Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

FaizaFoxy naomba nikuulize swali, naomba uwe mkweli na fair... (if you do not mind)...

Kabla sijakuuliza swali kwanza ni declare interest kuwa mimi ni suporter wa CHADEMA...

Naamini wewe ni suporter wa CCM...

Swali: Ikitokea siku, wewe ukiwa hai na ukiwa unai suport CCM, then CCM wakaondolewa madarakani, kikaingia chama kingine, Je, utaendelea kui-suport CCM (assume pamoja na kuondoka madarakani iwe haijabadilika kisera kwa mujibu wa vipimo vyako)?

Najua hili swali liko nje ya mada, lakini nimeona nikuulize tu hapa badala ya kuanzishia thread yake, na pia ningependa jibu utakalotoa liwe wazi... (sio private)
 
Nakubaliana nawe ktk mengi maadam sina tafiti ya maswala haya kwa undani zaidi maana nimetolewa hata mifano ya Watindiga!..binafsi, sioni tatizo la watu kuhifadhi tamaduni zao wakati huo huo wakichukua yaliyo bora kwenye tamaduni za kigeni, tofauti na sisi tunaotaka hawa Watindiga waache kabisa tamaduni zao za hifadhi ya misitu, wanyama na nguvu kazi ya asili za uchungaji ili waingie mjini kupuyanga matokeo yake ndio haya na hao Masai siku hizi nasikia ndio Mashoga!..

Kuhusu Regia Mtema sidhani pia kama anafanya makosa kusema Mbunge unatakiwa uwe na ushawishi kwa sababu ndivyo inavyotakiwa kisiasa. Ndivyo siasa zinavyochezwa mahala popote toka anagombea Ubunge ni swala la ushawishi wake bungeni kuweza kupeleka maendeleo jimboni kwa sababu lazima tukubali kwamba Wabunge sii tu wawakilishi wa wananchi bungeni kwenda kukaa na kupiga usingizi wakitegema serikali imeshapanga kila kitu, bali pia wanatakiwa kuwa na uwezo wa kushawishi kulingana na ilani zao kwa nini tujenge barabara ya lami Igunga kwenda Tabora kabla ya daraja la Kigamboni na kadhalika. Hizi ahadi ndizo zilizompa kura hivyo ni lazima aziwakilishe bungeni.

Na yatakuwa makosa makubwa kwa mbunge kwenda bungeni akitegemea kwamba serikiali ityabuni miradi ya maendeleo ikiwa yeye mwenyewe hana mpango wa maendeleo ya jimbo lake, bila shaka sababu kubwa ya kugawa majimbo ni kurahisisha kazi ya utawala kuweza kupata wawakilishi wa wananchi badala ya rais ama viongozi wa serikali kuu kutembelea kila jimbo kutazma wataweza kupeleka kitu gani ktk maendeleo ya wananchi.

Mimi nilivyomwelewa Regia ni kwamba hakutegemea mbunge mwenye sifa na majigambo kama Rostam angeshindwa kabisa kuwapelekea wananchi wa Igunga maendeleo kwa kupanga vizuri sehemu za huduma kama shule na zahanati kiasi kwamba kaeleza kuna watu wanatembea maili 10 kutafuta maji, shule au zahanati..sehemu kubwa bado kabisa iko nyuma sana na sidhani kama haya ni makosa ya wananchi ati hawataki kubadiliko isipokuwa hakuna mazingira bora ya wao kuweza kubadilika..Amini maneno yangu mkuu wangu kama utaweka mazingira bora wananchi watabadilika tu, sisi huku majuu tumebadilika sii kwa kupenda isipokuwa imetulazimu tubadilike ili tuweze kuishi nchi hizi.

Haya ni mawazo mabaya sana na ni chembechembe za Ubinafsi kama wazungu wanavyotuona sisi weusi hatupendi maendeleo. Wanatuona wavivu na wajeuri tusopenda maendeleo lakini ukitazama deal packages zao huyaoni mazuri wanayotutakia isipokuwa wanachozungumzia ni jinsi ya kukutumia zaidi.. Na pengine hawa Watindiga, Wasukuma wa Maswa na wengineo hutazama kwanza malengo ya kuwepo vitu hivi maanake siku hizi watu wanajengewa shule na zahanati ili waachie ardhi na machimbo yao ya dhahabu... Tena wakiahidiwa kusomeshwa bure watoto zao na kupewa makazi mapya..

Ningeomba sana tujadili issues na sii kumjadili Regia ambaye kaiweka mada hii na kwa bahati nzuri sote hapa tunakubaliana kwamba sii Igunga tu ambako hakuna maendeleo, bali umaskini wa Igunga upo sehemu kubwa ya Tanzania na hapo ndipo tunatakiwa kuanzia mjadala mrefu kuhusu maendeleo yetu. Kumzungumzia Regia ndio simple minded lakini sii kumzungumzia Rostam kutokana na madai yake ya kupeleka maendeleo makubwa Igunga hali hakuna kitu kabisa..

Mkuu nakubaliana na wewe kwa mengi lakini sidhani tukishamchagua mbunge basi tukae tuu atatuletea maendeleo. Kwangu suala sion kutotegemea mbunge mwenye sifa na majigambo kama Rostam ashindwe kabisa kuwapelekea wananchi wa Igunga maendeleo. Suala kwangu ni baada ya kushindwa kupeleka hayo manendeleo Wana Igunga walifanya nini kuhakikisha anafanya aliyohaidi?

Sikatai kuwa mazingira bora yanasaidia wananchi kubabadilika. Lakini at the same time inabidi tukubali kuwa pamoja na mazingira bora still mtu anaweza asibadilike kama bado hajaamua kufanya hivyo. Sijaelewa unaposema huko majuu umebadilika si kwa kupenda isipokuwa imekulazimu kubadilika ili uweze kuishi nchi hizo. Mimi naongelea willingness ya kubadilika bila kulazimishwa. Hata wewe wenyewe ujiangalia kwa undani you just changed from the outset ili uweze kuishi huko majuu but the true inner of you, bado you are a truly an African. You are not a westerner na sidhani kama unajiita hivyo. Siku ukiamua kurudi Tanzania, you will just behave like other Tanzanians.

