Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Rudini sasa Igunga kama kutoa shukrani kwa kura zile nyingi mjaribu kurekebisha baadhi ya mambo ambayo yako katika hali mbaya zaidi kwa kutumia sehemu ndogo ya RUZUKU yenu. Taabu yenu kila mnakopita hata kwa maandamano huwa hamurudi tena hadi uchaguzi au maandamano mengine. Jengeni tabia kama ya akina VodaCom Foundation, wafikieni wenye shida na mahitaji zaidi. Kuwafikia watu masikini ni kuwajengea darasa, kuwachimbia kisima, kujenga josho la mifugo yao, nk. Mwaka jana mliipoteza Tarime kwa kuwa hawakuwaona tena baada ya uchaguzi ule mdogo.

Dah!
Nashukuru mkuu umenisemea!
Hii kitu nimekuwa nikiisisitiza mara kadhaa maeneo kadha wa kadha. Tatizo lililopo sijui kama wahusika wanalisikia na kulifuatilia hilo.
Maana huwa tunatoa mapendekezo kibao, lakini wahusika mhhh! Always kimya....hata response hakuna..no or yes.
 
Tutaandika mengi sana lakini ukweli ni kuwa rostamu sio mtz (japo wasukuma wanasema ni mukuma) na kamwe hawezi kuwa na uzalendo na mtz yeyote na ndiyo maana kaenda hata kupiga kampeni chama chenye siasa uchwara kwani kwake yeye ni maslahi.....huyu kaja tz kufanya biashara kumwingiza kwenye mambo mengine km hayo ni kutowatendea haki watz.......................sio kwamba kakimbia siasa uchwara ila walitofautiana kimaslahi zaidi....bahati yake katukuta watz wote mabwege dunia nzima kwani hapo alipo anachezea tuzo ya dowans aichukue tu basi na kwa sababu ya dowans ndiyo maana alikubali kwenda kwenye kampeni igunga......dowans ni mgawo halali wa kikwete,rostam,lowasa,ngeleja na wengineo..........
Kweli watz mabwege kwani rotamu na kikwete na lowasa wanaiba watakavyo na hakuna wa kuwafanya kitu
 
Tumekuwa na Mwalimu kwa miaka zaidi ya 20 akiwa Rais wa Nchi hii. Mkoa anaotoka kuna barabara moja tu ya lami inayotoka Mwanza- Musoma- Sirari. Kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope kako pale Musoma. Butiama haina chochote cha uhakika. Hili la Mbunge au kiongozi yeyote wa kisiasa kuwaletea maendeleo watu wake nimeliona Kilimanjaro tu.
Hii ni kali ya mwaka,inaonyesha tu desparation.Mwalimu siyo tu kwamba hakufanya hayo.Pia hakujulimbikizia mali.Unafananisha kifo na usingizi.Wabunge wanapojipatia maendeleo wao binafasi kwa kutumia ufisadsi na wananchi kuendelea na umasikini wewe unaiitaje hiyo?Sera ya mwalimu iliyofuatwa na wabunge wengine wasio wa Kilimanjaro?Kweli umesihiwa.Ni bora ujisomee tu mawazo ya wengine.
 
Watu wanaoitwa waasi wanazaliwa miongoni mwa wazalendo, ila ni zao la mfumo kandamizi. Kwa siasa hizi tunazalisha taifa la waasi. Nchi kama Cote De Voire, Senegali, Congo zilikuwa na amani kupita Tanzania lakini leo hakufai. Ukandamizaji ukiendelea wanaokandamizwa hawataamini tena katika nguvu ya hoja bali hoja ya nguvu. Majeshi yatagawanyika na civil war itatamalaki. Tafakari chukua hatua.
 
Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hizi ni hoja za walioshindwa wangeshinda haya yote wasingeyasema. Ww ulitegemea kampeni za uchaguzi ziwe km unamtongoza mtu, hizi ndio siasa km huwezi achia ngazi rudi home ukasaidiane na mama kupiga deki na kufua na kupika

I wonder why do Moderators torelate your stupidity, you ought to banned indefinetely!
 
