina chama lakini cdm ijikosoe na ikikosolewa ikubali na kujirekebisha.
Hii naona kama ipo nje ya mada....ingeanza na mada mpya
 
quote_icon.png
By Inauma
Umeandika makala ndefu lakini bahati mbaya ni pumba tupu.nlitegemea utakuwa objective kumbe unaendeleza umaskini wako wa mawazo.apa tupo ht tusio na vyama.vp yule kiongoz wa kanisa alosema wana igunga wachague chadema..vp kule sumbawanga ambapo waumini walitengwa na kanisa..vp kule arusha ambapo kiongoz mkuu wa kanisa tena wa kanda nzima aliposema wazi kuwa waumini wake wachague Chaga Development Manifesto.vp mw'kiti wa cdm alipompiga kofi mwangalizi wa uchaguzi wa kiislam kule hai...mi sina chama lakini cdm ijikosoe na ikikosolewa ikubali na kujirekebisha.
Eti huna chama maneno na matendo tafauti kabisa ni kama mbingu na ardhi.
 
hakuna kiongozi tz mwenyeuchungu na watu wake wote hoples!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kila jimbo tz ni mataztizo mm naijua igunga sana ni aibu kwa ra hakuwa na muda na watu wake ni hela kwa kwena mbele pia haki za wana igunga anadaiwa pia sijaona kitu alicho fanya igunga
i hate this man
 
Asante dada Regia kwa thread yako nzuri na kututegulia kitendawili.
kumbe FaizaFoxy ni mwanaume? Sasa ya nini kujivalisha hijab? Yaani ni dume jike,lol ptuu! Kazi unayoifanya humu JF ni ngumu na huwezi shinda nguvu ya umma..ptuu!
hivi hamna habari wana JF, Kwamba FF ni shemale? mimi namfahamu vizuri huyu mtu muda si mrefu nitazimwaga data zake zote jf
 
Mkuu inawezekana Kuna sababu nyingine zilizofanya wasepe lakini point yangu ni kwamba the only best way kumbadilisha mtu ni pale yeye mwenyewe anapokubali kubadilika. Unaweze ukajenga shule, ukajaza walimu na vitendea kazi bora lakini kama mwanafunzi hataki kusoma there is nothing you can do about it. Na kama wana priorties nyingine kama alizozungumzia Zing hapo juu ndio kabisaa.

Kuhusiana na post uliyomjibu Soby inawezekana Mh Regia Mtema pia hajui kazi za ubunge jimboni. Labda alitegemea kwa vile Rostam ni tajiri basi angetumia utajiri wake kuijenga Igunga. of course hii ni fikra kwa Watanzania wengi. Wanadhani majimbo yenye wabunge matajiri yananufaika zaidi. Mheshimiwa ana point lakini tatizo ni the way anavyotaka kui defend. Si umeona yule mbunge wa Ludewa wanadai katoa pesa zake binafsi kununua ambulance anavyo kuwa criticized. Kama unategemea mbunge ajenge hospitali, mashule, madaraja, n.k, serikali itafanya nini? Ni nini majukumu ya mbunge jimboni kwake?

Sawa Rostam alikuwa Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa. Mbona wabunge wengine hawapigi kelele?
Sawa alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake. Mbona kuna wabunge wengine wana ushawishi ndani ya vyama vyao lakini maendeleo majimboni mwao ni ovyo? Halafu what exactly does she mean anaposema kuwa Rostam angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake? Kwa hiyo Chadema ikuchukua madaraka, na Mh Mtema akiwa mbunge na mshawishi ndani ya chadema, atashauri mawaziri wapekele miradi jimboni kwake? Vipi wale wabunge ambao hawana ushawishi ndani ya vyama vyao lakini wako mstari wa mbele kuleta maendeleo jimboni?

Yes, alikuwa mbunge tajiri sana lakini nini kazi ya mbunge? Does she mean kuwa mbunge tajiri anastahili to do more than mbunge ambaye sio tajiri? If so, basi tuchague wabunge ambao ni matajiri because they can do more majiomboni mwetu? Mkuu sio kwamba namfagilia Rostam. Point yangu ni kwamba kama ilivyokuwa kwa Rostam wabunge wengi sana hawawatumikii wananchi wao majimboni. Point yangu ni kwamba hili ni tatizo la kitaifa. Kama tunachukulia hili kama tatizo la Rostam tuu then, hatutatua tatizo. Hayo mambo 11 Mheshimiwa aliyoodheresha hapo yako almost Tanzania na sio Igunga tuu.