Mkuu kuna principles mbili za human behaviour. Principle ya kwanza ni kwamba people do not change. Principle ya pili ni kwamba kama mtu amekuwa akifanya kitu same way kwa miaka mingi atakuwa mgumu kubadilika which is moot since principle ya kwanza still applies. Kuna usemi mmoja wa Kiingereza unasema "You can take people out of the gutter but you can't take the gutter out of the people'. Huu usemi una ukweli kwa asilimia 99 ya Watanzania. Wapo wanaosema once people pass their early teenage years, they remain the same person for the rest of their life. Labda ndio maana wazee wengi hawapendi mabadiliko? Watu wengine wako tayari kufa ili wasibadilike.

Uinaitisha mkutano wa hadhara watu wanajaa wanashangilia yote unayosema na kusukuma hata gari gari. Unamaliza mkutano very confident kuwa lazima watakupa kura za kumwaga. Still unashindwa uchaguzi. Why? Mkuu nafikiri ni muhimu hasa kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani kujua kuwa behavior ya Watanzania haitokani na spur of the moment decisions or whims. Behavior za Watanzania zinatokana na vitu kama experinces zao tokea wazaliwe, experiences za familia zao za karibu, experiences za jamii wanayotoka na experiences of generations of people who have influenced the members of their community.

Ndio maana kwa mfano tatizo la umeme limeendelea kuwepo kwa miaka na miaka. Why? Kwa sababu kila kunapokuwepo na tatizo, Watanzania tuna tabia la kuliongelea sana bila kuchukua drastic actions kutatua tatizo. Pia tuna tuna kasumba kuyaacha matatizo na kumwomba Mungu ayatatue. Likitokea tatizo tuu utasikia Ewe Mungu tusaidie. We don't bother to address our problems. Kwa nini huko majuu likitokea tatizo hawamsubiri Mungu kutatua tatizo? Hii ni rooted behavour kwa Watanzania wengi sana.

Kwa hiyo wakati watu wanapo behave kwa namna fulani kuna maelfu ya miaka ya evolution kwenye matendo yao. No one can simply say they are being stupid or ignorant for behaving the way they do. Put yourself in their shoes for their lifetime and you would do exactly the same. Kwa hiyo watu hawatabadilika ghafla kwa sababu someone who has not earned their trust or respect tells them to.

You have to undo their deep-rooted beliefs one by one to get them back to the basics again. The deeper you dig, the more you will find that each of their behaviours was set in place for a legitimate reason. To undo it will require changing the factors and circumstances (mazingira?) that initially spurred each change. However, that will only and only be possible if they themselves are willing to change. So, simply changing ideology or rhetoric is not going to change people.
 
Mh Regia,nashukuru kwa ku-post huo uzi lakini I wish mngetengeneza documentary ili watu waione halfu kisha mnapokuwa mnakema jambo,mnapokuwa mnakataa japo na mnapokuwa mnatetea hoja hata kule bungeni watu waeweze kuwaelewa,tena nataka nikwambia hivi kwa kuwa hukuwa na muda uliojaa utlivu,ungeliweza kuyasoma maisha ya wana I gunga ukajua jinsi watu wanavyotenda dhambi za mauaji ndani ya nchi hii halafu hata tu kufika eneo la kituo cha polisi kwa kuonekana alitaka kukamatwa haukuna.
I gunga ni hatari,tena umenikumbusha mbali sana uliposema maji wanachota kwenye makomelo,nilitamani watu wangeona makomelo yanafananaje.Mh Regia umenikumbusha mbali sana tena umenitosha kidonda kabisa,maumivu ndani moyo yamenianza upya maana nilishasahau kidogo kwani hapa Dar napata maji ya kuchimbwa kwenye visima binafsi vilivyo kando kando ya pit latrine zilizo zagaa hapa uswazi-DAR.lakini kumbukumbu zangu zimerudi mwaka 1978/79 wakati niko kijiji kimoja kiitwacho MWANGONGO wilaya ya shinyanga vijijini wakati ule na leo ni wilaya ya Kishapu kwa mbunge wa magamba.wakati huo mama yangu mzazi alikuwa anaamuka saa tisa usiku au saa kumi usiku kwenda kuchota kwenye makomelo na anarudi kati ya saa tatu/nne asubuhi hivi.imeniuma sana kunikumbusha hilo,na hapo baba yangu alikuwa mwalimu aktika shule ya msingi mwangongo,na mimi nilikuwa na kaa chini kwenye matofali,labda kwa kuwa ilikuwa shule mpya ya msingi.
Point yangu ni kuna magumu zaidi hapo Igunga tena kuna shida balaa,unafuu upo kidogo kwenye center,mfano,Igunga mjini,Ibologelo,Nanga,Ziba,Choma,Nkinga pale kenye mission ya wapentekoste na ndipo ilipo hospitali kubwa maana siku za nyuma walikuwepo wamissionary wakii-run,Nsimbo na choma cha nkola,sehemu zingine ni hatari huko ndani ni kweli kuna watu wanatembea uchi na wengine vikaptula tu.
Watanzania miaka hamsini ya uhuru ndo hali iko hivyo,mama yangu alichota maji kwenye makomelo miaka ya 1978 na leo bado iko hivyo,ila wanataka tuiilipe Dowans,aaah jamani hapo tunatafutana ugomvi,kikweli narudi kauli yangu mimi kuipenda au kuishabikia ccm au hata kuipigia kura ccm ni dhambi mbaya kama kufanya mapenzi namama yangu mzazi,No way this terrible.tukisema ooh magwanda magwanda,hata hao wanaigunga nawapa pole sana na sijui kimetokea nini,Jamani mimi inaniuma maana nayajua maeneo ya Igunga,niliwahi kwenda Nkinga kitongoji kimoja nyuma ya hospitali ya mission ukielekea magharibi kama km 10/13 nilipikiwa chai kwenye ho mji kwa maji mazito yenye rangi kam umetia maziwa,nilitapika kwa njisi hali ilivyokuwa na ilikuwa mwaka 1999.

Ni kweli sina imani kama RA atasamehewa kwa hayo mambo
 
FaizaFoxy naomba nikuulize swali, naomba uwe mkweli na fair... (if you do not mind)...

Kabla sijakuuliza swali kwanza ni declare interest kuwa mimi ni suporter wa CHADEMA...

Naamini wewe ni suporter wa CCM...

Swali: Ikitokea siku, wewe ukiwa hai na ukiwa unai suport CCM, then CCM wakaondolewa madarakani, kikaingia chama kingine, Je, utaendelea kui-suport CCM (assume pamoja na kuondoka madarakani iwe haijabadilika kisera kwa mujibu wa vipimo vyako)?

Najua hili swali liko nje ya mada, lakini nimeona nikuulize tu hapa badala ya kuanzishia thread yake, na pia ningependa jibu utakalotoa liwe wazi... (sio private)


Hili swali lako au linalofanana na hili nimeshalijibu kwenye nyuzi nyingine. Kwa kifupi "NDIO" kama kitakuwa bado kipo hai.
 
FaizaFoxy,
Bibie wala huna sababu ya kunisikitikia kwa sababu unajaribu kukwepa ukweli. Regia ni kiongozi na mbunge aliyeteuliwa ambaye hana mamlaka ya kutembelea Tanzania nzima kujua wananchi wako ktk hali gani isipokuwa pale anapolazimika kulingana na majukumu alokabidhiwa. Na moja ya sehemu hizo imetokea kuwa Igunga ambako mstaafu Rostam alikuwa mbunge.
Tamat -Nimemaliza!
Mbunge wa taifa (wa viti maalum/kuteuliwa) kazi yake kubwa hasa ni kwenye policy-making/development.
Ni lazima ajue status quo ya nchi yetu katika mambo mbalimbali.
Ukiniambia leo ulikuwa hujui watanzania vijijini wana matatizo hayo, inamaanisha ulikuwa hufuatilii. Yaani 2010 alikuwa hajui, amejua hayo mwezi uliopita.
Kama waziri kivuli wa kazi, angetueleza mchango wake kuhusu kuongeza ajira kwa vijana mijini na vijijini.Hebu niambie muswaada ulioandikwa naye kuhusu hizi issues, hata kama haukupitishwa.
Mnanishangaza sana mnapowatetea wabunge ambao maishani mwao hawajawahi ku-sponsor au ku-draft muswaada wowote. Ubunge siyo kuuliza maswali na kusoma bajeti mbadala, ni kutunga sheria through miswaada. Ndio maana wenzetu huangalia records za mbunge wao kwenye voting na miswaada aliyoandka/pitisha/kataa.
Mnasifia vitu ambavyo havimake sense ndugu zanguni.Hapo kwnye red unasikitisha.
 
Regia ni kiongozi na mbunge aliyeteuliwa ambaye hana mamlaka ya kutembelea Tanzania nzima kujua wananchi wako ktk hali gani isipokuwa pale anapolazimika kulingana na majukumu alokabidhiwa. Na moja ya sehemu hizo imetokea kuwa Igunga ambako mstaafu Rostam alikuwa mbunge.

Mkuu nafikiri pia ni Waziri kivuli wa kazi na Ajira? A shadow Minister ‘shadows' or keeps an eye on the activities of the corresponding government Minister. This is a very important role within the system of checks and balances that is part of responsible government. A shadow Minister is the Opposition's spokesperson for a particular portfolio or policy area.

Shadow Ministers also develop their own policies for what they would do if they were in government. Being a Shadow Minister means you must act like a Minister-in-waiting. You have to keep a close eye on what the respective government Minister does, and let the public know what you would do differently.

Kwa vile alijionea mwenyewe hali ilivyo Igunga, as a shadow minister inabidi aje na policy on how Chadema ita address tatizo la ajira na kazi sio tuu Igunga bali pia nchi nzima. Kumtolea tuu povu Rostam haitoshi. As a shadow minister I am sure Chadema watakuwa wame allocate funds kwenye ministry yake kutembelea sehemu mbalimbali za nchi na kujionea hali halisi ya ajira na kazi. Otherwise, ina maana kama Rostam asingejivua gamba Regia Mtema asingeona aliyoyaona huko Igunga which is shocking really kwa a minister in waiting.
 
CHADEMA wanatuhumiwa kumvua DC Fatuma Kimario Hijabu TU.....,Mwigulu Nchemba anatuhumiwa kumvua mke wa Ustaadh kada mwezio CHUPI na hijabu.

Wafuasi wa CHADEMA wanatuhumiwa,japo Polisi hawajathibitisha mpaka tunakwenda JF kwamba wamemwagia kada wa Magamba tindikali na kuhatarisha uchaguzi.RAGE alikuwa na Bastola kiunoni ambayo ilitumika KUHAMASISHA uchaguzi.

CHADEMA moyoni,CCM machoni
 
Nawashukuru sana Wakuu Mkandara na EMT kwa kuja na hoja positive na zenye kujenga..Ninayapokea na nitayafanyia Kazi.
 

Mkuu mkadara unawajua au umewai kuwasikia jamii ya watu wanaitwa watindiga au wamang'ati. Unapoogelea hizi jamii development kwao ina mtazamo tofauti na jamii nyingine. So miradi ya mendeeleo kwa hizi jamii inatakiwa itambue hilo. Jamii hizo zinahitaji zaidi miradi ya kulinda mistu na mapori wanayoishi kuliko hata shule na hospitali.


Sijui kama kuna mtua ana takwimu za Population ya watu hawa na area wanayocover kwa movement zao

Kwa hakika hili ndilo tatizo kubwa kwenye nchi zetu za Africa na TZ nadhani tunaongoza katika kupeleka maeendeleo bila kufikiria sustainability ya hizo development concept. Nyerere alisema maendeleo ni ya watu kwaajili ya watu....very few elites wameweza digest hii concept ya Nyerere ndiyo maana wengi wanamwenzi kama cover tu ya kupata madaraka...

