FMES,
Tangu nisome makala yako jana imenipa kutafakari mambo mengi sana. Nafikiri tusikate tamaa kiasi hicho. Tegemeo letu limebaki moja yaani KARATA ya Mwisho. Hii nafikiri anayo Kikwete. Sasa inategemea Kikwete ataicheza wakati gani. Hii imenikumbusha ile story ya THE GODFATHER. Mzee Don Carleon alikuwa kaishiwakabisa nguvu. Hata jamaa zake wengine walikuwa wamenunuliwa na wapinzani wake. Siku ya MAZISHI ya SANTINO mwanae au SONNY ndipo alipofanya maajabu (Samahani kama ntakuwa nimechanganya). Wakati mazishi yakifanyika, watu wake walikuwa BUSSY waki-eliminate adui zake wote. Mazishi yanaenda, baba yuko KAZINI kwa sana!! Sasa inategemea Kikwete ana akili kiasi gani. Kama HANA AKILI basi kweli TUMEKWISHA. Kama kama wanamu-underestimate basi inabidi tuseme SOON UFISADI UTAISHA maana wameshajiweka wao wote kwenye KAPU MOJA. Nasema hivi kwa sababu moja kubwa sana. Mlisema kuwa yule BOSS Othman nani sijui ni Mpelelezi na ni RAFIKI WA KIKWETE. Hosea kapanda na hivyo aliyekuja ni mtu wa Kikwete na atakuwa kazini kukusanya DATAs. Riport zote za uchunguzi wa UFISADI ziko kwake. Wauza unga ziko kwake nk nk. Anaweza subiri LAST MINUTE akacheza ule mchezo walimfanyia Boss wa Fat yaani RAGE kule Tabora. Walimuweka ndani na sasa imeonekana HANA HATIA ila ubunge hana wala KITI hana. Nafikiri Muungwana kwa kutumia hizo riport zote anaweza KIHAKI na KISHERIA kuwakamata na kuwafungulia mashitaka Mamvi, ANBEN, Dialo. Mramba, Msabaha, R Azziz, Chenge, Mwanyika, Mamvi Son, nk nk.
KIKWETE KAZI KWAKO. UKIFANYA MCHEZO JAMAA WATAKUMALIZA. Siye tuko na wewe maana BETTER THE DEVIL YOU KNOW, ingawa huyu shetani FISADI, mhhh hadi unasema labda nijaribu mwingine...
JK asiwaangushe wananchi. Kwa kuwa HANA sababu ya kuwaogopa mafisadi, nina uhahkika akiwafikisha kwenye sheria hao hapo juu he will be a trailblazer for other African leaders and he will almost certainly win the AFRICAN LEADERS ACHIEVEMENT PRIZE by Mo Ibrahim. Prize Money worth more than Tsh 5,000, 000, 000 and 200,000,000 every year for life.