Elimu ya kwenye makaratasi

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Hellow JF,

Kwa miaka ya hivi karibuni waajiri wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu utendaji kazi duni wa waajiriwa ukilinganisha na ufaulu wao unao onekana kwenye vyeti vyao vya kitaaluma.

Sitaki kupinga au kuelezea sana jambo hili kwakua sina taarifa za kutosha na hata tafiti sijafanya. Lakini naweza kusema machache kutokana na uzoefu wangu kipindi nipo chuo:-
  1. Wanafunzi wengi wa vyuo vya kati pamoja vyuo vikuu hawatumii muda wao vizuri katika masomo yao, wengi wanawekeza muda wao katika kufanya mambo ya kijinga yasiyo na manufaa ya muda mrefu katika masomo na hata maisha yao. Mfano, wengi wanawekeza muda katika kuaminisha watu wengine kwamba wao ni bora, wazuri, wajanja, sio maskini na wala hawajapitwa na nyakati.
  2. Wanafunzi wengi wanapenda shortcut, hawapendi kujishughulisha, pia ni wavivu sana. Hali hii inawafanya washindwe kutumia bongo zao na ndio maana wanakariri sana,wanakosa ubunifu, hawajiongezi na ndio maaana Wanapata GPA makubwa lakini hawawezi ku-apply katika utendaji.
  3. Mfumo unaotumika kupima uwezo na uelewa wa mwanafunzi bado upo chini sana, hali hii inasababisha wazalishwe wanafunzi wengi wenye GPA kubwa ambazo hazina uhalisia na uwezo wao.
Ushauri wangu.
  1. Wanafunzi wajitambue
  2. Vigezo vya kujiunga na vyuo vya kati/Vyuo vikuu viongezwe. Hii itasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi wasio na uwezo kujiunga vyuo vikuu.
  3. Taasi z elimu ya juu zibadili mifumo yao ya kupima wanafunzi. Iwe knowledge and practices based education isiwe GPA based education.
Karibuni kwa maoni tujifunze zaidi.
 
Kwa jumla elimu yetu ni content-based badala ya kuwa skill-based. Ndio maana hivi sasa serikali inajaribu kubadili mitaala na kuja na kitu wanachoita Competence-based curriculum (Mtaala unaolenga umahiri) - sijui kama tuna mipango ya kutosha kufanikiwa.

Kwa hiyo, haishangazi kama mtu anakuwa amepasua vizuri maksi za mtihani lakini, kiutendaji (skills), akawa anapwaya.

Ndiyo maana ni MUHIMU SANA kujiendeleza NJE YA DARASA kwa maarifa halisi ya maisha sawasawa na kile unachopenda kufanya maishani.
 
Mtu aliyefundishwa masomo sekondari akafaulu akifundishwa kazi KWA mwaka mmoja atajua. Kazi atakayoifanya KWA miaka 20+

Tatizo waajiri wanasahau kuwa wao pia walichukua muda mrefu na seminar nyingi kumasta hizo kazi.

Mtu A,B,C,D ya Physics A level halafu afundishwe kazi KWA mwaka mmoja ashindwe?
 
Naomba ufafanue zaidi..
 
Kwa jumla elimu yetu ni content-based badala ya kuwa skill-based. Ndio maana hivi sasa serikali inajaribu kubadili mitaala na kuja na kitu wanachoita Competence-based curriculum (Mtaala unaolenga umahiri) - sijui kama tuna mipango ya kutosha kufanikiwa.

Kwa hiyo, haishangazi kama mtu anakuwa amepasua vizuri maksi za mtihani lakini, kiutendaji (skills), akawa anapwaya.

Ndiyo maana ni MUHIMU SANA kujiendeleza NJE YA DARASA kwa maarifa halisi ya maisha sawasawa na kile unachopenda kufanya maishani.
Nimekuelewa vzr Mkuu
 
Mpaka apende kazi ndio atafanya vizuri , wengi wanachoka sio kwamba hawan uwezo ndio maana unaona wanaanza kuchelewa ,mara excuses kibao hawafiki ofisini .

Hali hiyo ni kawaida sana kweny mazingira ya kazi ,ila kuna haya mambo mtu akianza harakati za kusoma ili kujiendeleza basi utendaji nao unapungua
 
KABISAA NAUNGA MKONO HOJA
 
Unataka kusema waajiri wanalalamika kitu ambach sio?
 
Ukisoma muongozo wa serikali haswa sheria za utumishi utakuja kugundua kuna uvunjifu mkubwa wa maadili ya kazi.

Mambo hayo kama kuchelewa, kufanya kazi kwa mazoea bila ya ubunifu ,ulevi wa kupindukia , mapenzi kazini haya na mengine mengi yanachangia kuharibu utendaji wa kazi.
 
HII ELIMU YA NADHARIA NA KUKARIRI TULIYORITHI KWA WAKOLONI IFIKIE MUDA TUIACHE
Mbona hata watanzania waliosoma huko nchi xa nje kama Ulaya na Marekani wakirudi nchini na elimu zao mnzosifia kuwa huko ziko vizuri mbona wakifika Tanzania hatuoni hayo ma competence based kwenye performance zao makazini na maofisini au kwenye biashara? Kulikoni wakati wao wamesoma nje huko.kwenye elimu bora?
 
Ukisoma muongozo wa serikali haswa sheria za utumishi utakuja kugundua kuna uvunjifu mkubwa wa maadili ya kazi.

Mambo hayo kama kuchelewa, kufanya kazi kwa mazoea bila ya ubunifu ,ulevi wa kupindukia , mapenzi kazini haya na mengine mengi yanachangia kuharibu utendaji wa kazi.
Tabia za wanafunzi nq mfumo unaotumika kuwaaanda, these factor remain constant
 
Mbona hata watanzania waliosoma huko nchi xa nje kama Ulaya na Marekani wakirudi nchini na elimu zao mnzosifia kuwa huko ziko vizuri mbona wakifika Tanzania hatuoni hayo ma competence based kwenye performance zao makazini na maofisini au kwenye biashara? Kulikoni wakati wao wamesoma nje huko.kwenye elimu bora?
MIFUMO HAIFANANI NAWEZA KUSEMA

Hakuna mazingira wezeshi na vikwazo mbalimbali vya kijamii, kiteknolojia,kisiasa na kiuchumi
 
Nimependa jibu lako lakn nataman ufafanue zaidi hapo kwemye hizo sababu tatu ulizotaja
kijamii - Fikra na mitazamo juu ya ajira kwa mtu aliyetoka ulaya kuja kufanya kazi huku anapata tabu kuzoea mazingira ya hapa kutokana na ile exposure ya nje, wenzetu mifumo yao ya kijamii ipo vizuri hasa uwekezaji kwenye maarifa na vitendo

kiteknolojia - Hilo halina ubishi vitendea kazi vya ulaya na huku tumeachwa mbali, mifumo ya ufanyaji kazi kule inarahisishwa na mashine nzuri ambazo zingine huku hatuna

kisiasa - utashi wa kisiasa juu ya sera za elimu na ajira katika nchi zetu unazijua, urasimu uliopo tofauti na ulaya ambapo ukiwa na skills nzuri hawana mbambamba

kiuchumi - nchi za ulaya nyingi, zimeendelea wakati huo nchi zetu ndio zinazoendelea kiuchumi.. Ulaya wanaweza kuwa na fursa chache za kiuchumi lakini wakazitumia vizuri tofauti na kwetu ambako fursa ni nyingi ila tunazitumiaje? Rasilimali zetu tunazitumiaje na unaona wasomi wetu ndio hao.. Angalia tu tenda ndogo au miradi mikubwa kati ya wazawa na wa ulaya nani anazingatiwa zaidi...

sijui kama unanipata? Hata ukienda kuomba kazi unaambiwa tunataka uzoefu, na wewe ni fresh from school... unajiuliza unapataje? Elimu yetu ndio kama hivyo kukariri kwingi halafu vitendo vichache
 
Nimekupata vzr Mkuu. Shukran
 
Back
Top Bottom