Kuna wake wanaobadili dini KISA mwanamke; mlishawajadili?!

Kuna wake wanaobadili dini KISA mwanamke; mlishawajadili?!

Yaani watu wache kusherehekea maisha kisha dini hiyo haipo.

Mimi binafsi napendelea wa upande wa pili yaani midadi kama yote mje mnihukumu nyie malofa.Yaani niache watoto wazuri kisa dini za kuletewa nasemaje, hiyo haipošŸ˜Ž.
 
Naomba kuuliza na kama mtu anajua au ana experience aweke mtazamo wake au maoni yake. "Je kuna watu wanabafili dini na wanaishi vizur tu wanatatuaje changamoto za kifamilia" naomba elimu wamewezaje? Nina chotala wang mmjoa wa kiislam likija swala la kujadili dini zetu linatukana mood kabisa
 
Ukiona mtu anabadirisha dini sbb ya mtu, basi kuna eneo hajamjua huyo Mungu wake vzr....

Siwezi badirisha dini sbb ya mtu never
Hana mbingu ya kunipeleka
 
Leo Stend ya Kahama nimekutana na Samweli. Samweli alikuwa KKKT. Pale kijijini alihamia mzee mmoja wa Kilokole kanisa la Moses Kulola. Yule mzee alikuwa na watoto wazuri sana. Samweli akampenda mmoja. Wale mabinti walilelewa kwenye ukiristo hasa, hakuna kumchezea mpaka ndoa. Lakini Samweli alijiapiza kwamba lazima ampate yule demu.

Samweli akatuma posa, ikakataliwa kisa yeye yupo dhehebu lingine. Samweli kwa kuwa alikuwa amejiapiza, akaona isiwe taabu, akaokoka, akawa anasali Kanisa la Kulola.

Kufupisha stori, Samweli akaoa yule mtoto. Sisi tulijua yule anazuga tu. Hakumaliza mwaka toka aoe, akarudi KKKT. Akamwambia yule binti wewe endelea tu na EAGT na mimi nipo huku, hamna shida. Ndugu wa binti wakachachamaa sana. Sikumbuki ile ndoa iliendeaje au bado wapo pamoja.

Nazungumzia wale jamaa waliobadili dini hasa Uislamu kuwa Mkiristo au Mkiristo kuwa Muislamu kwa sababu ya mwanamke.

Kwani Mlishawajadili? Kama bado basi leo tuwafikie
Yakobo alilima kibarua miaka saba kwa Laban kisa demu, usishangae.
 
Back
Top Bottom