Kuna uwezekano mkubwa Uchaguzi Mkuu 2025 zaidi ya wabunge 20 wa CCM wakapita bila kupingwa. Niko pale nakula popcorn

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Huu ni mtazamo wangu binafsi kuhusu hali ya kisasa nchini sijui ni nini kimetokea kwenye taifa letu. Hilo jambo litatokea si Kwa sababu watu wanamapenzi mema na CCM na wala si kwa sababu watu wana Imani na CCM na sera zake, bali itatokea Kwa sababu ya watanzania kukosa mwamko wa kisiasa ukilinganisha hata na jirani zetu wanaotuzunguka.

Ukisikiliza vijana wengi sana pamoja na wadogo zao kwa maana ya wale waliomaliza michakato ya kusoma na hao walioko shuleni, mwamko mkubwa sana umewekwa kwenye ushabiki wa mpira. Ni aidha Simba na yanga kama sio hivyo basi ni mpira wa huko ng'ambo.

Ukitathimini hata media nyingi zilizopo zimetoa airtime kubwa sana za mijadala ya michezo hususani soka, na habari za kisiasa zinapewa nafasi ndogo sana. Hii inamanisha walaji hupenda hivyo.

Hata hao wanaofanya habari za kisiasa, hufanya very shallow na wengine walishapokwa mitazamo yao kwa hiyo anachambua siasa kwa namna ambayo unajua kwamba hata nafsi yake inamsuta.

Ni katika mazingira hayo, CCM ambao huwa ni maopotunist watajipenyeza Kila Kona na wagombea wao na kuchukua hayo majimbo bila jasho lolote.
 
Back
Top Bottom