beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Vituo vya Mafuta vinajengwa kila sehemu hadi kwenye makazi ya watu. Kwanini Serikali inatoa vibali kwa sehemu hatarishi?
Kuna vituo vingi sana vya mafuta vinajengwa katika maeneo hatarishi kwa jamii na Serikali sijui inaridhia ujenzi huu kwa namna gani? Sijui kwanini haifikirii?
Nakumbuka Septemba 2022, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula aliagiza kusimamishwa kwa ujenzi wa majengo yanayojengwa kinyume cha sheria na kuondolewa vituo vya mafuta vilivyojengwa kinyume cha sheria ikiwa ni pamoja na kutozingatia umbali. Alitaka wabadilishe umbali wa kutoka mita 200 hadi mita 500 wa kituo kimoja kwenda kingine.
Aidha, Novemba 10, 2022, Waziri Mabula alisema Serikali imesitisha ujenzi wa vituo vya mafuta ili kutoa nafasi ya kufanya tathimini ya ujenzi wa vituo hivyo kufuatia ongezeko la ujenzi holela wa vituo hivyo
Lakini pia, mnamo Aprili 2023, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango aliagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kufanya ukaguzi wa kina juu ya vituo vya mafuta vinavyojengwa kwa wingi kwenye makazi ya watu mkoani Dar es Salaam ili kunusuru kusitokee majanga ya moto.
Pamoja na matamko yote hayo, Serikali imedhiirisha kuwa ya matamko kwani hakuna kilichoendelea wala kufanyika
Mfano Kituo cha mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe pale Tanganyika Packers ni hatarishi kweli kweli iwapo kutatokea mlipuko au madhara ni makubwa sana
Bado kuna Kituo kingine kimejengwa Mikochenk karibu na makazi ya Watu ambacho kimelamikiwa hadi na Mwanasiasa nguli, Prof. Anna Tibaijuka ila bado Serikali hii ipo kimya.
Huenda inangoja yatokee yale ya ajali ya moto wa mafuta na idadi ya vifo vile kama kule Morogoro ndio wanashughulikia na kuweka sana pale ambapo Watanzania watakuwa na huzuni kubwa ya kupoteza Ndugu, Jamaa na Marafiki.
Ramani kuonesha Kituo cha Mafuta cha Lake Oil kilichopo Kawe
Je, Serikali inasubiri hadi majanga yatokee na tupate maafa kama ya Morogoro kwenye ajali ya mafuta ili kuchukua hatua?
Natambua Waziri wa Ardhi wa sasa, Jerry Silaa amechukua hatua ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa maendeleo ya makazi, Deogratius Kaliminze ila hiyo haitoshi kabisa, mara nyingi sana hii hutokea na hakuna cha maana kinafanyika. Inadaiwa huyu mtu vituo kadhaa ni vyake kupitia syndicate aliyoitengeneza.
Soma: Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi
Pia soma: Waziri Silaa apiga marufuku ujenzj holela wa Vituo vya Mafuta na kusimamisha matumizi ya Kituo cha mafuta cha Barrel cha Mikocheni