Nimeshuhudia wanawake wakinyanyaswa na polisi eti tu ni wafuasi wa CHADEMA,hakuna hata mmoja aliyekemea,DC aliyevunja sheria yeye kwa kuwa tu ni DC na ni kada wa ccm,akaonekana amedhalilishwa.Nimeshuhudia vijana wengi wakibambikiziwa kesi,kwa kuwa tu ni wafuasi wa CHADEMA,ninapoandika sasa kuna vijana watano walishika gari ya mwenyekiti wa ccm wilaya ya Igunga akigawa hela rushwa,wakaripoti polisi,na baada ya polisi kukagua gari hiyo wakakuta begi lina zaidi ya 21milion,vijana wale wazalendo wakawekwa chini ya ulinzi,eti ni wanyanganyi wanotumia silaha,na bila utu wala heshima kwa binadamu wenzao,polisi wakawapelea Nzega siku ya Ijumaa,hadi Jumatatu walipopelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha,Vijana wale walisekwa ndani kwa siku tatu bila chakula wala maji,,u wapi utu wa na usawa wa binadamu?tunaelekea wapi kama taifa?na misingi gani ya taifa tunajenga?
Uchaguzi wa Igunga umekuwa na mengi ya kujifunza,kwa serikali ya ccm,wametumia rasilimali zetu,kwa ajili ya Igunga tu,ni aibu kwa ccm na viongozi wake,lakini kubwa na ambalo sharti wajifunze ni kuwa ,inapofika mahali Chama dola,chenye serikali,rasilimali pesa,rasilimali watu,uongozi kuanzia balozi wa nyumba kumi,kulalamikia CHAMA CHA UPINZANI,eti kinagawa hela,eti kimeingiza makomandoo,na Mungiki,ni wazi kuwa CCM kimepoteza mwelekeo na sasa kinaelekea kwenye anguko kuu.
Ni faraja iliyoje kuona kuwa sasa ukombozi wa pili wa taifa letu u karibu kuliko mategemeo ya wengi,kuna wengine wataona ni maneno ya kujifariji baada ya kushindwa Igunga.Lakini huu ndio ukweli na ccm ni mashahidi katika hili,wanajua nguvu kubwa kiasi gani walitumia kulikomboa Igunga,na bila msaada wa vyombo vya dola wasingeweza.
Uchaguzi umeisha,kuna majeruhi wengi,na ambao kesho ndio wapamabanaji wa ukweli,Jambo moja la msingi ni kwamba hakuna wingi wa silaha,risasi,mabomu,wala vifaa vya kisasa vya kijeshi vinavyoweza kuzuia umma unaotaka mabadiliko,umma uliochoka,umma unaolilia ukombozi,na kwa kadri serikali inavyozidi kuminya uhuru na demokrasia ndivyo umma unavyozidi kuamka na kupigania uhuru wao.Daima tutasonga mbele[/QUOTE]

Mkuu hapo penye red pamenifurahisha sana. Unajua inabidi tushangilie na kufarahi kwani wokovu wa watanzania umekaribia. Maonevu kama hayo hayaendi bure, na Mungu wetu anasikia kilio chetu na muda si mrefu ukombozi utakuja na si lazima ifike 2015. Ndivyo ilivyokuwa AFRIKA YA kUSINI, wazalendo walikamatwa, wakafungwa wakapigwa na wengine waliuawa, lakini hiyo katu haikuwa roho ya mapinduzi. Na kadri walivyowtenda vibaya wazalendo ndio harakati za ukombozi zilivyozidi.

Makamanda mliokuwa Igunga mtuwakilisha vizuri, sasa mwendo mdundo, hakuna muda wa kupoteza, yale maandamano yetu yaendelee na Dar yasichelewe sana, tunataka kuuonyesha ulimwengu Tanzania ilivyo.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Ukiona umeanznisha sredi halafu watu wanakasirika mpaka wanatoa mapovu na jasho inapendeza sana.Kuna vitu nimejifunza humu kuwa watu wapo tayari kwa lolote kwaajili ya kumtetea Rostam hata kama anakosea!it is amazing!
 
"When a true genius appears in this world, you may know him by this sign, that the dunces are all in confederacy against him." --Jonathan Swift

Now I know Rostam Aziz is a genius.