Mtu unawapelekea wamang'ati shule bila kuzingatia elimu unayoipeleka itawasaidiaje katika kuendeleza maisha yao hapo walipo; wanaona kila leo mito inakauka, majani yanapungua hivi vyote vina impact maisha yao na hakuna katika wale waliotoka kwenye hiyo jamii ambao wasomeshwa wameweza kusaidia katika hilo zaidi ya kushirikiana na maadui wao wa maendeleo (serikali na sera zake za kuwahamisha bila kuangalia jinsi mifugo inavyo athirika katika hilo zoezi) yao kupisha sheria za kuwafilisi then utegemee hao watu wahamasike kupeleka watoto wao shule? Kama elimu lengo lake nikumwezesha mwanadamu kumudu mazingira yake vipi iwe kwa hizi jamii kinyume? Wao wanaujuzi ambao haujawa documented (wengine tumezi document nakufanikiwa kupata vyeti) kuhusu jinsi ya kutatua matatizo yao; lakini kutokana na dhana ya kuwa na serikali yenye kufikiria maendeleo pasipo kuzingatia ni kwaajili ya kina nani na wakati gani wamebaki kuwa kama wakimbizi katika nchi yao! Laiti kama serikali yao ingeishi katika maneno ya mwasisi wa nchi..'Maeneleo ya watu kwaajili ya watu'
 
Nimeipenda signature yako

Na ya kwako pia imenigusa ila nataka kui-comment kama kweli unataka Kilombero i change hiyo concept kwenye signature yako siyo strategy nzuri...inaongeza burden kwa locals na kama huo mfuko utawekezwa na externals utaondoa ile sense of ownership kwa Locals na kuwa na impact sawa na aid...Angalia watu wa Sonjo walivyokuwa discouraged na promisses walizo pewa za micro crediting na moja ya miradi iliyowahi kuwapo hapo Kwa details contact me privately tu discuss jinsi ya kuibadili Kilombero na wewe kuwa mbunge mpaka uchokee mwenyewe...Money is a media of exchange and never on its own a resource....
 
  • Thanks
Reactions: ral
Hili swali lako au linalofanana na hili nimeshalijibu kwenye nyuzi nyingine. Kwa kifupi "NDIO" kama kitakuwa bado kipo hai.

FF leo umeni impress kweli kweli; kwahiyo nawe unaamini kimoyo moyo japo kwa mdomo utapinga kuwa CCM kipo hai kwasababu tu kina dola nje ya hapo hakiwezi ishi....Asante sana kwa ukiri huu big up!
 
rostam



Wakuu mbona tunakuwa wasahaulifu namna hii?????? Huyu tapeli si aliongea hotuba hii juzi juzi tu??????


1. HOTUBA YA MHE. ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA - TABORA


UTANGULIZI

WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo, napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake.

Wazee wangu wa Igunga, baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi nyote mmoja mmoja na katika umoja wenu kwa kuitikia wito wangu, kijana wenu, niliyewaomba nije nizungumze nanyi siku hii ya leo.

Nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba, kama si nyinyi wazee wangu na wengine wengi ambao hatuko nao hapa leo kwa sababu mbalimbali, ambao mmekuwa na imani kubwa nami nisingeweza kufikia hapa nilipofika sasa.

Wazee wangu, waasisi wa taifa letu walitufundisha kutambua na kuheshimu ukweli kwamba; ‘Uongozi ni Dhamana' dhana ambayo kila ninapokaa na kutafakari huwa inanirejesha nyuma na kukumbuka jinsi nyinyi mlivyokaa katika umoja wenu na kuniteua mimi, miongoni mwa vijana wenu wengi, kuwa mwakilishi wa Jimbo la Igunga tangu mwaka 1994.

Katika kipindi hicho chote cha utumishi wangu, nyinyi wazee wangu mmekuwa mhimili muhimu ambao umeniwezesha kutimiza wajibu wangu kwa bidii kubwa, maarifa na nidhamu ya hali ya juu nikitambua namna ambavyo mmekuwa na imani kubwa juu yangu.

Ari na moyo wa imani, ushirikiano na mshikamano ambao wazee wangu mmekuwa nao kwangu ndiyo ambao kwa kiwango kikubwa umetuwezesha kufanya kazi kwa pamoja, tukishinda changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilikabili jimbo letu katika kipindi chote ambacho mmeendelea kuniamini kuwa mbunge wenu kwa miaka 18 sasa.

Wakati nikitambua na kuheshimu ukweli kwamba katika kipindi chote cha ubunge wangu mmekuwa na imani kubwa nami na kuniunga mkono kwa dhati, naamini kwamba kwa upande wangu pia nimejitahidi kwa kadiri nilivyoweza, kutimiza matarajio ya wananchi wa Igunga.

Miongoni mwa mafanikio makubwa tuliyoyafikia kupitia ushirikiano wetu na uongozi wa pamoja ni kwamba, mwaka 1994 Igunga ilikuwa ni wilaya ya mwisho kwa maendeleo mkoani Tabora lakini leo ndiyo ya kwanza, taa za barabarani, bima ya afya kwa kila kaya, zahanati kila kijiji na shule nyingi kuliko idadi ya kata zilizomo kwenye wilaya.


Wakati nikitambua na kuheshimu ukweli kwamba katika kipindi chote cha ubunge wangu mmekuwa na imani kubwa nami na kuniunga mkono kwa dhati, naamini kwamba kwa upande wangu pia nimejitahidi kwa kadiri nilivyoweza, kutimiza matarajio ya wananchi wa Igunga.

Wazee wangu, nayasema haya nikitambua kwamba, kama ilivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini, mafanikio makubwa tuliyoyapata katika nyanja za elimu, afya, makaazi bora na kilimo katika kipindi hicho chote hayajaweza kumaliza changamoto zote za maendeleo ambazo zinatukabili.

