Suala la petrol stations aliloagiza Waziri wa Ardhi limeishia wapi?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,283
2,043
Wadau kama mtakumbuka, Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa alipoteuliwa moja ya mambo aliyoahidi kuyavalia njuga ni:

1. Ubadilishaji wa matumizi wa viwanja usiofuata taratibu wa kujenga vituo vya mafuta.
2. Ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya makazi.
3. Vituo vya mafuta kuwa jirani kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine.

Waziri aliagiza mara moja kusimama kwa ujenzi wa vituo vya mafuta nchi nzima. Pia, aliwaagiza makamishna wasaidizi wa ardhi nchi nzima kumpelekea orodha ya vituo vyote vya mafuta nchi nzima vikionyesha mambo 3 niliyoyataja hapo juu, na taarifa hiyo iwe imemfikia mezani kwake kabla ya tarehe 30/1/2024.

Binafsi, nilimpongeza sana Waziri na nikaamini wizara imempata mhusika. Kinachonishangaza ni kuenendelea kwa ujenzi baadhi ya maeneo wa vituo vya mafuta licha ya agizo lake kama Kigamboni na maeneo mengine ya nchi.

Swali kwa Waziri: Je, umeruhusu ujenzi wa vituo vya mafuta uendelee kabla ya ripoti yako kutoka juu ya vituo vya mafuta?
 
Back
Top Bottom