Most of MPs are not performing their duties as MPs in their constituencies. Hata waki perform wanakuwa wanafanya kazi ambazo zina belong to the executive kama kununulia wananchi ambulances. Mkuu utakumbuka tulijadili hii issue sana kwenye ile thread iliyokuwa inamshutumu Mh Zitto Kabwe kuandika proposal ya kuomba mabati ya shule Barrick Gold.
Nakubaliana nawe ktk mengi maadam sina tafiti ya maswala haya kwa undani zaidi maana nimetolewa hata mifano ya Watindiga!..binafsi, sioni tatizo la watu kuhifadhi tamaduni zao wakati huo huo wakichukua yaliyo bora kwenye tamaduni za kigeni, tofauti na sisi tunaotaka hawa Watindiga waache kabisa tamaduni zao za hifadhi ya misitu, wanyama na nguvu kazi ya asili za uchungaji ili waingie mjini kupuyanga matokeo yake ndio haya na hao Masai siku hizi nasikia ndio Mashoga!..

Kuhusu Regia Mtema sidhani pia kama anafanya makosa kusema Mbunge unatakiwa uwe na ushawishi kwa sababu ndivyo inavyotakiwa kisiasa. Ndivyo siasa zinavyochezwa mahala popote toka anagombea Ubunge ni swala la ushawishi wake bungeni kuweza kupeleka maendeleo jimboni kwa sababu lazima tukubali kwamba Wabunge sii tu wawakilishi wa wananchi bungeni kwenda kukaa na kupiga usingizi wakitegema serikali imeshapanga kila kitu, bali pia wanatakiwa kuwa na uwezo wa kushawishi kulingana na ilani zao kwa nini tujenge barabara ya lami Igunga kwenda Tabora kabla ya daraja la Kigamboni na kadhalika. Hizi ahadi ndizo zilizompa kura hivyo ni lazima aziwakilishe bungeni.

Na yatakuwa makosa makubwa kwa mbunge kwenda bungeni akitegemea kwamba serikiali ityabuni miradi ya maendeleo ikiwa yeye mwenyewe hana mpango wa maendeleo ya jimbo lake, bila shaka sababu kubwa ya kugawa majimbo ni kurahisisha kazi ya utawala kuweza kupata wawakilishi wa wananchi badala ya rais ama viongozi wa serikali kuu kutembelea kila jimbo kutazma wataweza kupeleka kitu gani ktk maendeleo ya wananchi.

Mimi nilivyomwelewa Regia ni kwamba hakutegemea mbunge mwenye sifa na majigambo kama Rostam angeshindwa kabisa kuwapelekea wananchi wa Igunga maendeleo kwa kupanga vizuri sehemu za huduma kama shule na zahanati kiasi kwamba kaeleza kuna watu wanatembea maili 10 kutafuta maji, shule au zahanati..sehemu kubwa bado kabisa iko nyuma sana na sidhani kama haya ni makosa ya wananchi ati hawataki kubadiliko isipokuwa hakuna mazingira bora ya wao kuweza kubadilika..Amini maneno yangu mkuu wangu kama utaweka mazingira bora wananchi watabadilika tu, sisi huku majuu tumebadilika sii kwa kupenda isipokuwa imetulazimu tubadilike ili tuweze kuishi nchi hizi.

Haya ni mawazo mabaya sana na ni chembechembe za Ubinafsi kama wazungu wanavyotuona sisi weusi hatupendi maendeleo. Wanatuona wavivu na wajeuri tusopenda maendeleo lakini ukitazama deal packages zao huyaoni mazuri wanayotutakia isipokuwa wanachozungumzia ni jinsi ya kukutumia zaidi.. Na pengine hawa Watindiga, Wasukuma wa Maswa na wengineo hutazama kwanza malengo ya kuwepo vitu hivi maanake siku hizi watu wanajengewa shule na zahanati ili waachie ardhi na machimbo yao ya dhahabu... Tena wakiahidiwa kusomeshwa bure watoto zao na kupewa makazi mapya..