Wazee wangu, ingawa nimekuwa na kawaida ya kukutana na kuzungumza nanyi mara kwa mara, mmoja mmoja na wakati mwingine katika umoja wenu, wito wangu wa leo una makusudi ambayo kwa kiwango kikubwa ni tofauti na yale ambayo tumeyazoea.

Japokuwa ujumbe ninaotaka kuzungumza nanyi wazee wangu, si mgeni sana masikioni mwenu, tofauti ya leo na mikutano yetu mingine iliyopita ni uamuzi ambao nimekusudia kuufanya na ambao nitayatangaza muda mfupi ujao.

YATOKANAYO

Wazee wangu, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu hali ya siasa nchini na hususani afya ya kisiasa na matukio mengine ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho mimi ni mwanachama wake na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) nikiuwakilisha Mkoa wetu wa Tabora.

Naamini kwamba katika kufuatilia kwenu mtakuwa mmebaini kuwapo kwa matukio ambayo kwa namna moja au nyingine yamekuwa yakitokea huku yakiligusa jina langu na wakati fulani nafasi yangu kama kiongozi wa chama hicho.

Wazee wangu, nayasema hayo kwa sababu mara kwa mara ninapokutana nanyi nikiwa katika ziara zangu jimboni na wakati mwingine mnapowasiliana nami kwa njia mbalimbali mmekuwa mkionesha kuguswa kushitushwa na kutaka kujua kulikoni kuhusu mambo hayo yanayotokea.

Mimi, kama mnavyonijua nyote, ni mtu muwazi na mkweli. Siku zote nimekuwa mwepesi sana wa kuwaeleza kuhusu kila kinachotokea ili kuwaondoa hofu na wakati huo huo kuwahakikishia kwamba masuala yasiyo na msingi hususani yale yanayogusa siasa za kitaifa hayawezi kutuondoa katika mstari sahihi wa kuwahudumia wananchi wa Igunga, mkiwamo nyinyi wazee wangu ambao mmeniamini na kunituma kuwawakilisha.

Nyinyi wenyewe ni mashahidi wazuri kwamba tangu matukio yanayogusa jina langu yaanze kutokea miezi michache tu baada ya Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikweti kuingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005, tumekuwa tukiyapuuza na tukaendelea kufanya kazi pamoja kwa bidii.

Bado naamini na nitaendelea kuamini kwamba tulifanya uamuzi sahihi wa kuyapuuza matukio hayo kwani mbali ya kuendelea kutimiza malengo mbalimbali yaliyokuwamo katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya CCM, pia mliendelea kuniamini kwa nafasi yangu ya kuwa mwakilishi wenu bungeni na hata mkaniruhusu nibebe jukumu jingine kubwa la kuwa Mjumbe wa NEC ninayewakilisha mkoa wetu wa kihistoria wa Tabora.

Wazee wangu, nyinyi ndiyo watu mnaolifahamu vyema jimbo letu la Igunga na hakika nyinyi ni sehemu muhimu ya watu wanaojua historia ya kisiasa ya Mkoa wa Tabora kwa miaka mingi hata kabla ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

Hakuna shaka hata kidogo kwamba, Tabora ni kitovu hasa cha uasisi wa siasa za vyama vingi hapa nchini. Ni wazi kwamba huwezi ukazungumzia chimbuko la vyama vya upinzani tunavyoviona hapa nchini leo pasipo kugusa mkoa huu ambao umekuwa chimbuko la wanasiasa wenye mizizi hapa na nchini kwa ujumla.

Majina ya wanasiasa wa aina ya wazee wetu, hayati Chifu Said Abdallah Fundikira na Christopher Kassanga Tumbo, Kasela Bantu (Mungu awalaze mahala pema peponi), James Mapalala, Profesa Ibrahim Lipumba na mengi mengine yana mizizi yao katika Mkoa wetu wa Tabora.

Kutokana na ukweli huo basi ni wazi kwamba, nikiwa Mbunge wa Igunga kwa vipindi vinne mfululizo na wakati huo huo nikiwa Mjumbe wa NEC kwa vipindi vitatu mfululizo, moja ya kazi ambazo nimezifanya kwa uaminifu na kwa bidii kubwa huku nikiungwa mkono na kushirikiana nanyi ni ile ya kuhakikisha kwamba mkoa huu pamoja na kuwa kitovu cha upinzani unaendelea kubakia kuwa ngome muhimu ya kisiasa ya CCM.

Si vibaya tukakumbushana kwamba, wakati nachaguliwa kuwa mjumbe wa NEC wa Mkoa mwaka 1997, jimbo moja katika mkoa wetu lilikuwa likishikiliwa na upinzani. Leo hii Tabora ni mkoa pekee miongoni mwa mikoa iliyotuzunguka ambao haukupoteza jimbo hata moja kwenda upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Mafanikio haya tuliyafikia kwa pamoja kutokana na ushirikiano wenu wazee wangu.

Wazee wangu, Waswahili wanasema usione vyaelea, vimeundwa. Kazi ya kuijenga CCM katika mazingira yenye mizizi hasa ya upinzani nikiwa mbunge na hususani M-NEC kutoka Mkoa wa Tabora haijapata kuwa rahisi na itaendelea kuwa ngumu na ambayo mapambano yake ni makali sana.

Wazee wangu, kwa namna ya pekee kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyinyi wazee wangu wa Igunga na wananchi wenzangu wote wa Mkoa wa Tabora kwa kushikamana na kuifanya kazi hiyo kwa bidii, uaminifu na mafanikio makubwa.

Matunda ya kazi hiyo kubwa yanaonekana. Pamoja na kuwa kitovu cha kihistoria cha siasa za upinzani, Tabora ndiyo mkoa pekee katika eneo hili ambao unaongozwa na wabunge wote kutoka CCM baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na hata kabla ya hapo.

Kwa sababu hiyo basi, wazee wangu, sote katika umoja wetu ukiacha mafanikio makubwa tuliyopata katika jimbo na Wilaya yetu ya Igunga, tunayo mambo mengine ya msingi ya kujivunia. Kwa moyo wa dhati na kwa unyenyekevu mkubwa napenda kuwapongeza kwa namna mlivyojitoa kukipigania na kukitetea chama chetu kwa ari na nguvu ya kipekee.

KUJIVUA GAMBA

Wazee wangu, chama chetu chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kimeamua kwa kauli na nia moja kujitathmini na kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo yenye lengo la kukiwezesha kiendelee kubakia chama kinachoaminiwa na kuungwa mkono na Watanzania walio wengi.

Dhamira ya mwelekeo huo wa kufanya mabadiliko ya ndani ya chama chetu ilitangazwa rasmi na Mwenyekiti wetu Rais Kikwete wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, mjini Dodoma.

Katika hotuba yake hiyo, Rais Kikwete aliyafananisha mabadiliko hayo na tabia ya kawaida na ya asili ya nyoka na wanyama wengine kadhaa ya ‘Kujivua Gamba'.

Wazee wangu hatua ya kwanza ya utekelezaji wa azimio hilo na mwelekeo huo sahihi ilifanyika mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya CCM ambacho mimi nilikuwa mjumbe wake.

Wakati wa kikao hicho, wajumbe wote wa Kamati Kuu na wale wa Sekretarieti ya chama chetu wa wakati huo kwa kauli moja tulikubaliana kujiuzulu, lengo likiwa ni kumpa Mwenyekiti wetu fursa nzuri ya kufanya mabadiliko ya uongozi yatakayotoa nafasi ya kupata mwelekeo mpya wa Chama.

Wazee wangu, tulifanya hivyo tukionesha kuunga mkono kwa asilimia 100 kile ambacho bado naendelea kuamini kuwa ni mawazo sahihi na yenye mwelekeo thabiti ya Mwenyekiti wetu ambayo kwa kiwango kikubwa yalikuwa yakiakisi matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa urais, ubunge na udiwani wa Oktoba mwaka jana.

Niliseme kwa maneno machache tu hili. Ingawa ni kweli kwamba Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana umekirudisha madarakani chama chetu kwa kukipa ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani kwa Tanzania Bara na Zanzibar, kiwango cha ushindi tulichopata kimeonyesha waziwazi dalili za wananchi kupunguza imani yao kwetu kuilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2005.

Tungekuwa ni chama cha siasa cha ovyo iwapo tungepuuza kupungua kwa kura za rais kutoka zaidi ya asilimia 80 tulizopata mwaka 2005 hadi kufikia aislimia 61 mwaka jana kiwango ambacho ni pungufu kwa asilimia 20 ya kura katika kipindi cha miaka mitano tu, hasa ikizingatia ukweli kwamba mgombea urais ni mtu yule yule.

Tungekuwa ni chama cha siasa kilichokosa umakini iwapo tungekaa pasipo kuchukua hatua zozote za kujiimarisha baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha wazi kukua kwa upinzani ambao umeongeza idadi ya wabunge na madiwani katika pande zote mbili za muungano.

Matokeo hayo ya uchaguzi ambayo hapana shaka yamekitikisa chama chetu yalitukumbusha wasia ambao tuliachiwa na Baba wa Taifa aliyesema; ‘Bila ya CCM Madhubuti Nchi Yetu Itayumba'.

Wazee wangu, kwa sababu ya kutambua ukweli kwamba hakuna haki isiyo na wajibu kama nilivyosema awali, mimi na wenzangu tuliokuwa katika Kamati Kuu tuliona ulazima, haja na umuhimu wa kukubali kwa kauli moja wito wa kututaka tujiuzulu ikiwa ni hatua moja ya kujipanga na kukijenga upya chama chetu.

KUJIVUA GAMBA KWAPOTOSHWA

Wazee wangu, kilichotokea baada ya kujiuzulu kwetu kila aliye ndani na nje ya chama chetu amekisikia na anakifahamu. Chama kilipata safu mpya ya uongozi iliyotokana na kuundwa kwa Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wetu mpya, Mhe. Wilson Mukama, na Kamati Kuu iliyokuwa na sura tofauti na ile ya awali.

Wakati tukitafakari na kuangalia mustakabali mpya wa kisiasa ndani ya chama chetu, ghafla yalianza kutokea mambo ambayo chokochoko zake zilianza kusikika tangu tukiwa ndani ya Kamati Kuu ambayo ilijiuzulu baadaye.

Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kilichagua wajumbe wapya wa Kamati Kuu na kuidhinisha uundwaji wa Sekretarieti mpya, dhana ya kujivua gamba ambayo naamini Mwenyekiti wetu aliianzisha kwa nia njema ilianza kuenezwa ikichukua tafsiri na mwelekeo tofauti na ule wa awali.

Wajumbe wawili wa Sekretarieti, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Mhe. John Chiligati, na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Nape Nnauye, walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuzi wa kuwapa siku tisini wale walioitwa watuhumiwa wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyo watafukuzwa na chama.

Wazee wangu, baada ya kushinikizwa sana na vyombo vya habari wawataje kwa majina wanasiasa waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC na ambao wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, wajumbe hao wa Sekretarieti walikwenda mbele zaidi.

Baada ya awali kuwaeleza waandishi wa habari kwamba majina ya watuhumiwa hao yalikuwa yakifahamika kutokana na kuhusishwa katika kashfa tofauti kama zile za Richmond, EPA na ununuzi wa rada, mwishoni viongozi hao walikaririwa wakiyataja majina ya wanasiasa watatu kuwa ndiyo ambao walikuwa wakilengwa na maamuzi hayo.

Wazee wangu, nilishangazwa na kushitushwa na namna porojo na fitina za kisiasa zilivyofinyangwa kwa mara nyingine tena baada ya kusikia jina la mbunge wenu ambaye ni mimi, likitajwa kuwa miongoni mwa yale matatu ya viongozi waliokuwa wakitakiwa eti kupima wenyewe na kisha kuchukua uamuzi wa kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya NEC katika kipindi cha siku tisini.

Niliseme hili mapema. Mshangao na mshituko wangu haukusababishwa na kutajwa kwa jina langu, la hasha, bali namna uamuzi halisi wa NEC na hususani dhana nzima ya ‘kujivua gamba' ilivyoweza kupindishwa na wajanja wachache na kisha kuendeshwa kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani cha watu.

Pili, nilishangazwa na kushitushwa na hatua ya viongozi wa chama changu ambacho nimekitumikia kwa bidii na uaminifu mkubwa kufanya juhudi kubwa hata kukivisha kikao kitukufu cha NEC uamuzi ambao msingi wa hoja zake ni vita vya kimakundi ya kisiasa yaliyo ndani ya CCM kwa upande mmoja na propaganda za vyama vya siasa vya upinzani na vyombo vya habari kwa upande mwingine.

Tatu, nilishangazwa na kushitushwa na ujasiri ambao umekuwa ukioneshwa na baadhi ya viongozi wetu wapya wa Sekretarieti wanaolitaja jina langu na kulihusisha na kile wanachokiita ufisadi ambao hata ukweli wa kimazingira na kihistoria ukiachilia mbali ushahidi wa wazi umeshathibitisha kwamba ni porojo za kisiasa zilizotokana na makovu na matarajio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na ule ujao wa 2015.

Wazee wangu, nyinyi ni mashahidi kwamba, mbali ya mimi mwenyewe kujitokeza kupitia vyombo vya habari na kueleza wazi kwamba sijapata kujihusisha katika vitendo vyovyote vya ukiukwaji wa maadili ya uongozi au vya rushwa, hakuna ushahidi wowote uliotolewa unaonihusisha na kashfa yoyote miongoni mwa zile zilizotajwa.

Wazee wangu, ni wazi kwamba kama chama chenye siasa chenye dhamana ya kuwaoongoza Watanzania kutoka katika lindi la ufukara, maradhi, matatizo ya makaazi na mengineyo siku zote tunapaswa kuwa makini katika kuhakikisha kwamba changamoto za kuwaongoza na kuwakomboa wananchi waliotupa dhamana hazitikiswi na mawimbi ya matakwa ya nyakati ama ya vyombo vya habari au wapinzani wetu wa kisiasa walio nje ya CCM.

Ni kwa sababu ya kulitambua hilo na hasa kuyatambua madhara yanayoweza kukipata chama chetu na nchi yetu iwapo tutaendekeza siasa za kupakana matope pasipo na sababu za msingi, kuchafuana kusikokoma na kulipizana kisasi ndiyo maana nimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi wazee wangu ili kuweka kumbukumbu sahihi.

MAAMUZI YANGU

Wazee wangu, nimetafakari sana na kimsingi nimefikia hatua ya kupima yale ambayo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa juu yangu na ambayo kwa mtazamo wangu unaoungwa mkono na wanafamilia yangu, marafiki zangu na washirika wangu wa kibiashara walio ndani na nje ya nchi, naona umefika wakati muafaka wa kuchukua hatua.

Kwa sababu ya kutambua uzito wa hatua ninazokusudia kuzichukua, niliona halitakuwa jambo la hekima hata kidogo iwapo ningefanya hivyo pahala pengine popote bali hapa Igunga mbele ya nyie wazee wangu.

Baada ya kukaa na wanafamilia yangu, marafiki na washirika wangu wa kibiashara niliona halitakuwa jambo la busara hata kidogo kuendelea kuvutana na viongozi wa chama changu na wanachama wenzangu wa CCM katika mambo ambayo yanaweza kumalizwa kwa njia muafaka.

Wazee wangu, sina budi niwaeleze kwamba, mbali ya athari za kisiasa na kifamilia, vita vya ovyo vya kisiasa kama hivi tunavyoviendesha na kuviendeleza ndani ya CCM na ndani ya nchi yetu huwa vina athari kubwa katika ulimwengu wa kibiashara. Athari kama hizo za kibiashara huingia ndani zaidi kuliko vichwa vya habari vya magazeti vinavyolenga kuchafuana, na athari hizo huwa kubwa zaidi kwa mtu kama mimi kwa sababu tofauti na wengine wengi hapa nchini, mimi ni mfanyabiashara wa kimataifa.

Katika ulimwengu wa kibiashara wa leo, vita hivi ambavyo vinaweza kuonekana kuwa ni vidogo tu vyenye malengo ya kuchafuana kisiasa, vinakuwa na athari kubwa katika uhusiano wa kibiashara kuliko hata wale wasioelewa wanavyoweza kukadiria. Ndiyo maana nimeona ni afadhali sasa niwape nafasi wale wanaoendesha siasa hizi uchwara na zisizo na tija waendelee na siasa zao hizo ambazo kwa bahati mbaya kwao, mimi sina muda nazo na siwezi kuwa sehemu yake. Na mimi kwa upande wangu niendelee na maisha yangu.

Kutokana na ukweli huo na sababu zote hizo basi, kwa moyo wa dhati na kwa nia thabiti, hatua ya kwanza niliyoiona kuwa ninapaswa kuichukua ilikuwa ni hii ya kuitikia wito unaotokana na msukumo wa ndani ya nafsi yangu wa kuamua kukomesha kabisa malumbano na mivutano isiyo na manufaa kwangu binafsi, kwa viongozi wa chama changu na chama chenyewe.

Msukumo huo si mwingine bali ni ule wa kuamua kuachia nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwa baraka za chama changu nisingelikuwa nazo.

Napenda kuliweka hili sawa sawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote za uongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zangu.

Aidha, nimefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kuwajengea heshima na imani machoni mwa wanachama na wananchi wengine, viongozi wangu ambao naamini baada ya mimi kujitoa watapata fursa ya kutafakari upya changamoto nyingine mbadala zinazowakabili ambazo msingi wake ni dhamana kubwa walizo nazo za kukiongoza chama chetu na nchi yetu kupitia Serikali yake.

Wakati nachukua uamuzi huu, natambua vyema kwamba, watatokea watu ndani ya chama chetu na nje ambao watafanya kila juhudi kupotosha au kupindisha ukweli kuhusu hatima yangu ya kisiasa baada ya kujiweka kando na kujipa mimi mwenyewe na chama changu fursa ya kutafakari kwa kina majaaliwa yangu na ya nchi yangu katika siku zijazo.

Nafanya hivyo nikiwa na imani thabiti kwamba, uamuzi wangu huu, hususani ule wa kuachia nafasi yangu ya ubunge, yatakipa fursa nyingine CCM ya kuendelea kuliongoza jimbo letu la Igunga katika kipindi cha miaka minne ijayo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kwa upande mwingine, uamuzi wangu huu naona ni fursa kwa viongozi wa Chama changu cha CCM kutafakari na kuamua njia wanayoiona wao ni sahihi kuichukua kwa hatima na mustakabali wa chama chetu na ambayo wanaamini itakipa nguvu mpya ya kisiasa dhidi ya vyama vya upinzani.

Sambamba na hilo, ninayo imani thabiti kwamba, uamuzi wangu wa kubakia kuwa mwanachama wa kawaida na mtiifu wa CCM utakuwa chachu kwa chama changu na kwa Serikali yake kuwatumikia wananchi kwa Ari Zaidi, Kasi Zaidi na Nguvu Zaidi.

Mwisho kabisa, nikimalizia naomba nitumie fursa hii kutoa heshima za pekee kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa aliyoifanyia na anayoendelea kuifanyia nchi yetu. Amefanya mengi na makubwa kuiendeleza nchi yetu na watu wake kuliko inavyothaminiwa na kufahamika. Kazi yake kubwa inashindwa kuthaminiwa na kufahamika kutokana na siasa chafu tunazoziendesha Tanzania. Wasia wangu kwa wanasiasa wenzangu, waandishi wa habari na Watanzania wenzangu kwa ujumla ni kuwa tunahitaji kuisaidia nchi yetu kwa kufanya siasa zenye mwelekeo wa kujenga ambazo ndiyo hasa zinapaswa kuwa siasa kwa maana halisi ya neno hilo.

Wazee wangu, baada ya maelezo hayo, nawashukuru sana kwa kunisikiliza na kunielewa.

Ahsanteni sana.

Mwisho…
 
FF leo umeni impress kweli kweli; kwahiyo nawe unaamini kimoyo moyo japo kwa mdomo utapinga kuwa CCM kipo hai kwasababu tu kina dola nje ya hapo hakiwezi ishi....Asante sana kwa ukiri huu big up!

Si kwa kuwa kipo au hakipo ndani ya dola, hayo ni maneno yako. Mimi naamni hakuna ataebaki milele duniani. Ukitazama historia ya CCM haikuanzia kwenye CCM ni mlolongo wa vyama na watu waliovianzisha kuwepo kwao, itikadi zao, na kumbuka vyama si msahafu usiobadilika.

CCM ni chama kipya ukilinganisha na vyama vikongwe duniani na dhanna ya Mapinduzi itapokwisha sidhani au siamini kama bado kitaendeleo kuwpo kama Chama Cha Mapinduzi. Kumbuka dhanna ya mapinduzi si endelevu ni dhanna yenye muda na malengo fulani kisiasa, utapinduwa nini daima? labda ujipinduwe mwenyewe.

Inatakiwa usiwe shallow katika mambo ya siasa, soma kiutaratibu hotuba ya Rostam hapo juu, aliyeibandika kutukumbusha kafanya la maana sana. Ina mambo mazuri sana yameongelewa kwenye hiyo hotuba.
 
Regia tunaomba ujibu swali ulio ulizwa mara kibao na Faiza. Wewe binafsi umefanaya nini tangu upate ubunge?
 
Regia tunaomba ujibu swali ulio ulizwa mara kibao na Faiza. Wewe binafsi umefanaya nini tangu upate ubunge?

Hana jibu, sera za Chadema ni kueleza maovu ya CCM inachekesha sana kuona wabunge wetu akiwamo mh. Regia Mtema walivyo na mawazo finyu, suala la kuleta maendeleo ni jukumu la serikali, wabunge ni wawakilishi wa wananchi hamaanishi kama mbunge ana uwezo wa kifedha basi atumie fedha zake binafsi kuleta maendeleo ya jimbo lake; ubunge ni dhamana si mali binafsi, sioni mantiki yeyote ile kumlaumu Mh. Rostam inayopaswa kulaumiwa ni serikali na wananchi wenyewe wa Igunga; inakuwaje wanaendelea kuchagua wabunge kupitia chama kisichowaletea maendeleo? Inawezekana wananchi Igunga hawajui kipimo cha maendeleo ama hawajui maendeleo ni kitu gani; waheshimiwa wabunge mnachopaswa ni kuwaelemisha wananchi ili watoe changamoto kwa wabunge na serikali wapate maendeleo. Hizi siasa za kulalama bila sababu za msingi hazitatufikisha popote, kuna wakati inabidi tukubaliane mambo ya msingi kama Taifa, tumezidi kudimimia kimaendeleo kutokana na kuwa na bunge linalotumika kama rubber stamp, onyesheni vitendo !

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Kuna kipofu akaacha gongo lake? Once ukiwa mbaguzi always unakuwa mbaguzi, hata ufanye nini, hicho huwa ni kibri cha kujiona wewe bora kuliko wengine, ni maradhi makubwa sana hayo, yapo ndani ya moyo hayatibiki.

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mbunge aanza kuchimba visima 60 jimboni [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 07 October 2011 18:41 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0diggsdigg

Mwanja Ibadi-Kilwa
MBUNGE wa Kilwa Kaskazini Muktadha Mangungu, ameanza kuchimba visima 60 vitakavyogharimu zaidi ya Sh720 milioni, katika vijiji na shule za sekondari zenye tatizo la maji.Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha wapiga kura wake, kuondokana na kero ya muda mrefu ya kukosa huduma za maji.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa uchimbaji wa visima hivyo, uliofanyika katika Shule ya Sekondari Ilulu, Mangungu alisema kwa muda mrefu, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo wa kukosa huduma za maji safi na salama.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom