Naomba kuchangia Uzi huu.
Kwanza mnaoidharau Rwanda kijeshi futeni hiyo mentality, ni nchi ambayo kiongozi wake amejidhatiti kuunda JESHI imara, utii na lenye ufanisi mkumbwa sana.
RDF ni moja ya majeshi ya kisasa kabisa Afrika hii.
Silaha kubwa ya JESHI LA RDF ni intelijensia Bora sana. Mnaweza msiamini hata ndani ya vyombo muhimu vya kiulinzi na kimaamuzi Kuna maajenti wa Rwanda. Serikali ya nchi yenu imefumbia macho ambapo wanyarwanda wameshika madaraka na nyazifa muhimu kwenye serikali ya JMT.
Je, Tanzania mtaweza kipi dhidi Yao? Mmeruhusu rushwa mpaka namna ya ku recruit vijana kuwaingiza kwenye JESHI letu, je, serikali ya Rwanda itasita kutoa mafungu Kwa akili ya maafisa walafi Ili wawaingize vijana wao jeshini?
Mkuu wa majeshi Afande J.J Mkunda alisisitiza kihusu raia wa kigeni kupata teuzi serikalini but who cares?
Tanzania inakuwa nchi kubwa yenye ushabiki wa kijinga katika mpira na siasa chafu zisizo na manufaa kwetu.
Kagame anajua by numbers haiwezi Tanzania lakini yeye kaja na njia ya kujua mmeamkaje, mmekula Nini, mmefanya Nini na mnatarajia kufanya Nini.
Rwanda wako smart kuliko mnavyodhani, JESHI letu tumelifanya butu Kwa sababu ya siasa za kishabiki, haliko huru Tena kiasi kwamba mwenyekiti wa Chama mkoa ana nafasi ya kumpa maagizo kamanda wa kijeshi.
SILAHA
RDF inaendelea kujiimarisha Kwa silaha za kisasa zaidi toka Kwa washirika wake wakubwa Russia na China.
RDF Ina mifumo Bora zaidi ya Air Defense Systems kuliko nchi zote za ukanda wa EAC ukiacha Ethiopia.
RDF ina viwanda vya ndani Kwa ajili ya light weapons na APCs ( magari ya delaya).
RDF ina attack and utility helicopters ambazo Zina uwezo wa kushambulia toka mbali Kwa mvua ya mashambulizi ya risasi na makombora ya masafa madogo.
Nimetaja silaha zao muhimu tu ( na zinazojulikana wazi) ambazo Kwa asilimia kubwa wapinzani wa Rwanda hawana.
Vita na Rwanda siyo sawa na Malawi Bali ni kazi pevu inayoitaka Tanzania kukaa chini na kuvipa uhuru, uwezo vyombo vya ulinzi.
Hitimisho:
Taifa letu🇹🇿 tunalipenda sana, lakini tusijiaminishe Kwa uwezo wetu wenyewe. Tujiimarishe zaidi.