Kupunguza viwango vya ufaulu wa masomo huzalisha ujinga katika Taifa

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,118
1,915
Madhara ya kupunguza viwango vya ufaulu wa masomo huzalisha ujinga mkubwa katika Taifa. Elimu ni jambo la kupewa kipaumbele katika Taifa kwasababu inaondoa ujinga na kuleta maarifa.

Yapo mataifa mengi yanayotilia mkazo swala la Elimu hata yameamua kupandisha viwango vya ufaulu badala ya kushusha.
Mfano Mzuri daraja la A linatakiwa lianze na alama 91-100
B 81-90
C 71-89

Wanafunzi wenye alama hizi ndio wanaostahili kupewa nafasi ya kuendelea na ngazi za juu huku waliobakia wakipaswa kujikita katika masomo yanayohusiana na fani tofauti.

Nini faida ya wasomi hawa kuchujwa kwa viwango vya juu? Faida yake ni kuwa Taifa litaongozwa na viongozi wasomi wa hali ya juu wenye uwezo wa kudhibiti ujinga ama maswala yote yanayoleta madhara yatokanayo na ukosefu wa elimu ama utashi.

Ndugu zangu, kuruhusu wanafunzi wenye viwango vya chini vya ufaulu kupata nafasi ya kufikia viwango vya juu vya elimu pasipo kujali alama za ufaulu ni sawa na kuruhusu Taifa kuwa na viongozi wenye viwango vya chini vya utashi na tatizo hili litazalisha madhara makubwa yanayosababishwa na ujinga.

Wizara ya Elimu mnashauriwa kutilia mkazo swala la Elimu kamwe msilegeze viwango vya ufaulu kwasababu vizazi vijavyo vitakuja kuongozwa na wajinga badala ya werevu.
 
Hivi unadhani ufasaha wa kazi ya Nursing kati ya A ya 100 na ya 75 za Physics vinautofauti? Shule za makatatasi zinachanganya sana.
 
Hivi unadhani ufasaha wa kazi ya Nursing kati ya A ya 100 na ya 75 za Physics vinautofauti? Shule za makatatasi zinachanganya sana.
Wakichukuliwa kwa viwango vya juu vya ufaulu watakuwa wafanyakazi bora katika Taifa hili
 
Back
Top Bottom