Pongezi Waziri Silaa kumsimamisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi vituo vya Mafuta vinajengwa katikati ya Makazi

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Hakika nichukue nafasi hii kumpongeza kwa dhati Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa kwa Maamuzi Magumu anayoyachukua katika Wizara yake.

Wizara ya Ardhi ni moja ya Wizara zenye WATENDAJI WA OVYO SANA wanaowachosha Wananchi kwa makusudi kabisa kutokana na kutofanya kazi zao kwa UADILIFU na kuzingatia SHERIA na TARATIBU.

Watendaji wa Ardhi wamekuwa ni MIUNGU watu wawapo maofisini. Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Makazi nakupongeza sana kwani Idara ya Mipango Miji imekuwa inatuharibia sana Miji yetu. Badala ya kuipanga Miji wao wanaiharibu.

Kwa mfano hapa Sumbawanga Manispaa kuna Ujenzi wa KITUO cha MAFUTA katikati ya Makazi ya Wananchi na Ofisi ya CCM mkoa na Benki. Pia Kituo hiki kipo jirani kabisa na Vituo vya Mafuta vya siku nyingi umbali wa Mita 50.

Kituo hiki kipya kilikuwa ni Kiwanja cha Makazi lakini Mkurugenzi wa Makazi amekibadilisha Matumizi Mwaka 2021/22 kuwa Kituo cha Mafuta na Manispaa Wamemetoa Kibali cha Ujenzi.

Waziri hebu unda timu yako ya kuhakiki Uhalali wa Vituo vya Mafuta au agiza Makamishina wako wa Mikoa wakuletee Orodha ya VITUO vyote vya Mafuta ujiridhishe na Uhalali wake kwani Ukaribu wa Kituo hadi Kituo ni JANGA lingine kwa Wananchi SIKU AJALI ya MOTO ITAKAPOTOKEA.
 
Hakika nichukue nafasi hii kumpongeza kwa Dhati Waziri wa Ardhi Mh.SLAA kwa Maamuzi Magumu anayoyachukua ktk Wizara yake.Wizara ya Ardhi ni moja ya Wizara zenye WATENDAJI WA HOVYO SANA wanaowachosha wananchi kwa Makusudi kabisa kutokana na kutofanya Kazi zao kwa UADILIFU na kuzingatia SHERIA na TARATIBU.WATENDAJI wa ARDHI wamekuwa ni MIUNGU watu wawapo MAOFISINI .Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa MAKAZI nakupongeza sana kwani Idara ya Mipango Miji imekuwa inaTUHARIBIA SANA MIJI YETU.Badala ya kuipanga Miji wao WANAIHARIBU.
Kwa mfano Hapa SUMBAWANGA MANSPAA kuna Ujenzi wa KITUO cha MAFUTA katikati ya MAKAZI ya Wananchi na OFISI ya CCM MKOA na BENKI.Pia KITUO hiki kipo jirani kabisa na VITUO 2 vya MAFUTA vya siku nyingi umbali wa Mita 50.Kituo hiki kipya kilikuwa ni Kiwanja cha MAKAZI lakini Mkurugenzi wa Makazi amekibadilisha MATUMIZI Mwaka 2021/22 kuwa KITUO cha MAFUTA na Manispaa Wamemetoa KIBALI cha UJENZI.
Mh.WAZIRI hebu UNDA TIMU yako ya Kuhakiki UHALALI wa VITUO vya MAFUTA Au Agiza MAKAMISHNA wako wa Mikoa wakuletee Orodha ya VITUO vyote vya Mafuta ujiridhishe na Uhalali wake kwani Ukaribu wa Kituo hadi Kituo ni JANGA lingine kwa Wananchi SIKU AJALI ya MOTO ITAKAPOTOKEA.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Je, huo Waraka Mbovu wa Mipangomiji anaotuhumiwa nao alitunga yeye peke yake?Aliupitisha na kuidhinisha yeye peke yake? Nani aliyetoa kibali na kuruhusu huo Waraka wa Mipangomiji ambao unadaiwa kuwa ni mbovu kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali (Government Notice)?
Endapo Kama alishirikiana na wenzake, Je, hao washirika wake nao wamechukuliwa hatua gani za kisheria?? Je, Kumsimamisha kazi huyo mtu mmoja tu ndio suluhisho kwa tatizo lililopo?
The root cause of all these problems is the presence of Bad Constitution in this country. Tufanye Mabadiliko ya Katiba ya Nchi ili kuwezesha kufanyika kwa Mabadiliko Katika Mfumo wa Utawala wa Nchi na Mabadiliko ktk Uendeshaji wa Shughuli za Serikali. Endapo kama kungekuwa na Mfumo Shirikishi wa Utawala wa nchi kama ilivyo ktk nchi zenye Federal Government, huyu Kiongozi yeye peke yake asingeweza na wala asingekuwa na mamlaka ya kutunga na kupitisha Waraka au Sheria ya namna hii ambayo ina madhara mengi hasi kwa umma. Mfumo wa Checks and Balances ungemdhibiti, asingepata nafasi ya kujitungia Waraka mbovu kama inavyodaiwa.
We've to find out the proper solutions for our problems!
Hiki alichofanya huyu Waziri wa Ardhi Waingereza wanakiita kuwa ni "barking up the wrong tree."
 
Je, huo Waraka Mbovu wa Mipangomiji anaotuhumiwa nao alitunga yeye peke yake?Aliupitisha na kuidhinisha yeye peke yake? Nani aliyetoa kibali na kuruhusu huo Waraka wa Mipangomiji ambao unadaiwa kuwa mi mbovu kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali (Government Notice)?
Waliusimamia na kuipitisha wenye maslahi nao yeye alikuwa mbuzi wa kafara

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Vituo vya Mafuta ni Ajira hizo.

Sijaelewa mlalamikaji kama anataka vituo vya mafuta viwe nje ya miji au analalamikia vituo kuwa karibu. Au hata anasema mabadiliko ya hati ya matumizi hayaruhusiwi.

Analalamika zaidi kama vile hataki ushindani kuliko kuonesha taratibu hazikufuatwa!!
 
Sijaelewa mlalamikaji kama anataka vituo vya mafuta viwe nje ya miji au analalamikia vituo kuwa karibu. Au hata anasema mabadiliko ya hati ya matumizi hayaruhusiwi.

Analalamika zaidi kama vile hataki ushindani kuliko kuonesha taratibu hazikufuatwa!!
Huwezi kuwa na Vituo vya Mafuta umbali wa Mita 50 toka kituo hadi kituo pitia Sheria ya Mipango Miji juu ya Umbali toka kituo kimoja mpaka kingine Pia kujenga kituo cha Mafuta katika Makazi sio sahihi Vituo sio maduka ya Nguo au Vyakula

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom