Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,536
- 4,532
ONA NA MANENO YA CHILIGATI, ANASEMA JAMBO HILO HALIKUFANYIKA KWA SIRI KWANI KUNAWABUNGE WAWILI WALIONA
...Hawa waliona kila kitu
2008-06-16 18:12:54
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Wakati sakata la ushirikiana lililotinga bungeni likiendelea kuvuma, kuna habari kuwa wabunge wawili wanadaiwa kushuhudia `live` tukio hilo ambalo limekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati, ni kwamba walioshuhudia tukio hilo ni Mbunge wa Longido (CCM), Mhe. Lekule Laizer na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Anna Abdallah.
Kapten Chiligati amenukuliwa na vyombo vya habari leo asubuhi kuwa waheshimiwa Anna Abdallah na Lekule Leizer, walikuwepo na hawakuona kitu kinachohusishwa na imani ya ushirikina kikifanyika ndani ya Bunge.
Amekaririwa akitoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na waandishi kuhusiana na yale yaliyojiri kwenye kikao cha Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuulizwa swali linalohusiana na sakata hilo.
Akasema wabunge hao, walisema mbunge mmoja alikuwa ameongozana na ofisa wa Bunge kwa ajili ya kuonyeshwa kiti cha kukaa.
Akaeleza zaidi Kapteni Chiligati kuwa mbunge huyo aliyeonekana akizunguka kwenye viti amefanya hivyo kwa sababu awali alikuwa akikaa kiti cha mbele.
Hata hivyo, Kapteni Chiligati amekaririwa akisema kuwa tukio hilo hivi sasa linachunguzwa zaidi na vyombo vya dola.
``Tukio la mtu kunyunyuzia vitu ndani ya Bunge linachuzungumzwa...bado linachunguzwa, Spika (Samuel Sitta) alitoa taarifa. Hivyo tunasubiri matokeo ya uchunguzi ,`` akasema Chiligati.
* SOURCE: Alasiri