FaizaFoxy,

Mbona unaonekana ni mtu mwenye kutetea sana Magambas hasa huyo Rostam Aziz? Amekupa nini huyu mwanamme mpaka una msifia mpaka kupitiliza kiasi hicho???

Of all the people in Tanzania can you single out RA as a genius? Really you must be joking! Labda kama una maanisha kwa tafsiri yako KWAMBA GENIUS NI YULE FISADI MKUBWA ANAYEJIPATIA FEDHA HARAMU KUPITIA KWENYE MIKONO YA VIGOGO WA CHAMA NA SERIKALI YA CCM NA KUZISAFISHA(MONEY LAUNDRY)KWA KUWEKEZA KWENYE MIRADI NA KAZI ZA CCM IKIWEMO KUKODI HELIKOPTA ZA KAMPENI NA KUFADHILI MIKUTANO MBALIMBALI YA CCM KAMA CC NA NEC KULE CHIMWAGA NA DSM!!!

Kama RA ni genius kweli unaweza kutuambia kwanini Chama chenu cha Magamba-CCM kimemwita ni FISADI na GAMBA pamoja na hao wenzake a.k.a.mapacha 3 kina Lowassa na Chenge?
 
Pole saana mkuu!
Unajua hawa CCM kitendo cha kutumia hela yote hiyo (3blns) kwa uchaguzi mdogo kama huo halafu hawana ata aibu ni kwa vile wamezoea kutuhujumu sisi walala hoi........najua hiyo ni sehemu kubwa tu ya kodi yetu!
Anyway wengi wetu tulilala,na sasa thanks CDM kwa kutuamusha. In future mimi binafsi sitathubutu tena kukosea maana nitatekeleza ule usemi wa "Tenda kosa si kosa,Kurudia kosa ndo kosa!"
 
Hii ni kali ya mwaka,inaonyesha tu desparation.Mwalimu siyo tu kwamba hakufanya hayo.Pia hakujulimbikizia mali.Unafananisha kifo na usingizi.Wabunge wanapojipatia maendeleo wao binafasi kwa kutumia ufisadsi na wananchi kuendelea na umasikini wewe unaiitaje hiyo?Sera ya mwalimu iliyofuatwa na wabunge wengine wasio wa Kilimanjaro?Kweli umesihiwa.Ni bora ujisomee tu mawazo ya wengine.
Kwani Rostam ni Ubunge ndio uliompa mali zile? Alianza kutuibia kitambo tu. Ikitajwa Kilimanjaro tu unakunja uso ndugu yangu. Wabunge wenu ndivyo wanavyofanya hasa wakiukwaa uwaziri wa wizara husika. Tumeyaona haya na tumeyasikia pia. Tujifunze tu kuvumiliana na kuumeza ukweli ambao mara nyingi ni mchungu sana.
 
Dada yote unayosema hapa ni kweli kabisa lakini mbona hamkuyasema wakati mkiwa Igunga?

Ndugu yangu walisema sana na ndiyo maana watu waliwaunga mkono hadi wakawapa kura nyingi lakini wakashindwa kuzilinda zisichakachuliwe,

Maana challenge kubwa ya CDM si kuomba kura bali kulinda kura wanazopigiwa maana CCM ni wezi wakubwa sana kuanzia Usalama, NEC, Serikali, Msajili wa vyama, Polisi na Jeshi.
 
Kwani Rostam ni Ubunge ndio uliompa mali zile? Alianza kutuibia kitambo tu. Ikitajwa Kilimanjaro tu unakunja uso ndugu yangu. Wabunge wenu ndivyo wanavyofanya hasa wakiukwaa uwaziri wa wizara husika. Tumeyaona haya na tumeyasikia pia. Tujifunze tu kuvumiliana na kuumeza ukweli ambao mara nyingi ni mchungu sana.
Wewe unajuaje kuwa huo ufisadi alioufanya ume double mali zake?Unamfanyia kazi ya accounting?Utajiri wa wizi/kifisadi una levels zake na yeye alikuwa at the top.Eti imetajwa Kilimanjaro nakunja uso?Mkuu mnalipwaa na jamaa ama ni kitu gani?Sasa umeingiza na uwaziri.Baki kwenye topic acha kutapa tapa.Ukweli mchungu wa kuumeza ni nyinyi na RA wenu.Roho mbaya sana hiyo ndugu yangu.Tunajuwa kabisa he could have done something for the people.This is unjustifiable hata uje na maneno gani,fact remains as facts.Kama hao wabunge wanawasadia wananchi in leu of their personal interests,basi thats the stuff he should've done for the poeple.Utumwa wa akili peke yake ndiyo unaweza kukupeleka kwenye misimamo kama hii ya kumetetea fisadi dhidi ya wananchi masikini aliowatumilia kwa miaka zaidi ya 15.Shame shame!
 