Ningeomba sana tujadili issues na sii kumjadili Regia ambaye kaiweka mada hii na kwa bahati nzuri sote hapa tunakubaliana kwamba sii Igunga tu ambako hakuna maendeleo, bali umaskini wa Igunga upo sehemu kubwa ya Tanzania na hapo ndipo tunatakiwa kuanzia mjadala mrefu kuhusu maendeleo yetu. Kumzungumzia Regia ndio simple minded lakini sii kumzungumzia Rostam kutokana na madai yake ya kupeleka maendeleo makubwa Igunga hali hakuna kitu kabisa..
 
Asante Regia kwa kutufungua macho. Nilijua hali ni mbaya huko Igunga, lakini sikujua extent yake. LOH! Ama kweli FISADI HANA SABABU! Hivi nyie mnajua kwamba Rostam Aziz hana uraia wa kuzaliwa hapa nchini? Ni mhamiaji tu kutoka Iran? Wana-Igunga wanaifahamu vema asili yake. Kwao ni Uturuki!
 
hivi hamna habari wana JF, Kwamba FF ni shemale? mimi namfahamu vizuri huyu mtu muda si mrefu nitazimwaga data zake zote jf

So what? Umwage data zake ili iweje? Tuzungumzie hoja zake, si maumbile yake. Unapotea njia. Hutaungwa mkono kwa hilo.
 
Asante Regia kwa kutufungua macho. Nilijua hali ni mbaya huko Igunga, lakini sikujua extent yake. LOH! Ama kweli FISADI HANA SABABU! Hivi nyie mnajua kwamba Rostam Aziz hana uraia wa kuzaliwa hapa nchini? Ni mhamiaji tu kutoka Iran? Wana-Igunga wanaifahamu vema asili yake. Kwao ni Uturuki!
Kama wana-Igunga wanafahamu historia yake, kwanini walimchagua?
Kama CDM walijua yeye ni fisadi, na hajaleta maendeleo Igunga, kwanini hawakumsimamisha mgombea 2010? kumbuka uchaguzi uliopita ni miezi 11 tu. Kwa hiyo, waliokuwa wanajua Igunga ina maendeleo before October this year?
Kama jibu ni sio? Rejea swali la kwanza.
Kama jibu ni ndio, je tutakiaminije chama ambacho hata hakijui hali halisi ya mtanzania kila kona? Are you serious?
Yaani unakuja jamvini kusema kuwa ulikuwa hujui matatizo ya wana-Igunga kabla ya septemba mwaka huu?..Na wewe ni mbunge wa taifa?
C'mon guys, mnatia aibu!
 
Nakubaliana nawe ktk mengi maadam sina tafiti ya maswala haya kwa undani zaidi maana nimetolewa hata mifano ya Watindiga!..binafsi, sioni tatizo la watu kuhifadhi tamaduni zao wakati huo huo wakichukua yaliyo bora kwenye tamaduni za kigeni, tofauti na sisi tunaotaka hawa Watindiga waache kabisa tamaduni zao za hifadhi ya misitu, wanyama na nguvu kazi ya asili za uchungaji ili waingie mjini kupuyanga matokeo yake ndio haya na hao Masai siku hizi nasikia ndio Mashoga!..

Kuhusu Regia Mtema sidhani pia kama anafanya makosa kusema Mbunge unatakiwa uwe na ushawishi kwa sababu ndivyo inavyotakiwa kisiasa. Ndivyo siasa zinavyochezwa mahala popote toka anagombea Ubunge ni swala la ushawishi wake bungeni kuweza kupeleka maendeleo jimboni kwa sababu lazima tukubali kwamba Wabunge sii tu wawakilishi wa wananchi bungeni kwenda kukaa na kupiga usingizi wakitegema serikali imeshapanga kila kitu, bali pia wanatakiwa kuwa na uwezo wa kushawishi kulingana na ilani zao kwa nini tujenge barabara ya lami Igunga kwenda Tabora kabla ya daraja la Kigamboni na kadhalika. Hizi ahadi ndizo zilizompa kura hivyo ni lazima aziwakilishe bungeni.

Na yatakuwa makosa makubwa kwa mbunge kwenda bungeni akitegemea kwamba serikiali ityabuni miradi ya maendeleo ikiwa yeye mwenyewe hana mpango wa maendeleo ya jimbo lake, bila shaka sababu kubwa ya kugawa majimbo ni kurahisisha kazi ya utawala kuweza kupata wawakilishi wa wananchi badala ya rais ama viongozi wa serikali kuu kutembelea kila jimbo kutazma wataweza kupeleka kitu gani ktk maendeleo ya wananchi.

Mimi nilivyomwelewa Regia ni kwamba hakutegemea mbunge mwenye sifa na majigambo kama Rostam angeshindwa kabisa kuwapelekea wananchi wa Igunga maendeleo kwa kupanga vizuri sehemu za huduma kama shule na zahanati kiasi kwamba kaeleza kuna watu wanatembea maili 10 kutafuta maji, shule au zahanati..sehemu kubwa bado kabisa iko nyuma sana na sidhani kama haya ni makosa ya wananchi ati hawataki kubadiliko isipokuwa hakuna mazingira bora ya wao kuweza kubadilika..Amini maneno yangu mkuu wangu kama utaweza mazingira bora wananchi watabadilika tu, sisi huku majuu tumebadilika sii kwa kupenda isipokuwa imetulazimu tubadilike ili tuweze kuishi nchi hizi.

Haya ni mawazo mabaya sana na ni chembechembe za Ubinafsi kama wazungu wanavyotuona sisi weuzi hatupendi maendeleo. Wanatuona wavivu na wajeuri tusopenda maendeleo lakini ukitazama deal packages zao huyaoni mazuri wanayotutakia isipokuwa wanachozungumzia ni jinsi ya kukutumia zaidsi.. Na pengine hawa Watindiga, Wasukuma wa Maswa na wengineo hutazama kwanza malengo ya kuwepo vitu hivi maanake siku hizi watu wanajengewa shule na zahanati ili waachie ardhi na machimbo yao ya dhahabu... Tena wakiahidiwa kusomeshwa bure watoto zaona kupewa makazi mapya..

Ningeomba sana tujadili issues na sii kumjadili Regia ambaye kaiweka mada hii na kwa bahati nzuri sote hapa tunakubaliana kwamba sii Igunga tu ambako hakuna maendeleo, bali umaskini wa Igunga upo sehemu kubwa ya Tanzania na hapo ndipo tunatakiwa kuanzia mjadala mrefu kuhusu maendeleo yetu. Kumzungumzia Regia ndio simple minded lakini sii kumzungumzia Rostam kutokana na madai yake ya kupeleka maendeleo makubwa Igunga hali hakuna kitu kabisa..

Nakusikitikia sana kwa kuona kuwa ni vyema kumuongelea Mbunge aliyeondoka kuwa hajafanya hivi hajafanya vile na kufikia kusema mpaka huyo Mbunge ana majigambo? khaaaa! unanchekesha, katika wabunge ambao huwasikii kuongea bungeni nadhani aliyekuwa anaongoza ni Rostam. Rostam ni mtu wa action, kayafanya alioweza na asiyoyaweza hajayafanya aje mwingine ayafanye au upinzani uyafanye, si vyema kufikiria kuwa Mbunge ni chachu ya kutatuwa matatizo yote yanayomkabili Mtanzania. Si Mbunge, si chama cha siasa wala si Serikali. Ni mtu mwenyewe ndio anatakiwa awe wa kwanza kujikwamua kimaisha na kimaendeleo.

Nakuhakikishia kuwa si vyema kiongozi kukaa na kuanza kupakaza, manini? kwa kuelekeza hayo unayopakazia kwa mtu fulani. Huo ni upungufu wa mawazo na ukosefu wa maadili na uhaba wa mawazo ya kuongoza. Kiongozi anatakiwa kuwa anafanya na si kupakaza. Inasaidia nini? Haya umeshampakazia Rostam hajafanya, wewe umefanya nini> umeonesha hata njia ya watu wafanye hiki au kile?

Nimemshauri Mbunge Regia asome kitabu cha Dale Carnagie kiitwacho "How to win friends and influential peoples" nakushauri na wewe ukisome na kila mmoja wetu anaependa kujuwa ni nini uongozi. Kama kiongozi huwezi kujiongoza mwenyewe, hata kwa kauli zako, unategemea utamuongoza nani katika kutenda mema. Itabaki kwa unaowaongoza na wao kupakaza tu, kwani huo ndio uongozi wako. Kiongozi anatakiwa kila tatizo analoliona alichukulie kuwa ni "opportunity" ya yeye kulitatua na kulifanya liwe jema zaidi. Kiongozi mzuri ni yule anaelitatua tatizo na si yule anaeliatangaza tatizo (unaumwa na Mbwa halafu unatangaza kidonda?). Kutangaza matatizo aliyoyakuta Igunga bila kuyafanyia kazi na kuanza kumrushia madongo Rostam, kunamaanisha bado unamhitaji Rostam akakutatulie matatizo akupe na ufumbuzi.

Ni lini matatizo yatakwisha au nani atayamaliza? Kila "action" ina "reaction" ni mlolongo usio na mwisho. Leo hata nchi tajiri Duniani kuna wasio na nyumba za kuishi, kuna wasio na chakula cha kila siku, kuna wasio juwa kusoma au kuandika na kuna walioathirika na madawa ya kulevya kuna wizi, kuna, kuna, kuna... kwanini? si kwa sababu viongozi hawafanyi, viongozi wanafanya lakini kila wanachokifanya huzaa kingine ambacho nacho ni opportunity ya kukifanyia kazi. Kusema kuwa nimeshajenga shule basi sasa watoto watasoma, utajikuta unahitaji wanafunzi, unahitaji waalim, unahitaji maabara, unahitaji usafiri, unahitaji wahudumu, unahitaji makarani, unahitaji mlolongo wa vitu ambavyo vyote ni muhimu viwepo ili kui support shule iwe bora. Hali kadhalika kwa chochote ukifanyacho, Sasa leo ukianza kurusha madongo una maana huyawezi na unatafuta sababu za kushindwa kwako na mumtupia mwingine. Fanya uwezalo na uwawachie wengine "opportunities" za kufanya mengine.

Tanzania ni nchi changa sana lakini ina kila fursa ya kufanya makubwa kuliko nchi zilizoendelea zamani kwa sababu kuna shortcuts za kupita, hatuna mlolongo wa kutaka tuvumbuwe vipya vya kutusaidia, vilivyokwisha vumbuliwa na wenzetu ndio shortcut zetu na hatuzitumii ipasavyo mpaka sasa. Tuitumie fursa ya kuwa watendaji badala ya kuwa wapakazaji.

Tanzania mpaka leo Mwanasiasa kutumikia wananchi ni "huduma" na si wajibu au jukumu lake. Tubadilike kwa kutambuwa kwamba kuwa Mbunge si cheo, kuwa Mbunge ni utumishi na maboss wako ni sisi (wananchi). Kwa hiyo sisi tunakuambia kama mabosi wako, hatutaki utuletee fulani hakufanya hiki fulani hakufanya kile, tunata utuambie kuanzia leo tunafanya hiki ili tufikie hapa. Mbunge unatakiwa uje na "plan" za kiutendaji za kututoa kituo "a" kutufikisha kituo b,c,d,e...na kuendelea, utapoishia au tutapokuona hutufai tunakupiga chini tunamuweka mtumishi mwingine atutumikie, sisi tuko bize na kazi zingine. wewe kama Mbunge tufanyie haya...Na tutakulipa hiki na hiki na hiki, sasa kama wewe umeshindwa usituletee porojo za fulani kashindwa ili tusikuulize yako uliyoyaweza yako wapi?
 
Rostam ni mtu wa action, kayafanya alioweza na asiyoyaweza hajayafanya aje mwingine ayafanye au upinzani uyafanye, si vyema kufikiria kuwa Mbunge ni chachu ya kutatuwa matatizo yote yanayomkabili Mtanzania. Si Mbunge, si chama cha siasa wala si Serikali. Ni mtu mwenyewe ndio anatakiwa awe wa kwanza kujikwamua kimaisha na kimaendeleo.

Unaweza kufafanua hapo
  • Majukumu na kazi za mbunge hasa ni nini
  • Kotokana na majukumu hayo ya ubunge Huyu Rostam kafanya action gani hasa ili wengine wa CCM na wapinzani waige
Faizafoxy said:
..........katika wabunge ambao huwasikii kuongea bungeni nadhani aliyekuwa anaongoza ni Rostam
Ninavyjua mimi kutomskia mbunge ni udhaifu sababu katika moja ya moja ya majukumu yake mbunge yeyote aliyemakini anatakiwa kusikika.
 
FaizaFoxy,
Bibie wala huna sababu ya kunisikitikia kwa sababu unajaribu kukwepa ukweli. Regia ni kiongozi na mbunge aliyeteuliwa ambaye hana mamlaka ya kutembelea Tanzania nzima kujua wananchi wako ktk hali gani isipokuwa pale anapolazimika kulingana na majukumu alokabidhiwa. Na moja ya sehemu hizo imetokea kuwa Igunga ambako mstaafu Rostam alikuwa mbunge.

Na wala sii kosa kabia kumzungumzia mtu aliyestaafu mbona kila siku mnamzungumzia Nyerere hapa kwa mabaya na mazuri yake tena huyu hatuko naye tena hapa duniani? nambieni sababu wewe uloona ubaya kumzungumzia Rostam lakini sivyo kwa Nyerere!..Mbona tunamzungumzia Mwinyi na Mkapa na hata viongozi waasisi wa vyama na Mapinduzi wakati wengine wameisha kufa..

Na usipoweza kutangaza tatizo nani atakayeweza kuliona tatizo, Rostam ni tatizo iweje iwe kosa kumzungumzia kwa sababu hakuwa he was the problem not part of the solution ya mjadala mzima wa Igunga. Kiongozi nin yule anayeweza kuonyesha mabaya ya upande wapili na hata kusema makosa aloyafanya kiongozi aliyetangulia ili wananchi wapoate kuona tofauti za mawazo na mipango ktk kukabiliana na tatizo, hivyo usiseme kabisa kwamba kiongozi kazi yake ni kurekebisha pale penye makosa...Je, yule alofanya na kuacha makosa sii kiongozi?

Halafu hakuna mtu alosema matatizo yatakwisha, na kama ingekluwa rahisi hivyo Mwenyezi Mungu asingewaleta mitume wake kwa sababu anajua wakifika matatizo yote yatakwisha. Hivyo sii swala la kumaliza matatizo bali kuwatengenezea mazingira bora ktk maisha yao ili wapate kujipatia maendeleo. Kwa wale wasiojua kusoma na kuandika wapelekee shule na mipango ya elimu hata iwe ngumbaru, mbona tuliweza wakati wa Nyerere?.. hao wauza unga, walevi, wezi na kadhalika tatifiti zinaonyesha sababu kubwa ni ukosekanaji wa ajira.

Kama kiongozi unatakiwa kuweka mazingira ambayo yatamwezesha mwananchi na sii kukubali matokeo hata dini hairuhusu. Na kama kweli ingekuwa hivyo usemavyo wewe Mwenyezi Mungu asingewaleta mitume wake na vitabu akijua kwamba binadamu hawezi kubadilika. Lakini tumeziona tofauti ya uongozi kati ya mitume na hawa viongozi wetu wa leo ambao kazi yao ni kulaumu wananchi wakati policies na matendo yao yanapingana na imnai zao.

Utakuwa unajidanganya sana ukifikiria kwamba kuna shrt cut ktk maendeleo, haya ni mawazo finyu kwa sababu maendeleo sii utajiri kama wa nchi za kiarabu. Maendeleo ya wananchi ni uwezo wa kutosheleza mahitaji yetu ktk kila hitaji jambo ambalo elimu na ujuzi vinatakiwa sana laa sivyo itakuwa maswala ya kutunga mimba mwenezi Mungu atajalia uzazi...Yes, nakubali kwamba kiongozi ni utumishi na utumishi huo una vipimo vyake ambavyo Rostam kashindwa kuvionyesha..Rostam hakuwa kiongozi bali alikuwa mfanyabiashara mzuri sana na pengine kiongozi mzuri ktk biashara zake lakini sii uongozi wa wananchi.

Tamat -Nimemaliza!
 
Tatizo lako kubwa kwenye mada nzima ni uelewa ulioambatana na utetezi wa dhambi. Dhambi kubwa ya Kiongozi na hata ambae si kiongozi ni kuanza kurusha madongo yasiyo na kipimo wala mfano. Mfano unaposema umekuta watu wanatembea uchi ukaanza kumponda Rostam kuwa hajawavalisha nguo au hajafikisha ujumbe wa kuwa kuna nguo siku hizi, naona hapao hujamtendea haki Rostam wala hujajitendea haki wewe mwemyewe. Mifano ya nguo imeshatolewa huko nyuma, sina haja ya kuirudia.

Kusemwa kwa kiongozi ni kwa maendeleo na si kwa kuwa hajafanya hiki au hajafanya kile. Kusemwa kwa kiongozi ni kuwa kafanya hiki hakikuwa sawa na sasa sisi tunafanya hiki, naona umenielewa na kama bado nakuomba tena jitafutie hicho kitabu nilichokushauri wewe na Mbunge wako wa kuchaguliwa. Hata Nyerere tunapomsema tunasema kafanya hiki au kile ambacho kimetufikisha pabaya hatusemi kuwa hajafanya hiki au hajafanya kile. Kusema kuwa Rostam hajafanya chochote chema Igunga kwa miaka 17 ni ukosefu wa uelewa. Ungeniambia kuwa Rostam kafanya hiki lakini sisi tunaona hapa tupafanye hivi ndio bora zaidi hapo ningawaelewa japo kidogo.

Hata hiyo Mitume unayoisema sujaona Mtume akisema kuwa mtume fulani hakufanya hiki au hakufanya kile, naona kuwa kila tunaemsoma kaja kuendeleza na si kuponda wenzake.

Mbunge awe wa kuchaguliwa au wa kupewa kiti cha hisani kazi yake ni kutumikia na si kupakazia wenzake, mantiki ni ileile mtumishi wa umma.

Kuhusu Rostam kuwa hajafanya, hilo tutakesha hapa, labda uniambie kafanya hiki na hakikuwa sawa na ssisi tunaona tfanye hivi ili tuboreshe.

Wasomi ni lazima na wasomi tunao wengi sana na wengine wengi hawako hata hapa Tanzania wako huko ambako elimu zao zitasaidia zaidi.

Kuhusu shortcuts, nadhani hujanielewa "point" yangu. Mfano, leo kuna haja ya kuanza kutengeneza kiwanda cha kutengeneza engine ili uipate hiyo engine uifanye iwe jenereta la kufuwa umeme? la, si hivyo, shortcut ni kununuwa jenereta. Kwa hiyo, shortcuts zipo nyingi sana kwa nchi zetu zinazoendelea kwa kutumia mafanikio ya nchi zilizoendelea amma kuwaleta wasomi wa fani zao waje kutuonesha njia amma kwa kupeleka wataalam wetu wakaone ni nini kitatufaa zaidi, shortcut. Hizo ndio shortcuts na hata hizo nchi zilizoendelea wanazitumia, hukuti leo Muingereza kila anachokitengeza au alichokivumbuwa yeye kinamtosheleza, anazo na shortcuts anazochukuwa kutoka kwa walivyokwisha vumbuwa wenzake au anavyoweza kuvipata kiurahisi zaidi. Sasa nambie shortcuts hizo kuwa hamna.
user-offline.png
Regia Mtema

nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Sasa niambie hizo ndio kauli za amma Mbunge wa kuchaguliwa au kuteuliwa, zinaashiria nini kama si ubaguzi?

Sitegemei kauli kama hizo kutoka kwa yeyote anayeitakia mema nchi yake. Kumbuka, Regia si mara ya kwanza kuonesha hisia zake za Ubaguzi, kisha zitowa hizi kauli mpaka bungeni, Naendelea kukusikitikia ikiwa na wewe ni mmoja wa kuona hayo ni sawa.

Naendelea kukuasa, soma. Elimu haina mwisho na labda utaelewa ni nini nnachokipinga. Sipingi maendeleo napinga kurudi nyuma kimaendeleo na tukianza fulani hajafanya hatutaendelea maisha, tuanze kwa fulani kafanya hiki mimi nikiboreshe au nikibadilishe ili kuwe na tija zaidi.

Kama ulivyokubali kuwa hao wateja wanatokana na kukosa ajira, ukumbuke kuwa hiyo ni "opportunity" ya wengine kutafuta mbinu za kuzumbuwa ajira mpya zitazowafaa wateja, kuvumbuwa madawa ya kuwatibu, kuvumbuwa njia mbadala za kuwaondolea uteja na mengi mengineo, lakini si kuwa ajira hakuna kwa sababu viongozi hawafanyi au kiongozi wa kabla hakufanya. Naona umenielewa.

Tuwache madongo. Tutatutwe matatizo, matatizo kuendelea kuyawekea list kila siku na ukayabadili juu chini katika kila list ni kuyaongeza na si kuyatatuwa, Kuyatatuwa ni kuyaona na kuyapangia mikakati na si kurushiana madongo. Rostam kafanya mengi sana kuliko ujuavyo, labda hayi mengi hayakuwa "good enough". Lakini kusema kuwa Rostam hajafanya ni kama kusema Gadhafi au Saddam hawajafanya, ni kitu ambacho si ukweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom