Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,541
- 139,849
Leo Stend ya Kahama nimekutana na Samweli. Samweli alikuwa KKKT. Pale kijijini alihamia mzee mmoja wa Kilokole kanisa la Moses Kulola. Yule mzee alikuwa na watoto wazuri sana. Samweli akampenda mmoja. Wale mabinti walilelewa kwenye ukiristo hasa, hakuna kumchezea mpaka ndoa. Lakini Samweli alijiapiza kwamba lazima ampate yule demu.
Samweli akatuma posa, ikakataliwa kisa yeye yupo dhehebu lingine. Samweli kwa kuwa alikuwa amejiapiza, akaona isiwe taabu, akaokoka, akawa anasali Kanisa la Kulola.
Kufupisha stori, Samweli akaoa yule mtoto. Sisi tulijua yule anazuga tu. Hakumaliza mwaka toka aoe, akarudi KKKT. Akamwambia yule binti wewe endelea tu na EAGT na mimi nipo huku, hamna shida. Ndugu wa binti wakachachamaa sana. Sikumbuki ile ndoa iliendeaje au bado wapo pamoja.
Nazungumzia wale jamaa waliobadili dini hasa Uislamu kuwa Mkiristo au Mkiristo kuwa Muislamu kwa sababu ya mwanamke.
Kwani Mlishawajadili? Kama bado basi leo tuwafikie