Wewe unajuaje kuwa huo ufisadi alioufanya ume double mali zake?Unamfanyia kazi ya accounting?Utajiri wa wizi/kifisadi una levels zake na yeye alikuwa at the top.Eti imetajwa Kilimanjaro nakunja uso?Mkuu mnalipwaa jamaa nini?Sasa umeingiza na uwaziri.Baki kwenye topic acha kutapa tapa.Ukweli mchungu wa kuumeza ni nyinyi na RA wenu.Roho mbaya sana hiyo ndugu yangu.Tunajuwa kabisa he could have done something for the people.This is unjustifiable hata uje na maneno gani,fact remains as facts.Kama hao wabunge wanawasadia wananchi in leu of their personal interests,basi thats the stuff he should've done for the poeple.Utumwa wa akili peke yake ndiyo unaweza kukupeleka kwenye misiamo kama hii ya kumetetea fisadi dhidi ya wananchi masikini aliowatumilia kwa miaka zaidi ya 15.Shame shame!
Simtetei Rostam. Ninachopinga ni kile kwamba nafasi yoyote ya kisiasa inaweza kumpa mtu uwezo wa kuleta maendeleo jimboni kwake. Hilo likifanyika mara nyingi ni matumizi mabaya ya madaraka kama walivyofanya akina Solomon Eliufoo kwenye elimu, CD Msuya na Mwanga yake, Basil Mramba na Rombo yake, Amir Jamal na viwanda vyake vya Morogoro,.....
 
Mkuu Nanyaro poleni na mambo yote yaliyowapata Igunga
kuna kitu kinanisumbua kidogo,je chadema imeshasoma ramani zote za ccm na matukio yote,,,je nini kifanywe??hivi Mkuu unafikiri bila kupiga hatua moja mbele kutokana na matukio tuliyojifunza huko nyuma tutafika mbali??nilileta post moja hapa last week inasema chadema andikeni report ifanyiwe kazi,,kama uliweza kuisoma naomba peleka kwenye vikao vya chama,
mkuu mimi binafsi ningependa kujua ni hatua gani inafata kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mwingine!
 
Simtetei Rostam. Ninachopinga ni kile kwamba nafasi yoyote ya kisiasa inaweza kumpa mtu uwezo wa kuleta maendeleo jimboni kwake. Hilo likifanyika mara nyingi ni matumizi mabaya ya madaraka kama walivyofanya akina Solomon Eliufoo kwenye elimu, CD Msuya na Mwanga yake, Basil Mramba na Rombo yake, Amir Jamal na viwanda vyake vya Morogoro,.....
Ok,kwa hiyo hao uliowataja utofauti wao na kina RA ni kwamba wao hawakuziweka zote mfukoni siyo?Maana sikuelewi,pengine wewe hunielewi.Hii nafasi ya ubovu wa katiba tulionao kina RA wameitumia kwa namna ya tofauti na hao uliowataja?Hivyo "vijisenti" wanavyovipata kutokana na hiyo loophole sasa wakaweke kwenye akaunti huko uswisi?Matumizi mabaya ya madaraka ni kuwasaidia wananchi na mazuri ni kujilimbikizia kwa ufisadi?Duh!Kweli kuna kazi,especially kwa wale wanaoonekana wanalipwa.Huwezi kutetea hii kwa namna unayofanya kwasababu ni nje ya topic.Na mazingira hayo yanapelekea wengi wenu kwenda personal,which again is taking it out context.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom